Tunapenda kuwatangazia Watanzania wote kwamba kutakuwa na Misa maalum ya Kumwombea rehma Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, siku ya Jumapili tarehe 14 Oktoba, 2007 kwenye Kanisa la St. Anne and St. Agnes
lililopo Gresham Street,
London,
EC2V 7BX
karibu na St. Paul’s Cathedral.
Tafadhali wote mnaombwa kuhudhuria pamoja na familia zenu. Mwenye kupata ujumbe huu na amwarifu mwenzake.
Mungu awabariki nyote mlioandaa Ibada hiyo muhimu. Tunawatakia kila la kheri.
ReplyDeleteMICHUZI,time is money,hasa huku duniani.sasa hii MISA inafanyika usiku,mchana,asubuhi au jioni. watanzania bwana ''''''
ReplyDeleteHivi wewe uliyepost hili tangazo ulishgawahi kuwaarika watu walau waje kumwombea babu yako? Acheni unafiki, what is done is done!!! Baba wa taifa alishafariki, ni sawa tu na akina Plato na Aristotle. Ulishawahi kusikia Wazungu wanahitisha misa ya kuwaombea watu kama hao pamoja na kwamba mchango wao katiak jamii ulikuwa hauna kifani. Wabongo kwa mtindo huu, kufika hatufiki. Tunatakiwa kuwaanda Nyerere wengine na siyo huyu aliyekwisha fariki. Kila siku watu wanapoteza wakati kumfikiria Nyerere. Naye pia alikuwa na mapungufu yake kibao.
ReplyDeleteNawaomba watu wawaenza wazazi wao na mababu zao.
huu ni ubaguzi,mbona sokoine na wengine hawafanyiwi misa?
ReplyDeletekwa nini nyerere.
anoniwa7:39 mimi sioni vibaya watu kufanya misa ya kumbukumbu.mbona inafanyika kumbukumbu ya sokoine kila mwaka? na hata mwezi uliopita kulikuwa na kumbukumbu ya diana? na pia hiyo misa inachukua less than 2hrs tena jumapili siku ya mapumziko. sidhani kama inaweza kutufanya tukashidwa kumuuandaa nyerere mwingine.nafikiri hiini imani ya watu.ila naomba huyo mdau aliye leta tangazo utuambie ni saa ngapi hiyo misa ita somwa nafikiri amesahau kwa bahati mbaya kama watu wenine wanavyo sahau.
ReplyDeletewewe zero hapo juu.Sokoine huwezi kumlinganisha na nyerere.
ReplyDeletekwa wakristu misa za kumbukumbu ni kawaida.Kama hukuwa na la kuandika kaa kimya.
Tufahamisheni misa saa ngapi.