Familia ya Bwana Chiume inasikitika kuwatangazia msiba wa mpendwa baba yao Marehemu Mzee Kanyama CHIUME (78) uliotokea juzi tarehe 21 Novemba 2007 hapa NewYork. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es Salaam, Tanzania na Lilongwe, Malawi inaendelea. Heshima za mwisho hapa NYC zitakuwa kesho siku ya Jumamosi Novemba 24, 2007 na zitafanyika kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 11 jioni, ikifuatiwa na misa saa 11 mpaka 12 jioni.
Anuani ni: Flynn Memorial Home,
1652 Central Park Avenue,
Yonkers,
NY 10710.
Kama ilivyo kawaida yetu, kwa watakaoweza kutoa mchango kusaidia kufanikisha mazishi ya baba yetu mpendwa, familia imefungua akaunti maalum ambapo mnaweza kutanguliza rambi rambi zenu:
Bank of America
Accounts #: 483-011-631-205
Routing #: 021-000-322
Kwa watakaoweza kwenda kuhani kilio na kutoa rambirambi, msiba upo kwa Mama mdogo wa familia, Bi Leah Semguruka,
anuani ni:
33 Tennyson St, Hartsdale,
NY 10530 (go to Yahoo! Maps for driving directions).
Tafadhali tembelea www.kanyamachiume.com kwa historia ya maisha ya marehemu na kutoa rambi rambi katika guestbook.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
1. New York, USA:
Nathan Chiume (son), Tel. 1-646-552-6347,
2.Lilongwe, Malawi:
Ephraim Kadokera Chiume (cousin),
Tel 011-265-8824-797,
3. Dar es Salaam, Tanzania:
Tasokwa Chiume (son)
Tel. 011-255-784-156730,
email planckscale@hotmail.com
William Mpambika Chiume (son),
Tel. 011-255-787-118815,
email mpambika@gmail.com
Eunice Mongi-Chiume (daughter-in-law)
Tel. 011-255-756-140153,
email echiume@gmail.com
Tafadhali saidia kufikisha ujumbe kwa ndugu na jamaa wengine. Ahsanteni sana kwa mshikamano na upendo wenu katika wakati huu wa huzuni. Familia ya Chiume.
------------------------------------------------------------------------------------------------
It is with deep regret and sorrow that we have to inform friends and the wider Pan-African community that our father M.W. Kanyama Chiume passed away peacefully last Wednesday, November 21, 2007, in New York City.
A service to celebrate Kanyama Chiume's life will be held this Saturday November 24th, 2007 at:
Flynn Memorial Home,
1652 Central Park Avenue,
Yonkers,
NY 10710.
Funeral arrangements to Lilongwe, Malawi and Dar es Salaam, Tanzania are still being finalized. As part of our African tradition, and for those who are able to send their kind contributions to the grieving family, a special account has been created for this purpose:
Bank of America
Accounts #: 483-011-631-205
Routing #: 021-000-322
If you would like to visit the family during the mourning period, the gathering is at the residence of their aunt, Leah Semguruka, at:
33 Tennyson St, Hartsdale,
NY 10530 (go to Yahoo! Maps for driving directions).
An online memorial has been created by the family in loving memory of Kanyama Chiume, whose life story is told throughout at www.kanyamachiume.com
Please sign Kanyama's guestbook and let us know you came to visit. For further information, please contact:
New York, USA: Michael (Kwacha) Chiume (son),
Tel. 1-646-662-6999, email kwachac@aol.com
Nathan Chiume (son),
Tel. 1-646-552-6347,
Lilongwe, Malawi:Ephraim Kadokera Chiume (cousin),
Tel 011-265-8824-797,
Dar es Salaam, Tanzania:Tasokwa Chiume (son)
Tel. 011-255-784-156730,
email planckscale@hotmail.com
William Mpambika Chiume (son),
Tel. 011-255-787-118815,
Eunice Mongi-Chiume (daughter-in-law)
Tel. 011-255-756-140153,
We thank you for your kind messages of comfort and support during this difficult time for us.
The Chiume family.
KWA NIABA YA WADAU WOTE KILA PEMBE YA DUNIA NATOA POLE KWA WAFIWA NA KUWAOMBEA MUNGU AWAAFU WAKATI HUU MGUMU WA MSIMBA. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA. E MOLA TUNAKUOMBA MLAZE MAHALA PEMA PEPONI MPENDWA BABA YETU MZEE KANYAMA CHIUME - AMINA
- MICHUZI


Poleni sana
ReplyDeletePoleni sana,Pole sana nathan tupo pamoja nanyi ktk sala
ReplyDeleteTasi na nduguzo, poleni kwa msiba wa baba.... Mungu awaongoze na kuwapa ujasiri kipindi hiki kigumu cha maombolezo...
ReplyDeleteTUTAMKUMBUKA MAREHEMU KANYAMA CHIUME!
ReplyDeleteKanyama Chiume,
Mahali pema peponi
Muumba aiweke roho yako;
Ewe mtoto mpendwa wa Afrika,
Ewe mtoto mpendwa wa Malawi,
Ewe mtoto mpendwa wa Tanzania,
Kwa yale uliyokipigania
Hadithi (legacy) yako
Itabaki siku zote!
Kifo cha Mzee Kanyama Chiume, mmojawapo wa “ngwazi” hasa wa “Nyasaland” - baadaye Malawi - ni pigo kubwa kwa Afrika nzima (kutokana na darubini ya Pan-Africanism), Malawi na Tanzania.
Wengine watajiuliza kwa nini namhusisha marehemu Kanyama Chiume na Tanzania?
Maisha ya Kanyama Chiume yalijikita sana Tanzania:
Miaka ya ujana wake alikuwa Tanzania:
Kasoma Tanzania.
Kampata mpenzi/mke wa Kitanzania na kuzaa naye watoto.
Kafundisha Tanzania.
Kakimbilia ukimbizini Tanzania. Kawa mwandishi wa makala maalumu ya magazeti ya The Nationalist, Daily News na Uhuru/Mzalendo (wakati wa harakati za ukombozi dhidi ya tawala za wazungu wachache huko kusini mwa Afrika) akiwa Tanzania.
Kawa mpigania uhuru wa Malawi
(awamu ya pili) akiwa Tanzania.
Kawa mchapishaji wa vitabu (kampuni ya PanAfric) akiwa Tanzania.
Kanyama alikuja Tanzania (akingali mtoto wa shule ya primari) kuishi kwa mjomba wake aliyekuwa akifanyakazi serikalini. Kasomea huko Ifakara (kama sikukosea) hadi kuwasili mjini Dar es Salaam kujiunga na Shule ya Kichwele (Uhuru).
Kafunzu kujiuga na masomo ya sekondari. Wakati huo, shule za sekondari nchini zilikuwa ni chache sana na za kibaguzi kutokana na tofauti za ngozi (ya mwili na nywele) na dini. Watoto wa Kizungu na Kiasia hawakutaka kusoma na wa Kimatumbi!
Watoto wa Kizungu walikuwa wakienda kusoma huko primary hapo Dochi, Lushoto, na hapo baadaye kwenda Nairobi na Uingereza, kabla ya kujengwa kwa shule yao ya St. Michael and St. George (Mkwawa).
Watoto wa Kiasia walikuwa na shule zao za Aga-Khan, na kadaicha, na wengine walikuwa wakienda kusoma India, Pakistani na Uingereza. Lakini kulikuwa na shule za serikali ambazo hazikuwa na ubaguzi.
Shule za secondary (territorial) zenye sifa zilikuwa ni Tabora School (ya serikali kwa watoto wa machifu, wafanyakazi wa serikali wa veo vya juu na watoto wa walalahoi wenye akili waliofaulu kushinda Territorial Standard Eight katika Daraja la Kwanza), ikiwa ni pamoja na Pugu (Wakatoliki) na Minaki (Waprotestanti).
Kanyama Chiume alikuwa ni kijana mwenye akili. Kashinda hapo Kichwele Primary School (Uhuru) Dar es Salaam kujiunga na Tabora School. Alipambana na “kejeli” za wakati huo hapo shuleni baina ya wanafunzi wa “Bara/Nyika” na “Mwambao/Pwani”. Yeye akatokea Dar es Salaam (“Mwambao/Pwani”). Wa-“Bara/Nyika” walikuwa wakiwaita kwa kejeli wa-”Mwambao/Pwani” kuwa ni “Waswahili”.
Kanyama Chiume alidhihirisha kuwa Tabora School ilikuwa na wajibu mkubwa wa kunoa “vichwa” na kufundisha maadili mema maishani. Kawa “kichwa” pamoja na wenzake. Wakafaulu kujiunga na Makerere University College na kupewa “nondoz” zao, kama mwana-blogu Michuzi anavyoziita. Kutoka Makerere alijiunga kufundisha Alliance Sekondary School Dodoma kurudisha ujuzi wa kunoa vichwa vya vijana wa ki-“Tanganyika”.
Kanyama hakuwa m-Malawi wa kwanza kuishi Tanzania. Wakati huo ilikuwa rahisi kwa watawala wa kikoloni kuwatafuta wafanyakazi wasomi kutoka makoloni yao ya karibu.
Wa-Malawi wengine walioishi
“Tanganyika“, kwa mfano, walikuwa wakina Oscar Kambona, Michael Kamaliza na Austin Shaba. Hawa walipata nyadhifa za juu ki-siasa na kuwa mawaziri katika serikali yetu.
Walipokuwa pia wakina Dr. Shaba, Dr. Charles Mtawali, Dr. Kweygr Munthali, John Phombeya, Simpho Msowoya na Wakili Sizya, kwa kuwataja baadhi tu.
Wakati wa kupigania uhuru ulipowadia, Kanyama Chiume alifunga virago vyake kurudi “Nyasaland” kutekeleza majukumu matatu:
Moja, kuunganisha na kuwahamasisha wananchi wa “Nyasaland at the grassroots level” ili kuwatayarisha kwa utaifa wao.
Pili, kupigania haki ya kuvunjwa kwa Central Africa Federation (Southern Rhodesia -Zimbabwe, Northern Rhodesia –Zambia na Nyasaland- Malawi).
Hao wazungu wachache walikuwa na njama za kutaka kuungana na wenzao wa Afrika Mashariki na kuendeleza himaya ya Mwingereza kutoka Cape Town mpaka Cairo ili kicked ndoto ya mbeberu Cecil Rhodes! Kwa bahati nzuri wazungu wa Afrika ya Mashariki walipinga sera hiyo.
Tatu, kukabili ukoloni wa Mwingereza ili uhuru wa Malawi upatikane kwa misingi ya Pan-Africanism.
Kanyama Chiume na wenzake ndio waliomkaribisha Dr. Hastings Kamuzu Banda kutoka “self-exile” majuu ili arudi nyumbani awaongoze katika mapambano ya kuleta uhuru. Lakini baadaye siasa za Rais wao zilikwenda kinyume cha walalahoi wa Malawi. Sera zake zilikiuka msimamo wa Afrika dhidi ya tawala za wazungu wachache huko kusini mwa Afrika. Dr. Banda aliungana na hao wazungu wachache, hasa wabaguzi Makaburu wa Afrika Kusini.
Kanyama Chiume na mawaziri walijiuzulu na kukimbilia nchi za nje. Kanyama akaja Tanzania pamoja na Orton Chirwa (Wakili Mkuu wa ki-Matumbi wa kwanza wa Malawi) na mke wake wakili Chirwa na Prof. G.M.P. Michongwe, kwa kutaja wachache tu.
Wakati wa siku zangu hapo Tabora School (1964), wanafunzi wawili wa-Malawi - - walipewa nafasi na serikali yetu wajiunge na Tabora School: Archibald (Kapote) Mwakasungura (Form Five yetu) na Kingston Msowoya (Form Three) kutokana na kwanza mkono mkono mawaziri wao waliofukuzwa na Rais Banda.
Mzee Kanyama Chiume (RIP)
Tuliobakia sisi twakuombea
Bila woga wala wasiwasi
Upumzike kwa amani;
Walio karibu na hiyo “nyumba”
Wakipiga miruzi ya vita kali uliyopigana
Huku wakipalilia ziotazo nyasi ;
Na walinde mema uliyopanda
Ya kumkomboa mlalahoi
Wa Afrika, Malawi na Tanzania
Ili hadithi (legacy) yako
Ibakie siku zote!
Kunradhini!
ReplyDeleteMiaka ya ujana wake alikuwa Tanzania: ISOMEKE Miaka ya ujana wake alikuwa Tanzania.
Kafunzu kujiuga… ISOMEKE Kafuzu kujiunga…
…kusoma huko primary hapo Dochi…ISOMEKE …kusoma shule ya primary hapo Dochi…
Shule za secondary… ISOMEKE Shule za sekondari…
…ili kicked ndoto ya mbeberu Cecil Rhodes! ISOMEKE …ili kukidhi ndoto ya mbeberu Cecil Rhodes!
Huku wakipalilia… ISOMEKE Wapalilie…