Hi Michuzi,
Vipi "weak end" inakwendaje?
Je wadau wanajua maana ya neno "Pedejee" au "Pedeshee"?
Hili jina linatokana na cheo cha PDG (ambayo hutamkwa "Pe-De-Zhee" kwa kiFaransa) ambalo kwa kirefu ni Président Directeur Général. Hiki ni cheo cha kiongozi mkuu wa kampuni au shirika. Ni sawa na CEO (Chief Executive Officer kwa Wamarekani) au MD (Managing Director kwa Wakerewe na sisi waBongo).
//Fred

waambie bwana.
ReplyDeletesio watu kazi kuvalia suruali kifuani wakadhani ndio u-PDG
Aisee! mimi nilikuwa najua mtu ukiwa na pesa harafu uvae suruali hadi tumboni yaani mundende ndio anakuwa predejee kumbe sivyo Asalamaleko walahi
ReplyDeleteBon mon freur, Uko sawa kabisa ila kimatamshi umekosea sio "zhee" ni "jhee" na ndivyo herufi "g" inavyotamkwa (kwa kifarnsa) "en la langue francaise"
ReplyDeleteNa wa chini yake huitwa De-Zhee (Directeur Général). (dRU dACHI)
ReplyDeleteKIINGEREZA CHAKO KIGUMU. SIJUI TUTAFSIRI MWISHO DHAIFU, SIJUI UNA MAANA GANI KAMA MWISHO WA WIKI NI WEEK END. WANASIAASA WETU HAWATAKI NASI TUKAJUA KIINGEREZA HII NDIYO TAABU.
ReplyDeleteAnon wa 6:50PM EAT umiteleza kiduuchu ni hivi "Bon mon frère" na chini ndani ya mabano (kwa kifaransa) na mwisho ni "en langue française" viji-maandishi vile vya lugha yenyewe.. uwage unacheki na babelfish ya altavista mwanawane... (dRU)
ReplyDelete