UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WASHINGTON DC -METRO (MARYLAND,VIRGINIA NA WASHINGTON DC ) UNAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WANAOPENDA KUWA WANACHAMA WA JUMUIYA KUWA TUTAKUWA NA MKUTANO MKUU JUMAPILI YA PILI BAADA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI OKTOBA 21, 2007 KUANZIA SAA 9 MCHANA KATIKA UKUMBI WA SHULE YA HYATTSVILLE ELEMENTARY SCHOOL .
5311 43RD AVENUE
HYATTSVILLE,
MD 20781
TUNAOMBA WANACHAMA NA WANAOPENDA KUJIUNGA NA JUMUIYA KUJA NA ADA YA MWEZI MMOJA AMBAYO NI DOLA 10 TU. ( $ 10.00).
AKSANTE
AUGUSTINO MALINDA
KATIBU MKUU - ATC METRO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. michuzi mbona hujaweka habari ya mzee situmwike baba yake flaviana situmwike..na yeye alikua mrembo wetu watu inabidi wajue kama amefiwa na baba yake leo.

    ReplyDelete
  2. I thought this umoja was gone! Maana sijasikia jambo lolote ambalo wamelifanya for the last 5 years since Balozi Nyanganyi ambaye alikuwa mlezi wetu aondoke 2002. Mawasiliano na watanzania wanaoishi hapa Metropolitan area yamekuwa mabaya.

    ReplyDelete
  3. Naona kikosi kinapasha misuli wa kuzua jambo. Hiyo jumuia yenu huko ni kituko tu, watu wanatafuta ulaji na umaarufu. Eti wanataka kuanzisha jumuia ya watanzania duniani kwani JK ndio anatoa ruhusa. Wao wangewahusisha wanachama wao hata kabla ya kumuona JK, chama kikiwa bomba kwa ufanisi, JK atakijua tu. Wahenga walisema "Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza". watu wanafanya usanii hata huko majuu, bora sisi tubaki hapa hapa bongo na Ze Comedy wetu.

    ReplyDelete
  4. NAMPENDA YASSIN JE ATAKUWEPO? NITAKUJA TU KWA AJILI YAKE TOKA LOS ANGELES.

    ReplyDelete
  5. Dooh ulaji huoooo! yaani ada dola 10 kwa mwezi x 12x Number ya wanachama! Kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  6. Namsikitikia huyo anayetaka kumfungia safari Yassin - Yassin na katibu wake wasanii kupita kiasi.

    Sababu kubwa ya kufa hicho chama cha Jumuiya ni uongozi wao mbaya na Usanii wa kutafuta umaarufu na kujijengea CVs.....

    Kisha Umoja ni kitu kinachokosekana kwa WaTz wa Washington DC metropolitan - Inasikitisha sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...