Kwa niaba ya kanisa zima la Umoja international Outreach lenye makao yake makuu hapa Dallas,Texas,ninapenda kutoa pole kwa Rais wetu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na familia nzima ya Dr Joseph Mbatia kufuatia msiba wa Mheshimiwa SALOME MBATIA.
Kanisa la Umoja litaendelea kumkumbuka Mheshimiwa Mbatia kama mcha mungu aliependa kusimamia haki wakati wake wote.Kanisa la la Umoja litaendelea kuwapamoja na nyie kwa njia ya maombi katika wakati huu mgumu."Biblia inatukumbusha kwamba sisi ni wapitaji hapa duniani na makao yetu yako mbinguni."
Pastor Absalom, Nasuwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hizi salamu za rambirambi ni jambo zuri sana.
    Lakini mbona tunasahau kwamba waliokufa katika ajali hiyo si Bi. Mbatia peke yake. Na dereva wake amefariki kwenye ajali hiyo, pamoja na utingo wa fuso naye inasemekana alifariki kwenye ajali hiyo.
    Katika salamu zetu za rambirambi tuwakumbuke wote hao na familia zao.
    Mwenyezi Mungu azijalie familia za marehemu wote waliokufa kwenye ajali hiyo nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na maombolezo. Amen.

    ReplyDelete
  2. nakubaliana kabisa na maoni yako. inadhibitisha kabisa kwamba mnyonge hana haki. Inabidi tukumbuke kwamba ndugu wa marehemu (dereva) nao wameumia kama ndugu wa mama S.M. inabidi nao kiubinadamu wakumbukwa katika hali ngumu ya janga lililo wapata.

    ReplyDelete
  3. inaonekana kazi yenu nyinyi wawili ni kukosoa kila comment inayowekwa humu cha maana watu wanatoa pole zao and they can mention whoever they want to mention kama wewe unataka kutoa pole kwa utingo na dereva weka comment yako

    ReplyDelete
  4. anaweza akawa ni mtu mmoja anajisupport mwenyewe. Hii mambo ya kutumia anonymous ni kutojua tu jina la mtu lakini kwa speech writting yake huyo ni mmoja. Alikosa la kusema tumwonee huruma tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...