wadau kunradhi, nimeamriwa niiweke tena juu hii mada ili wadau waendelee kuijadili kwa kina. kama mjuavyo tarishi hauwawigi, hivyo kazi kwenu...
Bro Michuzi,
Leo naomba niwakilishe mada nyeti na muhimu sana haswa ikiwagusa watanzaniatulioko nje ya nchi na naamini kama watu wakiijadili kisawasawa basi wengiwetu hususan wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi tutaifaidivilivyo na itaweza kutusaidia pale tunapotaka kufanya maamuzi muhimu yamaisha.

Mada: Je UKIMALIZA kusoma abroad (Specifically Bachelors, masters na Phd)URUDI nyumbani au UENDELEE na maisha abroad? Je ni kweli waweza lipwa au jilipa hela nzuri zaidi sawa au hata zaidi ya huku mamtoni? Je ni wangapi waliorudi wanafurahia maamuzi ya kurudi na kufanya kazi nyumbani? Je ni estimate ya dola ngapi kiwango cha chini makampuni Tanzania yatakulipa ukiwa na elimu kuanzia bachelors hivi??? hapa ni muhimu sana figure kamili zitajwe za mishahara watu tupate ka-idea!!

Akhsante,
Mdau mwakilishaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Bwana michuzi hii ni mada ya kipuuzi watu wengine waliopo nje ya nchi hujiona wapo tofauti sana na wengine hivi huyu jamaa anauliza kwamba yeye akirudi tanzania atalipwa mshahara kiasi gani hata elimu yake hajatuambia sasa sijui anataka tumueleze nini kwa taarifa yake hapa nyumbani wapo wasomi wengi sana mpaka wengine wamekosa kazi za kufanya yaani kuajiriwa tena wanaelimu ya juu san walizopatia hapa UDSM sijui unataka shahada ya vipi uikose hapa mlimani kwa taarifa yako elimu uliyonayo hiyo ya kufoji usitubabaishe nayo kabisa wewe utabeba box huko nje mpaka basi hapa nyumbani hatuna shida na mtaalamu yeyete sisi tunao wengi mpaka wengine hawajapata nafasi za kuajiriwa na sasa wamejiajiri wenyewe wewe huna elimu ya kuwazidi vijana wetu endelea kuvuna matunda huko ulipo hapa vijana wapo sawasawa hatukuhitaji

    ReplyDelete
  2. Duuuh HII MADA HII Ngoja niwahi kuosha VIBIBI VIZEE...

    ReplyDelete
  3. Du hayo madogo ya jamaa hapo juu mhhh unatutisha mbona tuliyosoma nje ya nchi au ndio chuki bonafsi bwana elimu ni elimu tu qualification ni sawa genaral knowledge ni kitu muhimu sana ok.huyo nae kama anataka kurudi home harudi kama vipi wewe endelea kua carer assistant hapa mpaka ukizeeka wakupeleke kweny mahomess ok

    ReplyDelete
  4. Huyu mtu anatuboa na mambo yaliyo obvious. Ulipoenda huko nje hukufanya Risk Analysis? think twice this issue is irrelevant usitupotezee muda. Mimi nipo nje na nmesoma degree zangu zote 3 hukuhuku but siwezi kaa kusumbua watu mara kumi wakati nina uwezo wa kufuatilia mwenyewe. USE UR COMMON SENSE BUDDY!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Mwuliza swali, inakuwa ngumu kukupa jibu sahihi kwani sijui wewe unaelimu gani. Vile vile elimu haimaanishi mshahara, japokuwa inakupa mwelekeo wa mshahara. Nina uhakika hata huko kwako majuu lipo hilo (mwaweza kuwa wote na Masters lakini mwingine akawa CEO akalipwa zaidi ya EURO 10000 na mwingine akawa mfanyakazi wa kawaida kwenye same co. akalipwa chini ya EURO 2000. Hivyo, cha maana ndugu yangu tafuta elimu yenye quality kisha katafute kazi yenye quality. Ukitaka kusuibiri majibu ya hapa kwenye blog basi tupo wale wa EURO 800 kwa mwezi Dar na wale wa EURO 15000 kwa mwezi Dar. , we mwenyewe umesikia kwamba Mh. Mkono kwenye kampuni yake analipa USD 500 kwa saa kwa mtanzania na USD 1000 kwa saa kwa raia wa nje. Sasa zidisha mwenyewe utapata ni kiasi gani kwa mwezi. Inategemea sana na urefu wa KAMBA yako ndugu.

    ReplyDelete
  6. hii mada ni nzuri,lakini imekuja juu mara nyingi kiasi kwamba nimeanza kujiuliza.je ni mada tu au kuna mtu anafanya research?kama ni research nadhani ethics zinahitaji iwekwe bayana ili watoa maoni wajue matumizi ya maoni yao,la sivyo ni kinyume cha haki na taratibu za kutumia watu kwa utafiti.kama ni mada tu ya kijiweni basi tuendeleze mchakato...zemarcopolo.

    ReplyDelete
  7. michuzi,mbona jibu ni rahisi sana,nyumbani hakulipi hata chembe na ndio maana wasomi wetu wanakimbilia kwenye siasa.kwa hiyo ni ishara tosha kuwa elimu bongo haina maana,iweje wasomi wetu washindwe kwenye chaguzi na watu kama hadija kopa,john komba,nk.

    ReplyDelete
  8. Bwana huyo anasumbua..! Sisi wote tuliosoma nje na kurudi tulifahamu fika working environment ya TZ. I am sure Africans wote South of Sahara na North of South Africa wanafahamu hali ya ajira na mishahara ilivyo makwao- kwa hiyo asituzingue!!!

    ReplyDelete
  9. USIRUDI BWANA. WE KAA HUKO HUKO UENDELEE KUZICHANGA. MAISHA POPOTE BANANGE

    ReplyDelete
  10. michuzi hii naomba uniwekee kwenye ukurasa wako.

    Kanisa la kiinjili la kilutheri birmingham,uk. linapenda kuwatangazia watanzania wote na wale wanaoongea lugha ya kiswahili,kuwa tumeanzisha ibada ya kiswahili ambayo hufanyika kila jumapili ya pili ya mwezi,na tutakuwa na ibada siku ya tarehe 9/12/2007 kuanzia saa 5.00 asubuhi siku ya jumapili birmingham univasity pale st francis church hall,east gate.unaweza kufika kwa basi au train hata gari binafsi parking zipo.mnakaribishwa wote.
    Tafadhali atakaye soma tangazo hili amwarifu na mwingine. kwa maelezo zaidi wasiliana na Postor John Evanson,telephoni namber 01442257058,07958681217

    ReplyDelete
  11. Suala hapa sio kuwa walio Ulaya warudi au walio bongo waende Ulaya!mbona hapa bongo watu wanaenda kufanya kazi Buzwagi,Geita,Bulyanhulu,nyamongo Nk.hizi ni sehemu za vijijini na maisha ya upweke na wakati mingine ubaguzi,lakini wanafuata hela nyingi zinazolipwa na makampuni ya madini.baada ya ku-make life yako unaingia Mjini,Dar unakula maisha,viyo hivyo hata mlioko ulaya kama unabeba boksi leo,cha maana uwe na malengo ya kusave hela zako baadaye urudi nyumbani kula matunda,"mchumia juani....."isipokuwa sasa,kama una degree yako nzuri,na huko nje unabeba boksi au kuopiga shower vibibi,bongo kuna opportunities,karibu! multinational companies,mabenki ya kimataifa,Donor funded projects,nk huku hakuna mizengwe ya serikalini,unafanya
    interview kama uko fiti wanakuajiri,mishahara ya kuanzia kwa bachelor degree ni around 800,000tshs-1,600,000tshs,most of the American funded NGOs wanalipa hadi 2000USD kwa mtu mwenye degree moja.naongea kwa experience yangu mwenyewe,i have a medical degree,ninalipwa 18000 USD,nikisafiri ni flight,nalipiwa kulala mpaka 100,000 hoteli,per diem 45000 na hii haihusishi taxi ,internet nk,pia nimepewa simu,postpaid 130,000 kwa mwezi wananilipia.na siko mwenyewe kwenye kazi kama hizi,i know a score of my friend with similar jobs.likewise migodini kazi fresh,free air tickets avery two weeka nk...so,kama mambo yako safi popote ulipo,mtoni au Bongo au kijiji chochote,la msingi ni ku-make money,usiogope kurudi Bongo kama umemaliza shule na kazi huko ni BOKSI,na pia mlioko Bongo kama hakieleweki,angalia uwezekana wa kutimkia mamtoni!!!!

    ReplyDelete
  12. Michuzi, achana na huyu jamaa. Last time alipewa maoni na watu zaidi ya 70. Sasa anataka nini tena?! Au unafanya Research ya nondoz zako? Acha hizo! This guy is not ready to take risks. Njoo u test zari, la sivyo baki huko huko. Usitake kutuchafulia Ijumaa yetu, watu tunakwenda kuchoma mbuzi saa hivi tukishushia na Africa's Finest(Castle Lager)- O'C -Sinza.

    ReplyDelete
  13. Huu sasa ni upuuzi,hata mtoa maada mwenyewe nazani hajakwenda shule na ana upeo mdogo wa kufikiri,hivi ni matatizo mangapi yanayokabili Tanzania( rushwa,huduma mbovu za afya,ukosefu wa ajira,miundo mbinu mibovu,elimu mbovu,ajali za kila siku,nk),Sasa watu na akili zao wanakaa kujadili swala la kukaa nje au kurudi nyumbani,Kweli Watanzania sasa tunazihirisha upeo mdogo wa kufikiri.Kwa kweli sioni hata kama kuna haja ya kuiita hii ni maada.Huu ni upuuzi.Mtoa upuuzi jaribu kufikiri mambo ya maendeleo.Kama mtu karudi nyumbani hilo ni swala binafsi na kama kabaki nje ni swala binafsi.Watanzania tuache ujinga au ndio lile swala la kichwa cha mwendawazimu.Haya!! yangu macho.

    ReplyDelete
  14. Babu mi ningekushauri rudi home.Inategemeana, hapa ukerewe watu wanasema mengi lakini kila mtu kutokana na experience yake. Mimi nipo hapa Ukerewe miaka mingi,own bussiness earning around £8000 a month. Hapa bwana kwa wanafunzi pagumu ila kama paper zimetulia unafanya chochote kama wenye nchi yao uwe au usiwe na Elimu yoyote. Hivyo kwa standard ya maisha hapa ni poa kuliko bongo.Kwa Elimu uliyonayo kama paper zimetulia hubebi box wala vibibi, na unadaka kila week, pamoja na nyumba wanakulipia wakati unatafuta kazi. Kama huna paper we rudi vumbini lakini kwa elimu yako pia vumbi utalisikia mtandaoni tu.Wakerewe wengi hapa ni raia na ni rafiki zangu wa karibu, graduates wote wana kazi bomba tu earning £2500 a month going up. Many are self employed earning thousands a week.
    GOOD LUCK

    ReplyDelete
  15. Mimi nina PhD. Mshahara wangu kwa sasa ni kama shs.5,400,000 kwa mwezi. Zaidi ya hapo kuna huduma zingine kama za bima ya afya, pensheni; na kama jobless nitalipwa na serikali huku kiasi fulani cha pesa sio shini ya tshs. milioni moja, na nyumba ninayokaa nitapewa fidia ya kodi. Nirudi Tanzania??

    ReplyDelete
  16. Michuzi naona huyu jamaa hakusikia la mkuu,yaani baba yake. Sasa ngoja sisi wa DUNIANI tumfundishe. Kijana mwanafunzi unaye soma huko njeni kwako mada imeshachuja. Watu tulifikiri unahitaji ushauri tukajipinda KUPOTEZA muda kuchangia mada kumbe wewe bwege mtozeni. Sasa kamuulize aliyekupeleka huko uliko labda atakusaidia. Kama hukuelewa mwanzo hutaelewa tena na wala si mwelewa. Na hata hicho kisomo si dhani kama utahitimu badala ya kuhitimishwa. Tafuta Mppppyyyaaaaaaaaaa. SIYO HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII. OK

    ReplyDelete
  17. angalia wala vumbi wasivyo na good manner,swali rahisi lakini wameanza matusi ya kazi za watu na wanaona wanaona wanapotezewa muda,kaa kimya kama hamuwezi kujibu ni hasira za maisha magumu au wivu tuu?
    wenu mbeba box.

    ReplyDelete
  18. nyie watanzania wa nyumbani kaeni na upuuzi wenu kama mlivyo maana hamnjui maisha na wala system ya nyumbani haifundishi maisha ya kweli,hamna Watanzania wengi wanaojenga ni wale wanao filisi makampuni, wala rushwa na wala si watendaji na watoto wa mjini kama akili mbovu zao zilivyo na wanavyojiita.badala ya kusimama kidete kujifunza kwamba watu wanatakiwa wafanye kazi na serikali iamue kutengeneza ubora wa maisha kwa kusisitiza watu wafanye kazi na ihakikishe kila kazi inamuezesha mtendaji wa hio kazi kuishi na kulipa madeni! ila nyinyi mnakalia umimi tu,hakuna mtu mmoja hata awe tajiri vipi anaeweza kutengeneza mabarabara, hospital na huduma za jamii.wachina walianza kusafiri zamani wana urai wa marekani na ndio wawekezaji na warudisha hela kwao na leo china na India ndio zina boom. hata hao wahindi wa nyumbani wamesafiri wanapassort mbili mbili na wanarudisha hela kwao, leo mppuzi unataka tu watu warudi nyumbani kwa kauli za kejeli eti box, watu wanasomesha ndugu zao hapa,wanalisha wanafamilia na hawana haja ya kujipendekeza kwa mtu ili ale, wewe unaesema una mshahara wa maana hapo nyumbani ndio mtumwa mkubwa kila kukicha unamnyenyekea kwa kumuita muheshimiwa,kila kukicha una dream kazi zenye madili.. fanyeni kazi na tengenezeni utamaduni wa kufanya kazi na sio kua na imani za kitumwa.acheni huo upumbavu tumechoka na umasikini wa hilo taifa na watu wake.

    ReplyDelete
  19. Mheshimiwa uliyeuliza swali,kama maoni zaidi ya 70 ulopewa last time hayajatosha basi wasiliana na REDET au ESRF wakufanyie research,labda utaridhika na matokeo yake.Nadhani wadau wengi walikuwa waungwana mara ya kwanza kwa kukupatia mawazo yao ya moyoni kabisa lakini sijui hujaridhika au vipi.My simple advice is:maisha ni popote depending na residence status yako,family background yako,level yako ya education na pengine afya yako (kama ina mgogoro na huko uliko unapatiwa huduma bora then ni vema ukabaki hukohuko,au kama una asthma halafu uko Siberia au huko kwenye extreme weather,then pengine joto la bongo litakusaidia).Finally,kwa vile uamuzi wa kuja huko uliko ulikuwa personal (implying that huku-seek maoni ya wadau) nadhani uamuzi wa kubaki au kurudi unabaki kuwa personal pia.At the end of the day,utakaenufaika au kuathirika na uamuzi wa kurudi au kubaki ni wewe mwenyewe.Ukitaka mawazo mengi utaishia kuwa spoilt of choice na pengine mwishowe ni kufanya blunder ktk maamuzi yako.
    Good luck

    ReplyDelete
  20. Aliyoomba mada ibandikwe upya sio mtoa mada ila ni mdau mwingine humuhumu kama mkisoma comment zote! acheni kukurupuka! Watu mada imewagusa wakaomba iwekwe juu wadau waendelee kumwaga mambo.

    ReplyDelete
  21. Wewe Anonymous wa 4.40 ndio unaekurupuka.Alokwambia mada imemgusa ni nani?Mbona hatujaona meseji kwa Michuzi kwamba mjadala urudiwe?Kila mtu anabeba mzigo wake wherever they are.Tusimchoshe Michuzi na maswali yanayohusu maisha yetu wenyewe,maana itaanza na nibaki au nirudi then kesho itakuwa nioe bongo au huku ughaibuni,au zaidi ya hapo nione au nisioe.Utu uzima ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi wewe mwenyewe.

    ReplyDelete
  22. Nyumbani ni nyumbani, lakini vitu vinavyokatisha tamaa ni RUSHWA - kila sehemu kuanzia unafika airport, unapita matrafic, hospital n.k sehemu zote swali la kwanza lazima lina mazingira ya kuomba Rushwa...I hate this!! Wizi, ujambazi... na mbaya zaidi linalokera ni tofauti kati ya yule aliyekuwa nazo (nyingi ni pesa zinazonuka) na yule asiekuwa nazo...Inauma sana uko kwenye second hand car yako toka Japan unapita barabarani watu wamesimama kama utitili..hakuna Public transport..Vipanya vibovu..roho inauma sana.. sio kwamba watu hawawezi kusave kununua magari mitumba lakini kwa nini kila mtu awe na gari..inauma sana..tuimarishe miundo mbinu.mimi na wewe peke yetu hatuwezi.. na hatuwezi kuwapa lift ndugu zetu wote..tutaoshia kusononeka moyoni na kutopata hamu ya kurudi nyumbani tukukikumbuka ..Rushwa, wizi, ujambazi, mazingaombwe ya uchawi, uvivu uliotukuka kwa vijana wenzetu wengi nyumbani, uzembe na tamaa za baadhi ya viongozi wetu, na kadhalika..Mora atupe nguvu, nia na ari ya kuweza kushinda vitu hivi kama wenzetu tunavyowaona..

    ReplyDelete
  23. Look this is simple.. kama huyu "cha maswali" anaishi US ama UK si asubiri JK akija amuulize hilo swali??? mama unaishi UK then njoo pale wembley kesho usiku ubebe na hizo nondo zako ukaamuulize hayo maswali balozi.. sijui kama hata atakuwa na muda wa kukujibu but im just suggesting! otherwise u might need to do "RISK ANALYSIS" kabla hujafunga vilago kurudi bongo maana madafu nayo yanashuka kila siku,UTAJIJU!!!!

    ReplyDelete
  24. Jamani, kwani kuna kilicho kigumu hapa, Bongo hata walio na pesa zao hawalali usiku! kinachoboa bongo unasota kupata hela yako ili maisha yawe mazuri lakini wengine wakiamua kuja kuchukua wanakuja kubeba kilaini na ukipambana nao wakubake wewe na familia yako, na wakupige risasi kama wakiamua. Huku tunabeba wabibi, lakini tunalala usingizi hakuna kushusha net kama vile umelala kwenye jeneza. Khaa, acha nipumzike Mbu, vibaka, malaria, kero za mawifi, na bila kusahau UKIMWI. najua Tz wenye pesa wanakufa kwa UKIMWI kuliko wasio nacho, ivo mnaojidai mnalipwa nyingi angalieni vichangu nao wanataka kuponea apo apo kwenye mshahara wako! NI MTAZAMO tu.

    ReplyDelete
  25. michuzi nami nikikuomba uirudie tena hii mada kwa mara ya tatu utakubali! nadhani majibu yalikuwa ya kuridhisha na kutosha hapo nyuma, watu sabini walijipinda na kumjibu huyu mtoa mada, anataka tu cut and paste back here!! toa mpya, na tutakujibu poa tu.
    mkereketwa

    ReplyDelete
  26. Mheshimiwa Anonymous wa [Friday, December 7, 2007 4:17:00 PM EAT] Thank you for driving the point home. Nafikiri we have all said it, but you have given it another perspective. Good Job!

    ReplyDelete
  27. MH. J.K alishasema kuwa kubaki
    bongo ni kugawana umaskini sasa kwanini tugawane mavumbi , short life span ,etc ...vijana tokeni nje muone wenzenu wanafanya nini...siyo kubaki kupiga porojo zisizo za msingi kwenye vijiwe visivyo vya maana .Nenda abroad uone watu wanavyochakarika , wanavyofanya kazi kwa bidii otherwise nkono hautaingia kinywani huwezi kumtegemea yeyote yule ni wewe na akili yako na nguvu yako tu .
    Hashim , New Zealand

    ReplyDelete
  28. Kazi kweli kweli!sasa we mtoa mada jamani!hizo degree zako ni za nini?maana usikute kumbe ni za kucheka watu au ni za kitu gani?!sasa cha msingi fanya hivi!we rudi nyumbani tu yaani hauna jinsi na mi nadhani umeingilia mlango wa kutokea,we rudi usije ukaleta msala bado mapema kabisa!umenisikia?

    ReplyDelete
  29. Nadahani hii ni mada nzuri kuizungumzia kwani wengi waliopo Bongo hawaelewi kwa nini watu wakija dunia ya kwanza hawarudi nyumbani. Tatizo ni kuwa nchi yetu bado haijaipa priority kazi ambazo zinaitwa "RARE PROFESSION" Kama Daktari, nurse, computer specialists, Laboratory technicians, scientist n.k. Kwa mfano nikizungumzia huku States, nurses wa aina yeyote (CNA, LPN, RN) analipwa vizuri kuliko maofisa wanaofanya mahesabu kwenye mabank, kwa sababu kazi yao ni highly risk kwa maisha yao samething applies to the doctors na watu wa maabara, mapharmacist. Hebu niambie tofauti ya mshahara wa nurse, doctor na karani wa bongo (there is no difference) Madaktari na manurse wanafanya kazi kubwa lakini wanalipwa chenji ndiyo maana wizi wa madawa na vifo vimezidi. Tatizo ni mfumo wa mishahara lazima uangalie mambo muhimu, usalama wa kiafya wa mfanyakazi, gharama ya elimu aliyotumia kupata ujuzi na muda uliotumika kupata elimu. Mtu aliyekwenda shule miaka 7 na mwingine kaenda chuo miaka 2 how could you pay them the same? HAYA NDIYO MATATIZO TULIYONAYO BONGO. MFANO PHARMACIST HUKU ANAANZA NA $ 60,000 TO 75,000, Register nurse tunazungumzia $20 - 30 kwa saa. TELL ME WHO WILL GO BACK TO BONGO AND RECEIVE TSH 400,000/ MONTH (HUU NI MSHAHARA WA SIKU MBILI WA REGISTERED NURSE HAPA USA).Natumaini JK amefanya kazi nzuri ya kurekebisha mishahara lakini sina details how good it is mwenye habari tafadhali tujulishe.

    ReplyDelete
  30. Mimi nadhani tujadili hii mada si kwa mabishano yasiyojenga ukweli ni kwamba nyumbani ni kuzuri mtu asikwambie kitu.haijalishi ni kiasi gani cha pesa unapata majuu lakini zawesha isha bila kujua unafanya kazi kulipa bills nadanganya ndugu zangu? maana mimi pia niko huko huko majuu.kuna watu kweli wamefanikiwa wachache lakini walio wengi ni kugumu.kwa mawazo yangu kuna watu waliondoka nyumbani miaka mingi iliyopita wakija kusoma na hawajasoma mpaka leo jamani niwe mkweli msirudi nyumbani maana nyumbani kuna wasomi sana na kazi ni nyingi pia lakini hakuna atakaye waajiri maana hamna elimu na hata ukirudi utashangaa watu walivyoendelea utakuwa nyuma mno hivyo utafit kwa sasa .lakini kama umesoma na unaelimu yako rudi nyumbani kuna hela na muda wa kuzitumia huku ni kazi tu hakuna ujirani kama nyumabi kila mtu yuko busy .mimi natamani hiyo june mwakani itafika lini nimalize shule nirudi nyumbani maana naona maisha mazuri yananingoja nyumbani.Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  31. ujumbe wangu nafikiri ni kumwiga baba wa Taifa Hayati J.K alitumia busara na hekima sana katika kutumikia nchi yake bila kudai msirahi ya juu ya mshahara ingawa alikuwa na uwezo huo. Na ninamshauri mheshimiwa ikiwa anania ya kurudi kufanya kazi hapa Nyumbani basi aje afanye makubalia na serikali na kulingana na Kiwango cha Elimu yake na aoneshe kazi yake kwa watanzania.

    ReplyDelete
  32. Ndugu zangu "wala vumbi" na "wabeba box" kwanza nawasalimia nyote. Kwani nyinyi ndio mtakuwa wa kwanza kumsitiri popote pale duniani mkisikia mbongo mwenzenu amekufa au anaumwa.

    You are my people, I salute you.

    Jamaa ameuliza swali ambalo anajua kama atafanya makosa ya kimaamuzi atajilaumu mpaka anaingia kaburini.

    Mimi binafsi yangu niko Marekani miaka 9 nimekwisha pazoea. Mimi ni Computer Programmer naandika softwares and web programming. Nina degree ya bsc info. tech, nina maisha mazuri lakini sitawasahau ndugu zangu TZ, najua bongo maisha ni magumu lakini ni nani wa kuwasaidia jamaa zetu huku, ni sisi huku tunaoingiza pesa nzuri kwa kufanya kazi yoyote, hasa hapa Marekani. Nina wajua vijana kibao wa kibongo ambao ni madereva wa "fork lift" wanaingiza pesa nzuri sana lakini sijui kama wana-invest huko bongo.

    Binafsi yangu nimejenga kwetu mjini "one of the best houses in town", man, its a beauty. 3 bed rooms, 2 master bed rooms,2 bathrooms, 2 half bathrooms, kitchen, dinner room, large living room, library, and storage room.
    Hii nyumba iko Tanzania.Imenigharimu lakini hivyo ndivyo nataka kuishi niwapo Bongo, na vitu vyake vya ndani kama Tv, kompyuta nilituma kontena toka huku, vingine nimenunua hapo hapo bongo kama double doors refrigerator "firiji ya milango miwili", na deep freezer "jokofu".

    Vilevile hapa nimenunua nyumba nzuri sana, si unajua huku tunavyonunua nyumba, benki "mortgage company" inakukopesha pesa yote ya kununulia nyumba na wewe unawalipa mortgage yao kila mwezi kwa miaka 10, 15 mpaka 30 ndio inakuwa yako kabisa bila deni. Lakini lengu ni kutumia "equity" thamani ya nyumba kufanyia mambo makubwa bongo, mpaka sasa equity yake ni $45,000. Kwani nimenunua nyumba kwa $170,000, na thamani ya nyumba sasa ni $215,000. Nasubiri kidogo kabla sijalamba hiyo $45,000. ambayo ni faida tupu.

    Bongo nina shamba la heka 50 ambalo limegawanywa kenye heka kumi kumi zinazobeba vitu tofauti.

    Ndugu yangu unaweza ukabaki nje hasa hasa Marekani na ukafanya mambo yako yote ya bongo ya maendeleo na hapa Marekani.Lakini inategemea aina gani ya degree umesomea , kama ni mtu umesomea,engineering na teknolojia ya sasa IT kazi ni nyingi mapaka utazikimbia,chukua hii anuani ya tovuti ya kazi kibao zanazolipa kwa nguvu lakini lazima madude uyajue siyo kubabaisha huku "www.computerjobs.com"

    Lakini kama umesomea masomo ya porojo utapita mbali kidogo utapata matatizo ya hapa na pale lakini mwisho ukishakuwa na experience mambo yanakuwa mswano tuu.
    Lakini lazima uwe na makaratasi. watu wa IT na wenye PhD mara nyingi waajiri wanakutafutia hayo majambo.

    Kumbuka ukiwa na PhD Marekani mara nyingi wewe ni mwalimu tuu wa college au university kwahiyo hizi taasisi zinachukua jukumu la kufuatilia green card yako. Na walimu wanaingiza pesa nzuri tu, si chini ya $85,000 kwa mwaka.

    Ila ndugu yangu kama uko ughaibuni ya India, Uturuki, Russia, ukraine, China , poland, bulgaria,
    South afrika na nchi nyingine,chukua nondo zako rudi Bongo. Hata nchi za ulaya ya Magharibi kwani kodi zao za makato ni kubwa sana, kwahiyo ile take home "net pay" ni kiduchu. Lakini kama una familia lazima uwafikirie watoto zako, ni bora wapate maisha bora ya kielimu na kimaisha.

    Uwamuzi ni wako kunyoa au kusuka.

    Salaam , "wala vumbi" na "beba box"

    Mdau
    USA.

    ReplyDelete
  33. Zingatia yafuatayo:

    Panda ndege hata kesho kama:

    1. Una jina kubwa

    2. Uko ready kujipendekeza kwa "wakubwa" na kusema "Yes sir" hata kama unafahamu hapo ni mahala pa kusema "No" (bila kuongeza sir mwishoni)

    3. Uko tayari kukubaliana na lack of the rule of law

    Usifikirie kurudi nyumbani kama

    1. Una prospects za kupata professional job ambayo itakufanya uishi comfortable

    2. Kama wewe ni critical thinker (maana critical thinkers hawana nafasi nyumbani)

    Be careful....

    ReplyDelete
  34. TANGU HII MADA IMEANZA NIMESOMA COMMENT ZOOTE KUANZIA YA KWANZA MPAKA YA 90 (70+20). YULE JAMAA ALISEMA ANAFANYA UTAFITI MUMPE MAJIBU MKAFURUSHA KAMA MBWA, SASA MNA UHAKIKA GANI KAMA HAKURUDI TENA KWA JINA LINGINE ILI APATE DATA?

    ILA NIMEGUNDUA MAMBO YAFUATAYO:-
    1. WATANZANIA WAKARIMU SANA WANAPENDA KUSAIDIANA MAWAZO (COMMENTS 90!)
    2. BAADHI YAO WANA PENDA MAJIVUNO NA KUJIONYESHA NA KUDHARAU WENGINE
    3. MAJIGAMBO MENGINE YANATIA SHAKA UKWELI WAKE UKILINGANISHA NA HALI HALISI YA MTU ANAKOSEMA YUKO ANATANUA
    4. WENGINE WANAPACHUKIA TANZANIA, KWA VISINGIZIO KIBAO LAKINI SABABU YA UKWELI ULIOJIFICHA NI UMASKINI ULIOPO TANZANIA NA UWEZO WAO WA KURUDI HUKO PENGINE NI MDOGO
    5. WENGINE WANAPENDA KURUDI LAKINI HAWANA UWEZO
    6. WENGINE WAMECHOKA KUISHI TANZANIA WANATAKA KUTOKA
    7. WENGINE WANA UWEZO LAKINI WANAENDELEA KUKUSANYA ILI WARUDI WAKIWA MATAWI YA JUU ZAIDI
    8. WENGINE WANA UWEZO ILA WANAPENDELEA KUISHI HUKO WALIKO NA KWENDA TANZANIA LABDA WAKATI WA LIKIZO KUSALIMIA
    9. MSHAHARA WA NJE AU TANZANIA SIO DETERMING FACTOR YA MTU KURUDI AU KUTO KURUDI.
    10. TANZANIA NAKO KUNA MISHAHARA MIKUBWA INATEGEMEA UMEAJIRIWA NA WAPI.
    11. HATA SEHEMU NYINGINE ZA NJE KUNA MAISHA MAGUMU KAMA HUNA STATUS YA KUELEWEKA AU HATA KAMA UNAYO INATEGEMEA NA NCHI ULIYOPO.
    12. WATANZANIA WAMECHOKA NA HUU MJADALA NA DALILI YAKE KARIBU MATUSI YATAINGIA ULINGONI.
    13. HATA KAMA NI RESEARCH, KWA KUTUMIA QUALITATIVE DATA NAFIKIRI MTAFITI AMEPATA DATA ZA KUTOSHA KUANDIKA DESETESHENI YAKE.

    HITIMISHO/CONCLUSION

    MICHUZI HIYO HAPO JUU NI SUMMARY YA KILICHOJIRI KWENYE MJADALA HUU, MDAU ACHUKUE HIYO SAMARI AKATENGENEZE ABSTRACT, NA HIZI DATA SASA NI WAKATI WA YEYE KUFANYA ANAYSIS.

    WASWAHILI WALISEMA NGOMA IKILIA SANA HUPASUKA! SASA UNATAKA NA HII IPASUKE? LETE MADA NYINGINE TUCHANGIE HII IMESHACHUSHA

    mswahili.

    ReplyDelete
  35. MCHANGO WANGU NI HUU,BWANA HUWEZI LINGANISHA MISHAHARA YA NJE NA TANZANIA HATA SIKU MMOJA,NIFUATISHE HAPA CHINI,
    1.Dr(medicine,dentist) mwenye degree ya kwanza Tanzania ananza na mshahara kama $350 hivi kwa mwezi ikiwa ataajiriwa serikalini na kama atenda Aga kan na kwingineko labda atalipwa $600-800
    OKAY,Dr mwenye hio qualification juu hapa USA(CA) ANALIPWA MSHAHARA KUANZIA USA $ 10,000 KWA MWEZI JE KUNA UWIANO WOWOTE HAPO?
    OKAY CHUKULIA HUYU BWANA WA US$ 10,000 ATAKUWA NA MATUMIZI YAFUATAYO KWA MWEZI

    -CAR NOTE $700
    -HOUSE MORG $2500
    -GAS-$200
    -GROSERIES-$300
    UTILITIES-$400
    MISCELLANEOUS-$500
    TOTAL-------$4600
    SAVINGS----5400

    TUJE NA JAMAA WA BONGO ANAYEPATA $ 500 KWA MWEZI

    -GAS-$200
    -GROSARIES-$80
    -RENT-$150
    -MISAADA KWA NDUGU-$50
    -MISCELLANEOUS-$50
    -UTILITIES-$30
    TOTAL-------560
    DEFICITY----60

    HAPO UTAPATA JIBU NDUGU YANGU NA NDIO MAANA ILI UISHI BONGO NI LAZIME.
    1.UPOKEE RUSHWA
    2.UFANYE DEAL CHAFU(IBIA MWAJIRI)
    3.FALSEFY DOCUMENTS WITH INTENT TO GET ILLEGAL MONEY
    4.MONEY LAUNDERINGS(DIRTY MONEY INCLUDING DRUGS etc)

    ReplyDelete
  36. Wacheni watu wapumzike malaria na vibaka, yaani hata kunywa bar huwezi eti mtavamiwa na kunyanganywa simu, khaa.

    ReplyDelete
  37. Michu,

    kusema ukweli hii mada safi sana kama watu wangeichukulia seriously. Lakini ndio hivyo tena, watembeleaji na watoa mada wa hii tovuti wengi tunapenda burudani zaidi kuliko ishu za maana kama hizi.

    Kama watu tunapenda maendeleo ya wenzetu, walio nje na ndani ya nchi ni vizuri kubadilishana mawazo na kujadili vitu kama watu wazima. Ishu kama ajira, ni kampuni gani zinalipa kufanyia kazi, ni stock gani zinapanda chati, ni taaluma gani ina market bongo etc. Nchi haitaendelezwa na wanasiasa au sera za chama ni sisi wenyewe ndio tutaendeleza nchi kwa sasa na vizazi vijavyo.

    Umoja ni nguvu jamani, sote sisi ni ndugu, na Tanzania ni yetu sote.

    Kuna watu wanadiriki kutukana wenzao kwa kuwa wamekamata nondozz, jamani ni ujinga gani huu? Tuwe wastaarabu na tukomae kidiplomasia.

    Mdau wa Newala.

    ReplyDelete
  38. Kwani we anony wa 4.40pm ni ndio admin wa blog hii?Mbona hatujaona mahala panaposema kwamba aliyeomba mada hii iendelezwe ni tofauti na yule aliyeileta mara ya kwanza.Kwavile katika original post hakuna jina la mwombaji,mtu pekee mwenye kuweza kujua aidha hilo ni Michuzi pekee.So,wewe ndio umekurupuka,just like hao wanaokurupuka na maswali ya kizembe kuhusu maisha yao binafsi.

    ReplyDelete
  39. Anon wa kwanza kabisa naona huna point ila chuki binafsi na walio majuu.. kifupi hata tulio majuu wengi tumepita hapo mlimani hayo unayoeleza pumba kila degree haipo hapo..pia international exposure muhimu sana hasa kwa elimu za juu kwani wafikiri kama kusoma kitabu cha juma na roza? kuna manjonjo yake kama hujui tulia.. mambo ya kurekebisha ung'enge nayo muhimu si unaona mambo yenyewe hate UDSM wanategemea vitabu vya mtoni au wanafudisha kwa vitabu vya DUP? huku unapata editions fresh toka oxford na cambrige .Hali ikiruhusu kusoma mtoni muhimu usiwakatishe tamaa wenzio.

    ReplyDelete
  40. Huyu anaeuliza hili swali hajielewi. Na hakika ni kati ya wanaokubaliana na ule usemi wa zidumu fikira za.........hata kama hizo fikra hazikubaliki wao waitikia ZIDUMUUUUUU.

    ReplyDelete
  41. Watanzania bwana, mada imetulia badala muendelee kuijadili mnaanza kuponda tu, we kama umechangia si unyamaze huoni wengine bado wanatoa maoni kwenye hii nyeti. Mtu alieenda shule atakubaliana na mimi kwamba mada hii nzito ndo maana bado watu wanachangia, sasa nyie mliochoka kaeni kimya someni page zingine acheni watu tuendelee hapa mpaka kitaeleweka tu. Jamani watu wa ma private company vipi figure za mishahara hiyo bongo? naona wa USA tu ndo wanatoa figures zao.Tajeni basi na nyie viwango hivyo? tehetehe liendelee hilo..

    ReplyDelete
  42. Ndugu zangu mnaongea sana mkiwa huko mkifika hapa kiswahili chote mfukoni... ...cousin wangu amekuja mwezi wa tisa Califonia kusoma master. Kabla ya kuja huku kila siku tukiongea naye ....yaani mimi nikimaliza kitabu tu narudi home Nijenge nchi. Yaani nashangaa wewe umemaliza shule ukaamu kuhamia huko...Mimi nilikua namsikiliza tu...Halafu huyu ni mtu wa pili kuniambia hivi...Guess what?!!!! hii sio uongo juzi ananiambia ehe bwana hivi ile lottery inaisha lini vile nisije nikasahau kucheza...Mara sasa hivi naangalia makampuni yanayoweza kunisponsor visa nikimaliza shule...Nilicheka kufa...hata miezi sita haijaisha nikamwambia umeshabadilisha mawazo?....

    Yuko bongo bwana mpaka utoke nje ya nchi ndio unajua wasanii wengi...

    Kwa hiyo nawaambia tokeni muone acheni kusema tu. Kama unaona jua kali bongo toka sio mseme tu...

    Kurudi kwetu muhimu...lakini mlia juani.....

    Tanzania everybody is chopping your dollar Sasa sisi kwetu wasanii wetu ndio wana do this to their own citizens. Just chop your dollar

    ReplyDelete
  43. hii ni mada nzuri but 4 sum strange reason kuna watu wanaongea 4 the sake ya kuongea tu.matusi chungu nzima..
    kwa mtazamo wangu,kurudi nyumbani ni suala la mtu binafsi, meaning a very personal issue.
    Mimi nilikua huko Ukerewe kwa miaka mingi,kuanzia high school mpaka university.na nilikaa kwa miaka 2 zaidi nikifanya kazi, legally.
    Niliamua kurudi nyumbani ili nijaribu maisha.Kusema kweli it has been the best decision I have ever made.
    Nimeajiriwa na kampuni ya nje na wananilipa US$ 3ooo. All my medical bills are taken care of na nina allowance ya simu na fuel as well.
    Kila mwezi natumia US$ 1ooo,na ninasave Us$2ooo.Nimeanzisha a boutique and nina a small catering firm which delivers snacks every morning to some cafes in town.Hivi vyote nimeweza kuvifanya kwa hio saving yangu ya lika mwezi.Kitu muhimu bongo is not how much you are earning, but how much you can save and what you invest your savings on.
    Bongo ukituliza akili,ukaepuka anasa zisizoisha,utafanikiwa tu.Ila ni muhimu kuwa na elimu manake vyeti vya huko,a little experience na exposure does actually make you very marketable huku.
    samahani nimejibu mada kwa kiingereza zaidi natumaini hamtanishambulia sana.
    much love
    ex ukerewe chic

    ReplyDelete
  44. Annon wa 7:19 mwisho nimependa mchango wako!

    ReplyDelete
  45. Anon 2;48 unalosema hulijui kwani kusoma vitabu vilivyotoka ulaya ni issue? usiwe mshamba kiasi hicho kutembea uchi kwa vile umevaa bikini iliyotoka ulaya watu waione Kwa mara ya kwanza napenda kumpongeza 1;19 kwa mchango wake hasa ktk kipengele kisemacho BAONGO UKITULIZA AKILI NA KUACHA ANASA ZISIZOISHA UTAFANIKIWA TU.ila ninachoweza kuongeza ni kwamba hata bila elimu hiyo mnayoisema ya juu mafanikio bado yapo makubwa tu mradi upate nakukubali ushauri mbalimbali utakaopewa na wengine ulio na mwelekeo bora mfano kuna mtu anaitwa MFUGALE ambae ni mmiliki wa mahoteli mawili makuu ya picock hotels historia yake ni nzito hana hizo elimu zinazosemwa humu ktk mjadala kifupi ni juhudi na maarifa ndiyo itakufanya uishi vizuri popote duniani ,kuhusu hali mbaya ya kimaisha Tanzania si kweli hata ulaya kama hujitumi utaishi vibaya tu mbona masikini wengi wapo huko ulaya?kuchanganya mambo ya kulinganisha mishahara ya nje na nyumbani si sahihi kama mnataka tuwe sawa na ulaya rudini basi na hayo materials yenu turekebishe uchumi hali ya uchumi wa nchi hauruhusu kutoa mishahara mnayotaka kila mmoja wetu ni mtaalamu ktk fani yake sasa wote nyie tukiwauliza mpo huko mnafanya nini utasikia mimi ni computer programmer mwingine sijui ni enginner wa nini sijaona mtu wa kilimo sisi tunasema rudini na mtubadilishe sio kukaa huko ndugu zenu wanakufa njaa hapa home ,hivi kuna sifa gani ukawa nje ya nchi na kulalama hovyo na wakati unayoelimu nzuri ambayo ingeweza kutusaidia sote kama utakuwa hapa nyumbani na baba yako,mjomba wako,mdogo wako,n,k pamoja ya kwamba umesota sana kupata elimu ni vyema basi elimu hiyo tuitumie sote umezaliwa TZ UMEKULIA TZ sasa unaona ufahari gani kung'ang'nia nje kwa kuogopa hali ya maisha TZ while your family are here in Tanzania watafurahia lini matunda ya usomi wako je kwa kuwaletea raba na jens naomba mjaribu kufikiri mara mbili2

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...