bado niko katika mambo ya elekezi hapa ngurdoto na wadau wanaopenda kujua zaidi juu ya sehemu hii waende www.thengurdotomountainlodge.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. unajua siye watu wazima tushakuelewa ni kwamba upo kwenye zoezi la kuimarisha nyumba yako, ni jambo zuri kwa kweli nakutakia semina elekezi yenye mafanikio.

    ReplyDelete
  2. We Michuzi unatutambia na hiyo ngurudoto yako umehsafika hotel inaitwa GURUMET kule Serengeti wewe?
    Malazi ni US $ 1250+ kwa siku. sio madafu, ni Dola.
    Huko mpaka Koffi Anan anakuja huko kimya kimya. We vipi wewe!?
    Tena si ajabu ulikuwa unalala Arusha mjini asubuhi unachukua kifodi mpaka hapo. Au ulifadhiliwa na mtu?
    Nenda kaone GURUMET kule serengeti!

    ReplyDelete
  3. ngurdoto ni mandhari tu ila huku kwa kawaida ni kama mabweni ila kule presidentila kuko sawa vibaya,Michu next time chungulia Arumeru river lodge,Mountain village utakuja uniambie.

    ReplyDelete
  4. oyaa michuzi tuletee orodha ya watu walioshinda NEC CCM.

    ReplyDelete
  5. Aibu, huko pool wanashuka na ndala na kaptula, sasa wewe umeshuka na kiwi na umenyoosha. Michuzi kwa usanii namba 1

    ReplyDelete
  6. ni sawa kabisa gurumet ni 1250$ lakini mi nalipia wateja wangu 600$ sasa sijui wewe walikuingiza mjini wakakulamba hiyo 1.2k$ ziko nyingine kama mbalagetihalafu kuna ngorongoro crater lodge room mpaka 800$ ngorngoro farm house, lakini ziko mbali na mji. ngurudoto sio mbaya ziko room kuanzia 150$ mpaka 2k$ inategemea na kijimfuko chako kinavyosema, aliyesema arumeru river lodge nampongeaza hata mountain village nayo siyo mbaya, kuna nyingine kama nduruma lodge kigongonni lodge zote zina mandhari ya kueleweka na unawezasema hauko karibu na mji arusha is a beautiful place

    ReplyDelete
  7. wabongo kwa maneno yaani maneno ya Amani hakuna hata siku moja michuzi wewe jirushe mwayaa wee elimu yako ndio inakupa starehe zote hawajui umesoma hawa wakimbia umande wanabaki kusifia hotel za wahindi na wawekezaji badala ya kumsifia mrema kafanya la maana

    ReplyDelete
  8. Wasi wasi wangu ni kwa wabeba maboksi kama wanaweza angalau kupata maisha kama haya walau mara moja kwa mwaka huko ughaibuni....Mhhhh???

    ReplyDelete
  9. "Wasi wasi wangu ni kwa wabeba maboksi kama wanaweza angalau kupata maisha kama haya walau mara moja kwa mwaka huko ughaibuni....Mhhhh???"

    Jesus,your hate for Tanzanians overseas is annoying,this is like the fifth time i'm seeing such a comment from you.
    Not only do you constantly assume we have $6.50 an hour jobs,you also assume that all of us are broke...
    But I do wonder why you constantly make such comments,could it be that it is in fact YOU who can't afford things ;) ?may I ask what job you have and how much you make in a day?I'm 100% positive your daily income is a joke compared to what some Tanzanians are making LEGALLY over here.

    ReplyDelete
  10. Halafu kwani kubeba maboksi kosa la jinai? Mtu hamwibii mtu, wala hamwibii mwajiri wake aidha pesa kwa mambo hewa (deals) au muda wa mwajiri kwa kwenda kufanya mambo yake binafsi huku unalipwa mshahara (hayo ndiyo maisha ya bongo) au hakwepi kodi kama anafanya biashara, anabeba maboksi yake kihalali kabisa, anapata pesa yake anakula vizuri na bado hizo hizo anawatumieni mlipie ada za watoto wenu shule. Maana ukisikia simu au barua kutoka Bongo mara kadhaa ni ya kutaka msaada wa pesa. Mnasahau kuwa ni za wabeba maboksi. Kwa taarifa yako kuna kazi kibao na wabongo wanafanya huku. Wengine wako shule wanasoma, na wengine wako kwenye field za IT na field nyingine unazoona zinatangazwa kwenye website za US, Canada, na UK kuwa zinahitaji wataalam. Huko US wengine wanafanya kazi mpaka NASA upo hapo? Nampongeza aliyekuuliza wewe unafanya nini? Hapo pengine ni computer ya ofisi saa hizi unaiba muda wa mwajiri wako! USIDHARAU KAZI YA MTU WAKATI HUWEZI MLISHA YEYE NA FAMILIA YAKE!
    Wivu mwingine hauna maana, bado DV-Lotto ipo apply na wewe upate Green Card lakini kama umefika high school!
    Nchi nyingine kama Senegal na Ghana zina watu kibao nje na hao hao ndio wanaingiza pesa za kigeni kwao through remmitances, huko Burundi hao wabeba maboksi wanajenga mahekalu ya nguvu mji unabadilika mwanawane acheni madharau.

    Namaliza Kugandamiza, message sent!

    ReplyDelete
  11. we anon nov 5 7.29 pm
    mbona unawivu hivyo
    wabeba maboksi, wabeba maboksi !!!
    loh !!!! uoni hata haya
    kubwa zima akili huna
    kwani walishakuja kwako kukuomba malazi au chakula?
    hao hao unaowadharau ndiyo wanao saidia nyumbani na kujenga majumba
    inawezekana wewe hata mama yako hajawahi kuiona shilingi yako jopo uko Bongo
    jamani acheni chuki
    hatutaendelea namna hiyo
    wewe nani kakunyima kwenda nje
    mfyuuuuuuu !#@##$ ( fyonzo )
    sizitaki mbichi hizi
    jamani nyie endeleeni na kazi zenu msiwasikilize hao wagonjwa wa akili
    ilimradi mkono uende kinyani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...