mama salma kikwete akiwapa pole mahujaji waliokwama uwanja wa ndege dar kwa siku kadhaa


Na Mobini Sarya




HATUA ya kampuni ya Ndege (ATC) kushindwa kusafirisha Mahujaji kwenda Hijji imeonekana kumgusa Rais Jakaya Kikwete hadi kuingilia kati na kuamua kuomba msaada wa ndege toka Falme za kiarabu.

Rais Kikwete amefikia hatua hiyo baada ya mahujaji waliokuwa wasafishwe na ATC kushindwa kuondoka baada ya kukosekana Ndege kama ilivyokuwa imeelezwa hapo awali.

Safari hiyo baada kushindikana huku ATC ikiendeleza ahadi zake za subiri baadaye kidogo, Rais Kikwete amedaiwa kukerwa na hatua hiyo hadi kufikia hatua ya kumtuma Mkewe Salma Kutoka Dodoma aliyekuwa amekwenda kuhudhuria Sherehe za Uhuru na kuja kuwasikiliza Mahujaji hao.

Kikwete alimtuma Mama Salma kwa niaba yake hasa kwenda kujionea hali halisi na pia kuzungumza nao ili kuweza kupata ufumbuzi wa tatizo hilo, katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) walipo kwama mahujaji hao akiwemo Mkwe wake Mzazi wa Salma, aliyeambatana na familia yake pamoja na Meya wa Kinondoni, Salum Londa .

Salma Kikwete aliwasili JNIA majira ya saa mbili usiku na kuwaeleza mahujaji hao kwamba Rais yupo pamoja nao pia ana nia ya kulitatua tatizo hilo na ndio maana yeye( Salma) yupo hapo ili kufahamu tatizo lipo wapi ili wapate njia ya kulitatua.

Mwenyeki wa ATC Mustapha Nyang’anyi aliwaambia mahujaji mbale ya Mama Salma kuwa Ndege imekwisharuka kutoka Saudia na ipo Angani itataua wakati wowote hivyo kundi la kwanza la mahujai 379 wajiandae kwa safari.

Kufuatia hatua hiyo mahujaji waliingia uwanjani na kuafuata taratibu zaote ikiwamo kukaguliwa kwa ajili ya safari ilokuwa ianze saa saba usiku. Baada ya hapo kundi la pili lilifuatia, likiwa katika hatua za mwisho kukaguliwa wakaambia kua ndege ile imerudia ilipotoka kutokana na kukosa kibali cha kupita anga za Ethiopia na Sudani.

Ilipotimu majira ya saa saba ndege kubwa ya Emirate iliwasili nakusababisha Mahujaji kutaharuki kuwa ni ndege ilikuwa inakuja kuwachua, kumbe ilikuwa ni ndege iliyobeba mahujaji 200 kutoka nchini Komoro waliokuja kuungana nao katika safari kuelekea Saudia kupitia ATC.

Baada ya muda mfupi waliwasili abiria wengine 22 kutoka DRC na Shirika la Ndege la Kenya .

Hali iliyopelekea mahujaji kufanya mkutano na ATC kuanzia saa tisa usiku hadi saa 11 alifajili ambapo Rais Kikwete alishiriki mkutano huo kwa njia ya Simu nakuhoji kwanini ATC ilitoa taarifa kuwa ndege imeisharuka na mpaka sasa Ndege hiyo haijafika.

Katika utetezi wa ATC, Juma Nchia ambaye ni katibu wa Mahujaji wanaosafiri kupitia Hajj Trust alisema, Viongozi wa ATC walijiteteta wakidai kuwa Balozi wa Tanzaia nchini Saudia Jaji Mstaafu Hamis Msumi ndiye aliwapa taarifa hizo na ambaye kwa muda huo alikuwa hapatikani katika simu yake.

Hali hiyo imeelezwa kuwa ndio iliyopeleka Rais kkuomba msaada wa Ndege kutoka Falme za kiarabu ambapo Mfalme mmoja ambaye hajajulikana alikubali kumpa ndege ambayo ilikuwa inasubiriwa hadi jana huku kukiwepo na tetesi kuwa rais alikuwa amesema lazima atawawajibisha viongozi wa ATC.

Hata hivyo ATC nao walisema kuwa wamekodi ndege tatu kutoka katika shirika la AL –WASAM ambazo kubeba abiria 379 .

Kiongozi wa mahujaji amesema kuwa pamoja kuwa ATC wameanza kuwapa chai asubuhi pamoja na chakula cha mchana na kuwapeleka kwenye mahoteli lakini bado shirika hilo linawajibika kwa kila namna katikla usumbufu walioupata.

Aidha baada ya ATC kuona imekuwa Kero wamelazimika kuchukua mahujaji waliowatoa Zanznibar, Komoro na kuwatafiutia mahoteli pamoja na wanaotoka hapa nchini ingawa baadhi yao wamegoma kwenda mahoteli wakitaka wajue hatima yao.

Baadhi ya hoteli walizopelekwa ni Land Mark, Ubungo Plaza, Millenium Tower pamoja na Golden Tulip,




Hadi saa kumi na mbili jioni ya jana kikao kilikuwa kinaendelea na hukuna ndege ilikuwa imeshaawasili huku leo ikiwa ni siku ya mwisho kwenda huko Madina.




Wakati huo huo, Waziri Mkuu Edward Lowassa asubuhi hii anakwenda kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kuonana na mahujaji wanaokwenda kuhiji Mecca Saudi Arabia ambao wamekwama kutokana na matatizo ya usafiri wa ndege.

Lowassa anatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Dar es Salaam saa 2.00 asubuhi, kuwaona na kuwafariji mahujaji hao na kuwaelezea jinsi serikali inavyojaribu kutatua tatizo lao.

Mahujaji hao wamekwama kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kwa siku kadhaa sasa baada ya kukosa usafiri wa kwenda Mecca kwa ibada hiyo ya hija.

Awali taarifa zilisema kuwa kuna ndege iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) kwa ajili ya kuwasafairisha mahujaji hao lakini ilikuwa haijawasili.

Mipango imekuwa ikifanywa ili kuhakikisha kuwa mahujaji hao wanasafiri haraka kwenda Mecca kwa ajili ya ibada hiyo maalum ya kuhiji mujibu wa nguzo kuu za Uislamu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Aibu tupu!!!

    ReplyDelete
  2. This is not right, not fair, mimi si Muislamu lakini hii kitu imeniuma sana, huwezi kuwachelewesha watu kwenye safari yao namna hii. Mbaya zaidi ni kwa nini walikubali kuwasafirisha wakati hawana uwezo? Uzembe mkubwa na matokeo yake ni hasara kwa ATC na kero kwa mahujaji. Aibu sana kwa nchi yetu, tunaonekana kwamba hadi leo bado hatujui uzito wa ahadi ya kibiashara. Itakuwa safi sana kama Rais ataondoa vigogo wote wa ATC, wote kuanzia Mwenyekiti wao wa Bodi hadi Wakurugenzi, toa wote tu, tuanze upya. Hii siyo biashara, siyo huduma, ni uhuni.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana ndugu zetu, muwe na moyo wa subira, maana hamjui mwenyezi mungu ana nia gani na nyie.
    Hata hivyo mna roho ngumu sana kupanda ATC!

    ReplyDelete
  4. Huwezi kujua labda Mungu amewaepusha na balaa fulani au jambo fulani baya, tatizo letu sisi binadamu huwa hatuelewi mipango ya Mungu.

    ReplyDelete
  5. THAT'S A HELL OF A LOT OF EMBARRASSMENT FOR THE GOVERNMENT.BUT, AT LEAST I'M AMONG SOME TANZANIANS WHO ARE NOT SURPRISED WITH THIS MESS.

    INCOMPETENCE IS RAMPANT IN OUR COUNTRY.IF WE HAVE DOCTORS WHO CAN BANGLE A MEDICAL PROCEDURE SUCH AS OPERATION - RECALL THE HEAD-LEG MIX UP RECENTLY?

    LET'S BE HONEST, WATANZANIA WENGI NI WABABAISHAJI,WAKIWEMO VIONGOZI WA JUU SERIKALINI.HUO NDIYO UKWELI.

    I'M PRETTY MUCH SURE THAT THE STORY IS GOING TO MAKE INTERNATIONAL HEADLINES, IF IT HASN'T SO FAR.

    ALL THIS HAPPENS KWASABABU WANAOFANYA GRAVE BLUNDERS HAWAADHIBIWI, MATOKEO YAKE DISCIPLINE YA KAZI INAKUWA ZERO.

    ASTAGHAFIRULLAH, MWENYEZI MUNGU TUSAMEHE SISI WAKOSEFU TUSIOJUA MAKOSA YETU.

    ReplyDelete
  6. Mpaka mkwe wa Raisi akwame ndio viongozi waangalie. Hili sio suluhu la kudumu. Uangaliwe uongozi, utendaji wa ATC Nzima na uwajibikaji kujenga misingi mizuri. Kwa hao abiria waliokata tiketi si wamelipia? Vipi ATC ichukue hela halafu hakuna ndege?? Aibu jamani nchi hiii tunaelekea wapi? Shirika linaendeshwa kisanii

    ReplyDelete
  7. nani anabisha kwamba bongo siyo tambarare,hivyo vitu ndiyo vinaonyesha bongo ni tambarare nyie wabeba mabox kaeni ulaya na wazungu wenu mnaowasifia ,sisi tuachieni na bongo yetu.

    ReplyDelete
  8. Someni kwa makini yaliyoandikwa na huyu ndg. yangu Mobin Sarya.

    "Rais Kikwete amedaiwa kukerwa na hatua hiyo hadi kufikia hatua ya kumtuma Mkewe Salma Kutoka Dodoma aliyekuwa amekwenda kuhudhuria Sherehe za Uhuru na kuja kuwasikiliza Mahujaji hao".

    Ama Mobin amechanganya mambo kiuandishi au itakuwa aibu maana RAIS hawezi kukasimia madaraka au wajibu wake kwa mkewe (asiye na wadhifa wa kiserikali katika tatizo husika) bali Kikwetwe kama mtoto mkwe anaweza kumtuma mkewe kuwajulia hali Wakweze na watanzania wengine waliokwama Airport!
    Tuwe makini katika utoaji wa taarifa!

    Nyakatakule Unyilisya Echalo

    ReplyDelete
  9. That is Tanzanian "TAMBARARESIM"

    ReplyDelete
  10. HIVI WAKATI WOTE ATC WAKIWAVUNGA MAHUJAJI NA HATA RAIS KWAMBA NDEGE IPO HEWANI WALIKUWA HAWAJUI KWAMBA KUPITA ANGA YA NCHI YOYOTE ILE SHARTI NDEGE IPATE KIBALI. NANI KAWAPA HAWA MAMBUMBUBU KAZI HIZI? NAYE AWAJIBIKE. HIZI SHUGHULI WAACHIWE WATU WENYE UWEZO. TANGU TUSOME MATATIZO YA MAHUJAJI MPAKA LEO NDEGE HAIJAFIKA? WANAOHUSIKA BADO WANAJIELEZA TU? MUNGU IBARIKI TANZANIA!!

    ReplyDelete
  11. Kuwafukuza kazi Viongozi wa ATC siyo suluhu ya matatizo ya shirika hilo! ATC hamna vitendea kazi(ndege),ndege zinakodishwa,ikipatikana fedha wanajinafasi badala ya kulipa madeni,ni aibu tupu!Rais anafanya Umatonya!!!

    ReplyDelete
  12. Jamani this is unbelievable! Huyo balozi wa Saudia anawezaje kutoa habari ambazo hazina uhakika? I thought kama Balozi anayetuwakilisha angekwenda uwanjani na kuhakikisha hizo ndege zinandoka! How does the system work? Mnaposema balozi huyo hapatikani maana yake hakuna ofisi au hapatikani kwenye simu yake ya mkono au ameamua kukimbia simu ili asiwajibike. Uongozi wa ATC they have nothing to do with this! Lazima tuangalie source of this confusion! Promise ilitolewa ya kuletwa ndege kusafirisha mahujaji iwe ya mdomo au maandishi, balozi anajulisha ATC kwamba ndege zimeondoka (ndiyo maana ya kuwa na balozi nje ya nchi), Mwenyekiti wa bodi ya ATC kawasilisha ujumbe (mjumbe hauwawi), sasa rais wetu J.K. anazungumzia kuwawajibisha uongozi wa ATC na Balozi wa Saudia aliyeleta habari hizo hajazungumzwa! Where is the managing director? I think nakumbika Balozi nyanganyi alituliwa kuwa mwenyekiti wa bodi na si mtendaji na hata hivyo ndiye aliyekuwa waziri wetu wa Mawasiliano na uchukuzi miaka ya 80 kama sikosei ambapo mashirika yote ya usafiri ndege, bandari na reli vilikuwa na hali nzuri kuliko sasa. Tulikuwa na ndege zinaruka all over Africa, Uarabuni na ulaya! Lets face it!

    ReplyDelete
  13. Kwa mtu anayeifahamu ATC alijua wazi hawana uwezo wa kuchukua kazi kama hiyo maana hata usafiri wa ndani ya nchi bado unawapa shida, ninajiuliza ilikuwaje wakaamua kufanya kazi hiyo na kujitia aibu?

    ReplyDelete
  14. Ndio watendaji wetu hao, na hapo ndio tunatarajia kujikwamua kutoka kwenye utendaji mbovu hiyo ni ndoto ya mchana kweupe. Tena hapo juhudi zinaendelea kwa nguvu hivyo kwa sababu tu kuna ndugu za vigogo hapo vinginevyo ah wacha kabisa. Aibu kubwa mno.

    ReplyDelete
  15. What a loss, they must all be fired wazembe wakubwa.

    ReplyDelete
  16. Namuunga mkono anony wa 18:00 kweli hii ni aibu tena aibu sana!Lakini kwa rais kumtuma mkewe kama tulivyohabarishwa hapo juu huu si uwajibikaji,yeye ni first lady sawa lakini ATCL iko chini ya wizara fulani ambayo ina waziri mwenye dhamana na mambo yote ya kiuwajibikaji why asimtumte huyo waziri?Au laa basi angelimtuma hata Waziri Mkuu wake atamtumaje mkewe au ndo serikali nzima sasa tunataka kuihamishia majumbani kwetu?Waziri anaehusika na miundmbinu yu wapi anapaswa awajibishwe kwa hili kwasababu yaelekea hajui majukumu yake mpaka rais anamtuma mkewe?

    ReplyDelete
  17. MICHUZI iweke hii kwenye Blog husiminye...

    Rais Kikwete ana mtihani Mgumu hapo maana ni lazima awajibike mtu NYANG'ANYI (ATC Board Chairman) MATAKKA (ATC MD) na Balozi MSUMI... Haya JK kazi kwako! Mtihani mzito huo lakini ni jambo laajabu sana,HIJA watu hawaendi kutalii.. kila kitu kinakwenda kwa mpangilio.

    JK tutumie wataalamu tulio nje tuje kurekebisha mambo huko. Huku ughaibuni kwa jambo kama hilo lazima hao wote niliowataja wangeachia ngazi! Watu nyumbani (TZ)hawana discipline ya kazi AIBU tupu!! Nchi yetu haiwezi kuendelea kwa mtaji huo! Aibu... Aibu... Aibu kweli. Watu wamezoea kufanya maskendo na kupeta!! This time wawajibishe ... Hili iwe mfano kwa wengine.
    Anonymous MKEREKETWA wa Hali mpya na Kasi mpya!

    ReplyDelete
  18. poleni sana ndugu zangu mahujaji, kweli roho inauma sana kuona mnaumia kutokana na uzembe wa watu wachache sana,nasikitika kuona bado Tanzania haiachi mambo ya kipuuzi kama haya...sasa nasubili kuona reaction ya Kikwete kwa maofisa hao wa ATC je atawafanya nin??kama ni mim kazi ndio basi kabisa...pia michuzi asante sana kutupa mambo mazuri kama haya..kazi nzuri..

    ReplyDelete
  19. Tunajua kwamba kuhiji ni mojawapo ya nguzo kuu muhimu za uislam, but mbona hili swala limechukua sura ya kiselikali zaidi? Kwani safari ya kwenda kuhiji normally huwa inasimamiwa au kuratibiwa na serikali?na km tatizo ni kucheleweshwa kwa abiria, kwani jamani hii ndio mara ya kwanza?Mii nadhani hapa Rais au Mkewe au PM wakitajwa, tuelewe kwamba wametajwa km wananchi/watanzania wa kawaida na sio kuhusisha na serikali as if serikali ndio inasimamia safari za aina hii,othewise tutaishia kuchanganyana na kutojua nani aulizwe nini,maana balozi ki msingi sii mtoa taarifa za anga na mambo ya no fly zones,haya yana wataalam wake wa anga na rada nk,na isitoshe mama kikwete anaweza akamuwasilisha mumewe katika shughuli zozote za kijamii na sii kiserikali,so tusipoteze maana na mwelekeo,cha msingi uzembe wa watu wasiowajibika uchukuliwe sii kwasbb ya safari ya mahujaji tu,hata kwa safari za treni yetu ya reli ya kati(a.k.a GOGO) ambayo kila siku inachelewesha watu au haifuati ratiba huko dodoma na hata dar...Wadau fumbueni macho!!

    ReplyDelete
  20. Hivi katika katiba ya Tanzania Mke wa Rais (first lady) ana nafasi gani ya kiutendaji ktk serikali?? Yaani Rais alishindwa kumtuma wazili wa miundo mbinu na mawasiliano au hata MZEE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU au hata mjomba wake Yusuf Makamba?? Keshokutwa usishangae katumwa First Son "Ridhiwani"

    ReplyDelete
  21. Watu walikua hawaelewi nini maana ya ATC. Maana yake ni Any Time Cancelation. Ndugu zangu waungwana wanaosota poleni sana tusipende virahisi vina matatizo yake.

    ReplyDelete
  22. MWAKA JANA ATC WALIFANYA MCHEZO KAMA HUU WATU WAKASOTA WIKI NZIMA LAKINI BAHATI WAKASAFIRI BAADA YA WIKI MOJA. MWAKA HUU WAMERUDIA TENA, MUNGU AKAWAAMBIA MCHEZO WENU SASA MWISHO CHA MOTO WAMEKIONA.

    TATIZO KWANI HAMLIJUI? NI KUTAKA VITU VYA RAHISI, DUNIA NZIMA NDEGE ZIKO DUBAI TU? WALIKUWA WANATAFUTA KARIBU NA DEZO ILI WAPATE FAIDA KUBWA BADALA YAKE WAMEPATA HASARA, WAMEBAKI MARA OOH NDEGE MBOVU, NDEGE SIJUI NINI? HIVI DUNIA NZIMA NDEGE ZA KUKUDI ZIKO DUBAI TU.

    KINACHONIUMA NI KUWANYIMA WATU TAARIFA, TANGU TAREHE 3 WANGESEMA UKWELI MPAKA LEO WENGINE WANGEONDOKA NA NDEGE NYINGINE.

    NA HUYO MWANDISHI NI MWONGO NA ANAYAKE, MAKALA YA MWANZO ALISEMA WAISLAMU WANATAKA KUMKATA MTU SHINGO, AKAONA HIYO HAIKUZUA TAFRANI NGOJA ATIE CHUMVI NYINGINE KUWA RAIS KAMTUMA MKEWE, NADHANI AKIONA COMMENTS ZA HUKU KWENYE BLOGU WATU WALICOMMENT SIKU YA KWANZA TU KUWA RAIS KAMTUMA MKEWE! ANATAKA KUOPTIMIZE HII SITUATION KWA MAMBO YASIYO KICHWA WALA MIGUU.
    KAMA RAIS ANGEINGILIA KATI NADHANI HAO MAHUJAJI WANGESHAONDOKA SIKU NYINGI AMEWAACHIA WENYEWE ATC WAHANGAIKE NALO NA UWONGO WAO.

    TATIZO LA 'HOW MUCH WILL I GET OUT OF THIS DEAL?' NDILO LITATUMALIZA, MANDEGE YA KUKODI YAKO KIBAO WANGEKODI SOUTH AFRICA, AU KOKOTE DUNIANI WANGESAVE PESA NYINGI KULIKO KUNG'ANG'ANIA MAHALI AMBAKO HATA MWAKA JANA WALIMESS UP.

    ReplyDelete
  23. MICHUZI,
    NACHUKUA NAFASI HII KUWAPA POLE SANA MAHUJAJI WALIOCHELWESHWA UWANJA WA NDEGE. INAUMA SANA. MIMI NI MKRISTO, NA NAONA WAISLAMU WALIOJIANDAA KISAFARI WAMEKWAZWA SANA MIOYONI MWAO. HAWA WATU WALISHAKUWA NA AMANI YA MOYONI, TAYARI KWA HIJA, KUPATA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU! LAKINI WAMEPEWA WAKATI MGUMU WA HATA KUWALAUMU WATU WA ATC, WAKATI SI NIA YAO, UKIZINGATIA WALISHALIPA NAULI.

    1. JK, KUMTUMA MKEWE SIONI KOSA LOLOTE KAMA WALIVYOSEMA WENGINE HAPO JUU. MAMA SALMA, NI KAMA KIONGOZI ASIYE NA WIZARA MAALUMU SERIKALINI. AKISAFIRI NA RAIS, ANAWEZA KUFANYA KAZI YOYOTE ATAYOMWAMURU RAIS. KWANI NI MANGAPI RAIS ANAJIULIZA KWA MKEWE KABLA HATA YA UAMUZI, AMBAYO HATA SISI HATUYAJUI? TUSILAUMU TU, LET'S USE COMMON SENSE.

    2). RAIS KUMTUMA MKEWE, MIE NAONA TU NI KAMA KUMCHOSHA, NA SIO KAKOSEA. ILA RAIS ALITAKIWA KUTUMA VIJANA WAKE,IKIZINGATIWA WAKO WENGI-EL,MAKONGORO NA WENZAKE NK.

    3). SISHANGAI KUONA RAIS ANAFANYA HIVO, MAANA YEYE NI MWINGI WA MANENO KULIKO VITENDO, NA HATA SERIKALI YAKE, UKIACHILIA MBALI WAROPOKAJI WA MANUFAA KAMA WAZIRI MAGUFULI. KAMA MMEGUNDUA SERIKALI YAKE, SIKU ZOTE WANATISHIA TU KWA MANENO, ETI ATAKAYEZEMBEA KUKIONA KATIKA AWAMU YAKE. JE, NI WANGAPI WAMEZEMBEA NA WAMEKULA RUSHWA, NA ANAWAJUA. YEYE NI MWOGA.
    HADI TUPATE TANZANIA YENYE MTU KAMA SOKOINE, NA HIYO SI TABAKA LA WALIOMO KATIKA SAFU.

    4). SABABU YA MSINGI KABISA YA TATIZO TULILOONA HAPO JUU, ZAIDI NI UMASIKINI NA VITENDEA KAZI DUNI. TUACHE HASIRA TU KUWALAUMU WATU WA ATC NA BALOZI WA SAUDIA. SABABU WALIZOTOA ZA KUKOSA NDEGE NA KUCHELEWESHWA NI ZA WAZI NA ZIPO JUU YA UWEZO WAO. JE, RAIS ANGEOMBA NDEGE NA KUAHIDIWA NA ISIJE, WATU MTASEMA NINI? HIZO NDIYO TUNAITA "CONTINGENT FACTORS", AMBAPO UNAPATA TATIZO LILILO JUU YA UFUMBUZI WAKO WA HAPO KWA HAPO.

    5). WATU WASILINGANISHE NA HUDUMA ZA NDEGE TANZANIA NA UARABUNI, ULAYA, AMA MAREKANI, AMBAKO NDEGE ZINARUKA NA KUTUA KAMA VINDEGE TOKA ASUBUHI HADI JUA KUTUA. SISI UWEZO HAUJAFIKA HUKO.

    6). NINA WASIWASI SANA NA KUKOSA KUGAWA MADARAKA KWA RAIS WANGU. HUWA NAONA ANAINGILIA SANA KILA KAZI. ITAKATISHA SANA TAMAA WATENDAJI WAKE. HATA KAMA WAKIWA WAZEMBE. RAIS HAWEZI KUJIGAWA MWENYEWE KILA SEHEMU AKAMALIZA MATATIZO. AKIAMUA TU UTAKUTA MWENYEWE AMEKUWA MKUU WA WILAYA, AU MEYA WA MJI, AU MSAMARIA MTAANI! UTAWEZA HIVO KWA WANGAPI? WEWE NI KICHWA CHA NCHI BABA!

    6). HII YA KUKWAMA KWA NDEGE NI NZITO SANA NIONAVYO MIMI SABABU INATAZAMWA MACHONI PA MATAIFA MENGI. ILE TU HABARI YA KUCHANGANYA WAGONJWA MUHI2 INAZUNGUMZWA KILA KONA HUKU NJE. OTHERWISE, HILI PIA NI TATIZO TU KAMA LA WASAFIRI KUKWAMA KULE DODOMA WAKIWA SAFARINI KWENDA KIGOMA AU MWANZA KWA TRENI. MBONA HUWA TUNAELEWA KUWA VYOMBO VYETU NI DUNI. IWEJE TUSIVULIMIE KIASI KWA HILI?

    HAPO HAKUNA KUFUKUZA MTU KAZI. AKIFUKUZA ANAJIPA KITANZI CHA KUHUJUMIWA NA WATU WAKE MWENYEWE. MAANA WATAMZUNGUKA KWA MENGI TU.

    ReplyDelete
  24. ANY TIME CANCEL (ATC)

    ReplyDelete
  25. Halafu mnataka turudi Bondo kuendeleza uchumi.... ATC imesifiwa sana hapa na Mheshimiwa Michuzi mwenyewe, sijui wananunua ngege nyingine, sijui wanataka kwenda safari za ulaya.... tatizo kama wanavyosema wadau wengi hapa sio kampuni, bali jinsi makampuni yanavyoendeshwa Tanzania. Hatufikirii wala kuwajali wateja, nashangaa sana kwa nini Mahujaji wametumia ATC, wanajua historia yake ni mbovu sana, nilipokuwa Dar ilikuwa inajulikana kama ANY TIME CANCELLED, inasikitisha bado hilo jina limewaganda. Mimi binafsi bora niende kwa miguu au niogelee kabla ya kutumia ndege ya bongo....

    ReplyDelete
  26. Mlalahoi, nakubaliana nawe na kila kitu isipokuwa na point yako namba 1. Kwani mke wa Rais hana nafasi yeyote ile katika utendaji serikalini. Wacha amshauri mmewe nyumbani, lakini sie hatustahili kujua kuwa hayo ni maamuzi ya mke wa Rais. Nasikitika sana kwa yote yatokeayo hapa Tanzania kwetu baada ya miaka 46 ya uhuru.

    ReplyDelete
  27. Hili ni tatizo la kupenda bure bure. Kwanini hao mahujaji wasilipe ndege wenyewe. Kuna mashirika ya bei rahisi kama Emirates na Quartar. Yote ya karibu na huko huko. Kama unahela unatakiwa uzitumie. Isifike sehemu ATC wakalaumiwa kwa sababu ya watu wengine ambao hawakuweza kujilipia kwenye ndege wenyewe. Mara nyingi tu ATC huwa iaacha au kuchelewa, lakini hatusikii watu wakilalamika. Iweje hawa kucheleweshwa iwe issue, tena ya kitaifa.

    Unajua, sisi Watanzani, lazima tutangulize uzalendo wa nchi. Tuwe makini na nchi yetu. Haimaanishi kwamba kwa sababu wewe uko sect fulani basi upewe kipaumbele. Je sects zingine zitakuwa vipi? Wote, kikatiba tuko sawa sawa kabisa. Hakuna wa zaidi. isije onekana kwamba wengine wako juu zaidi ya wengine.

    Zaidi ya yote, mwenye hela ndo anatambuliwa. Usiye nazo, usije leta jazba eti unataka kukaa kwenye runway ya ndege kwa sababu tu ndege yako uliotaka kusafiria haionekani!!!.

    ReplyDelete
  28. Ama kweli bongo imepevuka kwa demokrsia,rais anamtuma mkewe kwenda kutatua tatizo kama hili,huyo waziri mhusika wa miundo mbinu alikuwa wapi?hivi first lady kwenye katiba ametamkwa wapi kwamba anaweza kufanya/kutumwa kazi na mmewe mheshimiwa rais kwenye shughuli kama hii?lakini mbona abiria wa treni walipokwama kwenye kale kamji kadogo ka Kaliua mkoa Tabora hakumtuma tena kwa takribani siku 5 tena hawakuwa na msaada wa aina yoyote?JK anapaswa kujiangalia sana na hayo maamuzi mengine otherwise hata hao wahusika atawavunja moyo kwa kuingiliwa na mkewe kwenye majukumu yao!

    ReplyDelete
  29. Suala la mke wa Rais ni rahisi sana nashangaa watu wanapiga kelele. Kwanza hakuna ushahidi kwamba ametumwa na Rais. Pili, ana wazazi na dada yake katika mahujaji waliokwama, kama alienda kuwaona kama ndugu zake, halafu waandishi wakadhani ametumwa, tusimlaumu yeye wala mumewe. Tatu, kwa kuwa safari hii si ya kiserikali, na huyu mama si mtumishi wa serikali, kuna ubaya gani akitumwa kwenda kuwaona bila nguvu za kiserikali? Nne, kuwa Mke wa Rais siyo sawa na mke wa mtu mwingine yeyote, ni nafasi yenye ushawishi pia. Kumbukeni mke wa Rais wa Ufaransa alivyookoa manesi wa Bulgaria nchini Libya wasinyongwe. Mbona Mke wa Rais akitoa misaada hamlalamiki? Akienda safari na Rais mbona hamlalamiki?

    ReplyDelete
  30. bongo tambarareeee..ha ha haaaa

    ReplyDelete
  31. bongo tambarareeee..ha ha haaaa

    ReplyDelete
  32. Mimi kwa elimu yangu ndogo niliyonayo nakumbuka kusikia kitu kama anga za kimataifa ambako ndege huwa zinapita ni huko juu sana bila kuomba kibali cha nchi yoyote.
    Kama ilivyo baharini kuna umbali fulani ambako sio teritorio wota bali ni inteneshno wayers ambako meli zozote zinavua tu bila kibali.
    Sasa iweje leo tuambiwe ndege ilinyimwa kibali cha kukatiza anga za Sudani na Ethiopia!?!
    Kwa ni huyo rubani hakupaisha juu zaidi kwenye Anga za kimataifa ambako hakuitaji kibali halafu akaja kuishusha karibu na anga ya Tanzania?

    ReplyDelete
  33. Mlalahoi naona unawatetea kidogo watu wa ATC hasa ukiangalia pointi yako namba 4. na pia kusema hapo hakuna kufukuza kazi mtu.

    Jamani sijui Tanzania na makampuni kama ATC wanaprocedure za kazi hata kule muhimbili wale wapusuaji nadhani Procedures za kufuata hakuna.

    Jamani Tenda haiji hivi hivi, kwanza unakuwa na taarifa kitu gani unatakiwa ku-deliver, Step number one ni unafanya uchunguzi je unaweza ku-deliver?? ukishajua huwezi basi unawaambia jamaa very honestly samahani haya maji mazito sitaweza au kama umetambua unaweza ku-deliver meaning Ndege unazo, au mahala pa kukodi pa uhakika ushaongea nao na kuhakikisha ukiwapa tender kila kitu kipo kimaandishi na kuna kipengele kinachosema in case wasipo deliver ni muda gani kabla watoe taarifa na huu muda ukipita ni gharama za fidia kiasi gani walipe n.k, then unasema Ok nitaweza halafu step number two unafanya calculation ni kiasi gani utawatoza ili kukidhi mahitaji na kupata faida vilevile.

    Sasa Procedures zote zikifuatwa then matatizo makubwa kama hayo yatatambulika mapema na kuepukikwa.

    Sasa hawa wazembe tusiwavumilie, na kama walikuwa hawajui kazi basi aidha wafundishwe na kama walifundishwa wakazembea basi hakuna budi kufukuza na kuleta watu wanaoweza kazi au atleast kujifunza kazi. Wasioneane aibu kabisa, kumuonea mzembe aibu ni uzembe pia vile vile.

    ReplyDelete
  34. Inasikitisha mno, mimi nina dada ambaye yumo kwenye hilo kundi la mahujaji. Hizo 10% watu wanazozitaka ndio hizo zinawaumiza watu wengine. Ndege 4 zilikodiwa, mbili zimekuja zikachukua mahujaji wa Zanzibar na another group, wakaondoka as promised on Dec 8. ATC ikacancel the other two, promising kuleta ndege, mpaka leo zaidi ya wiki ndugu zetu wako stranded. Inshallah!!

    ReplyDelete
  35. Kwa kweli hii ni jambo la kusikitisha na aibu kwa taifa letu. Poleni mahujaji wote mliokwama hapo uwanja wa ndege.

    Haya sasa hatua inayofuata ni nini? Kuunda kamati ya kuchunguza chanzo cha hayo matatizo?

    Yaliyotokea yawe fundisho, na yasitokee tena katika miaka zijazo. Na kama ikibainika kuwa kuna watu wanaoshindwa kazi yao waondolewe mara moja.

    ReplyDelete
  36. Ni kweli kabisa utasikia kamati umeundwa. wawajibishe tu hao walio fanya upuuzi. Sijawahi kusikia tangu Nyerere aondoke kwamba kuna kiongozi aliyewajibishwa na Rais.

    ReplyDelete
  37. Haya wabeba mabox - nyie tupondeni tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...