niko na ndugu na jamaa kwenye kikao cha harusi. tamaduni hii imeshamiri vilivyo bongo na usiposhiriki unaweza kutengwa na jamii yako...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Utamaduni wa kushirikiana na kusaidiana katika raha na taabu ni urithi toka kwa Mungu maana alimuumba Hawa (Eva) ili washirikiane na kusaidiana na Adam. Lakini kwa udhaifu walioukubali wakashirikiana hata katika KULA TUNDA LA KATI WALILOKATAZWA!
    Nasi leo tupaswa kushirikiana latika vikao, michango ya hali na mali.
    LAKINI isiwe unafanya hivyo kwa udhaifu ulioukubali mfano:-
    Kwa Umaarufu (uonekane) au mtu unakubali kwenda kwenye vikao vya kitchen party mpaka unasahau majukumu mengine au mpaka unafukuzwa kazi au mnakutana mnachangisha fedha million moja na ninyi (wanakamati)mnatumia laki sita kwa kulewa chini ya kivuli cha matumizi kawaida ya kiutawala na sijui vunja jungu au unabobea kutoa michango kibao kwenye sherehe na misiba tuuuu wakati hutaki kuchangia shughuli nyingine za maendeleo kama vile elimu, afya n.k.
    Mwisho kwa wanaoomba msaada pia wawe na kiasi. Wasilazimishe kufanya mambo makubwa yanayozidi (kiwango) uwezo wao. Yaani unakamia tu eti mimi Harusi yangu lazima ivunje rekodi!! rekodi ya nani sasa, katika mashindano yapi, ili iweje???

    Nyakatakule Unyilisya Echalo

    ReplyDelete
  2. Hayo ni mawazo potofu brother Michu,huko kewtu ndo maana hatuendelei,mwezi uliopita nilikuwa huko kwa likizo nalishuhudia binamu yako alomost 5hours anashughulikia kadi za harusi na misimu kibao kuhusu kikao chajana yake cha harusi!ukweli hatuta fika mbali kama tutadekeza ujinga huu!5hours muda wa kazi masaa 3 yaliyobaki nalihesabu ilikuwa kupata supu kama lisaa 1 na nusu hivi!sasa ebu nambie huyu binamu yangu kwa ile siku alifanya kazi masaa mangapi?kama si saa 1 na nusun kwa muda wa kufanya kazi masaa 8 kwa siku?Iliniuma sana na hata yeye nilimweleza na hata yeye nafikiri atasoma huu ujumbe!

    ReplyDelete
  3. Sasa Bro Michu hicho kikao cha harusi umehudhuria ni kwa ajili Muoaji/Muolewaji alikuchangia kwenye harusi yako nini? Ni nadra sana kusikia Michuzi kahudhuria kikao cha harusi. Na hata ukihudhira nasikia ni bingwa wa ku-pleadge big amount lakini hutoi kitu na siku ya harusi unaingia ukumbini huku umebeba kamera zaidi ya mbili ili kujifanya uko busy. Na huanza kufakamia juice ili kuua soo wasije wakakusema hujatoa mchango.Au huwa unatoa halafu unachukua tenda ya kupiga picha hesabu zako ni kwamba utawapelekea maharusi na watu wengine picha zao ili kuwauzia na kurudisha pesa zako. Poa lakini kaka onyesha ujamaa kama siyo undugu kwa waliokuchangia.

    ReplyDelete
  4. Basi naona bro michu uko na uzi wako wa bwawa la maini..! Huku ukiburudika na coca...na si kirauri!!!!Ndovu inanikumbusha nyumbani..gongo kumi sasa..Duh!

    ReplyDelete
  5. nivizuri kuchangiana, lakini kama mtanzania tunafanya vikao vya namna hii marangapi katika kuchangia huduma muhimu kama afya na elimu au watoto yatima?

    hapa ukerewe kuna charity nyingi zinazo changia maendeleo ya jamii hazingojei serikali ifanye je sisi hapo nyumbani?

    au mambo haya yanafanyika katika makulaji tu? kwanini tusifanye kama Kenya wanaavyo changia mambo ya elimu(harambee)?

    ReplyDelete
  6. Jamni michu umetubania nasikia last weekend Faraja Kotta aliyekuwa miss Tanzania miaka hiyo ameolewa jamani mbona hujaweka walau picha yake mmoja blog hii naitegemea kwa mambo mengi na kila mara huwa nacheck kwenye hii blog kujipatia mambo yanayojiri mara kwa mara yule ni mtu maarufu aliiwakilisha nchi sio vbaya ungetuwekea picha yake jamani walau tukampungeza kwa wale ambao hatupata nafasi ya kumpongeza live. Hayo ni maoni yangu tu please if necesary yafanyie kazi .

    ReplyDelete
  7. TAMADUNI HII INAPOTEZA MUDA SANA NA RESOURCES NYINGINE PIA. WABONGO BADALA YA KUCHPA KAZI KAZI VIKAO TUUU, NDIO MAANA HATUSOGEI, KALAGABAHO!

    ReplyDelete
  8. Ina nia njema kwasababu mikusanyiko kama hii hujenga udugu na urafiki, ila kwakweli vikao hivi vimezidi sana..., na gharama zake ni kubwa.
    Nafikiri pia tuanzishe vikao vya kimaendelea, au vya kusaidiana. Kwa mfano kikao cha kumsaidia mgonjwa fulani, kikao cha kuwasaidia watoto waliokosa ada na vikao vingine kama hivi, kuliko vikao vya starehe tuuuuuuuuu!

    ReplyDelete
  9. Mi wala huwa sishiriki hivyo vikao.
    Na wanitenge tu!
    Na kwa taarifa yako SINA MKE wala MTOTO

    ReplyDelete
  10. Aisee hivyo vikao siku hizi vimekuwa ni sehemu za watu kutambishiana nani mambo yake ni safi zaidi.

    Wale wenye nazo hutangaza michango yao kwa sauti kuubwa kabisa kila mtu asikie.

    Wale choka mbaya (kama Michuzi) huwa wanakaa kimya halafu kikao kikiisha wanamvuta mwenyekiti au mweka hazina chemba na kutoa kamchango kao.

    Hata hivyo mara nyingi wale wanaotangaza madau makubwa tena kwa sauti za juu kabisa huwa ndio wanaongoza kwa kuingia mitini bila kulipa. Mweka hazina akiwa anafuatilia huwa anapigwa kalenda mpaka harusi inafanyika.

    Kwa hiyo kwa ufupi huwa wanatafuta sifa tu, especially wakiona kuna mademu wa rika lao (ambao may be walisoma nao enzi fulani, au waliwafukuzia wakapigwa chini) basi hapo ndio wanataka kujionesha kuwa wao wamewini maishani na mambo ya ni safi.

    Halafu kuna ishu nyingine ya Bwana harusi kutangaza kuwa atachangia kiasi kikubwa (aghalabu kuanzia laki sita hivi kwenda juu) ili kuhimiza watu wengine (hasa washkaji zake) kuchangia viwango vikubwa pia.

    Sasa utashangaa Bwana harusi anapoambiwa atoe hicho kiwango alichoahidi utasikia ooh laki moja nimenunulia suti, laki nyingine nimefanya mpango wa gari, na kadhalika mpaka baadae anakuja kutoa kiwango kidogo kuliko alivyoahidi, pesa zingine zote atajifanya ziko in kind.

    Siku hizi imekuwa balaa. Yaani sijui ndio maana wabongo hatuendelei. Mambo huwa hayaishii kwenye harusi tu. Kuna michango ya Kitchen Party, Bachelor Party, na mwishoni mwa yote wanakamati nao hukutana kuvunja kamati. Kama ulikuwa hujui maana ya kuvunja kamati ni kwamba wanakamati wanakutana kula cha juu (yaani pesa iliyosalia baada ya harusi kumalizika). Kwa harusi za kawaida (hizi za Tshs 5,000,000) utakuta cha juu kinachobaki ni kama Tshs. 200,000 hadi 300,000. Basi hapo wanakamati watakutana kwenye baa moja na kutafuna mbuzi huku wakishushia na serengeti baridi.

    Hivyo ndio vijimambo vya harusi na vikao vya harusi Bongo.

    //DM

    ReplyDelete
  11. Hivi vikao upuuzi na maudhi matupu hivi kwa nini mtu aoe au kuolewa kwa kutegemea michango? Kama hujajiandaa si usubiri au uoe au uolewe kinywa kinywa bila tarumbeta? Kwa nini upigiwe matarumbeta na magari kwa michango ya watu?

    Halafu kinachoudhi zaidi mtu unaalikwa wakati hata si ndugu kabisa wa Bwana au Bibi harusi.Na mtu anakung`angania mchango kama luba utafikiri ulimzaa.

    Harusi siku hizi zinaandaliwa na watu ambao si ndugu kabisa. Ndugu halisi hutupwa nje eti tu kwa kuwa ni maskini hawawezi kutoa viwango vile vinavyopangwa na hizo kamati koko za watu ambao si ndugu kabisa!

    Hata harusi zenyewe ndugu wa Bwana na Bibi Harusi hasa wale maskini wa vijijini hawawi na nafasi eti kwa kuwa hawakuchanga hela za kueleweka.

    Harusi gani hizo hadi baba mzazi na ndugu wa damu wa maharusi wanapewa kadi za mwaliko? Ndugu wa damu kweli wanahitaji kadi? Wao si ndio wenye harusi zao?

    Hivyo vikao visivyohusisha ndugu sio kuiga uzuingu bali ni ulimbukeni wa ma-bishow ya mijini yanayopenda mambo makubwa wakati familia wanazotokea ni maskini wa kutupwa.Hivyo wanataka kuiga kunya kwa tembo kwa kuonyesha uwezo wasiokuwa nao kwa kupitia michango ya watu ili nao waonekane wapo mjini na sherehe zao zilifana!

    Msiige kunya kwa tembo kama kauwezo huna kajifanyie kimya kimya hakuna atakayekudai wala kukuuliza.

    ReplyDelete
  12. Ujinga mtupu vikao vya kuchaniga harusi ya nini? Hili jambo lingeguzwa kwenye sekta ya Elimu ingekuwa vizuri sana. Hapo mpo kwenye vikao lakini nina uhakika wengine watoto karo za shule wanalalamika au mkiambiwa mchangie elimu ya juu mnataka kuandamana wakati harusi mnachangisha mamilioni. Naomba utamaduni huu uvunjwe haraka sana. Naomba hivi vikao vigeuzwe kwenye Elimu, tukianzia msingi hadi chuo kikuu

    ReplyDelete
  13. wana kamati wengine wanakupangia kiwango cha kutowa,hawajali kipato chako wala matumizi yako ya kifamilia.Utasikia michango inaanzia elfu 20 na kwendelea kama wewe una kielfu chako mbuzi chini ya 20 sahau.
    Jambo lingine la ajabu kwetu wabongo tunachanga maelfu kufanikisha harusi na kushindwa kuchanga maelfu ili kumtibu mwenzetu anayesumbuliwa na malaria mwishowe anafariki.

    ReplyDelete
  14. Comments nyingi humu zinalaumu vikao kama hivi. Mambo msemayo ni kweli, lakini nadhani mko likely kupata a positive response (ambayo nina uhakika ndiyo nia yenu) kwa kuanzia mahali pazuri yaani kwa kuona what is positive about the practice, halafu baadae mnaweza kushauri. Lazima nyinyi (ambao wengi mko huku Ughaibuni) muelewe kwanza culture na hali ya nyumbani kwa ujumla, halafu muelewe degree ya exposure ya watu wetu, kwa mantiki hiyo, kuwaambia mambo yao ni ujinga mtupu siyo uungwana, na haina tofauti na wakolono wazungu walivyoondoa na kudharau mila na desturi za mababu zetu wakisema zilikuwa za ki-jinga. Bottomline hapa ni kwamba kama nyinyi mmesoma (which I prefer to think you are) basi pasrt of the education should enable you to communicate na watu wetu effectively by being sensitive to their culture and norms. You can know all the truth in the world, but if you don't know how to communicate it to mankind, then you are just as useless!! Tusaidianeni kwa upendo!!

    ReplyDelete
  15. Wewe, Nyakatakule Unyilisya Echalo (Masikini Unuse Nchi)unafikitikila mtu Tanzania au duniani anaamini ya Adamu na Hawa?

    Sijui kama ulishawahi kuzungumza na wa-Twa (tuwaitao Mbilikimo) na kuwauliza walitoka wapi. Utashangaa!

    Wengine wengi wanaamini walitokea Bonde la Ufa na wala sio Bustani ya Eden.

    Wazungu siku hizi wanaamini hawakutokea Bonde la Ufa walitokea sehemu za Asia!

    AZrusi za ku-"show off"!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Bora hii mada imerudi tena ulingoni kwa njia nyingine na muafaka. Kuna siku Michuzi aliweka picha za shughuli zetu za uswahilini watu wakaponda kweli kweli. Lakini ni bora shughuli za kiswahili ngoma uwanjani na unafanya kulingana na uwezo wako. Sio hizo watu wanalazimishwa kuchangisha pesa na kama hakuchanga basi haalikwi kwenye shughuli. Hivi jamani huu ndio utamaduni wetu tunaojivunia sasa? Hata watoto wa familia husika pia hukatazwa kushuhudia harusi ya dada/kaka/mjomba/binamu (kadi huandikwa watoto hawaruhusiwi) kwa sababu ya kuogopa gharama. Hata hiyo ndoa itakuwa na baraka kweli?

    Kushirikiana ni muhimu turudi kama zamani tunashirikiana wote kwa shida na raha sio kukirihishana (kupeana karaha) kwa michango ya harusi, kipaimara, birthday, sijui graduation. Tufanye vitu kulingana na uwezo wetu. Hivi mkienda kanisani/msikitini mkafunga ndoa mkapika mlicho nacho mkala na ndugu na jamaa hiyo ndoa haitadumu?

    Watu wengine mpaka wanakopa ili kushindana mwisho wa siku wanaanza maisha wakiwa katika hali ngumu kipesa sababu ya madeni. Tabu yote ya nini hiyo jamani.

    Tubadilike jamani imefika wakati sasa tuangalie kipaumbele ni nini. Hapo January inakaribia watu wataanza lia na ada za shule sasa hivi, huku kwenye harusi ameahidi kutoa laki, nyingine elfu 50, (kwa mwezi waweza letewa kadi za mchango si chini ya kumi). Huku tunalia maisha magumu!!

    ReplyDelete
  17. Ndugu yangu unayesema kuwa watu wawe sensitive na culture. culture ya kabila gani hiyo? Culture ya wapi ndugu yangu wee. Hapo ni kuiga tu mambo tamaduni zetu haziko hivyo. Harusi ilikuwa ya wote kulingana na uwezo na ilikuwa jamii nzima wanashiriki kwa hali na mali. Hii culture mpya iliyokuja inaleta ubaguzi katika familia inavunja undugu inaleta msuguano na manung'uniko kwa wanaochangishwa na watakaochanga kidogo lakini hawataalikwa kwa kuwa haikufikia kiwango.

    Vile vile maharusi wanaanza maisha katika wakati mgumu sana kwa kuwa wanabidi wakope kama hawana uwezo ili watimize matakwa ya kamati. Shughuli ya kifamilia inatekwa nyara na kamati, familia kama ni ya kimaskini ina kuwa haina sauti wala hadhi. Bado tu tuichekelee hii kalcha mpya?

    Lazima tuikemee hii kalcha isiyo yetu. Siku moja Mgunga wa Mnyenyelwa alituimbia shairi linatuuliza kimantiki wakati wa misiba ndio tunaenda vijijini kusherehekea na jamii, tunapeleka vilio mbona na harusi hatupeleki huko kwetu tulikotoka. Ninalo. Sikuwa na jibu lakini ilitupa changamoto ya kutafakari haya mambo.

    ReplyDelete
  18. Ewe ndg. tulitoka wapi,

    Changia mjadala juu ya vikao vya harusi maana hilo somo la Evolutionism & natural selection ndilo ambalo wengine kwalo tumepata ndondo ya awali lakini baadaye nikawatoka wenzangu ma-Paleoanthropologists. Unafikiri ni asilimia ngapi ya Watanzania leo(nchini Tanzania) wanaamini kuwa
    mababu na mabibi zetu walikuwa MasokweMtu! Sambaza dodoso uone majibu.
    Mbona kama hawaamini ya Adamu na Hawa, Harusi nyingi bado zinafungwa Makanisani na Misikitini? Mbona wasiende kumtafuta mjukuu wa Dr. Leakey aliyeko Nairobi awabariki kwa maji ya fuvu la olduvai????

    Sikuelewa hitimisho lako ulipomalizia tungo yako kwa kusema 'Harusi za kushoo off!!

    Kwa kifupi kama wengi wenye busara walivyosema, ni kwamba ingawa wapo wanaofanya harusi kujionyesha si wote na kamwe suala la kusaidiana halitakwisha ndiyo maana tunatoa ushauri kuwa watu wafanye kwa kiasi na kwa kufuatana na uwezo na wa kuzingatia vipaumbele mfano pia kuchangia elimu, Afya n.k.

    Nanye Nyakatakule Unyilisya Echalo

    ReplyDelete
  19. Naona mantiki yako mchangiaji wa hapo juu, lakini tukiangalia the bigger picture nadhani unaipata point yangu. Mimi ninakubaliana kwamba hiyo inaweza kuwa siyo desturi yetu, lakini pia tukubaliane kwamba mambo mengine mengi tu siyo desturi yetu pia, lakini tunajaribu ku-keep desturi zetu kwa kuiga but at the same time maintaining the African flavor. Degree au extent (kiasi) cha kuiga kinaweza kutofautiana lakini nadhani unaelewa kwamba nia katika bigger picture ni nzuri - yaani kuboresha maisha ya mtanzania. Hao watu wetu nao wanapenda wapate raha, concept ya raha kwao ndiyo hiyo. Ni JUKUMU lako wewe msomi kuwaelewesha kwa upendo what is better for them, siyo kuwa tukana kwamba wanafanya upuuzi. Si huwa wanasema kwamba uko more likely kupata unachokitaka kwa kutumia asali kuliko ukitumia tindikali (Vinegar??) Point ni moja be nice wakati unaelimisha. Angalia hapa wazungu wanyokudharau, sasa kama na wewe unadharu watu wako, huoni kwamba you are not helping the situation?? Ni mawazo tu, nafahamu fika nia yetu wote ni njema, ila inabidi tuonekane kuthamini watu kwamba nao wana akili.

    ReplyDelete
  20. MICHUZI USHABIKI WAKO HUO UWE NA MIPAKA.WE NI MBONGO NASIO MUINGLANDO.

    ReplyDelete
  21. MICHUZI USHABIKI WAKO HUO UWE NA MIPAKA.WE NI MBONGO NASIO MUINGLANDO.

    ReplyDelete
  22. Bw. michuzi huu utamaduni ni lazima ufe. Mambo ya kuchangishana pesa kisha wachangiaji wakenda kuzitafuna kwa kugidia bia na manjonjo mengine yasokuwa na manufaa kwa siku moja tu halafu tunawaacha maharusi wanapiga miayo sio fea kabisa bwana. Hebu wanajamii tujaribu kuliangalia hili na ikibidi tuandamane ili kupinga maana kwa hapa bongo usipobeba mabango ukiangia barabarani hakuna mtu atakayesikuia kilio chako. Yaani hii tabia inapaswa ife kabisa.

    Ukiwaambia watu wakuchangie karo uende ukasome shule hakuna mdau atakayejitokeza lakini ukiwaambia wachangie ulevi utawapata wengi tu. Hivi sie watanganyika ( na waswahili wote kwa ujumla wake) ni lini tutaamka hasa tupende kuchanguia mambo ya maendeleo kuliko kuchangia mambo ya kupita tu?

    ReplyDelete
  23. KAMA HII MADA IMELETWA KWAAJILI YA KUPATA MAWAZO NA USHAURI. MIMI NAONA, WANAOTAKA HARUSI KAMA HIZI ACHA TU WAENDELEE KWANI HUWEZI KUWAZUIA, NI WATU WAZIMA, NA WANAFANYA KWA RIDHAA ZAO, KWA PESA ZAO, BILA KULAZIMISHWA. LAKINI, KWA UPANDE MWINGINE, HIZI HARUSI NDIO ZIMETUGAWA TOFAUTI NA ILIVYO KWA HARUSI ZETU ZA ASILI. HIZI HARUSI UTAKUTA ANAINGIA SHANGAZI MMOJA TU AU WAWILI, AU WANNE NK..WA BIBI HARUSI, NAO NI KWASABABU UTASIKIA WAMEPEWA KADI 50 KWA MFANO ZA UPANDE WA WAKWE. JE, KWA MILA ZA KIAFRIKA, FAMILIA ZETU ZILIVYO KUBWA, WENGINE WASIINGIE? TUJIULIZE, HUO NDIO UTAMADUNI WETU WA KIAFRIKA? MBONA MWENYE MCHELE KILO 2 HARUHUSIWI KULETA HUO MCHANGO, ILA PESA TU? NA TENA MWENYEKITI WA KIKAO ANAKUWA TOKA NJE YA UKOO MARA NYINGINE, NA ANASHIKILIA KANUNI KAMA YUKO BUNGENI! TUTAFIKA? HIYO mosi. Pili, UTAKUTA WALIOHUDHURIA VIKAO HAPO, HASA VYA MWANZO, WENGI WAO WANATEGEMEA MINGO ZA TENDA AU YA CHAKULA, AU PICHA, AU MATARUMBETA NK. HATA KAMA SIYO WAO, BASI WAPO HAPO KUMPIGIA DEBE MTU FULANI. HAPO KINACHOFANYIKA NI BIASHARA PIA! UKITAKA KUONA NI BIASHARA, NGOJA WAMNYIME TENDA YA PICHA MICHUZI HAPO, UTASIKIA MANENO! HATA KAMA BEI YAKE IKO JUU KULIKO WANAYEMTAKA APIGE, ITAPINDISHWA HADI MICHUZI APEWE, KISA NI MJUMBE MWENZAO. MIMI NAKUMBUKA NGUMI ZILIPIGWA KIPINDI FULANI, KATI YA MWENYEKITI WA VINYWAJI NA MWENYEKITI WA KAMATI KUU YA HARUSI. TENA WALIPIGANA BAADA YA HARUSI. MAANA MTU WA VINYWAJI, ALIUZA POMBE ZILIZOBAKI.
    SASA UNCLE MICHU, KUTENGWA UNAKOONGELEA WEWE NI KWA WATU WA UKOO WAKO AU WAJUMBE WANAOENDEKEZA HARUSI ZA NAMNA HII? MBONA HARUSI HIZI ZIMEWATENGA SANA NDUGU WA MAHARUSI NA KUTHAMINI TU WALIOCHANGA? HUKO SIYO KUTENGA? BWANA HARUSI AKITOKEA MORO NA KUFUNGIA DAR UTAKUTA NDUGU ZAKE WACHACHE SANA WANAHUDHURIA, SABABU YA KUTOMUDU GHARAMA. HUKO NDIO KUTENGA MIMI NAONA.

    MWISHO, UTAKUTA HELA SEHEMU KUBWA NI KWAAJILI YA KUJINAFASI WALIOCHANGA KWA MAMBO KAMA USAFIRI, CHAKULA, VINYWAJI,MZIKI, TARUMBETA, MC NK. KAMA TUNAFUATA STAREHE KWANINI TUSIENDE MAHALA NA KUSTAREHE NA FAMILIA ZETU? ZAWADI KWA BWANA HARUSI UTAKUTA NI TV AU FRIJI. NA BAADA YA HARUSI WANAANZA MAISHA YA SHIDA WAKATI HARUSI NI YA GHARAMA.
    ENDELEENI TU, MIMI HAYO SIYAWEZI.. MNITENGE TU!

    ReplyDelete
  24. MIE NIMEKUELEWA ISSA, NAONA UMEITISHA KIKAO SASA TAREHE YA HARUISI NI LINI ? TUAMBIE TUTAKUCHANGIA SIO UNAFICHA FICHA.

    ReplyDelete
  25. ndugu zangu i think we are missing a point here. mimi ninayeandika hii comment kwa standard za bongo ni kibopa(zimenitembelea).nikiwa na shughuli (harusi,graduation etc0 kwa kweli huwa ninaona karaha kuita watu na kuwaomba michango,lakini ndugu zangu believe me mswahili usipomuomba mchango ataona unajidai na hela zako na ukimpelekea kadi wallah haji,wadau mnabisha kwa hili? niulizeni mimi yamenikuta na nilikoma,harusi yangu waliishia kuhudhuria wafanyakazi wangu(kwa woga?).Hiyo ndo hali halisi kuchangishana sasa ndo norm na wala sio exception,tutaondokana vipi na hali hii huo ndo uwe mjadala.

    ReplyDelete
  26. Haya mambo yako sana huku bara lakini Unguja ukiwa na harusi ni wewe na jamaa zako na watu wakifika mlangoni wanapewa zawadi ya vilua au Udi na kitu chochote kile familia ambacho wanaona wanaweza kumudu. Na waalikwa wanakuja kama kawaida na maakuli yanakuwepo. Labda kwa kuwa zinakuwa hazina gharama kubwa kwa sababu hazina mambo ya Ulabu. Lakini wakati mwingine wenye uwezo wanalipia band za music wa taarabu. Cha msingi ni watu kufanya shughuli kulingana na uwezo wao. Na hao waalikwa kama hawakuchanga walicho nacho wanaweza kupeleka zawadi kwa bwana na bibi harusi, in cash au in kind. Mbona hao wazungu hawachangishi mtu kwenye shughuli zao? Sie huu utamaduni tumeutoa wapi wa kuchangishana pesa. Mtu asiniambie kuwa ni asili yetu hapana kwa upande wa kwetu sie asili ilikuwa kwa mwenye sherehe ndugu na jamaa wanakuja na chochote wakichojaaliwa kupata. Na hata wazaramo wao walikuwa wanajiandaa mapema kwa mfano wajomba na ndugu wengine wa umamani (matrilinear hawa) wanaanza maandalizi ya shughuli ya mtoto wa kike tangu yuko mdomo, watawekaa wee, kama ni nguo zitakusanywa mpaka binti anapovunja ungo na yu tayari kuolewa na kipindi anachokuwa amewekwa ndani basi na maandalizi yanaendelea polepole, mpaka siku ya harusi.

    Na hapo ngoma inachezwa kama siku hizi wanalete Rusha roho, na kinachopikwa ndicho kinacholiwa na watu hawalalamiki mbona siku ya 1 tumekula ugali, na siku ya mwisho tumekula wali. Hizi desturi za kulazimishana mtu lazima atoe kuanzia elfu 20 ndio aalikwe harusini tumezitoa wapi? Zimeshababishwa na nini? Tukijua chanzo tunaweza kujua namna ya kuepukana na hilo.

    Mwisho ni maharusi wenyewe lazima mfanye kitu ambacho hamna uwezo nacho? Nafikiri nyie wawili ndio mnaoweza kuwa na msimamo wa kuamua mnataka sherehe yenu ya ndoa iweje. Bila kufuata mkumbo na kulazimishwa na watu wengine halafu baadae mnabaki mnapiga miayo. Hiyo inawezekana, sikuwa na sherehe kubwa kwenye harusi yangu kwa sababu niliwaambia wanafamilia kuwa wakishangishana hizo pesa wanipe nimalizie kulipia ada University na nyingine zinisaidie kwa research ya dissertation yangu kwa kuwa nilikuwa mwanafunzi wa Masters Mlimani. Mbona hawakuchangishana!! na ndio ukawa mwisho wa kuburuzana na tuko kwenye ndoa mwaka wa 12 huu na watoto 3 na mahusiano mazuri na wanafamilia wote. Kwa hiyo suala la kutengwa ni hofu tu tuliyonayo kuhusu mambo yanayotengenezwa na jamii.

    ReplyDelete
  27. duh...machupa ya kangara na kimpumu pia...labda konyagi nayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...