
mkurugenzi wa mohamed enterprises na mbunge wa singida mh. mohamed dewji akisakata sebene siku staa walioporejea na ushindi dhidi ya bukia faso. mchana huu mh. dewji ametoa motisha kwa timu ya taifa ya bara kwa kuahidi kwamba endapo timu hiyo itashinda kombe la chalenji linaloanza jumamosi hapa dar na arusha ataizawadia dola 30,000 na atatoa dola 20,000 endapo watakuwa wahindi wa pili na dola 10,000 wakimaliza washindi wa tatu. ikumbukwe cecafa wametoa donge kama hilo hilo kwa washindi watatu wa kwanza ambapo ndio kusema mambo yatakuwa dabo dabo kwa kili staaz endapo watashinda. Mungu awape ni; donda?
usiache kuposti hii "atatoa dola 20,000 endapo watakuwa wahindi wa pili." nimekukamata mzee wa kubofya hahahahahah
ReplyDeleteMithupu, iwapo watakuwa Washindi wa Pili au Wahindi wa Pili. nyie ndio mnasababisha ponjoro aliekwenda kuuza sura China ionekane kulikuwa na namna! Rekebisha kwanza ndio nitoe yangu.
ReplyDeleteWabongo bwana, sa we anony hapo juu kwani ni lazima uandike...haya basi kakosea ila c umeelewa au? b blessed
ReplyDeleteHivi jamani, hebu tuambiane ukweli.
ReplyDeleteHivi hawa watu, hizi pesa zote za kumwaga hivi kila siku wanatoaga wapi jamani!?!
WEWE PEREZI HAPO JUU WACHA USHAMBA... UMEFIKA DARASA LA NGAPI????
ReplyDeleteULAYA WATU WANAPESA KULIKO HUYO MBONA HUULIZI WANAZIPATA WAPI??? NA HUWA HAWANA MADINI WALA NINI???
JIBU LAKE HUWA WANASHEAR NA VIONGOZI MBUMBUMBU..
Wapigwa vumbi mtabakia kukombolewa na maghabachori!!!!Unasema nondoz za first world hazina nguvu...hamshangai kwa nini viongozi wenu wanawatuma watoto wao kuchukua nondoz za huku!!
ReplyDeleteDu. Itakuwa poa si polepole kama tukawa na wengine kaa 20 kama huyu wakamwaga izo noti kuinua vipaji vingine. Ni mshabiki wa michezo na bado nalisuma kandanda lakini tuangalie na upande mwingine.Wamwage noti kwenye mifuko ya kuinua technologia ona mtoto kidato chasita bado hajui hata kutengeneza toy la umeme, wanamwaga mapene kwenye urembo, soka na tunasahau watalaamu wakesho. Wapi Cool Ndovu, Ngoilanga, Mwakilembe hao ni baadhi ya vichwa vingechangiwa fedha za kufanya project siajabu wangebadili nchi yetu na kesho tusinge omba wataalamu toka nje. Asante Michuzi.
ReplyDeleteanon hapo juu umeongea ukweli la muhim ni kuwa wanamwaga pesa ktk wakati muafaka kwa ajili ya political gain! hakuna cha kuchangia hapo kama anataka kuchangia apeleke pesa au vifaa ktk shule za msinngi anafanya hivyo kwa kujua watu mimacho imewatoka sasa kutaka kujua nini kinaendelea, au katumiwa kuchangia kiaina si unajua mambo ya kijinga nikune mgongoni nami nitakukuna pia, hii ni kuendelea kuumilk uchumi wa bongo kiaina, kazi ya motisha ni ya tff na sio watu binafsi changieni mashule ya msingi vifaa na si kutaka political gain kistairi.
ReplyDelete