





Wasanii wa kikundi kinachopiga muziki wa asili ya Tanzania kwa kuchangany aala za asili na kisasa ambao wanajulikana kama Zemkala band kwa sasa wapo katika maandalizi ya albamu yao ya kwanza kabisa ambayo inarekodiwa Dar.
Albamu hiyo baadaye itapelekwa nchini Finland kwa prodyuza Miika Mwamba kwa ajili ya kumalizia maboresho (mastering) na hatimaye kuzinduliwa kati ya mwezi wa Desemba 2007 au Januari 2008.
Tayari Zemkala wanatamba na singo yao ya kwanza ijulikanayo kama Pandumula ambayo kwa kweli mirindimo yake inagusa hisia na kwa wale wanaodhani kuwa kazi bora zakiafrika ni kutoka Magharibi tu basi wakae mkao wa kula.
Hivi karibuni wadau wataanza kupata ladha adhimu zenye vionjo halisi vya matembele...Nikiripoti kutoka mitaani ni mimi Chinga muuza Sidiria wa CHUZI NEWS.
Kwanini watu wapige muziki wakiwa vifua wazi??????
ReplyDeleteVijana wa "The Mkalas" a.k.a Zemkalas wakiongozwa na msanii wazamani wa sisi tambala bw,Kasembe ni miongoni wa vijana machachari katika uboreshaji uchezaji na mfufuo wa ala za kiasili kimatumizi. kutokana nakufagilia Midi na kompyuta Vijana wenye uwezo wa kutumia mwili katika uchezaji,akili,utunzi na ubunifu pamoja utwangaji ala asili wametoweka katika anga ya sanaa Tanzania. Bendi anzilishi kwenye category hii ni Watafiti later Tatunane sisTamabala...mdau wangu pale gotenberg kule Swedeni alie tokea hapa helsinki anawezakutoa Historia kamili ya Nyanja hii..Ni mimi mdau wa Helsinki kona za Chelsea nakwa wakubwa wangu wa Zemkala natoa salamu kendekende za Iddi na tunasubiri kwa hamu kazi yenu itakapo kamilika na kuingia sokoni..ni mimi mdau wenu.
ReplyDeleteI think it would be wise if they wore their shirts.
ReplyDeleteOOOOh what a garden ,better wear t-shirt jamani vitu vingine unaweza usione aibu ila mhh hii no way sio kifua cha kuacha wazi
ReplyDeleteHahahaha...nimechekeshwa na concern ya wadau kuhusu jamaa kupiga ala za muziki wakiwa vifua wazi. Well, hiyo ndo inaitwa Dar ambapo sasa hivi joto limeanza kufukuta na kufikia mpaka 32 degrees za Celcius. Mtu inakubidi itinge kifua wazi ndani ya studio.
ReplyDeleteHalafu nina swali moja, huyu jamaa Miika Mwamba hivi huyu ni mTZ au mfini? Hili ni swali tu sasa msijeanza kuniandama.