mdau obed mwakitalika katuletea hii leo.
Vazi la suti mara nyingi humfanya mvaajia aonekane nadhifu na mwenye heshima ndani ya jamii anayoishi hususani kwa akina baba kabwela. Pia kuna uvaaji wa suruali nyepesi, shati jepesi, kiatu cha mchongoko na tai inatangulia mbele watoto wa Dar wanasema vazi la "kipapaa".
Vazi hili kutokana na heshima lukuki linazopata kutoka kwa jamii hasa ya makabwela kama nilivyokwisha kusema awali limekuwa likitumika hata na wahalifu kama majambazi na matapeli katika kuwalaghai watu mbalimbali ambao ndio huwa walengwa wa uhalifu wao. Pia vazi hili hupendelewa kutumiwa na viongozi, na mabwana harusi au hata wakurugenzi na mabosi wa mashirika, taasisi, na makampuni mbalimbali.Lengo langu siku ya leo ni kuwaleteeni sheria zinazotakiwa kuzifuata mtu anapovaa suti la sivyo unaweza kujikuta upo matatani kwa kuvunja moja ya sheria hizo. Sheria zenyewe ni kama ifuatavyo. Unapovaa suti au tai hakikisha huvunji sheria hizi hapa chini:-
1. Ni marufuku kuvaa kandambili au malapa
1. Ni marufuku kuvaa kandambili au malapa
2. Ni marufuku kuvaa soksi mbovu.
3. Ni marufuku kujisaidia uchochoroni.
4. Ni marufuku kupenga kamasi barabarani.
5. Ni marufuku kupanda daladala.
6. Ni marufuku kuendesha baiskeli au pikipiki.
7. Ni marufuku kucheka cheka hovyo.
8. Ni marufuku kuomba change dukani au kurudishiwa change.
9. Ni marufuku kubeba mfuko wa plastiki maarufu kama rambo
10. Ni marufuku kuingia kwenye kibanda cha simu.
11. Ni marufuku kula magengeni.
12. Ni marufuku kuonekana unatafuna barabarani.
13. Ni marufuku kutembea na pesa za sarafu mifukoni mwako.
12. Ni marufuku kulia hata kama umeletewa taarifa ya msiba.
14. Ni marufuku kupiga miruzi.
15. Ni marufuku kuonekana unatoka mijasho kama unasukuma mkokoteni.
16. Ni marufuku kuongea kwa kelele.
17. Ni marufuku kunywa chai au kahawa kwa kutumia kikombe cha plastiki.
18. Ni marufuku kutembea kwa miguu.
19. Ni marufuku kukimbia popote pale.
20. Ni marufuku kunuka mdomo wala kikwapa hili kosa kubwa sana na hukumu yake mpaka mbinguni ipo.
21. Ni marufuku kusema uongo.
22. Ni marufuku kuonekana umekasirika unatakiwa uwe na uso uliokunjuka.
23. Ni marufuku kumchapa mtoto.
24. Ni marufuku kusababisha ubishi au mjadala uso na maana.
25. Ni marufuku kunywa pombe za kienyeji
26. Ni marufuku kunywa kinywaji chochote bila glasi
27. Kwa akina dada ni marufuku kuvaa sketi inayoburuza chini
27. Ni marufuku kucheza mdundiko
29. Ni marufuku kutembea peku
30. Ni marufuku kuchomekea koti
Mimi naona kuna sheir anyingi ziwe marufuku kwa watu wote either umevaa suti or not.
ReplyDelete1. wabongo...kukojoa vichochoroni, kupenga makamasi, kutema mate is big no no no
2. Kutoa majasho no no no deodorant zipo bei rahisi tu.
3. Kandambili barabarani na vumbi letu ndio mwanzo wa kupata Funza.
4. Kunuka mdomo tumia chumvi kama huna hela za dawa ya mswaki
Ustaarabu sio lazima uvae zuti...kila mtu awe msaarabu na suti au bila suti
Nafikiri hizi sheria ni za huko huko Bongo/Africa au za wale ambao hawajawahi kusafiri, maana yote yaliyoelezwa kuwa ni marufuku kwa kuvaa suti, huku Ulaya ni ya kawaida mno
ReplyDeleteHAYA MASHARTI NI HUKO AFRICA HUKU ULAYA MAISHA FASTA FASTA HAO WAZUNGU NDIO MABINGWA WA KUVAA SUTI NA:
ReplyDeleteKUTOKA NDUKI BARABARANI.
KULA SANDWICH BARABARANI.
KUFOKA BARABARANI NA HATA KWENYE TAARIFA ZA HABARI KWENYE TV UNAWEZA UKATHIBITISHA HAYA UKITYUNI CNN.
NA MENGINE MENGI AMBAYO YAMEORODHESHWA
Marufuku?
ReplyDeleteMpaka niko mtamboni bado sijaweza kutafakari ni nini anachokiona na suti...katika kuchambua nimeona kwamba huyu Bwana kabainisha fasiki na alikuwa kwenye dimbwi la mapululu tehe tehe e!!!!
Huyu mwandishi wa sheria za tai anasikitisha. Kiasili Vazi hili ni kutoka Majuu, Kawaida ukiiga lazima uige na taratibu za kitu ulichoiga kwa wenye nacho.
ReplyDeleteWao walioligundua si kitu kikubwa sana kama huyu jamaa anavyo chukulia, Mimi naona jamaa ukiangalia vizuri ana vipesa vidogo hivyo upelekea kuona walionazo hizi suti wanazo.
Ajue kuwa suti ni kavazi tu, hivyo hata UK, US na kwingineko watu hupanda daladala na suti, hula na kutukana nk, Mzee acha porojooo