mdau katutumia hii ya wanandoa mashombe wa kiingereza ambao wamejaaliwa kuzaa mapacha ambapo kurwa na dotto hao ambao wote ni wasichana mmoja mzungu mmoja ni mmatumbi pyua. wataalamu wanasema hii inatokea kwa nadra sana kwa kipimo cha mtukio milioni moja kwa tukio moja kama hili. wadau, hii imekaaje?
Home
Unlabelled
mapacha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huenda moja alibadilishwa hospitalini.
ReplyDeleteLakini ni kweli genetically inaweza kutokea kama wazazi wote wawili wana ancestors wa kizungu.
Hapa USA ilitokea kuwa wazazi wa kizungu walizaa mtoto mweusi na nywele za kipilipili kabisa. Kumbe wote wawili walikuwa na ancestors weusi ila walificha hiyo habari kwa ajili ya ubaguzi mkali hapa Marekani enzi hizo miaka ya 50!
mama ya watoto anajua siri yake
ReplyDeletehakuna uchawi hapo ni genetics na inheritance tu.Hao wana genes za wazazi wao wote,ambazo zitaendelea kurithishwa kwa mtiririko huohuo vizazi hadi vizazi.
ReplyDeleteMimi sioni cha kushangaa
LaLu
Hii kitaalamu inawezekana. Kila mmja wetu anazaliwa na genes za rangi ya nyeusi na nyeupe. Inategemea ipi kati ya hizo ni dominant gene. Ikiwa dominant gene ni nyeusi basi rangi ya ngozi itakuwa nyeusi, vile vile ikiwa nyeupe basi ngozi itakuwa nyeupe.Ikiwa recessive genes za baba mweusi na mama mweusi zitaungana, basi mtoto atakuwa Albino.
ReplyDeleteIkiwa baba/mama ni mzungu na mama/baba mwafrika. Hapa genes zao za rangi ni dominant. Hivyo watoto hutoka chotara, lakini upo uwezekano mtoto akawa mzungu au mwafrika katika uzao huu. Hivyo hivyo, katika uzao wa machotara hawa, HAISHANGAZI kuona watoto hawa mmoja akiwa mweusi na mwingine mzungu.Natumai sijakuchanganya zaidi.
Anonymous
http://drfaustine.blogspot.com/
That is stupid!
ReplyDeleteHIYO KALI BABU MICHU, LAKINI MBONA HATA MAMA ANAONEKANA KAMA SHOMBE ASILIA?
ReplyDeleteHii ni kweli kabisa, matukioa haya ni machache. Sayansi ya namna hii ilishawahi kuelezewa kwa undani sana na gwiji wa biolojia, Bw Gregor Mendel (1822-1884). Soma zaidi hapa katika kiungo hiki (http://anthro.palomar.edu/mendel/mendel_1.htm).
ReplyDeleteBy: mheshimiwa_2000@yahoo.com
Huyu alipiga wawili kwenye muda sio mrefu. Wakati yai linarutubishwa ngoma zote zikaanguka, yaani mayai mawili yakarutubishwa moja toka goli la kwanza, na yai la pili toka goli la pili watu tofauti ngoma ndio inatoa hiyo kitu. Haya sio identitical twins bali na mapacha wasiofanana. Goli la kisigino, mama anajua siri yake
ReplyDeleteHuwezekano wa mmoja wa watoto hao kubadilishwa hospitalini pia ni mkubwa sana.Hii imewahi kutokea.Ingekuwa vyema zaidi kama tungejua vipimo vyao vya DNA vinasemaje.Kama kweli hao watoto ni wa baba na mama mmoja,basi kuanzia hapo tunaweza kujadili vinginevyo.
ReplyDeleteHapa panahitaji uchunguzi zaidi wa ukweli kwani mwanaume anaonekana kuwa ni mhamiaji toka uarabuni au asia na mwanamke ni mhamiaji toka afrika, marekani zote mbili au nchi za karebiani. Lakini yote hayo si hoja ni lazima kujua hisitoria ya babu na bibi zao.
ReplyDeletehivi haya maneno chotara na shombe ni tafsiri sahihi ya watu waliochanganya damu? shombe alikuwa ni mcongo aliyekuwa na damu ya kizungu. nachoelewa ni kuwa chotara ni mchanganyiko wa kihindi na kiafrika (chotri)sasa waafrika wengine wasio wakongo au asiye mhindi wanaitwa nani kwa kiswahili sahihi? nataka tu kujua labda wewe michuzi unaelewa
ReplyDeleteMimi naona tumuulize BUSHOKE mwenzetu huyo anaweza kuwa MUME BWEGE!!!
ReplyDeleteNamuonea huruma sana huyo mtoto wa kizungu akikuwa anaweza kufikiri hao sio wazazi wake masikini lao mambo mengine bwana!! Anatia huruma
Jamani msiwaonee uwivu wenzenu watoto wao ni wazuri sana hongera zetu, mimi kwa nafsi yangu nahisi huyu ni zeluzelu wa kishombe maana kwakweli wanafanana hakuna cha kuiba hospitali wala cha mama anajua mwenyewe alikotoa, hakuna cha goli lilipingwa muda si mrefu wala nini acha uwivu we 3:51 am mama anajua siri yake nini wewe angalia wakwako wanafanana acha hizo.
ReplyDeleteMimi walasishangae kwani hapa kwetu wapo wengi wanazaliwa na weusi na mtoto hanakuwa mzungu kabisa. mimi ninamapacha na wote wazungu kabisa sasa mimi nilihiba kwa mwanamke mwenzangu.hakukuiba kwani wa kwenye yai moja ndio maana wote wakike walihigia kwa wakati mmoja.hongela sana.
ReplyDeletemichuzi baba anafanya night shift sasa wewe unazani nini hapo.Mwambie jamaa acheck kama miguu inafanana na jirani wao hapo.
ReplyDeleteKumbe Bushoke alichemsha,jamani mlikuwa wapi kumpatia shule kama mambo haya jamni?Inatia raha angalia jamani walivyopendeza!
ReplyDeletejirani kapiga tiktaka hapo!
ReplyDeleteHAPO HAKIELEWEKI KITU MPAKA JERRY SPRINGER AU MAURY ATUAMBIE DNA INASEMAJE NINA WASIWASI KUNA MTU ALIFANYA KUFURU....
ReplyDeletekasera
Hii kali.
ReplyDeletekitaalamu ni vigumu kutoa maelezo yasiyo na ukinzani juu ya ishu hii.
hawa ni 'identical twins', watoto wa jinsi hii wametokea kwenye yai moja( la mama) lilikutana na mbegu ya baba moja. kisha lilivyokuwa linasafiri likapasuka mara2. watoto wanaotokea wanakuwa na jinsia moja na kufanana sana kwa kila kitu.
kuna uwezekano mapacha wanaofanana kutofautiana baadae kama wakiishi mazingira tofauti( environmental factor).
ugumu wa hawa ni hiyo environmental factor haipo sababu ni watoto.
nafikiri itafungua ukurasa mpya wa kisayansi na tafiti nyingi zaidi.
Dr A.A.M(BW)
hawa watoto inaonekana ni wa ivf, mama yao amepandikizwa kwa bahati mbaya mbegu za kwao na za watu wengine ambao ni wazungu
ReplyDeleteHii inawezekana kwani nilikutana na mapacha hapa Marekani mmoja mweusi na mwingine mzungu. Nilibishana nao waliponiambia ni mapacha mpaka waliponiletea picha za utotoni. Wazazi wao mmoja mzungu mwingine mweusi.
ReplyDeleteMhhh!! Jando linatisha!!! unaona vijimambo hivyo???
ReplyDelete