Sullivan Yawaalika Watanzania Kwenye Sherehe Mjini Washington DC
Rais Kikwete kuhutubia, Dkt. Migiro aalikwa, Boyz II Men kutumbuiza
Washington, D.C. USA, Nov. 23, 2007
Taasisi ya Leon H. Sullivan imewaalika Watanzania wote waishio nchini Marekani kwenye sherehe ya chakula cha jioni ya tuzo maalum itakayofanyika Desemba 13 kwenye Hoteli ya Marriot Wardman Park, jijini Washington DC.
Kwa mujibu wa Rais wa chombo kilichoundwa Marekani hivi karibuni na Watanzania waishio nje ya nchi (TADI), Yassin Njayagha, mwaliko huo umefuatia mazungumo kati ya Taasisi hiyo na TADI mjini Washington wiki chache zilizopita.
Akinukuu maofisa wa Taasisi hiyo, Yassin ambaye pia ni kiongozi wa Watanzania waishio mjini Washington DC, alisema sherehe hiyo ya tuzo ambayo ni ya tano kufanyika, itawatambua na kuwatunukia viongozi waliojitolea kutetea wanyonge duniani.
Yassin aliongeza kuwa Sullivan imemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, kutoa hotuba ambapo atazungumzia kuhusu Mkutano wa Nane wa Sullivan uliopangwa kufanyika mjini Arusha, Tanzania kati ya Juni 2 hadi 8, 2008. Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa aina hii kufanyika Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa waandaaji, Watanzania ambao wamepewa hadhi ya wageni maalum, wanatakiwa kujiandikisha Sullivan kupitia kwa Ann Graham anayepatikana kwenye simu nambari 202-736-2239.

Aidha Watanzania wameshauriwa pia kuwasiliana na viongozi wa TADI kupitia simu 301-379-0693, 240-601-8094 na 240-338-4917 iwapo watahitaji maelezo zaidi kabla ya siku ya mwisho ya kujiandikisha, Novemba 30.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro, naye anatazamiwa kuhudhuria sherehe hizo zitakazopambwa na wasanii waliowahi kushinda Tuzo ya Grammy wa kikundi cha Boyz II Men, ambao wataimba wimbo wa kumpongeza Marehemu Leon H. Sullivan.
Taasisi ya Sullivan ilipewa jina hili kwa heshima ya kiongozi maarufu mpigania haki za wanyonge wa jijini Philadelphia, Marekani, Marehemu Mchungaji Leon H. Sullivan. Taasisi hii ilisajiliwa mwaka 2001 mahsusi kwa kuhamasisha kujitegemea, kutetea wanyonge na kuunga mkono uongozi wenye uwajibikaji kwenye jamii.
Mwisho.
Imeandikwa na Mobhare Matinyi,
Mkurugenzi wa Muda wa Mawasiliano wa TADI,
matinyi@hotmail.com.
Simu Selula 1-240-277-5527.

Tembelea: www.thesullivanfoundation.org na www.thesullivansummit.go.tz

Kikundi cha kutumbuiza wamepatia kabisa BOYZ II Men......
ReplyDeleteTHIS IS COOL . VIJANA WAMEJITAHIDI WAMEANDAA MKUTANO NA KUNIPA MWARIKO. SASA NIMEPATA SABABU YA KWENDA KUMUONA MKE WANGU. MAMBO SI HAYO....
ReplyDeleteI agree anonymous this is cool ni wakati kumuona mke wako si basi unajuwa mambo chapu chapu tu.
ReplyDeleteThis is for the President, his family and friends, friend and friends. Some Tanzanians living in USA have learnt their lessons. They know the game nothing suprises us. Kama hu belong kwenye group basi subiri mpaka EL's turn. Aint nothing happening.
are boyz 2 men still hot?are we still in 90's or something?
ReplyDeleteHehe na Edo naye angekuja ili wanonane na Boyz 2 men wenzao wapate kudesa mavazi
ReplyDeleteThe Late Sullivan was from Philadelphia, so is are the artists Boyz II Men. I guess that is the reason why they decided to invite them. And who said that to be invited somewhere you need to be on the chart? Use brain, do be too Mswahili!
ReplyDeleteKwa nijuavyo mimi ni kwamba hawa Leon Sulvan wamefanya mengi kwa nchi mbali mbali za Africa kama Nigeria,Zimbabwe,Gabon,Ghana na sasa ni Tanzania.Hawa wtu wako kwa ajiri ya kusaidia wanyonge ki afya,elimu na umaskini .Kwa hiyo jamani tujitokeze kwa wingi ili tuone wenzetu wanavyo tujali.
ReplyDeleteTaratibu Waungwana hiyo kitu sio Bure!Kama wengi wanavyofikiri,Wasilianeni na Nyaghawa ili mjue Entrance yake.Lakini ni vyema wengi mjitokeze na isiwe kama ile ya kumpongeza Mama Migiro.Hawa jamaa wa Sulivan Foundation wanajali sana maswala ya Africa!!.Dignitaries watakuwa wengi hapo kwa maana hiyo utanashati na ustaarabu ni kitu cha kuzingatiwa..
ReplyDeletetujitokeze kwa wingi hehehehe umealikwa????...ndugu yangu usije ukajitokeza tu bila micard ..mara mashavu yakakushuka na baridi ilivyokali sijui utashangaa wapi DC
ReplyDeleteHii sherehe ni bure, hakuna kadi, unatakiwa kupiga simu kwa Sullivan na kujiandikisha - BASI. mmeshaambiwa Watanzania wamepewa hadhi ya ugeni maalum, mnataka nini tena? Wabongo bwana siye kwa kuwa negative hatuna mfano, sasa nini hakieleweki hapo?
ReplyDeletewew unayesema watanzania kwa negarives nini maana ya hii sentensi Watanzania ambao wamepewa hadhi ya wageni maalum, wanatakiwa kujiandikisha Sullivan kupitia kwa Ann Graham anayepatikana kwenye simu nambari 202-736-2239.
ReplyDeleteina maana watanzania wote au watanzania "ambao" means baadhi??
Labda kiswahili kigumu tumeshindwa kuelewa....