NAPENDA KUMTANGAZA MDAU BRIAN MARIKI (NDIYE MWENYE MTUNGIKO HUO HAPO JUU) ALIYE HUKO HOUSTON, TEXAS, MAREKANI, KUWA NDIYE MDAU ALIYEBAHATIKA KUWA WA 2,000,000 KATIKA GLOBU YETU HII YA JAMII NA NDIYE MSHINDI WA ZAWADI YA $500 KAMA ILIVYOTANGWAZWA. HONGERA SANA BRIAN KWA USHINDI HUO, MCHAKATO WA KUKUTUMIA ZAWADI YAKO HIYO YA $500 UMESHAANZA NA TEGEMEA KUIPOKEA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.
NACHUKUA NAFASI HII KUWAPONGEZA WADAU WOTE AMBAO WALIJITAHIDI KUSHINDA ZAWADI HII KWA UDI NA UVUMBA ILA BAHATI HAIKUWA YAO NA ASIYEKUBALI KUSHINDWA SI MSHINDANI. NAFURAHI KUKUTA KWAMBA NILIPOKEA EMAIL TAKRIBAN 1,300 NDANI YA DAKIKA 20 NA KUJIKUTA NAHEMEWA KWA MWITIKIO MKUBWA WA WADAU TOKA KILA PEMBE YA DUNIA.
ASANTENI SANA WADAU WOTE NA KAMA NILIVYOAHIDI NATAFUTA WADHAMINI WENGINE ILI TUWEZE KUWA NA MASHINDANO YA MARA KWA MARA NA ZAWADI NONO.
NITAKUWA MTOVU WA ADABU ENDAPO KAMA NITASAHAU KUWASHUKURU WADHAMINI WA SHINDANO HILI AMBAO SI WENGINE ILA COMPUTERCONSULT LTD WALIO JENGO LA INTER CONSULT KIJITONYAMA, DAR. NI MATUMAINI YANGU WADHAMINI WENGINE WATAJITOKEZA KUCHANGAMSHA GLOBU YETU HII YA JAMII


HONGERA KAKA MICHUZI!!! HONGERA MSHINDI!
ReplyDeleteLakini hesabu zangu zinaniambia umetembelewa na watu MILIONI TATU! Kumbuka kuna wale MILIONI MOJA waliofutwa na mashine ya kuhesabia.
ENDELEZA LIBENEKE KAKA! TUKO PAMOJA.
Kaka Michuzi shikamoo! Naomba nikupe Hongera kwa kuwa na hii website yenye mambo mengi mazuri, binafsi naifurahia kwani ina mambo mengi ambayo nimeweza kujifunza na kuyajua. Pia hongera kwa mshindi! then naomba next time uweke wazi sifa za kuwania hilo shindano litakalo kuja. Mungu akutangulie kwa kila jambo.
ReplyDeleteno! no! no! sikubali kabisa mimi ndio nilikuwa wamilioni mbili, niliingia saa 7 kasoro usiku, tuzo yangu hiyo.. lazima niende mahakamani, nimeshaanza kuwasiliana na advocate Mkono tunafungua kesi leo..
ReplyDeleteCONGRATZ BROOOO....ENDELEZA LIBENEKE SI TUPO NYUMA YAKO..HONGERA MSHINDI
ReplyDeleteHongera kaka Michu! Si tupo hapa H-touni(Houston) na tunamfahamu huyo mshindi..Lakini hanauhusiano wowote na wewe..Zawadi imetolewa kihalali..Pongezi kwako, tuendeleze libeneke!
ReplyDeleteJamaa kala pesa ya bure kabisaa baada ya kuidanganya counter. Michuzi next time usitoe pesa za bure maana wajanja watakula pesa yako kama hivi. Ni mambo ya computer tu. Chao
ReplyDeleteMICHUZI SISI WADAU WA BONGO HATUKUBALI, SIO HAKI KABISA KUTUSHINDANISHA NA WENZETU WA UGHAIBUNI...WEWE MAMBO YA HAPA UNAYAJUA, MTANDAO SLOWWWW UKI-CLICK UNASUBIRI MPAKA UNALALA, UMEME UNAKATIKA KATIKA, COMPUTER NYUMBANI HATUNA, SASA TUTASHINDANA VIPI NA WENZETU WENYE MA-HIGH SPEED, MAKOMPYUTA NYUMBANI WANACHEZEA? SIKU NYINGINE CHUKUA 10 NYUMBANI NA 10 UGHAIBUNI CHEZESHA BAHATI NASIBU UTUPE CHANCE SAWA!.
ReplyDeleteThe Housemate most deserving the US$100 000 is...
ReplyDeleteRichard - to turn his life around
Maureen - she suffered a lot as a kid
Ofunneka - for being the mother of the House
Tatiana - to boost her modelling career.
kaka michuzi nimependa kuirusha hii maana nimeingia kwenye website ya bigbrother hivyo kwa ushirikiano wa watanzania wote tunaoweza kuitangaza nchi yetu tafadhali tusiwe na kinyongo tukumbuke kwamba huo ni mchezo tuu kama bingohttp://www.mnetafrica.com/bigbrother/ waosha vinywa msifikiri mimi ni Linda dada wa richie mimi ni mzalendo halisi na mwanaharakati mtarajiwa.
NAPINGA MATOKEO HAYA MSHINDI ASIKABIDHIWE ZAWADI MPAKA TUPATE HAKI SAWA KAMA ALIVYOSEMA MWENZANGU HAPO JUU.WATU WA BONGO HATUJAPATA HAKI YETU KWA KUWA MITANDAO IKO SLOW SANA.
ReplyDeleteWADAU WA BONGO TUNAWEKA PINGAMIZI KWA MSHINDI NA SJINSI SHINDANO LILIVYOENDESHWA.
Hongera mdau itakusaidia hiyo ni sawa takribani na masaa 50 ya boksi hayo,ambapo hapa Uk cku hini ni paund 5.8 hadi 6 kwa masaa 20 ama siku mbili za masaa 12 kwa cku ama tatu za masaa8 kwa cku.Jamani Bahati yake hiyo.Na mlio Bongo poleni kwa utofauti wa masaa,lakini hii ni changamoto labda baadaye iwepo fairness of conditions ingawaje bahati huwa haina mlomlongo wa vipengele.
ReplyDeleteMwisho tukumbuke kuchacharika kwa maisha na kuliendeleza Taifa letu.
Wadau wa bongo wameshaanza kulalamika..oh ughaibuni high speed. Sasa bongo kwani hakuna high Speed? Oohh ughaibuni komputa nyumbani, je bongo huna komputa nyumbani? Michuzi katuwekea picha maisha yalivyo tambarare bongo..sasa mnalalamika nini?
ReplyDeleteHivi nyie wabongo mnanini!?!?!,yaani mnashindwa kufurahi mtu mwingine akifanyikiwa!.
ReplyDeleteKaka Michuzi,hawa watu watasema mpaka kesho...achana nao!.
Mtanisamehe,ila inasikitisha kuona jinsi gani watu wanavyotafuta visingizio.
Mshindi kashapatikana,bahati yenu ilikuwa mbaya.Acheni kusema!
Brian hongera sana.
wabongo acheni roho mbaya!.
ReplyDeleteHaaa haaa ni jinsi gani inavyoonyesha ndugu zetu mlio ughaibuni mnaishi maisha ya dhiki, haaa haaaa kweli na nyie mko kwenye mchecheto wa kugombania $500. Mmmm kweli ninaamini wanayosema maisha ya watanzania ugahaibuni ni ya shida!! Hebu someni mrudi tuliendeleze taifa letu, mbona sisi huku tunaishi raha sana jamani though tunapata kidogo sana!!! Mmmm KAZI IPO!!
ReplyDeleteMichuzi hongera kwa mashindano, but haki haikutendeka imagine shindano limefanyika usiku wakati wabongo tukiwa tunakula mbonji, it seems wadau wako wengi wako nje ya nchi siyo, poa kumbuka wewe ni MZAWA! Next time make sure unaangalia majira ya saa ili kuepusha migongano.
ReplyDeleteWabongo acheni hizo...eti ooh high-speed,nyie mnajuaje kama anatumia dial-up!.
ReplyDeleteVile yuko marekani haimaanishi kuwa mambo yote shwari.
Mimi mdau wa Ottawa,Canada nampa hongera sana mwenzetu wa Houston,Texas.
Hivi nyie wabongo mnanini!?!?!,yaani mnashindwa kufurahi mtu mwingine akifanyikiwa!.
ReplyDeleteKaka Michuzi,hawa watu watasema mpaka kesho...achana nao!.
Mtanisamehe,ila inasikitisha kuona jinsi gani watu wanavyotafuta visingizio.
Mshindi kashapatikana,bahati yenu ilikuwa mbaya.Acheni kusema!
Brian hongera sana :D :D
Inasemekana Bongo mambo tambarare sasa kwa mtaji huo kila kitu ni sawa acheni ulalamishi, Ila mshindi kutumiwa mia tano toka bongo noma si ungeagiza achukue ndugu au jamaa babaake!
ReplyDeleteHahahahaha jamani mwachieni mshindi. Hata week haijapita mlisema life ni tambarare bongo tu kama abroad sasa imekuaje kuwa sio halali tena.
ReplyDeleteNi haki yake na hata likianzishwa shindano lingine jueni mshindi atatoka USA. Na wala sio kwa kuforge wala nini ila ukweli ni kuwa na wala sio nataka kuanzisha mjadala mwingine hapa na mtake msitake lakini utambarare wa Internet upo USA.
Nilitembelea UK siku si nyingi nilishangazwa na jinsi watu walivyo na computer nzuri majumbani mwao lakini hamna internet service. This is true kwa hiyo bongo msilalamike hata watu wengine wengi tu wa nchi nyingine wanatumia computer za kazini, library na internet Café.
hehehehehe tambarare.....kaka Michuzi lete shindano lingine
by the way congratultion on reaching another milestone. Watu tumekodolea macho dollar million mbili tukasahau ushindi wako..
Na kama sikosei kuna aliyesema bongo siku hizi kama New York hakuna haja ya kuwa ughaibuni sasa lawama za nini?
ReplyDeleteHII NI MBINU ILIANDALIWA NA MICHUZI WADAU WA BONGO TUKOSE ZAWADI HII.NARUDI TENA WADAU WA BONGO TUMEWEKA PINGAMIZI YA KUTOLEWA ZAWADI YA MSHINDI
ReplyDelete"HII NI MBINU ILIANDALIWA NA MICHUZI WADAU WA BONGO TUKOSE ZAWADI HII.NARUDI TENA WADAU WA BONGO TUMEWEKA PINGAMIZI YA KUTOLEWA ZAWADI YA MSHINDI"
ReplyDeleteDamn ok,so it's a conspiracy now lol?
"Haaa haaa ni jinsi gani inavyoonyesha ndugu zetu mlio ughaibuni mnaishi maisha ya dhiki, haaa haaaa kweli na nyie mko kwenye mchecheto wa kugombania $500. Mmmm kweli ninaamini wanayosema maisha ya watanzania ugahaibuni ni ya shida!! Hebu someni mrudi tuliendeleze taifa letu, mbona sisi huku tunaishi raha sana jamani though tunapata kidogo sana!!! Mmmm KAZI IPO!!"
ReplyDeleteSo let me get this straight:
Because a person chose to participate in a competition that happened to involve money,this automatically means the said person who participated in the stated competition is in a bad financial position?
Money is Money,any logical person will tell you that:If you're financially challenged=you work hard to rise above the challenge.If you're financially balanced=you work hard to maintain the balance.
Your Logos is completely off track because you've provided a weak argument,closely followed by a ridiculous claim that is backed by no reason.Thus(Ironically),it appears that it is you that needs to hit the books ;)
"Hivi nyie wabongo mnanini!?!?!,yaani mnashindwa kufurahi mtu mwingine akifanyikiwa!.
ReplyDeleteKaka Michuzi,hawa watu watasema mpaka kesho...achana nao!.
Mtanisamehe,ila inasikitisha kuona jinsi gani watu wanavyotafuta visingizio.
Mshindi kashapatikana,bahati yenu ilikuwa mbaya.Acheni kusema!
Brian hongera sana."
Thank you very much :D !
"Wabongo acheni hizo...eti ooh high-speed,nyie mnajuaje kama anatumia dial-up!.
ReplyDeleteVile yuko marekani haimaanishi kuwa mambo yote shwari.
Mimi mdau wa Ottawa,Canada nampa hongera sana mwenzetu wa Houston,Texas."
LOL exactly!Thanks!
We SAWA na nyie mnaokandia watu wa ughaibuni kukucheza hii game....ndio maana hamtatajirika milele. Trump, Bill gates, Oprah wote wana hela kishenzi lakini hawaachi hata penny ipite pembeni. Sasa nyie mkikalia kusema watu wa abroad wananjaa kazi ipo huko kwenu. What is a burden of having an extra $500 in your pocket today? Muulize Brian today..
ReplyDeleteI was all for the winning too, but the real enjoyment was derived from the joy of being the number 2 million counter. My co-workers were playing the game all day with me. It was funny and we didn’t even know how we actual missed.
Stop complain just remember it wasn’t your lucky this time.
Sawa get a life. Comments nne halafu zote zinaji contradict zenyewe. Vipi wewe? Mara wadau mlioko ughaibuni mna njaa, mara mimi niko Canada!!!! Sasa Canada sio ughaibuni? Hebu usitupotezee muda kwa comments zako za kinafiki. Inaelekea umeshikwa na hasira sana...Comments nne topic moja...find a job ...
ReplyDelete