
mkurugenzi wa makumbusho ya taifa na jumba la utamaduni dk. paul msemwa akionesha sehemu ambayo ujenzi wa studio ya muziki ya kisasa na mgahawa vitapokuwa. mradi huu unaogharamiwa na serikali ya uswidi kupitia shirika lake la maendeleo la sida pamoja na serikali ya bongo ni mojawapo ya juhudi za kuwa na sehemu za kisasa kwa ajili ya maonesho ya jukwaani, sanaa za mikono na muziki kwa vijana pamoja na shughuli zingine za kijamii. jina la makumbusho ya taifa limeongezewa na 'jumba la utamaduni' kuua dhana ya kwamba makumbusho ni sehemu ya kuhifadhia na kuonesha mambo ya kale, bali ni sehemu ya jamii kuvinjari kwa shughuli za sanaa na utamaduni


kweli proffesional nyingine cjui vp!!!! sa mbn huyo jamaa km co dr. vile...au ndo sanaa zenyewe hizo!!!
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteMi mdau wa sanaa tena za maoyesho. Angalao kilio kimesikika cha kuwa na jukwaa la kisasa. Lakini hebu tujiulize jamani, suala la kuwa na jukwaa lilizungumzwa kwa miaka takribani 20 iliyopita, serikali ikakaa kimya kama vile haisikii.
Sasa hivi jukwaa linajengwa (baada ya wadau kujifunga kibwebwe na kuwaangukia waswidi chonde chonde tutoleeni karaha hii), na kila kitu kinachoitwa Jumba la Utamaduni kinagharamiwa na waswidi kwa asilimia kubwa mno (zaidi ya90%). Wakati wa mapambano serikali haikuwahi hata kutuma mjumbe.Kilichofanya lijengwe hapo ni baada ya kutafuta eneo na likakosekana.
Waserikali sasa wanajidai ndo wamefanikisha. Utasikia na kwenye ilani ya Chama cha Mabepari chini ya abunuwasi JK ...wasanii kilio chenu nimekisikia na serikali yangu imewajengea mahali muruwa kabisa mjimwage...
Swali langu ni; hivi hilo litakuwa Jumba la Utamaduni wa Tanzania au uswidi? Kule Bagamoyo baada ya kuchoma lile jukwaa la waswidi, wamejitolea kujenga tena. Tunashukuru tena sana
Lakini kiasi cha ufadhili ni kikubwa kiasi kwamba waswidi wanatoa maneno tena kwa maandishi na machapisho yanasambazwa kuwa kama si wao utamaduni Tanzania ungeshakufa kama Azimio la Arusha na Ujamaa. Nakiri wamemwaka pesa kwenye utamaduni kuanzia Chuo cha Sanaa Bagamoyo mpaka Mfuko wa Utamaduni
Hivi hii serikali pesa za walipa kodi zinakwenda wapi? Hospitalini hazipo, barabarani hazipo. Mifukoni mwa watanzania hazipo
Naomba Michuzi usiibanie hii kaka
Twende mbele turudi nyuma hawa wascandinavia wanaifaidi bongo kichizi,hii so called misaada inawwafaidisha kishenzi.Hawa watu wameshikilia rasilimali za bongo kama vile ni zao.Nyie mnakalia kubishana ooh eti bongo tambarare,ooh majuu mwake wakati nchi yetu inadidimizwa na wajanja wakishirikiana na hawa mazeruzeru.Haya kazi kwenu
ReplyDeleteFOR HEALTH AND SAFETY REASON HE SHOULD NOT BE THERE WITH THAT CLOTHES....HE SHOULD WEAR PROPER CLOTHES TO BE ON THAT SITE....
ReplyDeleteTUMESHAZOEA WATANZANIA, KILA KITU KIZURI CHA MAENDELEO LAZIMA MZUNGU AGHARAMIE KWA AJILI YETU. NAMNA HII HATUTAENDELEA KABISAA..HTAUJENGI BARABARA MPAKA UMOJA WA ULAYA UGHARAMIE, HATUTIBU WAGONJWA WA UKIMWI MPAKA MAREKANI WAGHARAMIE, HATUJENGI MASHULE MPAKA WAJAPANI WAGHARAMIE, VITABU VYUONI MPAKA WAJERUMANI WATOE MSAADA.. SISI KAZI YETU KUNUNUA LAND-CRUISERS TUU ..AAH TENA HARAKA SANA.
ReplyDelete