mdau, ungekuwa jk ungewafanya nini hawa maafisa wa mipango miji kama hawa wa dar?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Maisha tambarare.JK afanye nini???Unalalamika nini??Na ulisema Bongo maisha tambarare??

    ReplyDelete
  2. HAPA WAPI?

    ReplyDelete
  3. michu mimi swali langu huwa ni moja tu!hivi hiki chuo tunakiita chuo kikuu cha ardhi,zamani UCLAS graduates wake huwa wanaenda wapi?kuna watu wanajiita mipango miji, hivi hawa kazi zao kuanzia asubuhi mpaka jioni, jumatatu mpaka ijumaa, tarehe moja mpaka thelathini, mwanzoni mwa mwaka mpaka desemba,kuanzia nchi hii ipate uhuru mpaka leo, huwa wanafanya nini hawa?wana kazi yoyote au ni kuuza chai tu?mimi nikisikia ndugu yangu kapata nafasi akasome uclas namshauri aachane na huo ujinga kabisa.ni tofauti sana na vyuo vingine kama ifm, cbe, udsm(bcom na koz zingine chache ambazo si kasa) na Muhimbili na iaa na tia na vyuo vingine vingine ambavyo elimu yao huonesha matunda directly, lakini kwa kweli hawa watu wa ardhi ni hovyo kabisa, aibu, kama mimi ningekuwa nafanya kazi huko wala nisingekuwa nasema, ningezuga mishen town tu, wanafanya nini?labda mama rita na magufuli wanawaaamsha kidogo sasa, mjini kabisa magomeni hapo hakuna ramani, njoo huku kinondoni ukishatoka tu makaburini vichochoro vimeanza, yaani shame upon you!ukienda arusha ndo ngarenaro ambapo ni mjini kabisa baada tu ya shoprite vichochoro,sanawari kote hopeless, mwanza ukitoka tu mjini hapo mabatini ni aibu!vichochoro, mimi ninachoshauri basi kama kuanza kufidia ni ngumu japo haya maeneo mapya yanayoanza kujengwaa si muyape ramani?mji kama arusha ndo kwanza unakua mwanza na hata dar, ila bado watu wanajenga bila ramani, si makosa yao ni makosa ya waliosomeshwa na kujiita wataalam huku utaalam wao ukiishia kutafuta tu mazingira ya kula rushwa badala ya kuisaidia nchi, shame upon you guys, nawahurumia sana, au hampewi nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru?hakuna town plan kabisa hata kwenye miji midogo inayokua kwa kasi kama kibaha, wachoreeni ramani ya mji iwepo kwenye ofisi za vitongoji mtu akitaka kujenga akaangalie kwanza kwenye ofisi ya kata je?anajenga sehem itakayokuja kuwa shule au barabara au eneo la akiba ya barabara au anything, kwa wale wenzangu mliowahi kusafiri katika nchi zilizoendelea mnaelewa nazungumzia nini, hata vijijini kuna ramani, mnashindwa na vijiji kama marangu kilimanjaro ambapo kuna mipangilio sahihi ya maeneo na mashamba, wake up guys and lets build our beloved country!kiongozi wa makazi wa un prof tibaijuka tunae hapa ila nae mama sijaona katusaidiaje kupata japo wataalam( consultants) wawape semina elekezi hawa vilaza wa ardhi, wamelaaaaala hakuna lolote!kwani kama kungekuwa na ramani nzuri hata kungelikuwa na shida ya foleni?hakuna maana alternative ways si zingekuwa kibao?ona pale kijitonyama makumbusho walau kuna kampangilio ktk tanzania hii makumbusho mbali na kwa vigogo maosterbay na masaki, kunakuwa na alternative ways za watu kuja mjini through mwananyamala to kinondoni ingekuwa hivo mji mzima i mean tanzania nzima, samahani nimeandika hii comment kwa hasira sana watu wengine wanalipwa bure tu, wavivu sijui au ni kubanwa na ''vigogo'' kutokuwa creative au hata sijui ni nini, mimi sijasoma mipango miji lakini hata wangeniambia mimi nipange mji mdogo kama same, himo makete au popote pale i could drop ideas, sasa nyie mpaka mna chuo kikuu cha ardhi halafu aiiiiibu, juzi juzi et wanachuo wa ardhi wanahesabu magari ali hasan mwinyi, nikaona hii nayo zuga!!ili nini kama si mkwaara tu?hamjaanza kupima huko yanapoenda mnaanza huku kwenye magorofa yanapotokea?ambapo possibiliti ya kuwalipa ndo hakuna kabisa!wake up tanzania fanyeni kazi inayoonekana acheni longolongo na ufisadi kila mahali nchi ni yetu sote fanyeni kitu cha kudumu vizazi na vizazi, nina imani sana na magufuli, na lowasa ni mtu wa vision i hope watajitahidi.thanks michu kutupa mahala pa kutoa maoni.Pj

    ReplyDelete
  4. utumbo mtupu watu wa mipango miji tanzania!

    ReplyDelete
  5. ningekuwa JK ningewapa challenge ya kuplan new town just outside dar....coz now its too little too late to make dar a better place

    ReplyDelete
  6. ningekuwa JK hawa jamaa sio tu kuwafukuza kazi na kuwasweka ndani kwa muda usiojulikana

    ReplyDelete
  7. Toa executive order timua wote na weka timu ya mipango. Kumbuka Mkapa alivyotimua wote halmashauri ya jiji na kuunda tume ya Keenja? Hivyo ndio inavyotakiwa na hawa wala rushwa wizara ya ardhi na maafisa mipango ya miji

    ReplyDelete
  8. Ningewapa uwaziri kabisaaa ili walingane na mawaziri wengine. Pia ningewapa nyongeza ya mishahara kwa kazi nzuri wanayoifanya.

    ReplyDelete
  9. It is true too little too late.

    Jenga mji mwingine pembeni. Huu mji hauna ramani kabisa. Just look hayo majumba ya matofali kweli ukianza bomoa bomoa ili upate ramani si miaka arobaini itapita hapo.

    Nenda Google map uone jinsi tuna eneo kubwa tu empty nje kidogo ya Dar. Kote kote kasoro upande wa bahari tu.

    Ila wanavyozidi kustreatch nje ya mji bila ramani ndio hivyo tena kesho mile 50 radius nje ya Dar yote itakua hamna ramani tu kama hiyo. Si walianza hivyo hivyo?

    Hamna sehemu zinazohifadhiwa kwa vitu muhimu kama Shule, hospital, vituo vya polisi, zimamoto etc ...kote viwanja vinapimwa na kuuzwa tu vya njumba za kuishi, hotel na bar tu...Sijui hawafikiri kuna maisha zaidi ya nyumba za kuishi, bar na hotel????

    Ila kwa sisi wabongo once ukishapata pa kulala, pa kula na kuserebuka basi life ni tambarare...Tumesafika na kuridhika

    ReplyDelete
  10. Nakubaliana kwamba Dar wanaweza kuanzisha ujenzi pembeni ya mji. Hii imeshaanza kule Bunju. Kule kuna ramani zake na viwanja vyote vimepimwa. Tatizo watu wanang'ang'ania kukaa sehemu walizo zizoea. Bunju kuzuri, hakuna msongamano.

    ReplyDelete
  11. UNAJUA UKIISHI NJE NDIO UNAONA KUWA BONGO TUNA MATATIZO MAKUBWA! FOLENI HIZO ZINATESA WATU KILA SIKU NA ZINADUMAZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI..ILA AAH, KIMYA, KUANZIA JK MPAKA MICHUZI MAMBO TAMBARARE TU!

    ReplyDelete
  12. Kwa Dar is TOO LATE!

    Hakuna kujenga nje yake, kwani Dar ndio mji peke yake katika Tanzania!

    Tawanya wizara katika miji mingine ya Tanzania, kama nilivyopendekeza hapo awali. Nitarudia kwa kifupi:

    Lakini tuendeleze miji mingineyo kwa kuhamisha wizara fulani kutoka Dar es Salaam. Kila mwaka tuhamishe kundi moja la wizara. Baada ya miaka kama kumi hivi, Tanzania itakuwa imebadilika sana!

    Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu. Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:

    Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.

    Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa ili viwe karibu na Bunge “tukufu”.

    Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Sheria (Katiba na Utawala Bora); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.

    Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Rwanda, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi. Mwanza iwe senta ya madini.

    Kigoma: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki, Burundi na hata Rwanda.

    Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko). Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama senta ya huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” – kwa ajili ya Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini. “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake! Mtwara iwe senta ya gesi.

    Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwanja wa ndege wa kimatiafa unaendelea kujengwa mjini Mbeya. Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini, ikiwa ni pamoja na kuinua hali ya utalii kwa mikoa hiyo ya kusini.

    Miji hiyo iwe na wizara ambazo nimeziunganisha. Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.

    ReplyDelete
  13. mfumo wa kuoneana aibu haukuwepo wakati wa utawala wa JK Nyerere. ni mfumo mbaya sana ambao hauwajibishi mtu. hii ni kwa sababu mwenye dhambi hawezi kumwadhibu mwenye dhambi mwenzake (he who goes to equity must go with clean hands). hii ndo inayosababisha miji iwe ya ajabu.

    ni kweli UCLAS wamelala na visomo vyao au hawafundishwi ubunifu. lakini mbona hata sokoine hatuoni wataalamu wa kilimo wanachofanya. mbona hata MOI wanafanya yale yale au hao wamesomea kwa docta Kairuki. kwa ujumla kuna kila sababu ya wanataaluma kuonyesha taaluma yenu.

    mimi ningekuwa JK Mrisho ningeua wote ili nitafute wengine ambao hawatakuwa spoiled na waliopo.

    ReplyDelete
  14. yaani we untaka kunihamishia mtwara hufai kabisa yaani mimi waziri kabisa nikakae mtwara? we born again taratibu usiwachokoze wenye nchi lol, kumbuka sisi ni wananchi na wao ni wenye nchi, kwa mujibu wa mawazo yao

    ReplyDelete
  15. This is Chaos ningekuwa JK ningekifunga chuo cha ardhi Milele..!! Hao wasomi wa Ardhi hawana upeo (exposure) wameshaona wapi mambo mazuri? Na hata wanapofundishwa darasani sasa wanapatia wapi mifano? How do they do their practicals kama hakuna mahali palipopangika? Chaos Chaos Chaos...halafu watu wakirudi kutoka nje ya nchi mnawapiga vita..kwavile watawazibia kula yenu...ngoja nikabebe mabox yangu...!!Nafikiri kuna haja ya kuwa na more practicals badala ya kukariri ma-formula tu...!! Chuo Cha Ardhi kifungwe..kupoteza tu pesa za serikali...!!

    ReplyDelete
  16. sijawahi kwenda chuo cha ardhi wala sina ndugu anaesoma pale, msaada,hivi hapo ardhi kuna maprofesa?kama wapo nawaomba mjiuzulu, uprofesa wa nini sasa?au wa kuandika research pepa na kuzikalia?heri hao wizara ya ardhi wao inaeleweka ni vilaza na waliopo wengi ila si wote ni wafuasi wa hela,na wale ambao si wafuasi wa hela wengi wao wanapigwa vita sana, naamini hivyo, ndio maana wanashindwa kuwajibika, na katikati ya mafisadi ni ngumu sana kuwa mtenda haki, ila utakuta ni mijifisadi flani michache kama mitatu hivi au minne ikitolewa tu kwenye oganaizesheni!mambo mswano, hapa sisemi jk,nasema magufuli,jaribu kuwaidentify hao mafisadi machache ardhi uyatupilie wizara ya mifugo ofisi ndogo simanjiroooooo!mjini wakae watu wenye akili za kimjinimjini.UCLAS NA WIZARA YA ARDHI KWA SASA IPO USINGIZI FO FO FO, HAKUNA KAZI WANAFANYA!SIASA TU!LABDA MAGUFULI NA WENZAKE WACHACHE NDO WANAFANYA KAZI, TANZANIA NZIMA, SHAME UPON ARDHI&UCLAS.PJ

    ReplyDelete
  17. Michuzi, Ahsante kwa picha hii. Inaonyesha jinsi gani nawe unachukizwa na vitu vingine hapa nchini mwetu, ambavyo havigharimu pesa nyingi lakini visipofikiriwa mapema na kutekelezwa, ndiyo tunaishia kugharimika maradufu.

    Kweli semina endelezi uliyoifanya hivi karibuni kule Ngurdoto imekuingia ipasavyo. Kwenye hii picha umeamsha hisia za wengi kwa kumtaja JK mwenyewe, kwani ndiye baba wa nyumba na anatakiwa apewe lawama na sifa zote za mwisho zitokeazo nyumbani mwake.

    Michango na maelezo yaliyotolewa na Anon wote na Born Again Pagan ni ya muhimu na inaonesha kero za wananchi walio ndani na nje ya nchi yao jinsi wasivyopendezwa na mandhari inayotawala maeneo mengi ya nchi yetu. Nchi nzima haina hata mji mmoja unaoonekana kupangwa kitaalam kwa asilimia 100 za mraba wake.

    Inashangaza kuona viongozi wenye Stashahada, Shahada na Vyeti mbali mbali vinavyoashiria ujuzi, lakini la kutia aibu ni kuwa ujuzi huo hauwekewi vitendo.

    Michu asante kwa picha. Kama jinsi unavyotuletea picha za furaha, naomba ukazane kutuletea picha kama hizi pia na zile za mashimozzz kutuonesha taswira ya nchi yetu katika utendaji wa wananchi, viongozi na mandhari yake!!

    SteveD.

    ReplyDelete
  18. Jji la Dar es salaam kweli limepangwa vibaya na hata kulinzi liko hovyo.

    Yaani watu wote jiji nzima wanaelekea katikati ya jiji kufanya kazi!!!! Asilimia zaidi ya 90 ya wafanyakazi wote wa Dar es salaam wako eneo dogo la kazi ambalo liko City Centre Kuanzia Raisi wa nchi hadi kibarua kuli wa bandarini.

    Yaani Mungu apishe mbali jiji hili likitwangwa bomu kutakuwa na kilio nchi nzima maana jiji hili lina watu toka mikoa yote Tanzania na wengi wao wanafanya kazi City Centre.Sasa likitokea la kutokea City Centre mbona itakuwa kasheshe!! WATU MBONA TUTAJAMBA CHECHE

    Watu wa mipango miji pangeni mambo vizuri.Hebu fikiri jiji nzima lina barabara 4 tu za kuingilia jijini MOROGORO,BAGAMOYO,PUGU,NA KILWA ROAD TU.Hizo ndizo kukitokea patashika nguo kuchanika ndizo watu wanazitegemea! Hata kutoroka jiji wakiona wamezidiwa!!!!!

    ReplyDelete
  19. Anony achia mbali jiji likipigwa bomu. Angalia nyumba zikiwaka moto zinavyoteketea. Na nyumba zetu ni za matofali. Je zingekua za mbao kama za hawa wenzetu ingekuaje?

    Nyumba ikiungua mpaka gari moshi lijue ni wapi ni masaa manne, litafute jinsi ya kufika hapo ni masaa mengine manne. Likifika kwa vile hamna fire hydrants kama gari lilikimbilia kuzima moto likasahau maji basi add two more hours.

    Tunahitaji ramani, tunahitaji kuallocate maofisi mengine nje ya mji, tunahitaji kuwa na sheria na wanaozivunja watiwe hatiani. Kama mtu ananunua kiwanja mahali hapakuruhusiwa wachukuliwe sheria wote anayenunua na anayeuza.

    ReplyDelete
  20. Unauliza wapi? hapo kipawa mwanangu

    ReplyDelete
  21. TATIZO LA TANZANIA: WENYE UWEZO NA KISOMO[HATA HICHO KISOMO(KIDODO,NA UNEXPOSED) CHA UCLAS] WANAWEKWA BENCH......SERIKALI INATOA 'POLITICAL' DECISIONS NA TECHNICAL ISSUES ZINAWEKWA PEMBENI KWA AJILI YA MASLAHI BINAFSI YA KISIASA, KAMA VILE KUTOBOMOA SQUATTER KWA AJILI YA KUTOPOTEZA KURA.MNAKUMBUKA SAKATA LA MSIMBAZUI NA MBUNGE FULANI ALIVYOTETEA?MASTERPLAN YA MKOLONI IPO KAMA SISI TUMESHINDWA KUTENGENEZA YETU.HATA HUKO BUM\JNU UPUUZI MTUPU, NO COMMERCIAL CENTRE, NO ADMINISTRATIVE CENTRE, NA JE NI LINI SERIKALI ITAWEKA MIUNDOMBINU??LAND RENT WANATEMBELEA MA VX TU.HATA HUYO MAGUFULI HANA MPANGO, ANGALIENI ALIKOTOKA BARABARA ZIMESHACHOKA[MWANZA NZEGA] HATA MWAKA 2 BADO!THE GOVERNMENT INAAKIWA KUTUMIA TECHNICAL PEOPLE SIO STUPID POLITICIANS

    ReplyDelete
  22. Nashukuru Michuzi umeweza kuona hali hii mbaya ya mpangilio wa jiji, tuna safari ndefu, utafikiri inchi imelaaniwa kwa sababu vitu amabavyo ni wazi watawala wanajifankuwa vya hawavioni kwani wao ndio wanaopaa kila kukicha kujaa huku Amerika au Ulaya na wanaona miji na vijiji vyote vilivyopangiliwa huku na wanaliona jiji na miji ya bongo ilivyokuwa vurugu mechi, lakini wanauchuna, mmmm nchi ya vichaa, kwa sababu ukitaka kujua mtu anavyoendesha mambo yake tazama kama jamaa anampangilio sehemu anayoishi, kama ukikuta mataulo yapo jiko badala ya bafuni basi hata akiwa ana PHD sita ujue unajihusisha na mwendawazimu.

    Haigharimu mapesa mengi kuwa na mpangilio unaoeleweka , lakini kutokuwa na mpangilio kutawagharimu sana. kwani inakuwa vigumu kuingiza miundombinu ya kisasa sehemu zilizojengwa ovyo ovyo, nazungumzia mawaya ya fiber optics cables, na matekenolojia mengine ya kisasa.na misongamano ya barabarani isiyokuwa ya kweli (artificial traffic jams).

    Inabidi michuzi uwaweke wazi hizi picha watawala wa nchi, kwani ni aibu kwa taifa la karne ya 21 kuonekana kama jalala.

    Na nyie wabongo ambao hamjatoka nje msiwe wapumbavu kufikiri kwamba wabongo waliojuu hawaijali Tanzania, 100% ya wabongo walio-juu
    wanaipenda nchi lakini jinsi wanavyoona nchi inaendeshwa bila ya sheria inaumaa sana kwani wanaona jinsi nchi za wenzetu zinavyoendeshwa kwa kila sheria waliyojitungia. Na watu wasiofuata wanapata kibano sawasawa. Wakati kwetu kila kitu ni upuuzi( everything in Tanzania is just a joke). Tuache wivu wa kijinga wakati watu waliojuu walioona zaidi wakikosoa ujinga unaoendelea bila ya kupewa dawa chungu inayostahili.

    Ndimi Mdau

    from the land of braves,hawks and falcons the dirty birds.
    Atlanta, Georgia- USA.

    ReplyDelete
  23. habari kaka michuzi.
    nimefurahishwa sana na aliyeweka picha hii,na kusikitiswa sana na ndugu anayejiita pj kulaumu chuo cha ardhi.
    ukweli halisi miji yetu haina mipango endelevu, wataalaam tumewaachia wanasiasa wanavuruga nchi,swala la kutokuwa na miji inayoeleweka si la maprofesa ardhi tu ni la watanzania wote, je bwana pj hujanunua kiwanja kisichopimwa,na we si mmoja wa wale wanaonunua ramani posta? ni watanzania wangapi wanawatumia wataalamu au ukienda kwa rafiki yako ukiona nyumba nzuri nawe unataka hiyo ukajenge kwenye kiwanja chako?tena bila ushauri wowote.watanzania kama tunanunua ramani ya tsh 3000 posta mpya unategemea nini?, professa wa chuo cha ardhi ndiye kakutuma?swala la miji mibovu kwa wadau wa fani husika linatofauti gani na rushwa inayo-ua nchi (wanasheria hawakusoma ardhi),je wahasibu/bankers wasiokuwa na huruma kusaini documents za uongo/mikataba feki(hawa hawakusoma ardhi.Ni wapi watanzania tuna mafanikio,waalimu upe-elimu inadidimia,uzembe sector ya afya,uliza mwananyamala Hospital wanakufa wangapi kwa uzembe, barabara zinazoharibika miezi sita baada ya kuisha -engineer amekula fungu na wanasiasa,gharama za ujenzi bot-wahasibu/washeria

    mwisho naitimisha kwa kusema watanzania kila mtu na fani yake awe mwadilifu na tusiwaache wanasiasa kuharibu nchi yetu.

    uliza manispaa nguvu ya diwani kutoa maamuzi ya vibali vya ujenzi.

    jk hana la kufanya ni wewe mtanzania umefanya nini kuakikisha kuwa mji wako unajengeka kutumia watalamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...