
Jana jioni, mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 18 (pichani) aliua kwa kuwapiga risasi wanafunzi saba na mwalimu mkuu wa shule katika kitongoji cha Tuusula, kaskazini mwa Helsinki, Finland. Baada ya kuwapiga risasi wanafunzi wenzakw, kijana huyo alijipiga risasi iliyomjeruhi vibaya sana, na baadae alifia hospitali. Kabla ya kijana huyo kufanya maafa hayo alipost video yake kuelezea malengo yake kwenye You Tube. Video hiyo aliita Jokela School Massacre.
Mdau Kilimanjaro, Finland


Binafsi na habari ya kusikitisha kuona damu za hao wasio na hatia wakitolewa kafara na huyo bw Pekka-Eric.
ReplyDeleteNaomuomba mwenyezi mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi.Amaina
Na awape moyo wa subra wale wate walioguswa na maafa haya wawe na ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
Pumziko la milele uwape eeeh bwana..na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani.amina.
KIITOSI
Wanakijiji wenzangu,
ReplyDeletehebu tembeleeni kwa kaka Majid Mjengwa siku ya jumatano november 7 kuna post ya mtu kabeba ndizi ya kupikwa.Someni hapo muelewe tunakoelekea na ajenda za siri za watu na wana si "HASA"
Kama mwalimu kakufelisha ,kuna demu kakutolea nje na wale wote manaojidai much know darasani unawatia risasi ili kuleta adabu
ReplyDeleteHahahaha wewe rhxoqsa umenifurahisha sana. Joker
ReplyDeleteHaya ndo matokeo ya amani inapozidi,watu hawajui tena madhara ya silaha za moto,maana inafika wakati hadi serikali inawamilikisha silaha watoto.Takwimu zinaonyesha karibu watu 6 kati ya 10 wa Finland wanamiliki bunduki,sijui za nini,ujambazi hakuna,wanyama hakuna ..kumbe? yatatokea mengi baada ya hili.
ReplyDeleteHaya ni mambo ambayo yanaigwa na wanafunzi/watu mbalimbali duniani. Chanzo cha mambo haya, na kwa staili ya kuacha vielelezo ni kutoka kwa taifa kuu Marekani. Dunia sasa inafikia mwisho wake. Yaani kijana wa miaka 18 anaona ameshaishi vya kutosha??? Nafikiri dunia inazalisha vichaa wengi!!!!!
ReplyDeleteLabda kuna amani kwa sababu kil amtu ana silaha kwa hiyo hakuna wa kwenda kumuonea onea mwenzie.
ReplyDeleteLabda hakkuna ujambazi kwa sabu majambazi wanajua kila raia sita kati ya kumi ana Binduki na kwaivo jambawazi akienda kichwa kichwa hajui nani ana silaha na nani hana kwa hio basi biashara ya ujambaza jamaa anaamua kuacha na kuenda kutengeneza Nokia simu badala yake.
Kichefuchefu!!! hawa vijana balaa kabisa.. sijui ni hizo dawa za kulevya ama ndo KIAMA.... hatuna mahala pa kuweka roho zetu kwa amani sasa na imekuwa kama desturi ulaya kwamba sasa mashuleni ndo kuna akina "RAMBO".. .. .. (dRU)
ReplyDeleteHAKUNA JEMA DUNIANI,NCHI HII KILA KITU KIPO, HAKUNA NJAA, HAKUNA UJAMBZI, HAKUNA SHIDA YA UMEME WALA MAJI WALA MIUNDOMBINU, HAKUNA SCHOOL FEES YAKO, MJOMBA, SHANGAZI,YAANI MAISHA NI TAMBARARE MPAKA WENGINE WANAKOSA PURPOSE IN LIFE, UISHI U-ACHIEVE NINI? HAKUNA CHALLENGE, KWA HIYO WANAISHIA KUCHEZA MA-VIDEO GAMES, KUANGALI PICHA ZA MAUAJI ZA KINA TARANTINO, NA KUISHIA KUFANYIZIA KWA VITENDO....THE ONLY WAY TO SATISFY THEIR CURIOSITY!
ReplyDelete