Ndugu zangu na marafiki zangu,
Natumaini wote ni wazima na kama wapo ambao wanaugua au wanauguliwa naombaMUNGU awasaidie katika matatizo hayo. Mie ni
Ernest Mtaya (pichani) na maelezo yangu zaidi yanapatikana katika www.ernest.4mg.com

Madhumuni ya barua hii ni kuwafahamisha natarajia kuoa tarehe 17 Novemba 2007 saa 10 kamili katika kanisa linalojulikana kama st.Peter's church liliopo Oysterbay karibu na shule ya Mbuyuni hapa Dar Es Salaam. Baada ya hapo kutakuwa na msafara wa BAJAJI sita kuelekea eneo la sherehe ambalo ni kijiji cha Makumbusho tena nje chini mwembe.
Sherehe hii itakuwa na vionjo vya kitamaduni zaidi ya "uzungu" katika msafara wa Bajaji tutakapofika eneo la Victoria tutabadilisha usafiri na kupanda GUTA lililotengenezwa kiustadi kabisa na kuitambua Bajaji nitakayokuwa na mtarajiwa wangu itakuwa imepambwakwa makuti.
Sherehe itashereheshwa na msanii maarufu wa jukwqaa Mrisho Mpoto kwa wasiomfahamu ni yule muimbaji wa wimbo wa SALAMU KWA MJOMBA pia kutakuwa na msanii maalufu wa Afro Reggae Jhiko Manyika ambaye amerudi juzi tu kutoka ziara yake ya kimuziki ya Ulaya.
Mtumbuizaji mwingine ambaye atakuwa msimamizi wa mtarajiwa wangu ni muimbaji na mtunzi maarufu anayeitwa Karola Kinasha ambaye mbali na shughuli ya usimamizi kama Matron pia atatumbuiza kwa nyimbo zake tamu na sauti nzuri. keki , shampeni na jukwaa utamaduni wetu wa Afrika utapewa hadhi.

Cha muhimu ndugu na marafiki ni hii sherehe ya watoto ambayo nimefikiri niifanye ili watoto kwa mara ya kwanza washiriki katika sherehe ya Arusi la kwa nia ya kuwaaunganisha na kusaidiana na kutambua matatizo ya watoto wengine wenye shida zaidi yao.
Hivyo basi siku ya pili ya sherehe yaani 18 Novemba 2007 kwa niaba ya mchumba wangu JUDDY nimeandaa sherehe ya watoto ambapo nimeawaarika watoto wa mataifa mbalimbali nia kubwa ikiwa ni kuwaaunganisha watoto wote bila kujali misingi ya rangi, dini na utabaka waaina yoyote, pia kuwafanya watambue matatizo ya watoto wengine ili wakue wakijua kuna watoto wenzao wenye shida zaidi yao na wawe na moyo wakuwasaidia kupitia wazazi wao, pia kuwafanya wafurahi kwa kucheza ,kuimba na chochote chema ili mradi wafurahi.
Hapa tutafanya utafiti wa kugundua vipaji vya watoto na kuwasiliana na wazazi ili kuona mwelekeo wa kuweza kuwasaidiakatika siku za mbele ambapo Mungu akinijalia nategemea kuanzisha taasisi itakayohusika na shughuli za watoto.
Nimewaalika watoto yatima wa Kurasini ili waweze kufurahi na wenzao na kama kuna yoyote atayeweza kusaidia kwa chochote kile hasa kwa walengwa wakuu ambao ni hawa watoto yatima anakaribishwa kusaidia anaweza kupiga simu hii 0713-23 31 74
Michango itapokelewa hata baada ya sherehe kwani baad ya sherehe mimi na Juddytutaelekea Zanzibar kwa mapumziko ingawa tutatumia mapumziko yetu kutembeleavituo vya watoto wenye shida na nyumba za kutunzia wazee.

Tayari kwa niaba ya Juddy nawashukuru Duka la vifaa vya elimu lilopo Upanga la KALL KWIK Bookshop kwa zawadi zao ambazo zitatolewa kwa watoto wote wataohudhuria sherehe hii.
Pia wale walioahidi kusaidia nitawaandika mara nitakapopokea zawadi zao. nawashukuru pia wazazi ambao tayari wamechangia sherehe hii na napenda kuwaahidi michango yao itasaidia kuwaalika watoto yatima na itatumika kwa madhumuni yaliyotajwa kwenye kadi tu.
Nashukuru kwa kuniamini na naahidi sitawaangusha tufanye huu ni mwanzo tu. Ahsante na MUNGU awabariki wote na kuwajalia imani na huruma.

Ernest kwa niaba ya Juddy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Jirani kama tulivyoongea juzi..
    misosi iwe ya kawaida tu, sio iwe milenda, maboga,bodoz, kiembe akuu...
    Vibudu aka kuku viwepo bila kusahau chakula ya kwetu Machalari n so on...maana watu wa migomigo kwa kulaaa tumeshindikana...

    ITANOGA SANA MAANA ITAKUWA TOFAUTI

    Sis Pam

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Kaka Ernest mwenyezi mungu akujalie wewe na mkeo na karibu katika club ya wapendanao.Michu asante kwa habari hii maana huyu jamaa rafiki yangu sana na nilikuwa sina mawasiliano naye kipindi sasa kazi nzuri kaka.

    ReplyDelete
  3. oooh hongera sana Ernest! PlZ i wish ningekuwa Tanzania japo ningeiona hiyo harusi, najua itakuwa ya aina yake sana tena sana tuuu!! Plz hebu tuwekee pics za mtarajiwa wako tumwone maana umejiweka mwenyewe tu!!

    ReplyDelete
  4. Mzee hongera, ila JUDDY yupi? weka jina la pili, sababu ushatuweka roho juu wenye wachumba JUDDY. Tusilaumiane tukimgeuza mtu limau.

    ReplyDelete
  5. We ernest we mgeni kweli kwenye mambo haya ya "kiafrika" eenh!
    Ulitakiwa usiseme kwanza. Ungekaa kimya watu wastukie tu baada ya shughuli.
    Sasa we umeanika kila kitu juani, UTALOGWA wewe uugue hata kabla ya siku yenewe, au hivyo vibajaj vyako itakuwa kila unachopanda kinapata pancha.
    We vipi wewe? Uliza kwanza!
    Ohoo! Shauri lako.

    ReplyDelete
  6. Ernest & Juddy, nawatakia kila la kheri jamani.....Huo ni moyo wa upendo wa hali ya juu kushirikiana na watu/watoto ambao hawapo "as lucky as many" kushehereka katika siku yenu kubwa.....Manani awaongezee na kuwabarikia...

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Ernest najua huwezi kunikumbuka ila mimi nakumbuka vibaya sana. "Jennifer" Kama utakumbuka ITV ikiwafundisha watoto kuchora, tulikuwa pamoja

    ReplyDelete
  8. Ernest na Judy hongera sana kwa kuamua kufunga ndoa na kutotaka makuu, hasa mambo ya kuiga ya kigeni, na kutunza mazingira pia maana msafara wako hautachafua mazingira.
    Pili nawapongeza kwa moyo wa upendo mlionao kwa watoto, zamani harusi zetu za kiafrika, watoto walikuwa wanahudhuria lakini siku hizi kila mwaliko wa harusi ukipata umeandikwa watoto hawatakiwi, sasa uamuzi wako wa kuwaaalika watoto kusheherekea harusi yako, ingawa itakuwa siku ya pili ni wa kuigwa.

    Mtoto wangu siku moja alitaka kwenda harusini na mimi nikamwambia soma kadi imeandikwa watoto hawaruhisiwi wakati huo alikuwa binti wa darasa la kwanza, anajua kusoma angalau hivyo hivyo ngumbaru, akasoma kadi hatimaye akanijibu, "basi mama na mimi siku nikiolewa ntaandika kwenye kadi wakubwa hawaruhusiwi" Alionyesha hisia zake, iliniuma lakini ilinibidi niende harusini ndio majukumu yenyewe ya kijamii, usipoonekana utaonekana hutaki kushiriki na wenzio, lakini wakati mwingine tunakwazwa.

    Nakumbuka harusi zetu zamani ziwe za kikristo au kiislamu sherehe inafanywa nje kwenye uwanja, ngoma inapigwa watu wanacheza kwa furaha, hakuna cha mwaliko wala nini, wala kwenye familia husikii manung'uniko mwanafamilia au jirani kanyimwa kadi eti hakuchanga aumchango wake mdogo. Maendeleo haya yana Mambo!

    Nawatakia kila la heri katika maisha yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...