MWILI WA HAYATI SALOME MBATIA UNATARAJIWA KULETWA DAR ASUBUHI HII KUTOKA IRINGA KWA NDEGE. NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO HUYO ALIFARIKI KATIKA AJALI BAADA YA GARI LAKE AINA YA NISSAN PATROL KUGONGANA USO KWA USO NA LORI AINA YA FUSO SEHEMU ZA KIBENA JANA JIONI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU PAPO HAPO, IKIWA NI MADEREVA WA MAGARI YOTE MAWILI. WAOMBOLEZAJI WAMEFURIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU MTAA WA UGANDA, OSTABEI, NA MUMEWE DK. JOSEPH MBATIA AMENUKULIWA AKISEMA HAYATI SALOME MBATIA AMEFARIKI KATIKA TAREHE ILE ILE ALIYOFARIKI MAMA YAKE MZAZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Rest in peace Mrs.Mbatia.

    ReplyDelete
  2. Ni huzuni, may her soul rest in eternal peace...AMEEN!

    ReplyDelete
  3. RIP Mama. Ulikuwa mfano wa kuigwa Mama, Wengi tulitamani nidhamu uliyokuwa nayo kila tukuonapo! Hatuku nawe tena! Kweli tunasikitika. Pole Dr. Mbatia Mungu akutie nguvu wewe pamoja na watoto.

    ReplyDelete
  4. Hii biashara ya magari kugongana uso kwa uso, ni uzembe mkumbwa sana wa madereva. Hivyo kama hata viongozi wetu nao wanapatwa na maswahibu haya,labda serikali inaweza kushtuka na kuliangalia upywa swali zima la usalama barabarani.

    RIP Salome Mbatia


    By Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  5. RIP Mama - Kiongozi mwanamke mfano wa kuigwa na akina mama na wasichana wanaotaka kuwa viongozi. Sifa za mama ni toka enzi ya Chuo Kikuu wengi wanamsimulia alivyokuwa na busara, heshima na nidhamu. Tumekukosa Mama.

    MICHUZI.
    Nyie ni waandishi wa habari, mara nyingi ujumbe wenu unawafikia viongozi kwa haraka. Mimi sipendi na wala sitaki jinsi misafara ya viongozi inavyokimbizwa, mfano wa PM au Vice President na hata President mwenyewe. Kweli utaratibu huu wa kukimbiza magari uachwe hatuko Sudan hapa kwamba tutawaua. Hii ndiyo inayowafanya hawa madereva wa mawaziri kujidai ni madereva bora kwa kuwakimbiza hata kama hawapo kwenye msafari. Mimi naamini madereva ni wa zamani na magari ni yale ya kipindi kile. Haya "MAPULIZO" ya sasa yanapeperushwa sana na upepo. Hizo mbio za ajabu ajabu waache.

    ReplyDelete
  6. Huyu mama Mbatia ni Mke wa Mbatia Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha NCCR mageuzi?

    Kama ndiye sasa wanaishije? Mke CCM,mume NCCR Mageuzi? Kama ndiye CCM walimwaminije na kumpa madaraka makubwa wakati ni mke wa mpinzani mkuu wa CCM na sera zake?

    Mimi sielewi kabisa au MBATIA wa NCCR naye ni CCM?

    ReplyDelete
  7. Ilikuwa ajali mbaya aisee, Mungu azilaze roho za Marehemu Pema Peponi. (The link below contains a very graphic image, Ukigonga hapo chini utaona picha mbaya/inayotisha ya ajali hii, inashauriwa usigonge) Bofya HAPA

    ReplyDelete
  8. alikuwa msomi,kiongozi na mama wa kuigwa mwenye nidhamu, aiba na kujituma katika kufanikisha masuala mbali mbali. Taifa limempoteza mmoja mchango wake katka kipindi ambacho ulikuwa unahitajika.
    Poleni sana famila ya Dr. Mbatia kwa kumpoteza mke na mama wa familia.
    Mungu awafariji katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho ya marehemu sehemu njema peponi

    ReplyDelete
  9. Aliyepiga picha zote za ajali sii mwingine ni yule yule Zitto Kabwe ambaye aliwasili eneo la ajali muda mfupi baada ya ajali WHAT A COINCIDENCE!!!

    ReplyDelete
  10. Habari zaidi kutoka eneo la tukio, zilisema mbali ya Dkt. Mathayo, watu wengine walikuwa

    kwenye eneo la tukio na kutoa msaada mkubwa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe

    ambaye alikuwa safarini kwenda mkoani Ruvuma.

    Bw. Kabwe alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuwa alishuhudia magari hayo

    yakigonganga uso kwa uso na kulazimika kukatiza safari yake kusadia kuwahisha majeruhi hospitali.

    ReplyDelete
  11. wewe anonymous saa 9:49 pole sana huyu mama si mke wa Mbatia WA NCCR ni dada yake alafu maswali ya nini badala ya kutoa pole unaanza kuuliza wanaishije lelelile umbea huo wewe hata kama ni Mke wa Mbatia wa NCCR mageuzi kapewa cheo wewe inakuuma nini pole weee.? na kama huelewi si ukae kimya.

    ReplyDelete
  12. RIP Mama, poleni sana familia ya Mbatia...mhhhhhh hiyo picha inaliza sana jamani.
    MAY ALMIGHT GOD REST HER SOUL IN ETERNAL PLACE AMEN.

    ReplyDelete
  13. RIP Kweli hujafa hujaumbika!!!!!

    ReplyDelete
  14. Pamoja na kutoa pole kwa kifo cha mheshimiwa salome Mbatia nina maoni yanayoweza kupunguza ajali za waheshimiwa.
    Itakuwa jambo zuri magari ya waheshimiwa kwenda mwendo wa salama na sio wa kasi kama tunavyofahamu.
    Itakuwa vizuri wao waheshimiwa na madereva wao kuruhusiwa na Rais/waziri mkuu kusimama njiani mfano katika wilaya yoyote njiani na kujipumzisha kabla ya kuendelea na safari ndefu. Kila wilaya ina 'government rest house' hivyo zitumiwe vizuri na pia wanaweza kubadilishana mawazo na viongozi wa wilaya katika 'informal meetings over lunch and dinner' wakati wakijipumzisha.
    Waweza pia kuingia ktk taasisi za kiserikali na kijamii au mbuga za wanyama njiani na nyingi tu zingependa kupata ugeni wa muda mfupi kuelewa maendeleo na matatizo za sehemu hizo wapumzikazo na kupeleka taarifa hizo kwa wizara vinazohusika.
    SENIORJUNIOR LONDON.

    ReplyDelete
  15. RIP

    Mbatia wa NCCR mageuzi ni shemeji wa salome, mumue wa mama salome ni daktari wa magonjwa ya akili.

    ReplyDelete
  16. Rest In Peace mama Mbatia. mdau Holland

    ReplyDelete
  17. Mama nakulilia sana kiasi cha kushindwa kujizuia, hasa nilipoona picha yako katika gazeti la mwanachi jinsi ulivyoumia na kuteseka mpaka ukakata roho. Mungu akakupokea ukawe malaika mwema kama ulivyokuwa hapa duniani. Kalale pema peponi mama yetu. Amen

    ReplyDelete
  18. Akina Mama Tanzania tumepata hasara. Dada Salome alikuwa katika mstari wa mbele kupigania haki zetu! Naomba serikali wachunguze hii ajali!

    REST IN ETERNAL PEACE DADA SALOME.

    ReplyDelete
  19. jamani mama salome Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi
    kingine ni serikali yetu ijaribu hata mambo ya private jets hata kwa watu wakubwa kama hao.
    im only saying

    ReplyDelete
  20. poleni sana familia ya wafiwa. Mungu awape moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  21. Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...