niko dar tranzit leo kuelekea sehemu na ile pyeeeee raha ya kwanza kukutana nayo ni hii...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. RAHA GANI KAKA MICHUZI.....JAMAA WAMEKALIA NCHA ZA VISU TU...KILA WANAPOENDA TZ KOTE WANAZOMEWA KAMA WEZI...MAANDIKA YANATANABAISHA KWAMBA HATA UFALME WA FARAO ULIVOANGUKA...TUMEONA VYAMA IMARA NDANI YA SIASA MACHACHARI KAMA (KANU)NDANI YA KENYA...SEMBUSE CCM????SIKU ZAO ZINAHESABIKA MICHUZI...HATA UCHAGUZI WA ELFU 2010 TAKWIMU ZA MACHO ZITAONYESHA JAPO WATAIBA KURA KM KAMA KAWAIDA...LAKINI NASEMA IPO SIKU WATU WATCHOKA NA ISHU ZA KINA MONGIKI ZITAJITOKEZA TZ HIII

    ReplyDelete
  2. Dah...!!! hakuna kitu huwa kinanikera muda wa kwenda kazini asubuhi pamoja na muda kurudi home jioni,yaani hii kero,EL alijifanya kupiga kelele lakini sijaona action yoyote zaidi ya kuweka njia 3 na kusababisha ajali zisizo na msingi wowote! Unakwenda kazini unatumia masaa 3 hadi manne kutoka mwenge hadi posta loh!! kama unasafiri vile ukifika kazini uko hoi kabla hujafanya kazi........Damn!!

    ReplyDelete
  3. sio dar peke yake miji yote mikubwa duniani hii ndio karaha yake,london foleni hadi saa tisa usiku!!

    ReplyDelete
  4. Kaka hiyo misamiati imezidi huko pyeeee ndio wapi? Utafika lini huko pyeeee kama mambo yenyewe ndiyo hayo tena.

    ReplyDelete
  5. kaka ndio maendeleo bongo, kila mtu anataka amiliki baiskeli, sasa hatimaye barabara hazitoshi, mi naona ushuru uendelee kupanda tu tuendelee kumiliki baiskeli sisi wateule wachache wa tabaka tawala

    ReplyDelete
  6. walaaah Michu wewe kiboko.....manake nakumbuka kuna wakati tuliambiwa mababa wa jiji (city fathers) waliamriwa kutafta suluhisho la nyororo..... basi wakaja na issue ya 3-1 asubuhi na jioni....kuangalia harakaharaka jua bado reeefu kwelikweli (kivuli)manake hapo saa bado mbichi (kama 3 asubuhi) lakini nyororo ndio hiyo na watu bado wanakula 2 kwa tupu (peupe return lane hapo)...... haya jamani hayo ndiyo mambo ya bongoland, kaaaazi kwelikweli.......

    ReplyDelete
  7. Dar Bwana, Barabarani Foleni, Tanesco Foleni, Bank foleni,kariakoo usiseme, bar zote zimejaa, guest mpaka upige simu kama ijumaa ndio kabisaaa....

    ReplyDelete
  8. The real cause of divorce is marriage; the real cause of "nyororo" is too many autos!

    Gari ndogo ziingiazo na zitokazo ndani aha Jiji wakati wa "rush hours" ziwe zimejaza abiria. Wenye magari madogo wafanye utaratibu wa kirafiki wa "car pools"!

    Hiyo itasaidia kidogo!

    ReplyDelete
  9. Poleni sana mlio dar hata huku ughaibuni kuna foleni lakini inaenda ya dar mpaka uagize na chai kabisa asubuhi

    ReplyDelete
  10. Hiyo ndio adha ya miji mikubwa popote ni hivyo lakini bora ughaibuni kuna alternative way hapo dar hadi mpande matuta

    ReplyDelete
  11. Kaka Michu.
    Kweli hilo tatizo la foleni ya magari ni gumu kulitatua. Lakini uwezekano upo. Na mwanzo pa kuanzia ni kuwa na usafiri wajumuiya yaani "public transport" ambao unaofanya kazi kiuhakika na kuweza kuweka mpangilio wa mida ya mabasi ("Time Schedule"). Pia, huo usafiri uweze kuwa na uwezo wa mabasi ya pole pole (all stops) na yandayo kasi (Limited Stops). Yani kwamfano basi la ubongo posta bila ya kusimama kituo chengine chochote kile. Cha zaidi mno ni kuwa pia na mabasi ambayo yanakalika na kuwa mtu ukifika kazini hautakuwa na haja ya kuoga tena.

    Badala ya kuwa na 3-1 system za magari. Fanya hiyo 1 iwe ni njia ya mabasi tu, na magari ya kawaida (hata ikiwa yamejaa watu wanne) yabaki kwenye hizo hizo njia mbili za kawaida. Utaona jinsi gani watu watakavyo wacha magari yao nyumbani na kupanda mabasi kwenda kazini.

    Ukitaka nitaweza kukupatia uchambuzi zaidi wa kuwa kwanini tunaweza kuanzisha mwenendo huo bila ya kuomba pesa kwa wahisani. Sisi watanzania kama tunazo hela za kununua magari ya namna hiyo na pia kuyatia mafuta (kiasi gani sikuzi mafuta bongo kwa lita?) basi tunazo pesa za kuweza kulipa kodi za mabasi ambazo zitakazowezesha huo mwenendo uendee kama nilivyo taja hapo juu.

    Wadau ongezeni mawazo.... tukiacha kusubiri wahisani na benki ya dunia na dada yake IMF ili watutatulie matatizo yetu basi ndipo tutakapopata ufafanuzi wa kweli.

    "In the history of the world, no customer ever washed a rented car"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...