Je Wanataaluma na Wasomi walio ndani na nje ya nchi, wafanye nini ili kuleta maendeleo ya kweli miongoni mwa Wanataaluma na Wasomi walio wengi na hatimaye kuleta maendeleo na kuiondoa nchi katika umasikini au kuleta utajiri bila kujiingiza katika siasa?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. michuzi tafazali weka hii mada inahusu hair products
    ili kujua kwanini dawa za nywele,na nywele za bandia zinatengezwa china,korea na watu wafanye nini kuhusu hilo swala wakati watumiaji wakubwa ni sisi weusi
    http://www.youtube.com/watch?v=p96aaTSdrAE&feature=related.

    ReplyDelete
  2. Michuzi eeh
    Swali lako ni la ajabu na halieleweki kwa jamii ya dunia ya sasa.
    KWA MJIBU WA:-
    1:Baba Yangu.SIASA ni sanaa ya kuelekeza na kusababisha kufuatwa kwa taratibu na sheria za nchi.
    2:WikiPediA:-SIASA ni Utataratibu ambao kikundi fulani cha watu hufanya maamuzi ya nchi.

    Kwa hiyo kama hizo ndo maana za siasa, kamwe hatuwezi kuleta maendeleo bila kujiingiza katika sisa.LAZIMA TUJIINGIZE KATIKA SIASA.Wasomi na wanataaluma wakijiingiza tu ktk siasa wanakuwa WANASIASA.Na wasomi wakiamua kukaa tu sehemu na kupanga maendeleo ya nchi tayari hicho ni kikundi cha watu kinachotoa maamuzi ya maendeleo ya nchi,na kwa mujibu wa wikipediA hiyo ndo siasa.

    Mimi Majita nimeshindwa kuchangia hoja hapa kwani kila ntakalo kuwanafanya na usomi wangu nitaishia kuhusisha SIASA.

    LABDA kama hoja hiyo itaondoa maneno "Bila Kujiingiza Katika Siasa" naweza kuchangia.Sasa naishia hapo kwani nikichangia inamaana nimetunga hoja yangu na kuichangia.Aidha nakushauri utoe maneno hayo tata.

    Dokezo tu ni kuwa wasomi wengi na wanataaluma wamesoma elimu nzuri kabisa na kuhitimu masomo yao vizuri ila HAWAJAELIMIKA.Wamesoma na hawaelimika.Siku wakielimika nchi Itaendelea.
    Majita

    ReplyDelete
  3. Adui wa maendeleo Tanzania ni rushwa,tamaa,kutoaminiana,kujuana na kubebana kulikopitiliza,ufuatiliaji na usimamizi mbovu au usioridhisha wa sera na mipango,watu kutojua wajibu wao na kutofanyia kazi ipasavyo(kudharau) kumbukumbu za kitafiti.Kiwango kidogo cha ubunifu(sera kama mkukuta nk zote tumetungiwa na wenzetu,je ni zote zinafaa kwenye jamii yetu?).Mambo haya niliyoyaeleza ndio yametufikisha hapa tulipo. Ili kujikwamua nafikiri jamii yetu tujitahidi kujitibia kilema chetu cha utekelezaji na ufuatiliaji,nionavyo mimi hapa ndwio msingi wa yote tukiweza kua na ufanisi hapa,maendeleo ni suala la muda tu.Hayati Sokoine alisifika kwa kua na uwezo mkubwa katika utekelezaji na ufuatiliaji hivyo maendeleo yanakuja kama kuna uongozi bora na sio maneno mingi

    ReplyDelete
  4. kAKA michuzi hebu nambie nasikia challenge inarusha na Great television je ninaweza kupata link ya kuipata hii TV online? au katika tv za Bongo ni ipi itajiunga kurusha?
    Nijuvyeni wadau kama kuna ajuaye maana kupitwa hii mechi ni kosa la jinai.Nasubiri

    ReplyDelete
  5. Let's see.Baadhi ya vigogo wa CCM wamepinga matokeo ya utafiti wa REDET.Spika nae anasema hakubaliani nao japo hajausoma kwa kina.Laiti matokeo ya utafiti huo yangesema kwamba umaarufu wa CCM umeongezeka au bunge linafanya kazi yake vizuri,basi ni dhahiri wangeyapongeza na kuyakubali.Inatueleza nini hapo?Kama tafiti za taasisi zinazoheshimika kama REDET zinapingwa kwa vile tu haziendani na matakwa ya watawala,unategemea watafiti (wasomi) wengine wapate changamoto wapi!Kama ilivyo katika nchi nyingine duniani,wanataaluma walio ndani na nje wanapaswa kuchangia maendeleo ya taifa husika kulingana na taaluma zao.Lakini kuna umuhimu gani wa kuchangia kitu ambacho kitapuuzwa?Ukiona mshindi wa BIG BROTHER anaonekana shujaa wa Taifa ilhali Mtanzania wa kwanza kushinda Nobel Prize Profesa Yanda amepuuzwa (ikiwa ni pamoja na wewe Michuzi kutomtaja) unategemea nini kwa wasomi?Unadhani kama mchango wa wanataaluma ungekuwa unazingatiwa tungeona madudu kama Richmond,IPTL au Buzwagi?Kama mwanataaluma niliyeko nje ya nchi nimefikia hatua ya kuthamini wale wanaothamini mchango wangu na sio wala rushwa na mafisadi.

    ReplyDelete
  6. Masahihisho:kumbe Michuzi uliinasa habari ya mzalendo mwenzetu aloshinda tuzo ya amani ya Nobel kupitia kwa dada Chemi.Ila mbona umeyachunia maoni yangu?Ulitaka mawazo,hayo ndio nilonayo.Weka hivyohivyo hata kama hayakupendezi (najua wewe mtu wa ccm).

    ReplyDelete
  7. wasomi na wanataaluma hawawezi kuchangia katika kuondoa umaskini ulio kithiri tanzania bila kujihusisha na siasa, nilazima washirikiane na wana siasa katekeleza yale wanayoona wasomi lazima kama taifa ili ifanikiwe kiuchumi ifanye nini.Nionavyo mimi viongozi wetu waju serikalini hawawthamini wasomi wataifa hili na kwa sababu hiyo basi hatutafanikiwa kamwe sikozote tutabaki tuki lalamika umaskini kukithiri vijijini mpaka hapo tutakapo wathamini wasomi wataifa hili kutoa michango yao yautafiti na kuyatekeleza ndipo tutakapo toka katika lindi hili la ufisadi na USEMI WA UKIPATA NAFASI CHUKUA CHAKO MAPEMA By raia mtiifu

    ReplyDelete
  8. Bwana Michuzi kumbuka maendeleo ya mtanzania hayataletwa na msomi wa ndani au nje au siasa ila maendeleo ya mtanzania yataletwa pale kila mtanzania atakapopona ugonjwa wa Rushwa, Uvivu, kupenda maendeleo yasiolingana na kipato wakati watanzania wengine wamefumba macho, ujambazi, wizi wa mali ya umma, umimi, kuongopea walala hoi, wizi wa kura za uchaguzi na ugonjwa usio na tiba wa kupenda hela zinazonuka. Hapa utaona tofauti kubwa kati ya watanzania wa nyumbani na Wale watanzania waliobahatika kwenda nchi za nje na kuona jinsi watu wanavyoangaika na kuthamini kazi zao bila kuwa rushwa, wizi, ujambazi, uvivu, uzembe, kuzibua vyoo, kubeba boksi etc..Watanzania hawa watakuwa wamepata nafuu ya magonjwa niliyoeleza hapo juu na hawatapenda kurudi nyumbani na kuambukizwa tena.. watasubiri hadi watanzania wote kule nyumbani watakapotoa matongotongo na kuona hawaendi mbele ila wanarudi nyuma kwa kasi ya ajabu..

    ReplyDelete
  9. its a difficult mada to discuss, sababu sielewi haswa nini kinatakiwa kuchangia. huwezi zungumzia nchi bila kuzungumzia siasa, hata serikali ni siasa, its one of the political party in power. sorry michuz

    ReplyDelete
  10. Wasomi tunatakiwa kuimarisha sekta binafsi na kujenga networks.

    Ukifikiria serikali huwa inachukua maximum 30% toka kwetu wananchi. Kwa hiyo ina maana kama wananchi tukijikusanya tuna pesa nyingi kuliko serikali. Kwa hiyo networks hizo zizidi kuimarishwa. Baadae iwe ni mambo ya kawaida kabisa kwa wananchi kujenga miundombinu kama barabara, vyuo vikuu, umeme na kampuni za kusambaza maji.

    Hiyo ndio vision ambayo wasomi inafaa tuwe nayo.

    dar.millionaire@gmail.com

    ReplyDelete
  11. Kama Dar International Airport hakuna hata feni za kupoza joto.
    Lakini ukiuliza unapingwa kwa sababu tu umekosoa unafikiri maendeleo yatakujaje?

    Kama wasema kweli wanatishiwa maisha yao, unafikiri wasomi watashiriki vipi ktk kuleta maendeleo?

    Na kama wafanyakazi wanalipwa mishahara ambayo kwa vigogo ni fedha ya kunywa pombe na nyama choma kwa siku moja. Hiyo rushwa itaondoka vipi?

    Kama unamlipa police mshahara mdogo sana, halafu unampa silaha alinde raia na mali zao! unategemea nini?

    unaweza kujaza kitabu cha maswali kama hayo. Cha muhimu ni watu wote kuwa waungwana, kuheshimiana na kuthaminiana.

    ReplyDelete
  12. Ili tuendelee hatuitaji wasomi kama watu wengi wanavyofikiri, maendeleo yanaletwa na watu wenyewe ka kuyapenda, usomi unakuwa ni kama kichocheo. lakini kama jamii haiko tayari (kama watanzania) hata ukimleta newton hakuna kitakachofanyika. yafuatayo ni mapendekezo yangu.
    1- badilisha mentality za watu ( kujenga utaifa na kuthamini chetu kwanza kama wakati wa baba wa taifa). 2 - badilisha serikali na mfumo mzima wa siasa (kwa mfumo uliopo hakutokuwa na maendeleo mpaka mwisho wa dunia)
    3. Jenga tabia ya watu kupenda kazi na kuchukia uvivu, na wahujumu wa uchumi ( Tuige mfano wa china)
    4. adhabu kali kwa wabadhilifu na wahujumu wa uchumi ( Watu hawa wahukumiwe adhabu ya kifo hadharani).

    ReplyDelete
  13. Hiyo nchi imefilisika,unafiki,majungu,ulafi,hata kama kashiba anakula tu na kuiba jasho la mtanzania.Kwanza tuache unafiki,kwa mfano juzi tu wanataalum wa REDET wametoa maoni yao kuhusu tafiti walizofanya kuona ni hali gani?watanzania wana imani na serikali yao.Kuna wapumbamvu nasema bila hata kufanya utafiti heti tafiti hazifanywi kwa muda mfupi[huyo kasoma shule ya wapi?].Naomba kuanzia sasa sio kuangalia vyeti tu lazima watu wapimwe na kufanya mitihani tena ili kujua kama viongozi wetu wano uwezo wa kutuongoza?.Rais ajue kuwa anatakiwa afagie au naye acachie ngazi.Tupo pamoja na rais na rais lazima afuate ushauri wa wataalam.Kama hafuati okey.INCHI YEYOTE ILE DUNIANI INAPATA MAENDELEO MAZURI NI KUTOKANA NA TAFITI NA USHAURI WA WATAALAMU WAKE [KAMA WEWE WATAALAMU WAKO NI WALE WA KUPIGA DOMO CCM OOOOOOYEEEEEEEEEEE,POLE SANA.

    ReplyDelete
  14. Kaka yangu nchi haijengwi na wanataaluma na wasomi tu. Nchi inajengwa ni kila mtu. Kama wasomi na wataaluma tu ndio wangejenga nchi basi viongozi wetu wote au kuwa mgombea uongozi ingetakiwa requirements iwe PhD and above....I mean PhD and 10 yrs of experience kabla hujaamua kugombea uongozi ...lakini sio hivyo...Nchi ni ya kila mtu na inajengwa na kila mtu...


    Kwa upande wangu ili nchi iendelee au kujiondoa umasikini anza na baby steps

    1. Know your people...yale mambo ya nyumba kumi kumi yangerudi kusaidia kupata idadi ya watu wote Tanzania bila kutumia mamilioni ya hela. Huwezi uakendelea kama hujui una watoto wangapi wa kuwalisha.... Kila mtu awe na mjumbe wa nyumba kumi na hapo ndipo patawezasha kupatikana kwa vitambuslisho n.k.

    2. Ukijua nani ni nani na anafanya nini na anaingiza hela ngapi kwa mwaka basi utaelewa jinsi ya kuallocate resources zilizopo nchini...

    3. Kodi ya the more you earn the more you pay ni muhimu. Hii hata kwa wafanya biashara sio kwa watu wamaofisini tu kila mtu alipe kodi. Na hizi hela sio ziende kwenye kuanzisha maidara tu na maofisi yasiyo na maana ni kuwasaidia wasiokua na kazi...matajiri na mashirika wakiona hela yao inaenda kwa wacheza bao mchana basi wata create jobs ili wacheza bao warudi kufanya kazi nao wachangie kodi.

    4.Give back to your community- Maendeleo yanaletwa na watu - Tuanze tabia ya kuchangia maendeleo ya nchi bila kutegemea kulipwa...Community service ni muhimu kwa nchi kupunguza gharama za ajabu ajabu.

    Sio lazima serikali itegemewe kupeleka maji vijijini...kama mtu unaishi huko una hela peleka maji kwa kijiji, kama mtu una hela fungua library watu wajue kusoma, kama unahela do something for your country...Huku watu wakifa tunaona wills zao kila siku zinasema hela hii iende kusaidia shule hii, hospital hii, kanisa hili etc lakini wabongo kwa uchoyo wills zetu ni watoto wetu tu basi hata kama mtoto wako amebarikiwa tayari na ana uwezo wakuishi mpaka afe bila kutegemea hela yako basi utamwengezea nyingine tu...Wape watu wasio na uwezo na utabarikiwa sana tu ipe kijiji chako kitafanya la maana na hiyo hela....

    5. Tupunguze idara sizizo na mbele wala nyuma na title zisizo na mbele wala nyuma...Income ikiwa ndogo kuliko matumizi ni deficiency. Je bajet za bunge vitabu vyake vuna balance kila mwaka au zikisha somwa hadharani the rest ni Mungu ndio anayejua? Kila siku tuna spend more than we earn and then tuna carry on madeni tu.

    6. Globolization ni nzuri lakini tuajiri watu wa nyumbani kwanza kabla ya kuwapa nafasi watu wa nje...Na hii iwe law anyeivunja ashitakiwe...kama kuna position fulani ya kazi kwenye shirika au office yeyote ni lazima zitangazwe kwa muda wa kipindi fulani wakikosa mtu anaye qualify kutoka nchini basi ndio watafute expart kutoka nje. Sasa hivi wamarekani wengi wamekimbilia nje ya nchi kwa vile kazi zilipungua na kazi zikirudi watarudi na wataajiriwa na nchi yao kama kawaida kabla ya wageni...Sasa sisi tumesahau watu wetu na kuwapokea watu wa nje wengi tu na kuacha vijana wasomi wakiwa hawana kazi. Ni shule ngapi za kitaifa zilizofunguliwa zina walimu wanaotoka congo, kenya, Africa kusini etc...? Unataka kuniambia mtu aliyemaliza chuo kikuu hawezi kufundisha darasa la kwanza mpaka form 4 ya medium english school hata kama major yake haikuwa education? Wake up guys....Kulivyo na shortage ya walimu US kamauna degree unaenda unafundisha high school vizuri sana tu.....

    7. Rushwa rushwa sushwa ni adui wa nchi....bila kuzuia hii hata iweje hamna kitakachoendelea..Kungekua na sheria kali ya rushwa basi kila kitu kingeenda kwa law na vizuri sana na wasio na hela wangeishi vizuri sana.Sasa hivi huendi mahali au hupati kitu bila kutoa kitu kidogo....Je tutaendelea hivi...Najua hatuwezi kuondoa kabisa rushw alakini hata tukigusa 50% tutafika mbali sana...

    uongozi ungeanzia chini kwenda juu sio juu kwanda chini....Yaani nina maana raia-mjumbe wa nyumba kumi- then mtaa-then town - then kata-then- sijui tarafa na kuendele...sio uongozi uliopo wa sasa rais- waziri- mkuu wa mkoa- wilaya etc....

    Good management na kujua wakureport kwake sasa hivi nadhani raisi akituma jambo lifanyike nahisi linaishia katikati kwa vile hamna mtu wa kumfikishi raia legally...kuna link in miss some where.... in reality there is no connection btn Our president and a regular citizen.......

    Nchi zilizoendelea atleast unajua kuna rank na wapi panaenda wapi...sisi hapo juuu TZ tuna vyeo vingi na watu wengi lakini ukienda kwenye ngazi za kata na vijiji kote kumesahauliwa na raia wako wenyewe wenyewe tu yaani it is chaos like a circus

    ReplyDelete
  15. "kamwe hatuwezi kuleta maendeleo bila kujiingiza katika sisa."

    "LABDA kama hoja hiyo itaondoa maneno "Bila Kujiingiza Katika Siasa" naweza kuchangia.Sasa naishia hapo kwani nikichangia inamaana nimetunga hoja yangu na kuichangia."

    "its a difficult mada to discuss, sababu sielewi haswa nini kinatakiwa kuchangia. huwezi zungumzia nchi bila kuzungumzia siasahauri utoe maneno hayo tata."

    ...YALEYALE YA "TUSICHANGANTE DINI NA SIASA", THESE GO TOGETHER...NI MIFUMO YA MAISHA.


    ...ILI HILO SWALI LAKO LIJIBIKE, UCHAGUZI UWE WA KIKWELIKWELI SIO MCHEZO WA KUIGIZA

    ...MATATIZO YANAANZIA KWENYE UCHAGUZI

    ...MPAKA SIKU HIZI KUNA BAADHI YA WABUNGE WANAZOMEWA!!!

    ReplyDelete
  16. Siasa ni utawala wa kuingoza jamii.Ni jukwaa la kuionyesha jamii kwa vitendo uwezo ulionao wa kisomi. Hivyo hakuna sababu ya kuzuia wasomi wasiingie katika siasa.

    Wasomi kuingia katika siasa ni vizuri sana tena sana maana ndiko kwenye kipimo pekee cha kujua uwezo wa Elimu au usomi wa mtu kama kweli unaweza jibu hoja za matatizo halisi na shida halisi walizonazo raia katika nchi.

    Kama msomi akiingia katika siasa akapewa cheo iwe kwa kura au kuteuliwa na cheo kikamshinda unajua wazi kuwa huyo si msomi bali ni mtu aliyekariri mitihani au alihonga akapata course work marks za bure ambazo sasa hawezi kuzitetea kwenye marks halisi.

    Wasomi waelewe kuwa kuzitetea digrii zao hakufanyiki darasani bali ni kule kwenye vyeo viwe vya ubunge,uwaziri,ukuu wa mikoa,wilaya,uongozi kwenye vyama,mashirika n.k.Msomi kazi yake si darasani au ofisini tu.Kwenye jamii ndio msomi anaweza onyesha umahiri wake wa usomi wake.

    Eneo ambalo wasomi waweza dhibitishia umma wa jamii kuwa wana kitu kichwani ni kwenye siasa.Siasa inawapa uwanja mpana sana wa kuthibitisha uwezo wao wa kuitumikia jamii kwa elimu yao wanayojisifia kuwa wanayo pale wanapoteuliwa au kuchaguliwa katika vyeo mbalimbali vya siasa.

    Tatizo la Tanzania ni kuwa kwa bahati mbaya tuna baadhi ya wasomi mabwege ambao wakiingia katika siasa huitumia siasa kuonyeshea ubwege wao tofauti na nchi zingine kama Marekani na Ulaya ambako wasomi wakipewa kazi ya kisiasa ni moto wa kuotea mbali kwa jinsi nchi watakavyoipeleka vizuri mpaka mgeni utamani kuhamia huko na kuukana uraia wa nchi utokayo kwa jinsi watumiavyo vyeo vya kisiasa kuonyesha uwezo wao wa vile walivyosoma.

    Baadhi ya wasomi wetu wakiingia katika Siasa hawajali tena professional ethics wanabaki kuwa watu wa blabla tu.Ndiyo maana hata watu wa kawaida hawaoni kama kuna umuhimu wa kuwa na wasomi katika siasa.Mfano niliwahili uliza unafikiri kijiji kinahitaji mwenyekiti mwenye digrii ya uchumi? Akajibu wa nini? Hakuna haja hata Raisi hakuna haja ya kuwa na msomi.Wa nini? Hata vijini wasiosoma wamekata tamaa na wasomi.Wamekata tama na wabunge,serikali,Mahakama na wasomi pia.

    Hata wasomi wenyewe sasa hivi wako frustrated baada ya kuona kuwa wasomi wengi wanashindwa kuonyesha uwezo kwenye siasa, sasa kelele imeibuka hata miongoni mwa wasomi wenyewe wakiwemo maprofesa kuwa si vizuri wasomi waweko katika siasa!!!! Lakini hili mimi naliona kama vile wasomi wanaona wakimbie aibu wakajifishe madarasani nyuma ya mbao za kufundishia baada ya wao kuonyesha kushindwa kuonyesha uwezo wao wa kisomi kwenye siasa kwa miaka 46 tangu tupate uhuru.Wanataka kujificha nyuma ya screen za Komputa na Laptop kwa aibu kwa kuogopa wasije kuzomewa kama wabunge wanavyozomewa kwenye misafara ya Kikwete na Lowasa.Mimi naona wanakimbia Challenge.Msomi gani mwoga wa Challenges? Mtu unasoma ili upambane na challenges.


    Napendekeza bodi za wasomi na mihadhara ya wasomi iwe inawaita wasomi wote walioko kwenye vyama vya siasa na vyeo vya kisiasa na kuwakalisha chini kuwaeleza wazi bila kificho udhaifu wao na kuwahimiza kuonyesha kuwa kweli wamesoma katika utekelezaji wa majikumu yao ili wasiaibishe taaluma walizosomea na vyuo walikosoma.

    Nchi hii ni ya wote wakulima,wafanyakazi,wafanyabiashara na wasomi.Na kila mtu ana haki ya kuwemo katika siasa.Sidhani hata kidemokrasia kama ni sahihi kusema wasomi wakae nje ya siasa ndipo wasaidie nchi si sahihi.

    Napenda wasomi waendelee kuwemo katika siasa ila kwa kweli wala si siri wasomi walioko katika siasa Tanzania na Afrika wanawaangusha wasomi wenzao na vyuo walivyosomea mbele ya mabilioni ya watu maskini wasiosoma wa Afrika.

    Wasomi wan chi hii waige wasomi wa nchi za Ulaya na Marekani ambapo msomi ni mkombozi wa nchi na wananchi na si mwangamizaji wa nchi na fisadi wa kupindukia ambaye hata wananchi wasiosoma kabisa hawataki hata kumwona.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...