WADAU MLIOWEZA KUTABIRI KWA USAHIHI MATOKEO YA MECHI KATI YA ARSENAL NA MANCHESTER UNITED WIKI ILOPITA MSIONE KIMYA NA WALA MSIKONDE, ZAWADI IPO NA ITATOLEWA TU.
SABABU YA KUTOCHEZESHWA DROO YA KUMPATA MSHINDI MMOJA ATAKAYENYAKUA $500 HADI SASA NI KWAMBA MFADHILI AMBAYE YUKO SAFARI AMEOMBA NIWATAKE RADHI ILI TUMSUBIRI AREJEE HIVI KARIBUNI ILI AWEPO KWENYE KUCHEZESHWA HIYO DROO NA IKIWEZEKANA ATOE YEYE HIYO ZAWADI KWA MKONO WAKE. NAPENDA KUWAHAKISHIA WADAU WOTE KWAMBA FEA PLEI ITAFANYIKA NA WATAOINGIA DROO HIYO NI WALE WALIOFUATA MASHARTI PAMOJA NA KUTABIRI MATOKEO HAYO KWA USAHIHI. NADHANI NIMESOMEKA...
PSSSST! HUWEZI JUA, HUENDA PENGINE MFADHILI AKAAMUA LOLOTE KAMA VILE KUWAFUTA MACHOZI WATAOKOSA HIYO $500 - ILANI: HILI NI WAZO LANGU TU WADAU....


Tulishangaa..maana tuliona giiiiii.. Michu, wazo lako libarikiwe, tunamuaminia sana jamaa, na imani tunaiweka juu ya hilo, akirudi mgusie, maana tuliopatia ni wengi, so swala la kifuta machozi likichukua nafasi yake, itakuwa safi sana...
ReplyDeleteBless
yaaani michu hapo ndo ulipoongea jambo la mbolea...maana angalau now twajua tuliopatia kutabiri na kufuata ol de mashartiz tumebaki saba tuu sasa msomeshe mfadhili musee kieleweke angalau kwetu sote wote saba mshindi na kifuta jasho kwa wengineoooo
ReplyDeleteMichuzi unazurura sana, mara zenji, mara a'town...Uko Juu...
ReplyDeleteEbwana tunakusoma kaka, tunaskilizia tu hiyo bahati na sibu, ili mwenye ngekewa aibuke na kitita. Ila sasa swala zima la hao wenye majina na sio email, itakuwa ngum kuingia kwenye droo, kwa sababu wakishinda, pia itakuwa ni ngumu kumjua kuwa mwenye hilo jina, ndio aliyeshiriki. Maana mtu anaweza kufungua email address chap chap kwa kutumia jina la mmoja wapo hapo, then ukimtangaza mshindi anaweza kuwa sio aliyeshiriki kubunia.
As you know kwamba email ndio kithibitisho tosha, kwani email iliyokwisha funguliwa au ambayo inamilikiwa na mtu already, hawezi kufungua tena mtu mwingine. Na pia kwenye vigezo vyako, ilitakiwa watu watumie email address....sante, wasalimie kina Hami Jei zenji.