Mwaliko wa Sikukuu ya Eid el Fitri
- Jumamosi, October 13, 2007
Assallaam Alleykum wa-Rahmatullah wa-Barakatuh!

Ndugu Waungwana!Mama zetu wapenzi - Aunty Fatma, Aunty Zabibu (Mama Lila), Aunty Mariam na Aunty Fatma Soud na Familia zao, kwa pamojawanawakaribisha katika hafla ya Eid el Fitri na kuuaga mwezi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, itakayofanyika katika Club House ya Cherry Ridge Subdivision, siku ya Jumamosi tarehe 13 October 2007, kutoka saa 7:00 Mchana (1:00PM) mpaka saa 12:30 Jioni (6:30PM) Inshaallah!!!

Chakula kitaliwa saa 7:30 mchana (1:30PM) Tafadhali sana Muda Uzingatiwe

Note:
Shughuli hii ilikuwa ifanyike nyumbani kwa Aunty Fatma, lakini kutokana na kuongezeka kwa Jumuiya yetu imebidi tuihamishie kwenye nafasi zaidi, Alhamdullillah!!! M'Mungu atuongeze zaidi!

Club House - Address:Cherry Ridge Subdivision.
3571 Cherry Ridge Blvd Decatur,
GA 30034-5010, US

Club House iko mkono wa kulia unapoingia tu katika Subdivision, utaona Tennis Court baada ya Tennis Court ni Club House.
Note:
Shughuli ilikuwa iongozwe na Sheikh Mkuu wa Atlanta (aliye uhamishoni) lakini kwa sababu zisizoweza kuzuilika Sheikh wetu hatoweza kuhudhuria... Inshaallah tunaomba ma-Sheikh wengine wajitokeze kuweza kusimamia shughuli hii...
Sala za Dhuhr na Asr zitasaliwa hapo hapo kwenye Club House.
Atakayesikia Mualiko Huu tafadhali amjulishe mwenziwe na mwenziwe amjulishe mwenziwe na mwenziwe amjulishe mwenziwe....
WOOOOOOOOOOTE MNAKARIBISHWA...!!!
Tunaomba muda uzingatiwe! (Tafadhali Car-Pool inapowezekana)
Kufika kwenu ndio ukamilisho wa shughuli yetu!!! Ahsanteni!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...