wadau kunradhi, kuuliza si ujinga. haya magwanda niliyakuta sehemu sehemu...nikajiuliza na hadi leo sijapata jibu. kazi yake ni nini yanavaliwa wakati gani ukiziangatia yako kama taulo lililoshonwa kikotikoti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. ya kulalia hayo babake..

    ReplyDelete
  2. Brother Michuzi hayo ni makoti ya kuvaa ukitoka kuamka tu unapojiandaa kwenda kuoga na baada ya kuoga hasa kwa wale tusio na master bedrum yenye kijibafu ndani kwa ndani!Na ndo yanafaa kwa zile nyumba zetu za uswahilini ambako watu hupenda kujifunga taulo au khanga wakati wakijiandaa kwenda kuoga kwa lugha ya wenzetu yanaitwa bath robe!

    ReplyDelete
  3. anko hayo ni mavvazi ya kubandulia wake za watu hasa kwa wale mnaoishi mabanda ya uwani.Ukimtokea mke wa mtu umevaa hilo gauni hata mke wa mwenye nyumba yako lazima atajilaza kichalichali bila ya nongwa

    ReplyDelete
  4. Michuzi amezoea ile taulo ya kusokotea kiunoni kwa sana hadi inakuwa kama miniskirt, halafu ndo anatoka nayo asubuhi na kopo la maji na mswaki mkononi kuwahi foleni ya bafu la uswazi. teh teh teh

    ReplyDelete
  5. Weweeee uvae uswazi hiyo unajipenda au haujipendi unaweza ukarogwa,
    hapo waachieni wabeba mabox basi watajifanya wanayajua balaa,we michuzi mchokozi kweli,
    na hilo mi naona akivaa sheria na mavazi atapendeza tena wakati anataka kwenda kuoga pale,na ile rangi yake,yarabi toba mie hoi,

    halafu inatakiwa uwe UNAOGA,sio unajimwagia dude lenyewe jeupe,yaani unaooooga kuladadeki
    sio na kikopo(ah ah)yaani kwenye bafu bafu sio bafu jina
    sasa chongeni sasa hayoooooooo

    ReplyDelete
  6. hayo ninayo kama matano na mengine niliwanunulia wajomba bongo kule,hayo unavaa ukitoka kupiga bublebath ..hapo najua wengi hamuelewi nina maana gani,hakuna kujifuta na taulo hapo unatoka kwenye jaccuzi unalivaa hapo hapo huku unapigwa na upepo ukauke lakini upepo mliozoea huko ni ule unaotoka kwenye machine bafuni,najua na hapo mtajiuliza upepo gani huo,haya sasa mjue huku mabafu yetu yana upepo wa kukaushia nywele nywele na ngozi mataulo tuliacha siku nyingi,kama mna swali mwambieni michuzi awasiliane na mimi nitawajibu sasa sina muda wa kuwajibu wote nyie najua mpo wengi

    ReplyDelete
  7. MMICHUZI hao box boyz wasikuzingue. Hizo ni sale sa Kung-fu huwa tunavaa Masensei kabla na baada ya pambano na wakati wa mapumziko

    ReplyDelete
  8. Michuzi una ugomvi na wabeba mabox?, najua unawachokoza ili wajifanye wao WANAJUA SAANA. Jamani hii hata huku bongo tunajua, badala ya kufunga taulo, mkono wa kushoto umeshika kikopo, kulia una mswaki uko kwenye foleni ya kuingia chooni asubuhi, unavaa hii kitu kuogopa taulo kuanguka.

    ReplyDelete
  9. Tehe Tehe 3.52.00 mkorofi, yaani hata mke wa baba nyumba! Na mimi nitalinunua moja nimkazanie mama mwenye nyumba, bomba huyo!

    ReplyDelete
  10. Mimi kwa kweli ni mtu wa box lakini huwa naziona tu,na ninafahamu mtu huzivaa akitoka kuamka na kabla hajapata kitafunwa na anaweza kushinda nalo kama hatatoka kabisa kwenye winter hii mbaya.Jamani karibuni tupige box,lakani nikinyakuwa degree kwa Brown hawanioni kabisa,afadhali nikafie nyumbani naona wakina wazalendo wameamua kufanya mambo yao barabarabara kabisa ila wanhitaji support.Ingaw naona Mafisadio wananyemelea yakafisadi mtandao wa watu.Tafadhalini Nyerere alisema Tanzania itajengwa na wenye moyo safi.Waacheni vijana waijenge Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Hilo vazi katika lugha ya kiingereza linaitwa bath robe; hutumika haswa ukiwa umebadili uende kuoga au kama umetoka kuoga ili kujisitiri.

    ReplyDelete
  12. Hizo ni Joho za Majaji.Acha uchokozi

    ReplyDelete
  13. Hapo km vile kuna utata, yes inaweza kuwa bath robe au nguo za masensei...ila mi nafikiri ni yale mavazi wanayovaa kwenye saloon za wanawake wanapokuwa wanatengenezwa nywele zao!!!! A,B na C yote sawa...

    ReplyDelete
  14. Semina endelezi a.k.a Ngurdoto mountain lodge imekufungua macho sana babu yangu.Huko kisii hizo tunatumia msibani.

    ReplyDelete
  15. Michuzi, aina ya mavazi hayo yanaitwa SKIPITUNTA, yalivumbuliwa sayari ya STRUPITA. Mnamo miaka ya 1480, aliens wawili waliyadondosha kwenye mkutano mkuu wa jimbo la WARUMI wakati PILATO akiwa anahutubia.

    Serikali yake iliamua kuyahifadhi mpaka pale Emperor KAKUNDI WA MALI alipo tawazwa kushika enzi ya himaya ya WAMISRI. Wamisri walichukua ufalme wa Pilato baada ya kushinda katika vita vinne mfululizo.

    Vizazi kama sita vilipita, na katikati ya mwaka 1590 palitokea njaa kwenye himaya ya Mali. Kimondo kilidondoka katikati ya mji wao na kuharibu mazao yote. Mrithi wa mfalme, KIPINDUNONDO, akijulikana kama mwanamme wa shoka wakati huo na wakati huo akiwa na miaka 84, alimua kuendeleza ufugaji wa ng'ombe walio kuwa wamesalia baada ya kimondo kudondoka.

    Ili kuendeleza kizaz cha ng'ombe hao, ambao ndio walikuwa chakula pekee katika mji NDUNDUMO, mfalme KIPINDUNONDO alibariki mavazi hayo mawili na kuwatuma washenga wanne kuyapeleka kwenye zizi walilokuwemo ng'ombe hao. Washenga walitakiwa kuwavika ng'ombe wawili SKIPITUNTA hizo. Kwa kuwa ng'ombe hao walikuwa na njaa ya kupindukia, walianza kuyatafuna mavazi hayo.

    Ng'ombe waliyala mavazi yote mawili. Bahati mbaya hiyo ndiyo ilikuwa mauti yao. Ng'ombe wote wawili walikufa papo hapo. Mfalme kutumiwa habari alisikitika sana. Ili kuwa enzi ng'ombe hao, aliagiza wananchi wa himaya yake, kila kaya kutengeneza SKIPITUNTA mbili.

    Basi ndiyo maana leo hii ukiona SKIPITUNTA hizo zina kamba katikati kama ishara ya kifungo cha kuenzi ng'ombe hao daima. Na mara nyingi popote utakapokuta mavazi hayo, yanakuwa yamewekwa mawili mawili kama ishara ya ng'ombe wawili. Na kikubwa ni kuwa, kule MALI NA kwa WATESARONIKE ng'ombe akifa huzikwa kwenye SKIPITUNTA.

    Michuzi, baadae ndugu, nami nimeamua kujiandikia yangu kuhusu bathrobes... ha ha ha!!

    SteveD.

    ReplyDelete
  16. Haha haaaa! SteveD ndugu yangu umedata. Nice story - OC'-Sinza.

    ReplyDelete
  17. tehe tehe jamani yani wabeba mabox wanajifanya kila kitu wanajua,jamani hayo marobe hata huku bongo yako kibao na tunayatumia michuzi anataka kuwchosha tu wabeba mabox,yani huku bongo kila kitu kipo ni wewe mwenyewe tu unavyojiweka maisha yako msifikiri bongo ni ile ya zamani hata colgate hatupati.bongo kama newyork ndogo.rudini muone lkn muhakikishe mmesave hizo hela zenu za mabox mana huku watu wana pesa si mchezo.GOODLUCK WABEBA MABOX.

    MASHLY

    ReplyDelete
  18. MHESHIMIWA ISSA..ASLAM ALEYKUM MAALIM..NAONA UNATUONYESHA "..JEZI.." MECHI ILIKUWAJE KAKA "..MTU KAPIGWA BAO NGAPI.." LUGHA YA PICHA...

    ReplyDelete
  19. ...NYIE VIPI HAMUONI HIZO JEZI ZIKO MBILI HAPO..?

    ReplyDelete
  20. Inferiority complex kibao.Ohh Bongo kama New York kama London kwanini Bongo isiwe Bongo kwetu sisi tuliopo nyumbani na mlenda wetu na kipindupindu chetu.

    ReplyDelete
  21. watu bwana !!! wabeba mabox wabeba mabox !!!
    mbona mnachuki na wivu hivyo ?
    hasa huyo anon nov 21 at 10:59 am
    wewe unajitia watu wanahela bongo ooh sijui nini
    wewe unayo hayo nyumbani au ndiyo sizitaki mbichi hizi
    jamani acheni dharau wakati kutwa hamuishi kwenda kuunda mistari kwenye mabalozi ya watu kisa mnatafuta visa.
    huna lolote mshamba mkubwa wewe
    nenda zako kavae msuli uko ukitoka bafuni
    mfyooooo ( yes nakufyonza )

    ReplyDelete
  22. Achane utani, mtu kauliza swali zuri, muelezee hayo ni yanini, hata mie yalitoa ushamba hotelini...There is no stupid questions but answers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...