
mbunge wa kigoma magharibi mh. zitto kabwe aliporejea dar baada ya kusimamishwa bungnei miezi sita ilopita. hivi majuzi jk aliwateua wabunge wa kutoka kambi ya upinzani (mh. zitto kabwe wa chadema na mh john cheyo wa udp) katika kamati ya kupitia mikatabaa ya madini, hatua ambayo imepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wadau hasa wa kambi ya upinzani. je hii imekaaje?


hapo wamekwisha, wanataka kumtuliza
ReplyDeletewajanja sana ccm, wameamua kumsogeza karibu ili waongee nae kiutu uzima ,sijui kama ataongea tena hela sio mchezo bwana ,we tokea cheyo aingie bungeni ,aende na rais kwenye misafara kadhaa kule marekani mmemsikia akisema chochote kwisha habari yake
na huyu wanamvuta kijanja ili wamfunge mdomo pesa sio mchezo
haki haitakuwepo tena hapo ,
kwani wote hao wanatafuta pesa
mlioko ulaya endeleeni kubaki huku hamna mpango ukifurukuta unatulizwa
jamani jamani jamani, tumechoka ufisadi, wakishampa sitting allowance watambana hasiwezi kufurukuta tena, maana hata mie sina imani na hiyo timu nzima ukizingatia yumo na idd simba? ni balaa tupu
ReplyDeletemzee michuzi hivi mimi sijaelewa hiyo kamati inapitia mikataba ya madini,au inapitia sheria inayohusu madini,?ili mikataba ijayo isainiwe vizuri.halafu kama nikupitia sheria ya madini we are too late hasa kwenye upande wa dhahabu,kwa nini nasema hivyo tanzania ni ya 3 au inaongoza kwenye gold ambayo saa hivi imehiti sana kwenye soko la dunia,kama ilivyo mafuta sasa kama tanzania imo kwenye wauzaji wakubwa wa hayo madini,naamini kabisa dhahabu tuliyonayo sasa ndio stock iliyopo,sidhani kama tuna dhahabu nyingine ,inatusibiri tuchimbe kama sio tumeisha yagundua yote na tayari mikataba imeisha sainiwa,kwa hiyo hata tukibadili sheria ya madini itakuwa na manufaa kidogo sana,labda tuombe mungu tugunduwe madini mengine yenye dhamani kubwa , kama hiyo kamati ni yakupitia mikataba iliyopo sasa itakuwa super ,je swali hao wawekezaji walikubali kupitiwa upya hiyo mikataba?kwa sababu ukisha sign mkataba umesign ,huwezi kugeuka nakusema oh nilikosea ndio maana ukiambiwa sign kitu chochote lazima usome kwanza kabla ya ku anguka mkono wako,ila kama mikataba hiyo ilisainiwa kwa influence ya rushwa hiyo mikataba itakuwa batili,na serikali inaweza kupita upya na hata kumpa mwekezaji mwingine,ushauri tanzani wanatabia ya kusign mikataba na kufanya siri ,sababu eti ni siri ya mwekezaji na sirikali na mikataba haipo standardized ,nafikiri tungekuwa na standardize mikataba yetu ikaandaliwa tanzania na kila anayekuja kuchimba madini anasign huo huo,tukiancha style ya sasa ndio inaleta rushwa kwa sababu waziri anaweza ku pendelea kampuni moja kwa kubadili vipengele kwa faida zake binafsi,na mikataba iwe wazi kwa faida ya taifa mwekezaji akija anawekewa mezani anaambiwa sign hutakia ondoka.
ReplyDeleteBandari Dar yamezwa na makontena
ReplyDelete2007-11-21 09:13:27
Na Richard Makore
Meli za nje ya nchi, zimesitisha safari zake nchini kutokana na mrundikano wa makontena zaidi ya 12,000 kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Sababu iliyosababisha meli hizo kusitisha safari zake ni kutokana na kuhofia kukosa nafasi ya kushushia mizigo yake ikiwemo makontena na magari.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (TAFA), Bw. Otieno Igogo.
Bw. Igogo alisema, licha ya Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa kuunda kamati ya kushughulikia tatizo hilo lakini hivi sasa hali imezidi kuwa mbaya.
Kadhalika, Bw. Igogo alisema, wafanyabiashara kutoka nchi jirani wameanza kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Mombasa nchini Kenya badala ya Dar es Salaam ili kuepuka mizigo yao kuchelewa.
Alifafanua kuwa Kampuni inashughulikia utoaji wa makontena katika Bandari hiyo (TICTS) imeshindwa kufanya kazi hiyo kutokana na uhaba wa vifaa na ukiritimba.
Alisema hivi sasa kampuni hiyo imezidiwa na mizigo ya makontena na kwamba kuna haja kwa serikali kuchukua hatua za dharura ili kuondoa tatizo hilo.
Aliongeza kuwa ucheleweshaji wa utoaji wa mizigo ikiwemo makontena katika Bandari hiyo utasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi.
Alimuomba Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati sakata hilo ikiwemo upitiaji upya wa mkataba wa kampuni hiyo ya kigeni ya TICTS ambayo alisema imeshindwa kazi.
Alisema Rais anatakiwa kuchukua hatua hizo ili kujua TICTS ni kampuni ya nani na kwa sababu gani kwa muda mrefu imekuwa ikifanya kazi kwa ukiritimba bila ya kuulizwa na mtu.
Aidha, Bw. Igogo aliishauri serikali kuwaruhusu wafanyabiashara wenye uwezo kujenga bandari nyingine ili kuondokana na usumbufu na ucheleweshwaji wa utoaji wa mizigo.
Alitoa mfano kuwa hivi sasa hakuna mizigo yoyote inayotoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa ya Tanga, Mtwara na visiwa vya Zanzibar.
Uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam ni kupokea makontena 7500 lakini hivi sasa yamefikia 12,000 miezi michache baada ya Bw. Lowassa kuitembelea na kuitaka kuondoa mrundikano huo.
BONGO BWANA FOLENI MPAKA BANDARINI.."..NCHI JIRANI WANACHUKUA BIASHARA KIULAINI.."
ReplyDeleteKama Kabwe amekubali kufanya kazi na tume hiyo; huo utakuwa ndio mwisho wa kelele za mkataba wa Buzwagi.
ReplyDeleteKwa sababu ya usiri (confidentiality clauses) kuhusu mikataba; Kabwe hataweza kuzungumza hadharani tena habari ya mikataba ya madini maana tayari ameiona mikataba hiyo ambayo ni siri kati ya wahusika (hata bungeni mikataba huwa haijadiliwi). Na atakuwa anakiuka maadili endapo atazungumza hadharani kuhusu mikataba hiyo.
Na akikosea tu akaenda majukwaani kuzungumzia mikataba ya madini amekwisha: Sheria itachukua mkondo wake na yeye aweza kufungwa au kupoteza ubunge!
Mi sijaelewa kwa nini wapinzani wanasita labda kuna mazingira ya kuzibwa midomo lakini nani wa kumziba mdomo Zito, thubutuuuuuu
ReplyDeleteZito bro, ndio njia ya kumbwa msaamaha na we ule hela ya kamati si unajua kuna kukirimiwa mkienda migodini tena. wakati wako huu na ujue ukila hatuta kuelewa.
CHADEMA acheni kupiga mayowe,huo ndio mchezo wa siasa,alichofanya Jakaya ni ku pull the rug under your feet,issue ya buzwagi kwa CHADEMA ilikuwa turufu kwao na sasa mtoto wa mjini JK kaipoka.acha kuzoza,tulieni,jipangeni,tafuteni hoja mpya muiuze kwa watanzania.hii biashara ya kufukazana haiwafikishi popote unless na ninyi mnataka kuwa lyatonga mwingine.
ReplyDeleteChadema walimpora toka CCM sasa anarudi taratibu CCM tatizo liko wapi.
ReplyDeleteCCM walijitia ooh! Vijana hawajaiva kwenye siasa kiasi cha kuweza kugombea kwenye majimbo wakamtema. Kijana Kabwe akatimkia Chadema ambako aliwagaragaza CCM kama watoto kwenye kinyang`anyiro cha ubunge kabla hajaenda kuligaragaza na Bunge kwa hoja kali.Bunge lenyewe liliona kama kitoto kitukutu tu kitakwama tu lakini sasa bunge limepata somo maana mtoto mtukutu kasababisha hadi vipengere jeuri vya kudhibiti wabunge viondoke.
Inavyoonekana CCM ya akina Msekwa imegundua makosa sasa imeamua kujisahihisha kwa toba ya kiutu uzima kwa kumrudisha Kabwe taratibu.
Namhurumia Mbowe aliyempora CCM halafu akajitwika Kabwe kwenye Helikopta kumzungusha nchi zima! Mbona atalia machozi bila miwani!
Labda niwaonye wapinzani wajue kule kwenye NEC ya CCM kuna Msekwa na Salim Ahmed Salim wajuaji tishio wa siasa za ndani na nje ya nchi.CHADEMA isitegemee mteremko tena kisiasa kama ilivyozoea huko nyuma.
Hii itakua manipulate, na kama kweli alisema uongo bungenui kwanini serikali imuamini sasa kwenye hio kamati ya madini?
ReplyDeleteCCM imejua wazi kwamba Zitto ndio tishio lao ndio maana wamempa pesa ili afunge mdomo.
HAKUNA MTU ALIKUWA MLALAMISHI KAMA SEIF (CUF).
ReplyDeleteMOJA YA SHARTI LA MUAFAKA WA KWANZA NI KUMTAMBUA SEIF KAMA WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU ALILIPWA MAFAO YAKE TANGU ENZI HIZO SASA KIKO WAPI SI HUYO KIMYAAAAA!! NA MUAFAKA UNAENDELEA.
Hapa tutake tusitake. Ni baadhi ya wanaCCM na Makampuni ya madini hawataki Zitto awemo kwenye tume, maana ataona mengi. Wanawatumia wana Chadema wachache ili waharibu.
ReplyDeleteKulikoni jamani? upinzani uko kila sehemu kwa manufaa ya taifa. sasa kama shughuli aliyopewa ni kwa manufaa ya umma kwa sasa au baadaye tatizo liko wapi?
ReplyDeleteKuwa mpinzani haimaanishi chuki binafsi. Ni tofauti za kiitikadi tu. Mwisho wa siku kama mikataba ikionekana ina kasoro na kurekebishwa ni manufaa ya taifa.
Mdau wa Newala.
Jamani cha ajabu hapo ni nini? mambo sheria za madini yameleta migogoro, raisi ameteua tume kuifuatilia, wananchi wote wanajua Zitto ana uchungu na nchi yake in this case raisi pia, ndio maana katika hiyo tume mtu kama Zitto hakutakiwa kukosekana hongera uteuzi wa Zitto mwacheni akachangie kurekebisha mambo, nyie mlitaka CCM peke yao wawe kwenye hiyo tume? kama Zitto angekosekana nani awekwe sasa?Karamagi?
ReplyDeleteJambo la kushangaza hapo ni moja tu: viongozi wetu taratibu wanasikiliza vilio vyetu na atleast mtu mmoja amepewa ujumbe wa kamati bila kujuana.
Wanamuandalia safari ya kwenda mbinguni. wanjua hata stahimilu upuuzi kwenye mikataba yao na akitakujiondoa tu wanae. Utashangaa kafa kiajabu ajabu tena sio tz huko huko bondeni sauzi suburini msiniite mi mchawi.
ReplyDeleteTANZANIA TUTAFIKA KWELI. NJAA ITATUPONZA. SASA HUYO NAE NDIO HIVYO ANAONJESHWA TAMU, HAMTAMSIKIA TENA HUYO. HOO KUPIGANIA HAKI , HOO SAUTI YA WANYONGE KWISHA, SASA HUYO ANANYEMELEA UWAZIRI HIKI NDICHO KITAKACHO MUWEKESHA UBUBU KABISA. USIFANYE MCHEZO NA CHUKUA CHAKO MAPEMA (CCM). HUYO MLIOKUWA HAMUMTAKI NA KUMSIMAMISHA BUNGENI LEO MNAMPA UWANA KAMATI KIKO WAPI? CCM MZIZNI MTAFANYA WATU WAJINGA BWANA IPO SIKU IPO SIKU!!!!!!!
ReplyDeletePiga ua, Mkutano Mkuu wa Chadema wa kumchagua mgombea urais 2010 utampitisha Zitto.
ReplyDeleteKama hamuamini Mwambieni Mwenyekiti asome alama za nyakati.
Zitto tayari anazo digrii na ameonyesha anaweza kuigeuza Chadema kuwa na sura ya kitaifa.