Watanzania Uingereza wamwalika Rais Kikwete
na TA, london
na TA, london
JUMUIYA ya Watanzania waishio Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania imemualika Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kongamano kubwa la kujadili maendeleo ya Tanzania litakalofanyika London mwezi Aprili, mwakani.
Hayo yalisema na Balozi wa Tanzania nchi Uingereza, Mwanaidi Sinare Maajar, katika sherehe ya sikukuu ya Uhuru wa Tanzania zilizofanyikaJumamosi iliyopita katika ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa Wembley.
Balozi Maajar ambae ametokea kuwa kipenzi cha Watanzania waishio hapa, alisema kongamano hilo litakalosilikisha Watanzania wenyewe waishio Uingereza, wasomi wa vyuo,wafanyabishara na watu wengine maarufu waliokwishawahi kuishi au kufanyakazi Tanzania.
“Nataka kuwaambia Watanzania wenzangu kuwa sisi Ubalozi kwa kushilikiana na Jumuiya ya Watanzania tumemualika Rais na amekubali kuja kushiliki katika kongamano letu, lengo lake ni kujadili mambo mbalimbali ya Tanzania,”alisema Ballozi Maajar.
Katika sherehe hizo iliyohudhuliwa na halaiki kubwa ya Watanzania, iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza, ikiwa ni shughuli yao ya kwanza kuifanya tangu uongozi mpya uchaguliwe mwaka jana.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Bw. Abubakar Faraji alisema hatua hiyo ni mwanzo wa uongozi wake kuangalia ni vitu gani ambavvyo vinaweza kufanyika lakini vikaisaidia serikali huko nyumbani kwa faida ya Watanzania wote.
“Kweli tuna mikakati mingi ambayo kama mambo yatakwenda kama tulivyopanga tunaweza kufanya mambo mengi na makubwa kwa faida ya Watanzania wa hapa Uingereza na huko nyumbani,” alisema Faraji.
Alisema kongamano hilo litaweza kuwa mfano kwa jumuiya nyingine za Watanzania duniani kote na kuondoa dhana kazi kubwa ya jumuiya hizo ni kusaidiana kwenye misiba na kuandaa sherehe, bali na kuandaa makongamano makubwa kama haya ambayo yataweza kuisaidia nchi.
Katika sherehe hizo, mbali na Balozi Mwanaidi Maajar, wengine ni mbunge wa viti maalumu wa Singi, Mh Martha Mrata aliyekuwa kiongozi wa kuimbisha wimbi wa” happy birthday Tanzania”, Naibu meya wa Wilaya ya Ilala, Mohammed Yakub,Mwenyekiti wa CCM London,Bw. Maina Owin, na muasisi wa tawi la CCM Uingereza, Bw. Sharrif Maajar.


Hii idea ya wadau wa Uingereza kuanzisha Tawi la CCM mimi binafsi sijaipenda kabisa, maana sasa tunashindwa kujua ni vitu gani vitakuwa chini ya CCM na jumuia ya Watz waishio UK. Sasa mfano mkubwa ni hapo unaona kiongozi wa tawi la CCM naye alitoa salamu za siku ya uhuru wa TZ, na wangine wakianzisha matawi ya vyama vya uoinzani, si undugu na ushirikiano uliopo hivi sasa utageuka kuwa wa kivyama nk.
ReplyDeleteMimi nasema tu sijui wadau wengine mnaionaje hoja hii.
Mzee wa TBS
Ni jambo la maana sana na ni hatua njema ya kupongezwa.Natamani kila mtanzania angefika hapa uingereza ashuhudie self discipline za watu katika maisha anyway hawa walioko hapa wana mambo mengi ya kuchangia katika maendeleo ya nchi.tuna uhakika kila jitihada zitatufikisha kwenye maisha bora kwa kila mtanzania.
ReplyDeleteNI VYEMA SANA WATANZANIA WANAVYOJIWAKILISHA VIZURI UK. RAIS KIKWETE NI MWEMA SANA.
ReplyDeletenadhani sasa ni fursa kwa JK kujenga mtandao wa watanzania waishio nje ya nchi kuweza kuja na kuendeleza nchi hii kwa njia mbalimbali ikiwemo na uwekezaji katika sekta mbalimbali,kwani watanzania waishio majuu ni wengi na wana moyo wa kuja kuwekeza hapa nchini lakini viongozi wetu ambao sio waaminifu katika mambo mengi mnawakatisha tamaa sana kwani hamjali sana maslahi ya watanzania.JK safisha jina bwana hapo Londoni ili wajue kama upo kazini na unajali maslahi ya watanzania nadhani itasidia kujenga umoja wa kitaifa kwa kujali utaifa wao kuliko ilivyo sasa.
ReplyDeletemlau
I don't know what difference does it make. Mr President like to show up on things like soccer match, musical fastival, miss something competitions, but economy forums? No No, this what he will he is going to say " a i'm busy working in the office". Poor Tanzania, that country sunk already.
ReplyDeleteNdugu Michuzi,
ReplyDeleteKwa kweli sioni faida yoyote ya hii mialiko ya Rais wetu nchi za nje. Cha umuhimu ni kuendesha biashara sio kuongea tu bila ya kuwa na misimamo ya kiuchumi. Wenzetu nchi za Asia kama Malaysia na Indonesia, wapo mbali. Wamechukua muda mfupi tu kujiendeleza kiuchumi. Tuna viongozi wengi wana Ph.D katika uongozi wa serikali lakini hatuoni cha maana kinachotendeka. Umeme bado matatizo, barabara bado hazijapanuliwa, maji machafu na rushwa kila kona ya uchumi. Hivi ni vitu vya kwanza kusahihishwa, sisi bado tunasota hapa hapa. Sheria z a kibiashara bado ni za kizamani, haki za watu bado hazilindwi mahakamani. Narudia, sioni sababu za kuongea tu kila siku, mikutano laki moja kwa mwaka hayatatatua matatizo yetu, tunahitaji watu wafanye kazi na serikali ibuni sheria ambazo zitawasaidia wananchi kujiendeleza. Zaidi ya miaka 20 tangu uchumi wetu uwe huru na siasa za ujamaa, bado hatujatatua matatizo yoyote ya wananchi. Wenzetu akina Korea Kusini walikuwa masikini kuliko sisi enzi ya 1960, angalia wako wapi sasa. Sisi kazi yetu ni kupiga domo tu na kwenda nyumbani saa kumi unusu na kufungua moja baridi. Tanzania hata walala hoi wameridhika na maisha yao, nje ya biashara yangu dar, wabeba maboxi wakiingiza elfu moja tu, wanafunga ofisi na kurudi nyumbani. lazima tuwe wabunifu na wachapa kazi hasa, kama tunataka maendeleo kama ya wenzetu, lazima tuwe na uchumi wa masaa 24 badala ya kufunga ofisi saa 11 jioni. La sivyo tutajikuta hapa hapa tuu kwa Michuzi miaka 20 ijayo tunaitana wabeba maboxi na Wala vumbi huku wenzetu wanaishi mwezini.
Na mie naomba kuungana na anony wa kwanza hapo juu, hivi sijui tunafinyanga kitu gani! Na sidhani kama watu wote waliopo nje ni wafuasi wa CCM hii ni hatari. Nadhani balozi ni wa watu wote hebu tuachane na hii dhana ya uccm itatumaliza, kikichukua chama kingine itakuwaje?!
ReplyDeleteWabongo kwa kweli ni mabingwa wa kuchonga, yaani tunachonga sana. Hatufanyi kazi kabisa ni ziara na sisi sisi na ziara. Serikali haina mwenyewe sasa, watu wanagawana tu kale kanyama ka sungura kadri watakavyo huko mawizarani. Uchumi unazidi kudidimia wakubwa wamekomaa eti uchumi unapaa!! Ni wakati sasa kwa wakubwa kukaa chini na kuangalia mwenendo wa nchi, utendaji huko mawizarani ukoje, yaani hakuna msimamizi. Kila kukicha unasikia stori tu mawaziri wanavyosigana, huyu kasema hili mwingine anakanusha. Wakubwa wanapishana tu hapo eapoti, huyu anatua, yule anapaa.
Kama ni mdahalo Rais angeenda chuo cha IFM kuna kitengo cha mikutano ya moja kwa moja pale badala ya kumaliza nauli na posho za safari. Balozi Maajar naomba mshauri hivyo mheshimiwa rais ili pesa itayobaki itumike kununulia hata panadol hapo amana hospital.
ATAKUJA TU MSIWE NA SHAKA, ZIARA HIZI NDIO KAZI MUHIMU SANA KWA MAENDELEO YETU KWANI MUDA TUNAO. LAKINI MBONA WAINGEREZA WAISHI TANZANIA HAWANA MATAWI YA VYAMA VYAO HAPA NAPA TANZANIA NADHANI HAWA WANAJALI MSANA UZALENDO KULIKO VYAMA. NYIE MNA AJENDA ZENU ZA SIRI ILI MSIKAGULIWE MUINGIAPO NCHINI TOKA UINGEREZA.
ReplyDeleteOut of point altogether!!
ReplyDeleteHuyu mwandishi wa hii habari anapaswa kuwa makini.... habari unayotegemewa isomwe na maelfu ya watu n vizuri kuproof read sio kuleta ikiwa na makosa kibao.... nadhani sio ethic za uandishi wa habari. Kiswali lugha yetu hivyo tunapaswa kuipenda na kuitumia ipasavyo.. kwa mfano balozi umeandika ballozi.. kote kunakopaswa kuwa ri umeweka li... na mtu asiseme typing mistake kwa sababu haitakiwa haraka ya nini soma kazi yako kwa makini kabla ya kupost...
kwa watoa maoni wakichapia inaeleweka wengi huwa wanakuwa na jazba na haraka...lakini muweka mada anapaswa kuwa makini.
mpenda lugha
Jamani nyie mlio nje ya nchi mbona manataka kuleta matabaka?sasa chama kama CUF nacho kikiunnda tawi lake huko mliko na then vyama vingine vikafanya hivyo2 tutaishije huko kwenye nchi za watu?Mbona wao huku hawana matawi ya vyama vyao?Tena wao uchaguzi ukiisha tu kila kitu wanasahau mpaka uchaguzi ujao lakini sisi mmmmh!Na hasa ukichukulia CCM na CUF huku kwetu na hasa Zanzibar ni sawa na paka na panya?Hata rais anapaswa kulikemea hili,naungana na anony hapo juu aliyesema kama ni mdahalo rais aende pale IFM na wao wajikusane kule waliko,hasa hata hadhi ya urais itapotea kwa mtaji huu.
ReplyDeletehuo mwaliko gharama za kwenda huko watatoa wao au ni hela ya walala hoi? Wekeni video conference aone. kwa ni akiend ayeye ndio mtaongea la zaidi... Kupoteza hela za watanzania...kama mnataka aje mumlipie hela ya mfuta ya nde nyie, na watu wakoe wote anao wabeba..sio mwaliko halafu gharama iw e kwenye bajeti ya nchi....Hiii sioni ina umuhimu gani kumwalika yeye ...mwakilishi anatosha kama mnahitaji sana mtu kutoka nbongo.... sometimes vitu vingine ni too much na vinazidi kumaliza uchumi wetu....
ReplyDeleteWangeondoa kabisa haya mambo ya vyama nje ya nchi....vyama vya upinzania navyo vikianza kuweka vyao nje ya nchi sijui watamwambia nani alikosea....au hapo ndipo utaanza kuweka law? Sasa na CUF wakianzisha chama chao hapo raisi akifika hata wasalimu raia wake ambao hawako kwenye chama chake...Je na hicho cham kikimwalika raisi wa nchi aatakwenda kuwatembelea? Watu tuko wachache sana nje ya nchi haya mambo ya vyama tutaanza kuwa na magroup... ambao hawajajiunga na CC sijui wao wakienda kwa balozi atawashughulikia kama wana CCM....matabaka tunayaleta wenyewe na tuko nje ya nchi ....mweeee mimi yangu macho.
ReplyDeleteCCM imeshajua 2010 upinzania mkubwa kwa hiyo inaweka kambi nje ya nchi....ya nini???????
I have been reading articles like these for quite some time now. I am starting to be concerned that there is a motive other than helping Tanzania as always claimed to be the case.
ReplyDeleteOne should ask questions about who is going to finance this trip if the president is going to attend.
Second, before the president attends, what exactly these CCM members UK have done for the country to deserve the presidential �costly� visit.
I have seen and I know how we Tanzanians live abroad. I can guarantee that more than half of those people have nothing to give back to the country. Perhaps some few pounds to send home to their immediate families and ignorant prestige that they live abroad; There is no difference between a lot of Tanzanians living in UK and those living at home, so there should be no preference. Another issue that I would not talk about is crime, because in UK, like US if a foreigner resides illegally is committing a crime. More than half of those CCM members in UK are criminals. These are the only criminals that I know of, who get to or try to �dine and wine� with the president. I got to meet Mwinyi and Mkapa in New York and I have seen the talk that we Tanzanians abroad do when these officials come to visit, I am always amazed at the crap they pull. It is true that when these officials are abroad they become easily accessible to Tanzanians whom have no proper residency and are living on a paycheck-to-paycheck basis. For once, they cannot even go back home whenever they wish and second, they don�t have any financial security to invest in Tanzania; I think its getting over our heads.
When we talk about the presidential visit we should talk about big investments, which will be beneficial to the country. If these CCM members in UK want to have their foreseen economic credibility, maybe they should start by coming up with ideas, proposals and financial capital. Then, start with deputy minister in the ministry of commerce (That trip will not cost the country much). Once they have any venture in Tanzania that benefits Tanzania, then the President can consider a visit.
I have an idea, bring the president and arrange a $500 plate dinner. Then the money raised should be invested or given to an orphanage back home. This is how the political parties do in the US to raise money and I am sure they do the same in the UK.
As I said earlier, because the president is easily accessible when he is abroad it�s getting over our heads that we can come up with unthinkable thing like this.
Another thing I would point out and overly concerned about is the ambassador�s credibility, which I have not researched. I am surprised that the ambassador is even thinking that this is a good idea. Some things never change.
Lastly, we all know how strong CCM is and its apparent that if you want to get your foot in Tanzanian politics you have to get through CCM. So it is a smart move for some in UK to try and manipulate that possibility. Accomplishing this from afar is more than a dream that would impossibly come true.
Good discussion my fellow Tanzanian, the one wrote a long response in English. My worry is, you sound so negative. Try to research what other poor nd illegal people who live abroad are doing for their motherland. Let me tell you, you can't start from the air, you need to have talk first (infact you said it yourself in a way). You do not need to have money first as it seems to be your belief. And even the dinner you are talking about, can only be successful if somebody like Head of State is invited. The UK guys are very right and we need others to follow in another different way.
ReplyDeleteMimi nitafurahi sana kama atakuja na pia nitapa nafasi ya kuzungumza nae,mimi nilibadili uraia kwa nia ya kutafuta maisha, lakina nilichokipa nilichimba kisima kijijini kwetu kitu ambacho hata mbunge wetu hajakifa,lakini nikija bongo na nia yangu ya maendeleo navijiyuro vyangu,nanyanyaswa nakusumbuliwa kuingia nchini kwetu mwenyewe,lakini mzungu ambae kaja kuwekeza kwa nia ya kuchota alimasi zetu na vitu vingene anapita vizuri bila matatizo yoyote, naomba wadau msingope tumueleze rais hili.
ReplyDelete