Hi bro Michu, naomba uirushe hii article ili tuwasaidie wadogo na watoto wetu waliopo mashuleni, hakuna wa kutetea maslahi yao zaidi yetu.......
Naamini wadau wengi wa blog hii mtakua mko aware na mambo mengi nitakayoyaongelea hapa kwa kuwa mmeyaexperience huko mashuleni mliposoma. Cha kushangaza ni kwamba hakuna mtu anaetaka kuyaongelea - si viongozi wa serekali, si walimu, si wana JF, nahisi watu wanaona tu kuwa ni part and parcel ya process nzima ya elimu. Nitalenga zaidi kwenye mashule ya boarding ambako kama wengi- nilisota huko kwa miaka sita.

Suala nyeti kabisa ambalo naona linaendelea kuwa ignored na serekali na wakuu wa mashule ni “Health and Safety” .Nilitegemea kwamba baada ya maafa ya Shauritanga mwaka 1994 ambapo wanafunzi 41 walipoteza maisha yao labda kungekua na mabadiliko na new legislations za kutoa guidelines kwa wakuu wa mashule zingetungwa. Lakini hadi leo kuna wanafunzi bado wanafungiwa mabwenini mida ya usiku hasa kwenye shule za wasichana. Ni mabweni ya shule ipi yana Fire escape routes leo hii? Fire extinguishers utazikuta Staff rooms tu, mabwenini hakuna kitu. Chemli, mishumaa na koroboi ambavyo ni main recipes za fire disasters bado vinaendelea kutumika mabwenini mida ya usiku, hasa kwa shule za vijijini- ndio maana kila siku mashule yanaungua lakini no one is doing anything!

Utakuta shule iko kijijini sana na mbali kabisa na mji, haina kituo cha afya na mbaya zaidi haina hata baskeli achilia mbali gari- lakini cha kushangaza serekali inakubali kuisajili.Mwanafunzi akipata maradhi au injuries ambazo ni serious usiku its very likely kwamba atakufa! Kwanini kusingekua na minimum standards ambazo shule inatakiwa ku achieve kabla ya kupewa kibali? Sehemu nyingine wanafunzi wanatumia muda mwingi kusaka maji kuliko muda wanaotumia darasani, cha kushagaza ukiwa mchafu kwenye ukaguzi utamtambua mwalimu wa zamu!!

Bado karne hii wanafunzi wa shule nyingi za boarding wanatumia dekio la ‘tambara’, hakuna cha gloves wala mop! Wakati nipo kidato cha pili, corridor ya darasa langu ilikua karibu sana na ’assembly’ ground na naweza sema labda wanafunzi zaidi ya mia 300 walikua wakiitumia corridor hiyo kwenda ‘mstarini’ lakini kila siku there must be a 14 or 15 years old poor boy crawling on his knees to get it cleaned and it used to be worse kipindi cha mvua, dongo la Moshi huwa linapenda kudandia soli! Sasa hebu jiulize hao wanafunzi wengine wanaopita hapo wamekanyaga nini na viatu vyao? Hapo kuna vinyesi , mikojo, and all sort of horrible creatures na huyo dogo ana ndoo na tambara lake tu na kusipodekiwa atakiona cha mtema kuni.
How much does it cost to buy a mop and a bucket kwa kila darasa? Huko vyooni ndo usiseme kabisa, kunahitajika cleaning chemicals-lakini naona this will be asking for much. Mbaya zaidi choo kikiziba,kwa kuwa hakuna alternative watu wanajazia humohumo tu- By the way adha ya choo nilikutana nayo hata nilipokuwa mlimani UDSM- vyoo vile vya kukaa viliwekwa kipindi hicho ambacho wanafunzi walikua wachache,chumba kimoja-mtu mmoja na sio sasa chumba kimoja watu nane, as a result hakuna mtu anaekaa kwenye toilet seat siku hizi, watu wanapanda kwenye seats (natamani ningekuchorea hapa!)

Sikujua kama bullying ni tatizo hadi nilipokuja ulaya coz nilikua na mimi nina mtazamo wa wengi kwamba its part and parcel ya hizo shule za boarding. Utanyanyasika ukiwa form one then ukifika form two kibao kina change na wewe unaanza kuwatesa ’njuka, ndama’ wanaofuatia .
I must say, I was a strong lad na I got away with it but ukweli ni kwamba mambo wanayofanyiwa form one huko mabwenini- they are horribly shocking! Na kibaya zaidi they are scared to report them kwa walimu. Dogo mmoja alitumwa akamletee maji ya kunywa mbabe mmoja, alipokataa mbabe yule akatoka kimyakimya na baada ya muda akarudi na kigeleni cha lita tano kikiwa kimejaa maji-“Si umekataa kunipa maji? niimekuletea wewe mheshmiwa na uyanywe”,aling’aka mbabe huyo huku akimtizama kwa usongo, dogo aliyanywa hadi ikabidi wababe wengine waingilie kati kumuokoa otherwise angepasuka tumbo! Ilikua ni kawaida kuamshwa usiku wa manane na kulazimishwa kuimba wimbo wa taifa.Ilifikia kipindi hadi wazazi walikua wakihamisha watoto wao kwenye baadhi ya mashule. Naamini wakuu wa mashule wanaweza kuwa taratibu nzuri zaidi za kukabiliana na tatizo hili na na hili linahitaji maelekezo toka wizarani?

Itakua dhambi nisipoongelea issue nyeti hapa- MSOSI coz najua hiki ni kilio cha wengi. Migomo mingapi imekua triggered na suala la chakula mashuleni? Ukiliingia darasani mwalimu anahubiri kuhusu balanced diet lakini unapoingia dinning hall unagundua kuwa mwalimu alikua akiongelea ndoto tu.
Ninaamini kabisa kwamba mkuu wa shule yang alikua anapata fungu linalotosha kutulisha vizuri (and were not actually asking for anything rather than variety na sio hiyo balanced diet coz naona bado ni ndoto huko mashuleni!) Hivi kweli ni haki kulishwa ugali na maharage kwa term nzima (usiku na mchana) na maharage yenyewe yameungwa kwa chumvi tu, wadudu kibao!and you can tell mnunuzi alipoenda sokoni alichagua yale ya bei rahisi kabisa. Hapo asubuhi breakfast ni uji usiokuwa na sukari wala mafuta (popularly known as sumu, sifongo).
I also learned about a huge conflict of interest coz Headmaster mwenyewe ndo alikua supplier wa misosi, kuni alikua anakata miti ya hapohapo shuleni na alikua akitumia lori la shule kwenye ma deal yake yote hayo. Utaona tu kwamba yeye alikua anamaximise profit bila kujali maslahi ya wanafunzi na kwa kuwa shule ilikua huko kijijini na tulikua tunamuogopa (kama sio kuogopa kufukuzwa shule!)- he simply got away with it!

Nilisoma shule za boys only lakini Im well aware of matatizo wanayoyapa dada zetu kwenye mashule ya wasichana tu au mchanganyiko, kubwa zaidi likiwa ni sexual harassment and abuse toka kwa walimu na most of the time wanakuwa hawana choice zaidi ya kukubaliana na matakwa ya walimu. Wakatae? Utapewa miadhabu kibao au kuishia kuwa suspended au kufukuzwa kabisa, na usitarajie kufaulu somo la huyo mwalimu kabisaaa!

Sijui kama waziri wa elimu anachunguliaga humu, lakini nawaombeni wana blog wenzangu muweke personal experiences zenu hapa ili tuwasaidie wadogo zetu na watoto wetu, things can be done, things can still be improved- I believe so.
Wasalaam,Kana Ka Nsungu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. ungemalizia jinalako vizuri ni kana kansungu mwelu.HII ISHU NI KWELI LASIVYO KILA SIKU WANETU WATAKUWA 'WANADEDI' TU

    ReplyDelete
  2. Kana Ka Nsungu, pokea TANO! umeandika msg ya nguvu, kweli na maana kabisa, yote uliyoyaandika ni kweli tupu na yanatakiwa kuanngaliwa kwa undani na kuchukuliwa tahadhari, kwani kwa wadau kuchangia na kutoa maoni mbali mbali itakuwa mchango mkubwa na hata msg kuweza kuwafikia walengwa,
    Sio kwamba ulichokisema hapa hakijulikanani kwa walengwa, mhh mh, kinajulikana sana ila sijui ni maswala ambayo yanafumbiwa macho au vipi hata sielewi, ila kuna madhara makubwa sana,kiafya na hata kisaikologia.

    Toka Shauritanga ipate maafa yale, kuna baadhi ya shule zilipata maafa ya moto pia, japo hayakuwa makubwa kama Shauritanga, mimi pia shule niliyosoma mungu alitunusuru kwani moto ulianzia kwenye mabanda ya nguruwe, waliwahi kuuzima na haukuleta madhara makubwa sana,

    Swala la ma shule kuungua moto kwa wakati ule liliwa affect sana kisaikolojia wanafunzi wa bodingi,and am sure ukienda Shauritanga leo hii mambo ni yale yale hakuna mabadiliko, no fire exit doors, no fire alams no nothing vya kujihadhari kwa jambo kama hilo likitokea tena, sio Shauritanga peke yake, shule nyingi tu tz mambo ya health and safety ni 'is not richabo' yani serikali yetu haina kipaumbele kabisa na mambo ya Health and Safety, sijui shule za kisasa hasa hizi international manake sijazitembelea na wala sijasoma huko,

    Kwa nchi za wenzetu health and safety ni jambo linapewa kipaumbele sana, iwe makazini mashuleni na sehemu nyingi mbali mbali, wanafanya hivi kwa sababu kama ni ofisi au kiwanda ukizembea wafanyakazi wote wakaumwa au wakapata ajali nani atakuja kazini si wote watakuwa gonjwa then kampuni au kiwanda hasara ya mabilioni,

    Kuhusu paragraph ya tatu, shule kujengwa mbali na mji, hakuna usafiri vituo vya afya mbali yani ni balaa,nina mfano halisi ambao umenitokea mimi binafsi, nilisoma huko moshi vijijini, ukitokea dar kuna basi la moja kwa moja hadi hapo kwenye ka mji/kijiji (ngoja tukaite mji A) au unaweza panda basi toka dar hadi moshi njia panda the ukapanda min bus hadi kwenye mji A, ukifika mji A unaweza kodi tax,baiskeli au pikipiki na hapo kama una hela kama huna hela ni kutembea mwendo wa saa moja au moja na nusu kukodi hivyo vitu hapo juu ni zaidi ya elfu tano, na wakati mwingine wakikuona mwanafunzi uko peke yako na unaogopa ogopa ( yani huwezi kushindana bei)wanaweza sema hata elfu 8 ambapo dar- moshi umetoka kwa elfu saba,

    Story inaanza hivi, siku hiyo nilikatiwa tiketi ya basi la moja kwa moja hadi mji A, safari ilikuwa nzuri hadi tukafika moshi, kabla yakufika mji A, basi likasimama kwenye mji mwingine na tukataarifiwa kwamba abiria wote wanaokwenda mji A wahamie kwenye min bus (min bus ilikuwa pembeni inasubiri) kwani basi lililotoka dar kuna tatizo limejitokeza na hivyo halitaendelea na safari, basi abiria tukajitoma kwenye min bus, wengine walikuwa wamefika mwisho wa safari yao, safari ikaendelea na huko njiani gari iliendelea kujaza na kushona hadi lumbesa, watu unawaona wananing'inia dirishani,

    Shule yangu ilikuwa mbali sana na njia ni mbaya kichizi, utelezi, na ni nyembembe na magari yanapishana kama kazi, kuna sehemu ni mbaya sana na inaogopeka sana kwani njia ilipasuliwa mlimani na chini kuna bonde refu, ni kwamba ajali ikitokea hapo hakuna kupona, basi sehemu hiyo tuliipita vizuri, mbele kidogo kuna min bus ilikuwa inakuja mbele yetu, hao madereva wawili hakuna anaetaka kumpisha mwenzie, kila mtu anataka kuonyesha ubabe, njia inateleza kilichofuata ni min bus iliyokuwa mbele yetu kutukwaruza ubavuni basi safari ndo ikaishia hapo,

    madereva na makonda wakaanza kubishana kosa la nani kosa lani, hapo giza lilikuwa limeanza kuingia, basi ikabidi wawasiliane na trafic waliwasiliana kwa njia gani mie sijui, baada kama ya dk 45 trafiki akaja, wakapima pika wakasema min bus yetu ndo ilikuwa inamakosa so inabidi iende kituoni, kituoni ni nyuma tunakotoka sio tunakokwenda, guess what, konda akasema abiria wote tushuke gari inarudi mjini, haya mie nikabaki nimeng'aa macho nikaona kila mtu anaanza kujikata ki slesi, kwa kweli sikuelewa, nikauliza sasa ntafikaje mji A, nkaambiwa nisubiri gari yoyote ikiwa inapita nisimamishe au kama vipi nitembeee kwani sio mbali hadi kufika mji A,

    Sikuwa na chakufanya, mie na mizigo yangu nikaanza kutembea sielewi ninakokwenda nafata watu tuliokuwa wote, mizigo kwa kweli ilikuwa ni mizito kwa mimi kuibeba, nikatembea uzalendo ulivyonishinda kuna mama mmoja alikuwa mbele yangu, nikamwita 'dada samahani naomba unisaidie kubeba mizigo mmoja'hapo sauti imebabdilika yakulia kabisa, mama yule akasimama na akanisaidia kubeba, akaniuliza nendako nikamwambia, akasema sio mbali kufika mji A, ila kwa masaa yale hana uhakika kama nitapata gari, baiskeli au hata pikipiki, basi vimilima vya moshi vile na mzigo mzito ni machozi tu ndo yalikuwa yanatiririka, tukafika mahali yule mama akasema yeye amefika aendako na anakatisha njia so 'mzigo wako binti', nikajisemea sasa nafwaa, nikamshukuru na kuaendlea na safari yangu, nitatembea weeee nikauliza watu wawili tofauti mji A uko karibu wanajibu sio mbali sana, natembea wee kufika sifiki watu wanazidi kusiha njiani giza linazidi kuwa 'tororo au totoro wadua' haya, yani migomba na miti iliyoshona basi ndo balaa, sasa nikaanza kutembea huku nalia, yani nililia siku ile, ikafika mahali nikasimama, moyo ukaanza kunienda mbio, nikawa naogopa sioni mtuu yani nikaweka mizigo yangu chini nikaanza kulia, sio kwa pole pole, kwa sauti kubwa tena, siunajua mtu ukilia sana kunakitu kinakua kama kwikwi inamaana sasa huwezi lia tena,

    Nikiwa nimesimama hapo nikasikia mtu anatembea kichakani, akatoka kaka mmoja, mie nikawa nalia tuu, akaniauliza unalilia nini?? nikawa namwangalia tu hata kusema siwezi, unatoka wapii, yani na hasira kusema siwezi, nikajitahidi nikamwambia mie ni mwanafunzi wa shule fulani, gari yamekwaruzana tukaambiwa tushuke gari inarudi mjini, sasa mie naenda mji A na hata hapa sijui niko wapi, basi yule kaka akasema mji A ni mbali kidogo na saizi ni usiku, subiri hapa nikamwite dada angu, akavuka barabara akaenda kwao, kama dk tano akarudi na mama moja na binti mmoja rika langu, basi nikamuelezea yule mama story nzima hadi hapo waliponikuta, yule mama akasema naweza lala nyumbani kwake, but is not safe incase chochote kikitokea kwani hawanijui na wala siwajui, ila kwa kuwa kuna shule hapo karibu kijana wake na binti yake watanipeleka shuleni hapo then itakuwa ni sehemu salama kwa mimi kulala,

    safari ikaanza sio kwenda mbele ni kurudi nyuma nilikotoka, 20 min walk tukafika hiyo shule, ilikuwa prepo time, basi akatafutwa mwl aliekuwa zamu, wale wasamalia wakanikabidhi, ticha akanipokea na kuniweka hapo kibarazani, akaanza kunihoji kujua kama kweli mie ni denti manake isije ikawa ni wale wale wachoma shule, nikamjibu maswali yote, na kumbe alikuwa anajua walimu wengi washuleni kwetu hivyo kila akiniuliza mwl huyu anafundisha somo gani namjibu, alivyoridhika akanipokea kwa mikono miwili,

    Tena sikulala bwenini nililala kwenye nyumba cha huyo mwl, nakumbuka nilioga maji ya moto na baridi ile ya moshi angenipa maji baridi wala nisingeoga, lol, na usiku ule nilikula chips, asubuhi alinitayarishia stafstah na akanipa wanafunzi wakunipleka barabarani hadi nipate basi, nikafika shule salama salimi na kila mtu alikuwa anashangaa nimetoka wapi sa nne asubuhi, kwani kwa wanafunzi watokao mikoani niunafika jioni, ni miaka 9 sasa but hadi leo huwa sisahau mkasa ule, all in all nawashukuru sana ile familia mama na watoto wake 2, hasa yule kaka alienikuta pale kwani angekuwa mtu mwingine labda ingekuwa story nyingine sasa, and againi namshukuru sana mwl 'Miss MGOMBA' wakati ule alikuwa anafundisha shule inaitwa Ungwasi, pale nilipolala, ulinisaidia sana, wherever u r, God Bless.

    Pole wadau nimewachosha kwa kusoma, story yangu ndo hiyo,imagine siningeweza hata kudhuriwa na wanyama wakali porini kule au hata wabakaji, ni watu kutokufikiria, yule trafic mzima na akili zake timamu hakuwa hata na busara, akaamrisha gari kuondoka wakati hajui abiria watafika vipi waendako, hakuelewa kuna wagonjwa, watoto, wazee na hata walemavu,sielewi nimwite jina gani, gari haikuwa imeumia kiasi kwamba haiwezi kutembea, anyway nisiwachoshe watu bure,

    Ukweli nikwamba huko bodingi school wanafunzi wanapata shida sana, na wazazi hata ukiwaambia hawapati picha halisi kwani hawaelewi nini kinatendeka, same apllies to serikali,

    well ninamengi tuu kuhusu boding school but Kana Ka Nsungu amezungumzia karibia kila kona muhimu,

    Nawatakia Wadau Wote Idd Njema,

    ReplyDelete
  3. Kaka ni kweli ulivyoongea na nafikiri uliipata ulivyokuwa njuka mpaka leo unakumbuka, lol hata mi nakuunga mkono au mikono. Ila nina kaswali kamoja tu, hicho kiswanglish wengine hatukijui, je umeandika kwa wanaokijua tu au kwa wote? Asante

    Ombeni

    ReplyDelete
  4. Duh! Umesahau kazi za kulima,na adhabu za kuokota kuni! Umenikumbusha enzi zangu minaki. Pale main campus hiyo mivyoo tulikutana nayo kweli ni risk sana japo tulimanage kutoka alive lakini kushuhudia mambo kama yale ilihitaji ubishi wa roho kimtindo! Mdau,from kansas

    ReplyDelete
  5. mkuu uliyosema ni kweli tupu. ila mimi nilisoma kwa koroboi bafuni usiku kwa kujificha..maana mwisho wa prepo ilikuwa saa tatu na nusu. N mind you nilisoma shule ya village kabisa mbako hata usingejua kwamba there is another life beyond five KM! Kweli Mungu ni mkubwa.

    Unayoyaongelea mi naona ungeandika waraka kwa waziri na ukatoa copy magazetini. Its horrible, but waheshimiwa wetu wanajifanya kwamba hawayajui...

    Anyway, experience yangu sidhani kama kuna mtu ataipenda humu, though at last nilifanikiwa kufika mlimani na kwingineko, ki ukweli nisingependa yeytoe aonje experience yangu!

    ReplyDelete
  6. Mbona hukuzungumzia tatizo la lesbianism and sodomy katika shule hizo? Au unajifanya hujui hilo? Au labda sio tatizo?

    ReplyDelete
  7. I will be really surprised kama kana ka nsungu hakusoma Galanos Secondary School! Probably miaka yote sita !
    Kaima

    ReplyDelete
  8. KANA NADHANI SHULE UNAZOZIONGELEA NITAKUA NIMESOMA KWENYE MOJA. NAKUMBUKA MKUU WANGU WA SHULE ALIKUA AKIPIGA BAO KICHIZI KWENYE TENDA ZA MSOSI NA KUNI.WANAFUNZI TULIKUA TUNAPEWA ADHABU YA KUKATA KUNI LAKINI NAJUA ALIKUA KWENYE VITABU ANAANDIKA KUWA AMEZINUNUA, HATA AKITUPIGA UGALI HARAGWE TERM NZIMA NAHISI KWENYE VITABU ALIKUA AKIANDIKA WALI NYAMA/SAMAKI KIBAO! NDIO BONGO HIYO, NA KUNA WATU WANALIPWA KUHAKIKISHA MAMBO YANAKWENDA VIZURI HUKO MASHULENI!

    ReplyDelete
  9. Dr. Remmy alishaimba, "niseme nini, niseme nini, niseme nini mieeee..., Sina la kusema"

    Kwa wale tuliosoma kiungani kwa dikteta Tetti (enzi zake zishapita nadhani) Tumepitia janga hilo kwa staili ya kikatili sana.
    Lile zee lilikuwa linatulisha maharage na ugali tuu, sometimes makande, mapure, huku linajenga mabaa na ma-gesti hausi. Mfano hai ni Ruwaichi ya Mikanjuni. Serikali inajua na inauchuna tuu.
    Kwenye mahafali yetu ya form four, 1994; Jakaya Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi. Wakati huo akiwa ni waziri wa maji, nishati na madini. Tulimwalika yeye kwa sababu mbili, kwanza tuliwa na matatizo sugu ya maji na umeme shuleni, na pia yeye ni mwanafunzi wa zamani wa Kiungani. Akatupa ahadi zake tamu tuu, mojawapo ni tangi kubwa la kisasa la maji. Leo hii 2007 amekuwa "Laisi" wa nchi hakuna hata ahadi moja alizozitekeleza.

    Tunahitaji mapimduzi huko nyumbani.

    ReplyDelete
  10. Ha ha ha haaa Kana ka Nsungu umenikumbusha mbaaaali 198... Wakati huo nasoma shule ya MORINGE SOKOINE MONDULI ilikuwa ina uonevu sana haswa kwa sisi njuka,wale waliotupokea walikuwa wanatuamsha kwa kutupiga Mikanda,ahsubuhi subuhi kama saa kumi za ahsubuhi wanatutuma maji ya kunywa kwa (Mustin-zinatumika sana Jeshini)umbali wa nusu kilomita basi ili kuwakomoa TULIKUWA TUNATOA DUDU zetu kisha tunayakojolea yale maji kidogo... LOL kama njia ya kujifariji.....

    ReplyDelete
  11. Naombeni nafasi ya pili hapa hap kabla hapajapoa. mi nafikiri Kana ametoa kama kauchokozi ili wengine wamalizie hivyo tusimuulize amesahau kitu fulani au amenyamaza, mi naamini kwamba hayo ndio aliyoyakumbuka yeye na hizo shule mnazozitaja ziko mjini mpaka waziri anakuja kwenye mahafali, mi nimesoma shule inaitwa balngdalalu hata mwenyekiti wa kijiji kumpata ilikuwa shidawacha hao mawaziri. Huko form one kazi anayo sio kidogo manake hana hata pa kujitetea waalimu wako wachache sana halafu wako busy na kazi zao binafsi kiasi kwamba hata darasani mwalimu atakuja kuwasalimia na kumwambia mmoja aandike notes ubaoni halafu anaondka zake.
    Shule ilikuwa na Tractor 1 lakini sisi tulijua ni la mkuu wa shule kwasababu lilikuwa likifanya shughuli zake tu, shuhuli za shule labda kama tumeshindwa kubeba magogo ya kuni na tulikuwa tunaambiwa tupasue kuni huko huko tuje na vipande kila mtu ajaze 1m2, ukweli ni kwamba tulikuwa tunasoma il muda uishe tukapambane na maisha. Division 3 ndo mtu alikuwa amefaulu kama div 1 shule zingine

    ReplyDelete
  12. mwana uliyeongelea minaki umegusa palepale kulikuwa na adhabu za kufyekea minazi acha mwanangu yaani kulikuwa na mwalim special wa hiyo minazi achana na mwlm wa zamu alafu kulikuwa na upupu wa kumwaga. sitaki hata kukumbuka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...