wadau kunradhi. sina nia ya kuzua ama kundeleza mjadala, kwani kuuliza si ujinga. ni hivi; mwaka 1991 nilibahatika kwenda ukerewe kusaka tujinondo fulani hivi. isitoshe kuna pande nilipigiwa la kubaki kupiga boksi na kunahii vibibi. sikuafiki, nikajirudia zangu bongo na kuendeleza libeneke. je, nilinoa stepu kwa uamuzi huo ama ningejichimbia huko huko?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 52 mpaka sasa

  1. Kama ulikuwa unapiga bo na kivinanii vibibi! naona ulikuwa uamuzi mzuri kurudi nyumbani.. lakini si wote tuko katika hiyo mipango ya ku piga box na kunannii vibibi!! Maisha ni kokote!! Ni Mipango tu!

    ReplyDelete
  2. Michuzi, bora umerudi maana ungebaki kule sana sana ungekuwa mkuu wa wabeba maboksi.

    ReplyDelete
  3. Ninapoandika comment hii nipo hapa Ukerewe, nimegoma kuwafanyia kazi Wakoloni, na nikimaliza Kijinondo changu cha Pili, narudi kwa mwendo wa kukimbia! Hongera kijana, una mawazo mazuri, tunawaona hapa, taabu tupu! Hata Michudhi, hapa bwana kama unakuja kupiga picha na kugeuza karibu, lakini kuishi, mmhhh, shauri yake atakae kuja wakati sisi tunaondoka!

    ReplyDelete
  4. kwanza unatakiwa kujua ukerewe ya miaka ya 1991 sio ya sasa, ukerewe ya miaka hiyo ilikuwa poa lakini sasa ukerewe imegeuka chooni hata kina sosi mafundi bomba wapo sasa sio ile ya miaka hiyo kaka.Nafikili kujiuliza kwako wala hakutakiwa wewe endeleza libeneke la bongo tukupe ubunge ule raha kaka maana unaijua bongo nje ndani.Watu kama nyinyi ni wachache hivyo kaa hapohapo mimi nilipata ishu kama yako nilikuwa kule mwaka 1992 lakini nikarudi na kajinondo na sasa poa kaka kule sasa wanaenda watoto wa miaka ya 1980.

    ReplyDelete
  5. Ulikua na uamuzi mzuri Michuzi..mi mwenyewe nna miaka miwili cjarudi home, naona km nimepotea vile...nyumbani ni nyumbani 2..huku baridi,clubs zenyewe hakuna bolingo wala bongo fleva...viwanja km Jolys na kili time hakuna!!! yani full tabu tu. ULIFANYA UAMUZI WA BUSARA SANA.

    ReplyDelete
  6. mwaka 1991 mpaka leo hii kwa UK, ungekuwa mbali sana sasahivi, anyway hata bongo hujachemsha, ungekuwa umechemsha bongo tungesema ungejua ungebaki, maana BORA KUCHEMSHA HUKU ULAYA, KULIKO UCHEMSHE UKIWA BONGO, bora huku tunabeba boksi bongo hakuna kiurahisi hii kitu, kuosha vizee, bongo kila mtu analea mzee wake, so bado tunarudi palepale, kwa wale tuliotoka familia za hali ya chini, mamtoni bomba sana, hata tubebe boksi, hata tuoshe vizee hata tunyanyasike, bado poa tu, mradi tunalipwa pesa yetu nzuri, na tunaendelea ndugu zetu na tunajijengea future pia nyumbani.

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi uamuzi wako wa kurudi wawezakuwa mzuri ama si mzuri kutegemeana na mipango yako baada ya kunanihii vibibi na kupanga maboksi.Kuna wanaotoka kwa hizo kazi na kuna wanaoachana nazo na kuja bongo na wanatoka vilevile.Inategemeana na tageti zako za maisha umeziwekaje.

    ReplyDelete
  8. Je ilikuweje ukawa umezungukwa na kuku wengi hivyo
    Maisha ni maisha na ukiwa na ujuzi waweza kuishi popote upendapo
    Mimi nipo hapa Ukerewe tangu august 1968
    Anon

    ReplyDelete
  9. ulinoa stepu ila kwa sasa ni mwanamtandao wa Jk pouwa kama unaria vile.vinginevyo nawe ungekuwa choka mbaya sana tuu.kinachonisikitisha bongo mtu akitoka huku hata awe vipi vitajiri vyenu huko vinapapatika sana.hata mawzaziri wenu huwa wakija huku tunawaona wanashangaa shangaa tu.
    halafu kingine wanaorudi huko wengi wao ni watoto wa walalahoi ambao walikuwa hawajawahi tanua huko bongo kwa hiyo wanarudi na vinondo vyao kushow off LAKINI SIE WATOTO WA MJINI BORN THERE, WE KNOW BONGO IN AND OUT HATURUDI NG'OOO KWANI HAKUNA JIPYA,Karikoo the same,vijilabu vyenu hivyo uchwara tu hakuna lolote.WATU tunajirusha huku WEST/EAST END,MWEEEEE!!!!!! yaani tunajichanganya na sio lazima tubebe mabox,akili ni nywele na kila mtu ana zake.
    CHA CHANDU-SHEPHERD BUSH,UK.

    ReplyDelete
  10. mjomba michuzi,ulicheza kwani uligeuza mapema kabla deal zako azijakamatwa na wajanja wengi,kuhusu vijibibi kunanini au box...kasema doctor remmy ongala zamani,kazi ni kazi,na unajua kwanini bongo watu wengi wanachemsha sana kimaisha???watu wanapenda kusema kazi fulani hainifahi lakini hapa mtoni utashangaa Bill gate anapaka nyumba yake mwenyewe rangi,Mengi amwagie maua bongo????ukiangalia hayo utaona watu wa huku pamoja na vibox wanainua mijengo na kusaport ndugu zao kuliko waliopo bongo.kwa kifupi ungechemsha bongo ungeililia mtoni.

    ReplyDelete
  11. kaka Michuzi Bora ulirudi, hongera sana.kweli wewe ni kiona mbali ndugu yangu. kwakifupi nadhani wote waliozamia/kuishi huku japo wanapata hela za vibarua lakini ukweli watu wanasota sema ndio hivyo tena kurudi bongo wanaona noma pakuanzia wala pakushika hamna huo ndio ukweli. Na kikubwa sana ni kwamba watu wengine walikuja huku kwa mikwara, kuja kusoma, badala yake baada ya kusoma hata fani walizosomea hawazitumii tena, kwahiyo mtu uzoefu wa alichokisoma hanna, na hata akirudi nyumbani hawezi ku fit kwenye soko la ajira. Maana experience alizonazo ni hizi kazi za kizushi ingawa huku zinatupatia riziki, huko bongo mtu hawezi zifanya kabisa hasa aliyetoka ulaya.Mfano, kubeba mabox n.k.
    Wajanja waliosoma na nondo za nguvu wamerudi zao Bongo kuendeleza libeneke.

    Kingine watu wanatamani sana kurudi Bongo, na wanatamani sana hayo maisha kwa kiasi fulani, sema unakuta watu uliosoma nao huko bongo ambao pengine rafiki zako wa karibu, kwa sasa mambo yao safi,michongo imekubali na wanazielewa. sasa kurudi huko ina maana utakuwa nyuma sana kwao, na jamaa wanakuona mzushi tu. Maana huna ishu.

    Kingine kaka Michuzi, zamani kuja ulaya ni dili sana, Ila jamani sio siku hizi sana, hata ukisema unatoka ulaya sio ishu sana. Na pia maisha huku yamebadilika sana, ulaya ya kipindi kile si ya leo.

    Cha msingi kama mtu unaona unaweza kimbizana na haya maisha well and good, ila kama mtu una njia ya kupata kazi bongo baada ya shule bora tu ujirudie, mambo kama safi ulaya mbona mtu unakuja tu kutembea na kurudi.

    Ila pia kwa ajili ya utandawazi jamani ruksa watu kuvinjari, ila nyumbani ni nyumbani. Mimi nikimaliza tu kitabu kwakweli naona bora nije zangu tu bongo, huu utumwa wa huku siuwezi.

    ni mimi Msema kweli

    ReplyDelete
  12. MICHUZI MAMTONI NI MAMTONI TU HATA UBEBE BOX HATA UWE MLINZI HATA UOSHE HAO VIZEEEE ILA AT THE END OF THE DAY POAUND;DOLLAR;EURO INALIPA USIJIDANGANYE MICHUZI PAY CHEQUE YA MWEZI MMOJA TU UNANUNUA HIVYO VI_BALOON VYENU AU MARK 2 MAYAI WAKATI HIZO KWANZA HUKU HAKUNA GARI ZA 1977 CCM INAZALIWA.KUWA ULAYA PEKA YAKE NI NONDOZZZ HUHITAJI HIZO ZA MLIMANI KILA SIKU MARA FFU WAMETIA TIMU MARA HUNA POSHO LAKINI HUKU SI HABA UFAHAMU WETU NA UKUNGU WA MACHO TUMEFUTA PAMOJA NA BOX ZETU :HIZO CAMERA ZENU SISI HUKU UNASHUSHATU ID YAKO UNAVUTA KITU SIYO MPAKA UMBEMBELEZE GABACHORI HAPO BONGO AKUKOPESHE

    ReplyDelete
  13. Michuzi,
    swala la busara sana ulifanya ulipoona tu ukerewe HAPAJAKUKUBALI(lakini hii ni kwa wengi).Watu kibao hapo wananganganiza kubaki wanapoteza muda.Mi nilenda nikaka kamwaka nikakapoteza tu ujinga maisha tight kama nini na vipicaddily vyao mnajazana ndani kama daladala zetu tu, University ndo nondo kama nini walimu wa chuo wako mean, watu wenyewe waingereza meaaan! So what I did nikarudi bongo lakini kwa sababu sikukoma na kutaka kwenda ulaya basi nikajaribu marekani na nnachokwambia sasa nikwamba US ni different world huwez compare kabisa na UK. Life is cool, people r friendly, kitabu wamekiachia makali KIASI and dolaz AVAILABLE everywhere!!
    Labda ungejaribu Marekani nawewe kama mimi!!!
    Conclusion: Kuliko UK afadhali usome bongo mlimani au usome kwenye ma Institution ya maana.

    Thanks America!

    US fan!

    ReplyDelete
  14. HAPO MISUPU INATEGEMEANA SANA NA U,ETOKOKA FAMILIA GANI.KAMA YA KAJAMBA NANI USINGE RUDI HATA KWA GRADER.KAMA UMERUDI BASI INAWEZEKANA BABA YAKO AU UNCLE WAKO ALISHAWAOSHA HAWA VI BIBI NA VIBABU NA KUWAPIGISHA NYETO SANAAA SO NDO MAANA WEWE UMEKULA GOOD TIME.WALIO TOKA KWENYE FAMILIA YA KAJAMBA NANI INABIDI WAFANYE KAMA BABA YAKO ILI WATOTO WAO WAJE KULA GOOD TIME.USIJIANGALIE WEWE BINAFSI MISUPU ANGALIA JAMII YOTE INAVYO TESEKA NA KUNYWANYASIKA KIMAISHA NA FUTURE.
    HAPA KUNA VICHOKA KIBAO NA WANAKUBALI KULIPWA ELA YOYOTE ILI WAWAOCSHE HAO VIBIBI INGAWA INCINI KWAO MAISHA NI MAZURI KULIKO BONGO.
    USIDANGANYE JAMII MISUPU.ONGELEA RUSHWA JILIZO OTA MIJIZIZI HAPO BONGO NI VIPI TUTAINGOA?.SIO WATU WANA BEBA BOKSI NA KUWAOSHA VIBIBI HAPA ELA WAKITUMA BONGO BADO WALA RUSHWA WANAZITAKA

    ReplyDelete
  15. Hapa UK ukitaka kubeba box utabeba, kunani hii vibibi ni wewe tu. Sio wote wako huko wengine sisi tuko na kazi za maofisini, ma call centre etc. Exposure, international experience vyote vinakuwa. Hata wewe Michuzi ungeweza kuwa mpiga picha wa The Sun, The Guardian etc sio lazima box ama vibibi!! Ukijiweka kibox box utabeba mpaka ukome!!

    ReplyDelete
  16. ulichemsha Michu, du ungekuwa ushakula zako pepa taratiiiibu unakula kuku kwa mrija

    ReplyDelete
  17. Uamuzi wako haukuwa mbaya kwani ulijua tuu alie kupa hilo pande ndio mpaka leo hii anaendelea kukubeba,wapo wapiga picha wengi tu tena highly qualified paparaz.sinto shangaa siku nikisikia umekuwa mpiga picha wa rais hata kama ni zito kabwe.

    ReplyDelete
  18. HAO walio baki huko wametoka familia tofauti ndio maana wanahangaika usiku na mchana tofauti na wewe unaosindikiza misafara ya WAHESHIMIWA ziarani na kuwasubiri nje ya milango wakati wakifanya Ngono.

    ReplyDelete
  19. ULIKUWA UMECHOKAAAA!! YANI ULIKUWA MTONI NDIO HALI HIYO, HALAFU HIYO PICHA SIJUI NDIO HIYO HIYO UNAYO!!! MAANA IMEPAUKA KISHENZI. DESIGN UNATEMBEA NAYO KWENYE KIPOCHI KURINGISHIA ULIPOKUWA HUKO BULGARIA, MAANA LONDON GANI HIYO, NGUO MCHOSHO, NJIWA WENYEWE HAPO NAWAONA WAMECHOKA PIA. BORA ULIVYORUDI MAANA HUNA TOFAUTI YOYOTE YA HAPO ULIPOPIGA HIYO PICHA NA SASA HIVI ULIVYO

    ReplyDelete
  20. we michuzi unapenda ligi sana,ok
    kwa anon Tuesday, November 20, 2007 11:48:00 PM EAT nakunukuu "ukerewe imegeuka chooni hata kina sosi mafundi bomba wapo sasa sio ile ya miaka hiyo kaka" ulidhani utakuja kiwanja na cheo cha babako kwenye serikali ya sisiemu sio??? equalizer hapa babu harakisha urudi bongo umsaidie dingi kuchonga dili za rushwa muendelee kusumbua kina sosi fundi bomba kama ulivozoea. bado unakiubongo kidogo sana, umefuata opportunity au umeenda kuangalia nani yuko huko??

    ReplyDelete
  21. Mimi siko hapo bongo mzee,so sijui hali yako,kama unaona upo safi basi maisha ni popote.Lakini sio kwamba ungebaki basi ungekua chini sana ya hapo,pengine ungepata mbinu nyingine nyingi na kazi nzuri.Kuna watu kibao wanaona bora wabaki pale kuliko mpese mpese wa bongo,labda ulikua na chanell mzee,usiombee ukiwa unaitwa MR. SIMJUI MTU hapo bongo utakua mwandaazimu au ikaliunge bendi na grand pa SEA

    ReplyDelete
  22. Fumbua macho mjomba! Sio kila aliyekuwa Ulaya anabeba boksi au kukaa na vizee. Watu wana kazi za maana kabisa hao wanaobeba boksi ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na wale wenye kazi za maana zinazohitaji nondo za maana siyo vijinondo. Ukienda Ulaya safari nyingine tafuta wanaofanya kazi za maana usiishie kwa wabeba boksi tu na wachamba vizee!

    ReplyDelete
  23. Ulikosea step kabisa ulikuwa unatakiwa ujitahidi tu kubeba box na kuvinanihii vibibi!sasa we ulkimbia aisee kweli wewe ni mvivu sana!ulikata tamaa mapema sana na ni lazima utakuwa unajuta sana!

    ReplyDelete
  24. kama ntapata kazi kama nilonayo hapa na malipo sawa na nnayopata hapa, ntapata usalama wangu na mali yangu kama wa hapa kiasi naweza kulala mlango wazi, kama ntapata huduma za muhimu bila kutoa rushwa, kama ntapata haki sawa kwenye sheria kama hapa, kama ntapata shule nzuri kama za hapa kwangu na watoto wangu, kama kutakuwa na uwajibikaji wa kila mtu hasa serikalini, walimu, mapolisi na madaktari kama ilivyo hapa sio kupasua pasua watu vichwa kimakosa
    NDO NTAFIKIRIA KURUDI BONGO, LA SIVYO NTAKUJA KUSALIMIA NIKIPATA NAFASI NA HELA YA NAULI

    ReplyDelete
  25. Michuzi kwa topic yako hii mutu amejibu vizuri sana. Sikuiandika mimi hii comments lakini inasema yote...watoto wa baba warudi nyumbani kuzidi kutanua lakini watoto wasio na kwao majuu kuzuri bwana..tunaweza hata kuwatumia ndugu zetu hela ya angalau nao wanywe soda Xmass wa enjoy....

    Wengine Birthday ya kwanza tulifanyia majuu...

    Jamani mimi mfano nitarudi vipi bongo? nilivyokuwa bongo nilidharaulika, hakukuwa na kazi na nilipopata kazi malipo hayakut
    osha hata wiki moja kuishi
    baada ya kufanya kazi mwenzi mzima, huku tajiri niliyekuwa namfanyia kazi akiwa anatanua mimi niliendelea kumtajirisha huku nikibaki na njaa, chumba chakupanga maji ya shida choo cha kuchuchumaa nje halafu kila mtu alikuwa anasema hayo ndio maisha na mimi nikakubali.

    Mahali nilikuja kushtuka kuwa hayo sio maisha ni siku nilipodondoka mamtoni, nilishangaa nikiosha vyoo mwenzi mzima jamaa wananilipa pesa ya kuishi mwezi mzima, nikashangaa chumba nilichopanga kipo selfcontained choo bafu kila kitu ndani, umeme 24/7, kula mlo
    mara tatu kwa siku.

    Nilijumuishwa katika ujenzi wa nchi za watu, kwa sababu jamaa walinipa kazi na kunikata kodi ya mapato ili nichangie maendeleo, nafasi ambayo nchi yangu bongo hawakunipa, kuitumikia nchi tunaweza lakini kama hupewi nafasi utafanyaje?

    Ushauri wangu wa bure kama wewe kwenu masikini fanya juu chini uje majuu, huku unahitajika na utatumiwa vizuri kuliko bongo, mtaji wako ni mtaji wa masikini kama alivyosema B.Mkapa ni nguvu zako. Bongo hutapewa nafasi ya kuutumia mtaji na kulipa mahitaji yako, hapa ukiosha vyoo utaisha maisha yanayofanana na watoto wa oysterbay au masaki yaani utaendesha gari, utavaa vizuri, utapata watoto wazuri wa geti,utatuma hela kusaidia nyumbani na hamna mtu atakudharau kwa sababu unakula jasho lako.

    Lakini kama kwenu bongo matajiri au sijui baba katibu wa wizara gani au sijui nani wako waziri wa nini sijui basi njoo juu usome halafu rudi kwenu uendeleze matanuzi, kwa sababu hata kuosha vyoo utakuwa unajisikia vibaya ulizoea kuoshewa na wafanyakazi,rudi tu uendelee kutesa tuache walalahoi tutese huku kwa sababu wakubwa wa huku wanathamini ujuzi wetu wa kuosha vizee na kubeba boxi, bongo tukibeba boksi hailipi.

    Conclusion: Kama umesoma then chaguo unalo either kubaki na unahitajika au kuingia bongo na unahitajika ni jinsi tu ya kupangilia, kama hujasoma na kwenu masikini basi the best solution ni kubaki na unamsawazishia middle class wa bongo na kumshinda kitu ambacho bongo usingekiona, bongo hata nyama ya kuku yenyewe anasa

    ReplyDelete
  26. wabongo tu wavivu sana tunapenda easy money ndio maana wengi hawakawii kukimbilia nyumbani.. ...mataifa mengine yanawasaidia watu wao wazamie USA na nchi nyingi kwa vile wanajua watu hao watawekeza kwao nyie mnajambajamba tu hapa ohhh mimi nilisindwa nikarudi ohh mimi nawaona wanapoteza muda jinga tu maisha kama yako mazuri bongo ni watu chache sana the rest ni joto ya jua tu...

    Na kazi za mabox nyie mnalalamika kila siku hamjui lolote semeni lakini watu wanaishi na kazi za maana tu msione wamekaa kimya..nyie mnapoteza muda kwenye computer za kazini kusema mabox bwana life is very different hata ukaweka mijadala mia mwenye macho haambiwi tazama

    Na kwa upande wangu Michuzi na talent yako kama ungezamia vizuri sio kienyeji tu wewe ungekua mbali sana..paparazi wanamake good money huku....wapiga picha wanatengeneza hela nyingi sana..

    ReplyDelete
  27. sasa haya kweli turudi
    http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/11/20/102889.html

    ReplyDelete
  28. vibibi havikukungalia ndo maana ulirudi, kwanza ungehakikisha hivi vibibi ni written off au vinafaa, ohh, wenzio ndivyo vinavyotuweka huku, na mijihela kibao!!!! umeshayamwaga maji sasa, kuyazoa tena basi! piga deki tuu uyakaushe.

    ReplyDelete
  29. kusema kweli mimi kurudi bongo itakuwa ngumu kwani nishazoea kupata **** za bure haya mamabo ya kurudi kwenda kuchunwa nitayaweza wapi?

    Pili huko Bongo naona kila mtu anajenga mie nishazoea mamabo haya ya kufanya kazi kulipa mortgage nitayaweza wapi?

    alafu naona kule bongo kila mmoja ameingiwa na wazimu wa kuoa sasa mimi siamini hii institution ya kuona mimi nataka kumungunyua tuuuu....labda niiishi na demu lakini sio mamabo ya kutiliana saini za ndoa hiyo itakuwa BIG NO

    sie wengine ndo tushafika huku baadae tunakula pensheni tuuu nidio maana unaona nikisoma wakina Mwanakijiji wanavyobishana kwenye siasa mie naona MAUZA UZA tuuu

    ReplyDelete
  30. hahahaha.. Michuzi bana.. sasa ulitaka ukae kwenu kule!!! au unataka kutuambia na wewe uliwahi kubeba box tehe tehe...

    ReplyDelete
  31. Wee Anony 1:22 Naomba nikujibu:- Maisha ni popote Mwanawane clikatai wapo wachache wana life nzuri ulaya na wengi wamechoka lakini usikandie ulikotokea BONGO SASA HIVI NI NEW YORK tena uwaambie na wabeba mabox wengine ambao wametelekeza familia zao wanaishi kwakujifichaficha. Watu wengi wabeba mabox waliopo Ulaya wana hali mbaya kiuchumi nazungumza thru experience usitake kutufanya sisi hatujui!Kwanza wengi hawana uhuru wa maisha yao wengi wao muda wao wa kukaa huko umeisha wanaishi kwakujificha, pili lishe sio nzuri wanashindia biscut km mateja na conflex kwa kula mlo mzuri full balance diet nitatizo km maharage, dagaa, mboga za majani n.k ata taste wamesahau nandio maana huwa mnaagiza, tena usitake nitaje majina kuna uhuru wa habari na wadada wengi waliowin wanaolewa na wanaigeria mataperi au wazungu wazee ili wapate unafuu wa maisha.Pili mnapopata misiba yandg wakaribu ata mzazi wako hamuwezi kuja JE NIMAISHA GANI JAMANI MNAOSOMA BLOG HII? Mnaishi km kwenye jumba la BIG BROTHER? tena afadhali ata big brother wanapigiwa kura wanarudi makwao? Sikatai wapo wachache wana maisha mazuri na si sana yakununua mboga tu! Mbona km hela ipo mnakuja baada ya miaka 6 nyumbani? Na mtu akifa kumleta miezi miwili? hela si ipo? Wengi wako huko choka mbaya maisha yakuombaomba ata tukija kutembea wanaomba tuwaachie japo jeans tulizovaa, Niliwatembelea washkaji huko viappatment vyenyewe ata kupishana watu wawili shida, wengine wanashindia maapple, Vyakula vingi wanakula vya supermarket sio fresh kushindia mikate life goes on, mkifanya party watu wanakusanya vihela kwny kopo miezi 3 na nguo wanaazima madukani ukichunguza sana picha wanazopiga nguo nyingi wanakodi dukani sharti wasitoe lebo wala msipige perfume! Na km mmepata nondoz yanini mbebe mabox? Na wengi wakija navidiploma vyao mnatutishia wakati bongo watu wanasoma correspondence schools na wanafanya mitiani ya ulaya mpaka masters! Mkija bongo YOU KNOW nyingi mbona km mnahela msije namagari kutoka huko ambayo mazuri mnakazana kuja kununua used? ukikaa mwezi mnaishiwa namagari mnauza? Asilimia 70 ya walio huko muda wao wakukaa umeisha na wengine washakuwa mateja njooni tu nyumbani wajameni mtapata laana zawazazi nyie msiotaka kuja kuona wazazi wenu.

    ReplyDelete
  32. Michudhi, au Misupu, bwana nakuomba funga mjadala huu. Unajua kabisa njia za kuondokea Bongo kwenda Ukerewe ni mbili. Ya maeneo ya Posta ya zamani na ile ya karibu na Kipawa. Walioondokea Posta ya zamani hawawezi kurudi hao, kwanza Passport hawana! Tena nondo kichwani hamna! Waliondokea Maeneo ya Kipawa wa Passport wanazo, hawa wanatamani warudi. Tunao wengi tuu hapa, hata jumuia za Wabongo waishio hapa wahawajajiandikisha wala nini, wanachenga tu, wengi wanajiita ni wakimbizi wa Rwanda, maana Somali wataulizwa nywele.

    ReplyDelete
  33. Ulifanya busara sana. UK ilikuwa zamani sio ya sasa hivi. Waingereza weupe wanaikimbia nchi hii kila dakika kutafuta maisha mazuri abroad. Mie mweusi nibakie hapa kutafuta nini? Nina education nzuri bora nirudi nyumbani

    I have been living in this country for 19years and now want to go back to Tanzania. I hate this country because of:
    1. Inheritance Tax
    2. Social engineering by the Liberal lefties
    3. Uncontrolled immigration with no 'quality' criteria
    4. The Political correctness agenda
    5. Human rights legislation tainting natural justice
    6. Danger on the streets from yobs
    7. Terrorist threats
    8. Poor education in schools (primary & secondary sch.)
    9. The 'rights' culture
    10. The compensation Culture
    11. The Labour party
    12. Taxation, Council Tax, Poor pensions, poor healthy service
    13. Low wages...etc etc

    For more details read these two links
    http://news.independent.co.uk/uk/this_britain/article2067620.ece

    http://www.overseas-emigration.co.uk/news/immigration-news/more-britons-planning-to-emigrate.html

    ReplyDelete
  34. Hapa nipo Ukerewe, habebi mtu box wala nini..shule imepanda, nimenunua nyumba, job ofisini, family poa. Box miaka ya sabini huko wakerewe wengi wametulia tuliiii, uraia wa kumwaga..hivyo vibibi your choice kama wewe ni mvivu au unataka kujirusha na madawa tu...ukijantena tembelea watu wa maana..Thanks Anony Mkerewe

    ReplyDelete
  35. Anony hapa juu unaeelezea matatizo ya Ukerewe. Get in touch I'll help you buy One ticket to Kiwalani DIA

    ReplyDelete
  36. Hebu ingieni YouTube msikilize wimbo wa Mzee Yusufu "Una Nyodo" au tazama video yake www.bongo.com

    Bwana yule ameeleza vizuri sana kuhusu hii mada ingawa kwa mafumbo kidogo sana.

    Hivi mahali fulani kwenye kitu wanaita "housekeeping" wanafunzi fulani wa kiafrika walikuwa wanasema hawawezi kurudi makwao kwa sababu tofauti. Wazungu waliokuwepo hapo waliwaambia wazi "rudini kwenu hatuwataki, tumechoka na EU immigration issue na nyie mnataka kuwa problem". Ni kweli wazungu wamechoka na hii issue ya economic immigrants watu wanatakiwa warudi makwao. Ndio maana kuna hate and racial crimes nyingi tu.

    Wengi wanaishi kama (wakimbizi)Warundi na Wanyarwanda, sasa nyie ndugu zangu mnapowaambia warudi kwao, kwao wapii, Burundi au Rwanda? Wengine hata passport za Tanzania hawana, hata kama alisoma alisoma kama Mrundi au Mnyarwanda na hicho cheti chake nani atampa kazi Mrundi amwache Mtanzania?

    Nchi za watu zimeendelea kweli kweli lakini kila kitu kizuri hakikosi kasoro, kuna matatizo kibao ya kiusalama hasa kwa wenye watoto, wasi wasi mkubwa sana, ama atauawa na watoto wenziwe au hata watu wazima au atatekwa, life is not peaceful at all.

    Na watu wanaishi kwa mikopo jamani, wa nyumba wa hivi kila mahali credit cards, sio kama eti maisha yanatosheleza hasa UK maisha magumu hata huko US pia watu wanaishi kwa mikopo unakupa hiki unakopa kile, unalipa. Hata nyumba ukitaka utanunua lakini kwa mkopo.

    Hakuna haja ya watu kujitanua eti tuna maisha mazuri kwa standard ipi? Maisha hayo mazuri unalinganisha kwa standard ya Bongo au ya huko uliko (Europe/America) Labda uwe umepata ajira ya serikalini au kwenye kampuni tena una nondozz mpaka jamaa wanaona bora wakutumie. lakini wengi wanaishi maisha duni, kufanya kazi masaa kibao ambavyo hata ILO walishakataza kwa sababu ya kiafya (Occupational Health & Safety Regulations)ili kutimiza mahitaji ya kila siku. Ili alipe paund 300 kwa 1 bedroom apartment au £400-500 kwa two bedroom apartment inabidi mtu ajipinde hasa, ukizingatia bado kuna bill kibao zinamngoja kama umeme, maji, Tv, internet, na kodi alizotaja mtu mmoja hapo juu. Na chakula na matanuzi juu. Hapo unalipwa casual labour kuanzia pauni 5 mpaka 6 kwa saa, kwa yule mwenye documents za halali, undegraund ni mpaka paun 3 au 4 kwa saa unalipwa. Ukizitazama unaweza kusema nyingii lakini si nyingi, kutokana na hali ya maisha ilivyo. Wenye maisha nafuu ni wale wanaolipwa mishahara. Na wenye maisha mazuri ni matajiri, na watu wa middle class angalau.

    Na huwezi kulinganisha na Standard ya Bongo kwa sababu ni vitu viwili tofauti, mfano pauni 300 hapa unakaa kwenye ka "rabbit hole" wakati ukiwa na hizo pesa Bongo nafikiri unalipa kodi ya mwaka kwa chumba kimoja au ya mwezi kwa nyumba standard. Huwezi linganisha maisha ya mahali ambako hakufanani. Labda tungesema are you better off where you are now or you will or might be better off back home. Uangalie haya maisha unayoishi kwa undani na ambayo utaishi ukiwa Bongo, both social and economical. Au utascrifice na uendelee kunyanyasika nchi ya watu (unless you are in those field they brain drain hutanyanyasika)au utarudi nyumbani.

    Analysis yake ni ngumu kwa sababu kuna vitu vingi vinainfluence maamuzi ya mtu. Ndio maana wengi hapa tunaudhika na kuamua kutoa frustration zetu badala ya kusema yale hasa yanayotusibu na pengine yangewasadia watu wanaofikiri huku maisha ni mteremko. Kwa sababu wengine tunarudije rudije? Hiyo pia ni issue wakati tulishakana sisi sio wabongo?

    Michuzi shem ulifanya uamuzi wa maana kurudi nyumbani mapema, maana hizo opportunities ulizo nazo home Ukerewe usingepata. Wakerewe wenyewe wanalalamika seuze wewe, nani angekuajiri wewe kwenye gazeti kubwa la serikali akamwacha wa kwao? Labda ungeingia jeshini ukaenda kupiga picha Iraq au Afghanistan hapo ungetajirika. Ndio maana kuna mapaparazi baada ya kuona ajira hakuna watu wanatafuta the most sought picture ili aiuze apate pesa ya maana. Wewe hapo unajipigia tu picha unayotaka kwa utashi wako! Wala usijute kama uko nje mbona unaenda sana tu na umeshatembea nchi kibao.
    Maisha ni popote lakini east west home is the best.

    ReplyDelete
  37. KAKA MICHU hapa hakutatokea jibu sahihi au lisilo sahihi wala ushauri wa aina mmoja maana watu tumepata uzoefu tofauti na tunaishi maisha tofauti tofauti na zaidi ya yote uelewa wa neno 'Maisha Mazuri' ni wa tofauti kwa watu mbalimbali. Zaidi ya yote,

    1. Mimi sijui kiwango chako cha elimu,ujuzi,uzoefu na pia vipaji vyako vingine ulivyo navyo au ulivyokuwa navyo ambavyo kwavyo ungeleta ushindaji mzuri katika soko la ajira UK.

    2. Mimi sijui una mahusiano kiasi gani na watu au mashirika mbalimbali na wanakuamini kwa kiasi gani hapo UK ukilinganisha na ulivyo ukiwa Bongo. Maana popote duniani suala la kueleweka au kuaminiwa au urafiki lipo na linaenda sambamba na nondoz zako ulizo nazo.

    3.Hakika sijui kwa unagaubaga maelezo ya majukumu na mazingira ya kazi halisi ya hilo pande ulilopigiwa la kubeba mabox na kunanii vizee (for that is a general terminology) na masilahi na marupurupu yake yalikuaje ukilinganisha na maelezo ya kazi halisi ufanyayo sasa, maslahi na hata marupurupu yake ukiwa Bongo.
    Mfano tu unaweza kufanya kazi ya jina kubwa la Udktari Tz katika mazingira ya hatari ya (kuambukizwa maradhi)kutokana na upungufu wa vitendea kazi na yenye malipo kiduchu kuliko mtoa huduma ya kukata kucha vizee ughaibuni ambaye anavifaa vya kutosha na mshiko wa nguvu! (Ingawa sio kweli kwa kila mtu kila eneo).

    4. Sijui kwako wewe binafsi ni vigezo gani na unavipangaje kwa kufuata umuhimu ambavyo kwavyo unajiridhisha na maana ya dhana hii iitwayo 'Maisha mazuri'.
    Mfano. Kwangu mimi, kuwa na uhuru wa kufanya mambo yangu pasipo kuwepo dhuruma ni kigezo kinachosimama juu sana ya uwezo wa kuwa na fedha nyingi za matumizi. kwa kifupi mimi ni type ya watu wanaoweza kufa na tai shingoni kwa ajili ya utu wangu. Yaani ni mfuasi wa falsafa ya 'kheri kuishi kwa kula konzi moja ya muhogo uitwao 'Imbute' kuliko kula keki na kusaza katika manyanyaso na utumwa'.
    Sasa wapo wengi sana ambao wanatofautiana na hii falsafa na wako sawa kwa uelewa wao na misukumo yao.

    Hata hivyo naomba niwasifu wengi mliotoa ufafanuzi makini na pia mniruhusu kutoa masahihisho kuwa
    si wote tulioko Ughaibuni tuna kazi ya aina moja ya 'kubeba mabox' na wala si kweli kwamba maisha yetu wote yanalingana huku. Mimi naishi Ulaya sasa mwaka wa tisa lakini pia kila mwaka naweza kuja nyumbani na tunawasiliana kwa emails na ninapiga simu si chini ya mara moja kila wiki Nyumbani na kwa marafiki zangu kuliko pengine wengi wetu walioko hapo Dar. 'COWON-I-AUDIO' yangu ina miziki na video za Kibongo ambazo zina hata staili ya 'njiwa' na nyimbo kama Cheupe Sandra n.k ambazo hata waishio Bongo wengi hawajazipata. Ninasoma magazeti yote ya kibongo na kusikiliza taarifa za huko kila siku naamini kuliko wengi sana ambao hata hawanunui magazeti huko Bongo mpaka siku moja rafiki yangu alinambia kuwa naishi Dar na sio Ulaya. Ni wiki jana tu nilikuwa pale Leaders nikishudia Burudani ya wana wa Kutwanga na Kupepeta iyoshuka kidogo ukilinganisha na siku za nyuma. Lakini pia nikiri kuwa matumizi hayo kwangu ni muhimu sana kuliko kujenga nyumba au kufanya biashara ili nipate faida. Hivyo thamani ya mali zangu zisizohamishika ni kiduchu kabisa kuliko matumizi yangu ya kila siku ya kusalimia watu, kujihudhurisha katika matamasha, kutoa michango mbalimbali hususani ya kusomesha Watanzania, kuvaa nadhifu na kushughulikia misosi ya nguvu.Na hayo kwangu ndiyo maisha mazuri ingawa wengine watakuwa na vipaumbele tofauti kabisa.

    Michu, mimi naamini pia kuwa utumishi wa mtu popote si tu habari ya kupata mshahara mkubwa au umaarufu katika jamii bali pia zaidi ni kuridhika na mazingira ya kazi (job satsifaction)ambayo hujumusha pamoja na mambo mengine usalama wa ajira (si tu mtu anaamua kukufukuza simply kwa vile wewe eti umejiunga na chama fulani cha siasa), jinsi mchango wako unavyothaminiwa, upatikanaji wa vitendea kazi vinavyopaswa na utimizaji wa ndoto zako na malengo ya Taasisi n.k
    Hivyo jibu la swali lako lilihitaji kujiuliza maswali hayo ukilinganisha hali yako ya sasa na ambavyo ungekuwa huko Uk, kitu ambacho pia ni vigumu sana maana ni hali ya kufikirika tu maana hatujui kama pengine ungekuwa tayari sasa unafanya kazi pia kwa mwajiri au waajiri wengine kuliko ulivyokuwa umeahidiwa mwanzoni.

    Kuna vikolombwezo vingine kibao vilivyofichika ambavyo navyo huathiri sana utumishi na maisha kwa ujumla navyo ni kama vile eneo unaloishi sasa au ungekuwa unaishi na hata hali yako ya ndoa (kama umeoa au la)na mkeo ana mapendeleo gani na ana nondo au vipawa gani na kama una watoto au la na wao wana mapendeleo gani.
    Mwisho hatujui kama ulikuwa umekaribishwa kufanya kazi kama Mhamiaji halali au asiye halali na kaka muendelezo wa maisha yako hapo UK ulikuwa umepata kibali kwa mujibu wa taratibu za uhamiaji au la.
    Kwangu mimi maisha yanaweza kuwa popote lakini sitamani kuishi isivyo halali popote maisha ya kifisifisi hata kama nita ahidiwa bingo la BBA kila siku!

    Ni mimi Nyakatakule Unyilisha Echalo.

    ReplyDelete
  38. Maisha ni popote tuu jamani inategemea na jinsi gani uanavyoyapangilia, kwani na hata huko bongo si kuna wabeba mabox? lakini si wanaishi tuu,ndiyo mungu amewapangia hivyo wabebe mabox jamani. NA WEWE UNAJIITA US FAN, MWEEE! ETI MAREKANI MAISHA POA KULIKO UKEREWE? HIVI KWELI UPO SERIOUS AU UANLETA JOKE HAPA? MAANA KWA MYUNDERSTANDING KAMA KWELI HUKO UNASOMA BASI HURUHUSIWI KUFANYA KAZI HATA MASAA 21. SASA MAISHA YANAKUWIA VIPI DOLLAR KEMKEM NDUGU YANGU? ACHA UTANI BANA WEEE UNLESS KAMA HUISHI USA KWELI NA HUJAWAHI KUKAA HUO MWAKA MMOJA UK, LKN KAMA NI KWELI UNAYOONGEA BASI UTAKUWA UNAJUA UGUMU WA MAISHA UPO WAPI KATI YA WANAOSOMA USA NA UK. NA KAMA ULIPATA UGUMU WA MAISHA UK BASI LABDA MAKARATASI YALIKUWA HAYAJAKUBALI NDUGU YANGU MAANA NINAVYOELEWA UK KAMA UNA MAKARATASI FRESH HUAPATI SHIDA YEYOTE ILE HATA KAMA HUTAKI KUBEBA BOX BASI UTAKULA NA KULALA TUU. SASA JARIBU KUWA MKWELI NDUGU YANGU SIYO UNAKANDIA TUU ILI KUJAZA NAFASI HAPA.

    ReplyDelete
  39. nov 21 8;37 kweli maisha potepote lakini kuhusu kufanya kazi ukiwa dent usa ....hiyo ni kwenye f-1 tu watu wanapiga kazi za maana tu masaa 60 kwa week na tax wanafile.

    mimi sio mwanafunzi tena nakaa na niece wabgu na anafanya kazi vizuri tu.

    Nimeenda UK this summer (london, reading, bristol, Leed na mji mwingine upo north sana).....bwana tusidanganyane life ni tofauti sana katika hizi nchi mbili...mtu asikwambie kitu mpaka ukanyage hizi nchi mbili uone tofauti...

    Maisha ya UK ni magumu sana tu...

    Michuzi kama ungewahi ...enzi hizo ungefanikiwa lakini sasa hivi ukijifanya kuhamia nchi nyingine ..itakua vigumu sana.

    Ni vizuri kuja nchi za nje bado kijana utu uzima haifai kabisa..ni kupoteza muda tu na kujiengezea pressure kwa vile kama huji na kela ya kuanzisha maisha yako kazi utakazoanza nazo ndio hizo mnaziita kubeba mabox kweli utaweza na umri huu

    Niliona Mtu mmoja aliwin green card akaja huku ...haikuchukua muda aliisahau na hiyo card akajirudia bongo...

    Maisha ni magumu kila mahali na ni jinsi gani wewe unavyopambana nayo ndio jibu..

    ReplyDelete
  40. Michuzi !

    Jinsi ulivyouliza swali lako inaonyesha ni jinsi gani ujaelimika . Pili mentality kama hizo ndio vitu vinavyofanya nchi yetu iendelee kuwa maskini . Kusema kuwa kubeba maboksi na kunanini vibibi ni kebehi za hali ya juu zenye nia ya kudharau kazi za watu. The issue sio kuwa unafanya kazi gani bali ni una benefit nini kutoka kwenye hizo kazi . Hizi nchi za magharibi zinaendelea kwa sababu watu wana heshimu watu regardless wanafanya kazi gani !

    Michuzi ,GOD forbid majambazi wakikuingilia nyumbani kwako usiku utapiga simu gani kupata msaada ? au bahati mbaya ukipata ajali mbaya ya gari utapiga simu gani kwa ajili ya huduma ya kwanza ? Mind you watu wengi sana bongo wanakufa kwa ajili ya kukosa huduma ya kwanza haiwezekani mtu asafirishwe na pickup halafu uexpect kupona . Hivi vitu vyote ni muhimu mtu kuangalia kabla ya kukurupuka na kusema bongo tambarare.

    Hivi michuzi achilia mbali maendeleo yetu binafsi , vipi kuhusu watoto wetu . Hapa Marekani nina uhakika wa mtoto wangu kupata elimu bora , na kama nikitaka mtoto wangu kuwa MD, Pharmacist au Lawayer ninaweza kufanya hivyo ...vipi kuhusu wewe michuzi ? Pia vipi kuhusu uwezo wao wa kuchanganua mambo ?

    Mimi nilianza kazi ya kusafisha vibibi sasa hivi mimi ni RN , I am not braggin hela ninayo make kwa mwaka hakuna waziri yoyote hapo bongo anaweza kumake ! Mambo niliofanya katika miaka mitatu watu wengi wa bongo hawataweza kuyafanya , pia hata nikiretire benefit zangu zitaniowezesha kuishi maisha bora popote duniani.

    ReplyDelete
  41. Wabongo wacheni uvivu, mimi ninavujua huku immigrants wengi wanapoanza kutafuta maisha wanaanza na kazi chini lakini muda kadiri unavoenda ndio wanapanda kwa kuchukua kazi nzuri zaidi na watoto wao mbao wanazaliwa huku wanakuwa teyari wameshakwisha funguliwa maisha tambarare pindi wanapopata manondo yao.

    Nyinyi wabongo mliopo Tanzania msifiri kupiga box ni sawa na kubeba mabox kibongo kwa kutumia mgongo kwani hilo haliluhusiwi huku
    hiyo ni safety hazard, watu tunaowaita wanapiga box ni wale wanaofanya kazi katika ma-supermarkets kwani hapo kuna kazi ya kutoa na kupanga bidhaa.
    Vilevile hizi ni kazi ambazo ndizo Wamerikani wengi wameajiriwa. Na vijana wao wasomi na watu walio-staafu ndizo wanafanya. Kwahiyo hapa marekani watu hawadharau kazi ya mtu kwani hata Boss huku ndiko alipotokea. Kwani hapa watu wanafanya kazi za box na kupiga shule.

    Mimi binafsi yangu nilikuja Uingereza na nikaishi mwaka mmoja mji wa READING nilifanya kazi HAYS kwa wale watu wa Reading wanaifahamu HAYS. Nililipa kodi kama kawaida na nikahifadhi pesa yangu kwa vile nilishawai kuja Amerika kabla ya kwenda Uingereza nilikuwa najua tofauti kubwa kati ya Amerika na Uingereza, kwani mfumo wa muingereza ni mgumu sana kwa wewe kuweza kufanya kazi na kwenda shule, kwahiyo nikaondoka na kuja Amerika ambapo kazi yangu ya kwanza ni kuuza "gas - station" kuanzia saa 4 usiku mpaka 12 asubuhi baadaye kwenda darasani , saa 3 asubuhi mpaka 10 jioni. nilifanya kazi hii siku 4 kwa week. Nilikuwa na fedha ya kukudhi mahitaji yangu vizuri tu na gari langu la kwenda sehemu yoyote. Pindi nilipomaliza shule mambo yakawa tambarare, sasa nina jumba, gari- SUV, nasomesha wadogo zangu bongo,mmoja amemaliza form 4 anasubiri matokeo, mwingine anaingia form 4, mwingine amefanya mitihani ya form 2 anasubiri matokeo, na mpwa wangu yatima yuko form 1 anaenda form2. Bongo nimemaliza kujenga mansion, na nimenunua mashamba yenye ardhi nzuri sana na vilevile hapa nina (401K).

    Sasa mimi sioni ni lipi baya kama mtu anapiga box( Anafanyakazi - Wal Mart, Publix, Krogger, Home Depot, Office Depot) Haya ni makampuni makubwa sana hapa amerika na ukijiendeleza utafika mbali sana. Na kwa wabongo huko nyumbani jaribuni kuwa wadadisi sio kuropoka ropoka , ndiyo maana watu wengi hawaandiki humu kwasababu wanaona inakuwa ni kupoteza muda kujaribu kuwaelimisha watu wasiokuwa wadadisi wanaojifanya tayari wanajua kuliko sisi tuiokuwa huku,

    lingine ni lazima tusaidie wazee wetu ndipo tunapata baraka tukiwa huku, kwani wazee wanaposhukuru kwa kidogo tunachowapa Mwenyezi Mungu anatuzidishia baraka zake kwetu.

    Mdau
    USA.

    ReplyDelete
  42. I don't mean to disrespect you Mr Michuzi or anyone but for the benefit of this forum, it would be so nice if you could tell us what sort of qualification you had acquired during that time (I mean 1991). I'm sure you didn't receive any "serious" "NONDO" from a know Uni or college!....prove me wrong!

    You keep saying "Tujinondo" but unfortunately you didn't mentioned what area of expertise your studies was!...I guess, if it was something "serious" by then, you could have stayed and worked in one of the blue chip companies in UK!...but because, there is nothing serious from you, neither majority of people back home, then you have chosen to use your forum as a bridge to insult people in a very systematic way! The people who contribute a lot to the economy back home! the people who don't take or receive pribe! The people who host you when you come to UK or anywhere alike!

    Last thing but not least, I would like to tell all people who comment in this blog that your minds work like an umbrella, so if you don't open it, it won't work!...time has come for all commententors and blog owners to clean their acts and starting to act like postive thinking creatures!

    ReplyDelete
  43. Michuzi umenisikitisha ...Thanksgiving yangu nitakuwaza wewe tu...yaani kurembea kote huko nchu za nje bado mind yako low hivi kama mtu ambaye hajatoka nje ya nchi bwana? Kazi ni kazi bora mkono uingie kinywani

    hao wanaokufadhili ukiwa nje ya nchi si wanafanya kazi hizo hizo kila siku ni majineno...Ni hasira wivu au unayako rohoni?

    ...ni ni unachotambia hapo bongo..? I don't see for real..Kama life ndio hiyo unaona umemaliza basi ni kwa vile hamna competition wewe ni kiboba wao..Ungekaa nje ujue maendeleo nini?


    Watu naona wanaandika so much kukupa ukweli lakini bado wewe na wa bongo ambao brain zime freeze ni kupoteza muda

    Basi kwa information yako unavyofanya kazi hivyo ungekua nje ungekua 10 times better..Nyumbani ni nyumbani lakini ukweli upo

    ReplyDelete
  44. Maisha ni popote tuu jamani inategemea na jinsi gani uanavyoyapangilia, kwani na hata huko bongo si kuna wabeba mabox? lakini si wanaishi tuu,ndiyo mungu amewapangia hivyo wabebe mabox jamani. NA WEWE UNAJIITA US FAN, MWEEE! ETI MAREKANI MAISHA POA KULIKO UKEREWE? HIVI KWELI UPO SERIOUS AU UANLETA JOKE HAPA? MAANA KWA MYUNDERSTANDING KAMA KWELI HUKO UNASOMA BASI HURUHUSIWI KUFANYA KAZI HATA MASAA 21. SASA MAISHA YANAKUWIA VIPI DOLLAR KEMKEM NDUGU YANGU? ACHA UTANI BANA WEEE UNLESS KAMA HUISHI USA KWELI NA HUJAWAHI KUKAA HUO MWAKA MMOJA UK, LKN KAMA NI KWELI UNAYOONGEA BASI UTAKUWA UNAJUA UGUMU WA MAISHA UPO WAPI KATI YA WANAOSOMA USA NA UK. NA KAMA ULIPATA UGUMU WA MAISHA UK BASI LABDA MAKARATASI YALIKUWA HAYAJAKUBALI NDUGU YANGU MAANA NINAVYOELEWA UK KAMA UNA MAKARATASI FRESH HUAPATI SHIDA YEYOTE ILE HATA KAMA HUTAKI KUBEBA BOX BASI UTAKULA NA KULALA TUU. SASA JARIBU KUWA MKWELI NDUGU YANGU SIYO UNAKANDIA TUU ILI KUJAZA NAFASI. Michuzi utakuja kufilwa bila ya mate

    ReplyDelete
  45. Mmh OPRA wa Bongo huyo
    Mbona unawaponda sana jamaa wa majuu lakini ulivyoanzisha blogu ndio ulikua unakula nao futari? Hukujua wanaosha vizeee?

    ReplyDelete
  46. Waungwana comments hizi zinaonekana na watu wengi hapa!ila tu kwa kuongozea miye binafsi nimependezwa sana na jinsi mchangiaji Nyakatakule Elisha alivochanganua mambo!
    amejitahidi kwa ustadi mkubwa kuelezea scope ya mambo yalivo!
    keep it up mate!
    pia wapo wachangiaji wengine wameelezea vitu vya maana sana na kwa upeo wa kisomi hasa!nao pia hongera.
    KUULIZA si ujinga jamani!baada ya baadhi ya wachangiaji kuleta comparison baina ya UK na America nimejikuta nikiingiwa na shauku ya kutaka kujua zaidi kupi ni better kati ya Amerika na UK.
    NB:Miye sipo Tanzania wala UK wala America isipokuwa nimewahi kukaa UK kwa muda na nayajua maisha ya UK kiasi japo sio sana.

    ReplyDelete
  47. KWA ANONY: KHSU US/UK
    wE ACHANA NA MICHUZI ATAKUPOTOSHA.mi nipo hapa Bongo.Kwa taarifa nilizonazo na ushahidi wa jamaa zetu wa karibu bora uende UK.Kwani pananafuu ya maisha na unaweza kuwa na maendeleo nyumbani.Watu wanaosema UK maisha ni magumu sana niwale wasio kuwa na makaratasi.Lakini US nikama mbuga kama hujatoka kwenye famiilia inayoeleweka hutarudi nyumbani utaishia tu kula CORNFLAKES KWA MAZIWA,huwa wakirudi ni moja kwamoja tofauti ni hawa jamaa wa UK ambao likizo huonekana hapa bongo kwa wingi.Ila kitu muhimu ni juhudi binafsi hakuna maisha rahisi Duniani popote pale hata huko wapo waliofanikisha japokuwa wanahesabika ila si kwakubebwa kama michuzi.

    ReplyDelete
  48. Suala sio kuishi Marekani au uingereza , hoja hapa ni kujibu swali la michuzi ambalo lilikuwa limejaa kebehi . Lakini kukujibu swali la sina makosa kwa nini watu wa uingereza wanaonekana mara nyingi bongo nadhani ni umbali , uingereza kuko karibu na bongo .

    Michuzi , nadhani umezungukwa na watanzania wengi walioshindwa maisha ya huku ughaibuni sasa wanaishia kukandia tuu . Ughaibuni hakutaki watu lelemama wala misheni tauni kwani utakwenda jela . Badala ya kujilaumu wenyewe wanaishia kutafuta scap goat. Michuzi nataka nikuulize swali ni kitu gani ambacho umeachive ambacho unahisi mtu aliyeko ughaibuni hawezi kukifanya .

    Mwisho , nakuomba siku nyingine uwe makini na jinsi unavyopost maswali yako na utumie lugha ya kistaarabu na sio ya kejeli , kazi ni kazi bora mkono uende kinywani ! Ni lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu kazi za watu kwani kila mtu akiwa meneja nani atafagia barabara ? Michuzi , you owe sisi wasafisha vibibi an apology .

    ReplyDelete
  49. Kazi ni kazi mbona wewe ni mpiga picha tuu. Ina maana hukuona kazi zingine mpaka ukaamua uwe mpiga picha. Kwanza naamini ulipoanza ulikuwa unajishikiza tu. Lakini kutokana na pande za hapa na pale ikabidi uendelee nayo mpaka leo.

    ReplyDelete
  50. Ungekaa UK usingekua na tabia ya kudharau watu kutokana na shughuli wanayofanya maishani mwao. Unarub shoulders na mastaa wa Bongo unafikiri ndio mwisho?

    ReplyDelete
  51. atizo la michuzi ni ushamba.mie namfahamu long time toka anapiga picha za kuendeshea maisha pale Maggot(Ushirika club),Ymca na mbowe na yeye wakati huo anaishi nyumba ya kupanga Kipawa.Huna jipya.sasa hivi umeupata mtandao unawaponda watu wa ughaibuni ikija wakati wa kupiga kura wa kwanza kutuomba sisi.
    CHA CHANDU

    ReplyDelete
  52. Michuzi na wengine wote... maisha ni kuchagua. At the end of the day ni kufuatana na determination, persistency and satisfaction.Ubishi kuhusu bongo na overseaa!! How funn!! What about bros and sisters ambao hata kwa mbinde ukiwaleta Dar bado watarudi vijijini ?? Ok wapo watakabaki na kufaiti Dar baada ya kutoka mbwinde, na wengine kutokana na bidii zao , matunda yake huonekana. Huu ni mfano halisi between bongo na overseas. You get what you put in bro regardless where you are. We normally impose our own limit. Things are possible if you want them badly enough. Mimi siko ukerewe wala US, nipo another part of the world, nikmeona nitoe mchango wangu. Kwanza kama wengine walivyosema, ni lazima tuheshimiane bila kujali kazi, pesa au cheo (inaniudhi sana hii) mimi sasa hivi ni meneja na wazungu wanaripoti kwangu, ninapania kuwa mkurugenzi in next three years. Lakini naheshimu watu wote na nikigundua kuwa mtu atanataka kuwa rafiki yangu wakati anawakandia wengine, urafiki umekwisha. I believe you guys you can succeed in your life in whateever you want and enjoy plus where you enjoy to be either ukerewe, US, bongo, Tunduru, Nyarugusu. In addition, please respect people choices. I respect bro and sisters wnao amua kurudi bongo, wana sbabu zao, that is where they feel comfortable, na wale tunaobaki overseas tuna feel comfortable. If you are not comfortable, it is time to change before it is too late either rudi or ondoka bongo!!! And when you settle, work your ass off!! Bill Clinton said " If you don't try there is gurantee to fail. If you try there is no gurantee to succeed" It is your choice. Final note kwa wale wanaoamua kubaki overseas, turn youself to be fighter, don't let rangi yako iwe victims.... it is mind game. Baraka Obama is now a US president .. You do not have to be a president .. unaweza kushinda hata katika kubeba maboksi, ama ukawa bosi wa vindapa or other opportunity zikajiseti.. lakini you have to work hard.. Good luck to all of you in everything you do

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...