Shikamoo kaka michuzi,
Mimi nimetengeneza website ya KAMUSI ya bure kwa ajili ya kusaidia watu wote, watanzania na wageni ku-translate Kiingereza kuwa kiswahili na vice versa .
Shukrani,
Kapinga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hongera sana Kapinga.Ila mimi kwa kutaka kuhakiki kama Tomaso kwa wasomaji wa biblia nimejaribu neno moja tu na kukutana na neno kuwa "Word not found" nikafikiri ndo tafasiri ya neno hilo.Baadae nikagundua kuwa niliiagiza kamusi hiyo kuleta maaana ya kiswahili toka Kiingereza hivyo nikajua kuwa maneno hayo siyo maana ya neno hilo.

    Sasa sijui hii kamsi yako ni ya maneno ya kiwango gani??Sikujaribu neno "Come" kwani naamini ningepata maana kwa kiswahili na kama ni hivyo maneno ninayoyajua yote ndo umeweka na nisiyoyajua hukuweka.
    Wasalaam
    Majita

    ReplyDelete
  2. hi five maaan!.....kama uelewi tafsiri!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwa kutupatia kamusi, lakini nataka kuomba wadau wajaribu neno hilo.

    select swahili-English,
    Type: Book,

    Very interesting answer, nilijaribu vice versa itakuaje.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  4. Kaka tunatafuta website za translation ambazo tunaweza kuweka sentensi au paragraph nzima badala ya neno moja.

    Je unajua website yoyote inayofanya hivyo? Kwa sababu website za kamusi za kiswahili ziko nyingi.

    ReplyDelete
  5. nimefurahi kuona umetengeneza kamusi, na nilikuwa natafuta neno la kiswahili kulitafsiri kwa kiingereza kwa mda lakini sikupata jibu, kamusi za internet nimezimaliza. nimejaribu na yako vile vile hamna. ni neno CHANGO, kumaanisha kusumbuliwa na tumbo kwa wanawake. sasa nimeshindwa kusema hospitali naumwa nini huku ulaya, sijui chango kwa kizungu ni nini.

    ReplyDelete
  6. majita..ahsante kwa maoni yako..bado website ndogo na changa, kila tupatapo muda huwa tunaongeza maneno..

    ReplyDelete
  7. Unajua watanzania tuache utani , nadhani huyu mtu ana wazo la kuanzisha kamusi ...

    ReplyDelete
  8. jamani watz wenzangu ili kupata maendeleo tuheshimuni hata ile kuwa na wazo la kufanya jambo la inaonyesha wachangiaji wengi wanaamini moja kwa moja jamaa hawezi.tuwape courage wenzetu hata kuwa ana wazo.thanks misoup

    ReplyDelete
  9. Nakupa pongezi sana sana. Wakenya wanaharibu Kiswahili, tunahitaji watu kama wewe kwa kweli. Ila bado kazi kubwa inahitajika kwani maneno mengi ya Kiswahili cha kisasa na hata cha kawaida yamekosa Kiingereza chake, mfano kashikashi, kinyemi, na majina mengi ya viungo vya siri hayana Kiingereza chake, sijui kwa nini?

    ReplyDelete
  10. Mjomba,nani kakipa wadhifa huo wa kutunga hiyo kamusi?au umejichagua mwenyewe? unayo qualifications gani...hebu acha mambo hayo na wataalamu tu!!!

    ReplyDelete
  11. sikujua mtu anahitaji kupewa wadhifa wowote na mtu yoyote kufanya atakacho (ulitaka jk au prof wa ud atoe tenda nini??)...sema kama imekuuma wewe hukufanya kitu hicho..usiogope mdau jitume...the internet is full of opportunities to be explored...im sure there is something u good at..he he hehe

    ReplyDelete
  12. Wabongo bwana eti nani amekupa wadhifa...hahaha...kamusi zote zilizopo kwenye mtandao uliwapa ruksa...???? Bongo bwana watu wanajifunga mikono kuogopa kuwa creative kwa ajili ya nyie ...nani kakuruhusu....ulimwengu wa mtandao kama upo bongo una computer na internet service ..umeme wa mgao ndio the limit na kama uko nje ya bongo mweee sky is the limit....Kweli amesikitika hakuiwahi hiyo tenda yeye...???

    Halafu huyo anayetafuta jina la ugonjwa wake ....never never never usiende hospital ukamwambia doctor unaumwa sijui ugonjwa gani ulioambiwa huko bongo...Nenda waambie naumwa tumbo na dalili za maumivu ni zipi na watakupima na wakupe dawa...

    Mimi nilikuja najua naumwa migrane for ages kumbe niko sensitive na bright colors. Wala sio migrane ila kwa vile na kichwa cha migrane kinachukia mwanga basi nikawa kwenye kundi hilo... Dawa na glasses..nina miaka mitano sijui kichwa kile kinaumaje tena...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...