Gadi Promotions inafuraha kuwaletea kwa mara ya kwanza wakazi wote wa Holland, Germany na Belgium mwanamuziki anayetamba sana sasa hivi ndani ya Bongo na East Africa kwa ujumla DULLY SYKES, akishirikiana na ma DJ maarufu sana wa Holland - DJ's Erick Barack(East African Sound-Kenya) na Zouk (West Africa-Guinee)

Show hii Itafanyika Party Centrum Wesseling, Houttuinenstraat 26, Delft 2611 AJ.Tarehe 30 November 2007.
Show itaanza saa nne usiku (22:00hrs)mpaka liamba (04:00hrs) mnaombwa mfike bila kuchelewa.

Kiingilio Euros 20 kwa Booking(presale),

Euros 25 (Gate).
Booking
Tel:+31614811298
au +31634236408.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michizzzzzzziiiiiiiii umebania maoni yangu ya NSSF kisa nimembonda BMW na kurushia mawe utumbo alioongea Tabasamu Ngongoseke a.k.a Lucy Khhwele poa tu

    ReplyDelete
  2. Hiyo show ilishapita au bado? Maana advet.inaonyesha Fri.2 Nov na leo ni Fri.16-Au Michuzi umeamua kumfagilia Misifa tujue kuwa nae ameshatoka

    ReplyDelete
  3. karibu sana, lakini tumekuwa tukiona wanamziki wanaokuja huku wanasahau suala la muda. nakumbuka ray c na tid kule amstadam na ray c kule delft hawakutufurahisha sisi wapenzi. kama ni saa nne iwe nne sio saba. kama mnaona hamna vitu vya kutosha muda mrefu njoo na wengine.

    kwa waandaji tunaomba ukumbi wa kutosha. kaukumbi kale ka delft ni kadogo sana. bwana Chale nadhani hapo utarekebisha

    ReplyDelete
  4. Nimefurahi sana kuona kijana anatinga unyamwezini tena na vilevile nawaomba waandaji mjaribu kumpeleka katika radio station,TV, magazetini kukuza jina lake au watu wa huko wapate kumjua zaidi. Sio mnambwaga kwenye club za kibongo tuu, atajulikana vipi kimataifa.

    Na hii kwa mapromota wote wa kibongo nje ya nchi, ndio mnafaidika katika mauzo ya ticket lakini jaribuni pia kukuza vipaji vya wasanii hawa huko mamtoni kwa kuwapeleka katika vyombo vya habari wajitangaze, cultural festivals wa-perform live na kadhalika.

    Na kingine kinachosikitisha ni hiyo flyer yaani imechoka namna hiyo, kweli hii promotion. Hata bongo wanawashinda kwa kutengeneza flyer, hebu tengenezeni flyer za uhakika au mtafute mtu awafanyie design wala sio hela nyingi.

    ReplyDelete
  5. Michu asante sana kwa taarifa hii nzuri.

    1. Inaonekana ama mleta tangazo ndiye alikuwa amekosea na kuandika NOV 2 au mtoa hoja juu ndiye alikuwa anajitahidi kusahihisha kitu kisichokuwepo.
    USHAURI: Michu uungwana ni kuwa endapo unafanya kurekebisha chapuchapu yaliyokuwa yamesha andikwa na kupostiwa basi andika katangazo kengine kadogo tu kama angalizo ka kuomba radhi na kusema kuwa sasa tangazo lieleweke kama linavyosomeka sasa! Vinginevyo inakuwa kama mtoa hoja ama haoni au ni mzushi vile!

    2. Mambo ya kuzingatia kama walivyoeleza wengine hapo juu yazingatiwe. Mfano muda wa kuanza shoo na msije mkayeyusha shoo hii kama ile ya Twanga Pepeta kwa uongo wa Msiilwa (unaoikosti bendi mpaka sasa) wa eti walikosa viza wakati wengi wetu tulikuwa tukimsubiri sana Bigwa Mcheza Bokilo kijana anayeteleza kwa tumbo utafikiri KLM imeona Schiphol!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...