SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971 INARUHUSU MSICHANA KUOLEWA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 14 KWA RIDHAA YA WAZAZI WAKE. WADAU, HII IMEKAAJE?
ps: unaweza kuchangia mada hii ukienda hapa http://dailynews.habarileo.co.tz/ katika 'discussion pot'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. This is mad! Mzee Kikwete ana mtoto wa miaka 14 mimi nitest zali kama mzee atatoa baraka zake na ikiwa anakumbatia hiyo policy.Hii ni kama kuexploit watoto man.

    ReplyDelete
  2. Hii ni kama comedy fulani hivi, na kuna watu wanakubaliana nayo. Lakini mi siwalaumu wanataka kuwanyanyasa watoto.

    Msichana wa miaka 14 bado ni mtoto mdogo sana asiyejua lolote kuhusu maisha, in a long run lazima ndoa itakuwa na matatizo. kama mwanaume ni mkubwa na msichana ni wa miaka 14 baadae kutatokea kukibiana. Labdakwa mila kama za kimasai coz mwanamke hana say wala choice, which is too bad. mimi siiungi mkono kabisa sheria hii.

    ReplyDelete
  3. Michuzi,
    Naomba pia tuweke MJADALA JE MTANZANIA KUPEWA PASIPOTI KITANZANIA NI HAKI YAKE KIKATIBA AU MPAKA AFISA UHAMIAJI APENDE KUITOA.

    MDAU
    A-Towm.

    ReplyDelete
  4. MICHUZI,
    MJADALA?MDAHALO, Je mtanzania kupatiwa pasipoti ya kitanzania ni haki yake kikatiba au ni hisani(favour, kindness) toka Ofisi ya Idara Uhamiaji. Naomba mjadala huu ingawa umeingizwa kinyemela ktk suala la sheria ya Ndoa, Uwekewe 'posting' ya pekee.
    Mdau
    A-town
    Tanzania.

    ReplyDelete
  5. haingii akilini hata kidogo mtoto wa miaka 14 kuozeshwa mapema hivyo na hao wazazi wake watakuwa wana mtindio wa ubungo watakapomruhusu mtoto wao kuolewa,hata kama sheria itaruhusu hayo ni mambo yaliopitwa na wakati.kwa mimi binafsi yangu haina maana hii sheria itupiliwe mbali.

    ReplyDelete
  6. imepitwa na wakati they should change to 21 with parents consent.

    watu wa siku hizi sio watu wa zamani. msichana mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi akili yake na mambo anayofanya ni ya mtoto wa miaka 14 hata ugali hawezi kutengeneza

    kwa hiyo law mepitwa na wakati

    ReplyDelete
  7. Yakhee miaka 14 ni safi kabisa. Mtoto anakuwa m-bichi kabisa. Embe mbichi yaliwa kwa chumvi ukisubiri iive utakuta ina wadudu

    Halafu waambie Daily News waache kutoka kwa mgongo wako. Hatuna muda wa kupost kwenye blog mbili mbili.

    ReplyDelete
  8. HIYO INAWEZA KUWA SAWA.

    Msichana/Binti yeyote ambaye ni mtu mzima anaweza kuolewa bila tatizo lolote.Isipokuwa inategemea ni nani aliyetafasiri maana hiyo ya"MTU MZIMA"Kwa mfano:-

    1:Kwa mujibu wa WIZARA YA ELIMU,Mtu mzima ni binadamu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 13.Inafafanua kuwa nanukuu..."Mtoto yeyote aliyefikisha umri wa miaka 13 hastahiri kuandikishwa shule ya msingi kuanza darasa la kwanza kwani ni mtu mzima."Mwisho wa kunukuu.Hivyo basi Wizara inamwona msichana wa miaka 13 kama mtu mzima.

    2:Kwa Mujibu wa MILA NA DESTURI (Wajita)Mtu mzima ni yule aliyetahiriwa.
    Baadhi ya makabila mengine mtu mzima ni yule aliyeoa.

    3:Kwa Mujibu wa TANZANIA PENAL CODE ACT mtu mzima ni yule aliye na miaka zaidi ya 18.

    Hivyo basi binti wa miaka 14 anaweza kuolewa iwapo jamii hiyo imeamua kutumia maana ya mtu mzima kama 1 na 2 hapo juu.
    Majita

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli sheria iko sawa sawa kabisa. Kwani hapa bongo kwa umiri huo wasichana wengi sana huwa wankuwa tayari kuolewa. Kwani wengi sana huwa hawana nafasi ya kwenda mbele kishule, sasa wanaodai kuwa sheria ibadilishwe wanataka watoto wetu waende wapi baada ya kumaliza shule? Kinachotakiwa ni msichana awe amevunja ungo. Basi.

    Mambo ya kusema kwamba eti umri bado sidhani kama ni sawa sawa. Tutawapeleka wapi hawa wasichana wasioendelea na shule baada ya kumaliza shule.

    Bravo hiyo sheria. Iendelee hivyo hivyo tu

    ReplyDelete
  10. Watu mmeambiawa kujadili suala hilo (toeni maoni yenu kwa nini sheria hiyo inafaa au haifai). Sasa watu wengi wanakimbilia kutoa hukumu kwamba sheria hiyo inawanyanyasa watoto bila hata kunyesha kwa nini zinyanyasa watoto.
    Majita tu umetoa mwelekeo mzuri namna gani hoja hii inaweza kujadiliwa. Tatizo letu ni moja tu sisi watanzania. Tunasahau utamaduni wetu. Sheria ya nchi yoyote dunia inamtazamo wa kiutamaduni (embedded in culture).
    Kwa hiyo wakati sheria hiyo inatungwa kulikuwa na chembe chembe za mtazamo wa kitamaduni.
    Je utamaduni wetu umepitwa na wakati?
    Neno kwa ridhaa ya mzazi nalo liangaliwe vizuri, je wazazi wote wanamtazamo sawa kuhusu binti kuolewa? au tunahaja ya kuangalia ridhaa ya mtoto badala ya mzazi?
    Kama kuanzia miaka ya 70 sheria hiyo ilitekelezwa, kulikuwa na madhara gani mpaka tuseme sheria hiyo ibadilishwe?
    Mkumbuke kuwa wakati ule watoto wa miaka 14 walikuwa hawapo shule. Hivyo kwa kuwa watoto wengi wenye miaka 14 kwa sasa wanakuwa shule automatically hiyo sheria haitafanya kazi kwa mazingira ya sasa.
    cheers

    ReplyDelete
  11. sioni ubaya,
    kwani wasichan wa sikuhizi shughuli wanazianza na utoto, sasa ukiona mtoto wako wa kike, umri miaka kumi na mbili moto wa kuotea mbali, haoni hasikii, kwanini ungoje hasara, mtafutie mume, aanze mapema, sije akakutia hasara na vijukuu na magonjwa juu. mwana kulitafuta mwana kulipata. sheria imeundwa mahala pake.

    ReplyDelete
  12. Wewe bwege anon wa12:51 hapo juu acha ujinga nini cha kujadili kwa mtoto wa miaka kumi na nne wangeruhusu basi hata kupiga kura kuanzie miaka 14.Hakuna cha kujadili scrap this stupid law.

    ReplyDelete
  13. Mimi nafikiri sheria hiyo ilitungwa kuzingatia kuwa mwananke hubalehe alikiwa na umri kuanzia miaka 14 na kuendelea hivyo anauwezo wa kutengeneza watoto na kuhalalisha ukomavu wa kimaumbile bila kujali ukomavu wa akili.Hivyo basi ni muhimu sana sheria hii ikaangaliwa upya kutokana na kuwa walioitunga kipindi kile hawakuwa na upeo wa mtazamo kuwa siku moja mwanamke atasoma,kufanya kazi na hata kuongoza nchi.Kutokana na kuonekana kwa mapungufu hayo inabidi iangaliwe upya angalau kufikia miaka 18. Namna hii itapunguza watu kuwaoza watoto wakiwa na umri mdogo hata kuwatoa mashuleni.Mwanamke aliye komaa kichwa huendesha jahazi la ndoa kwa umakini na busara kubwa.

    ReplyDelete
  14. hapa mimi naona kuna vikundi viwili
    CONSERVATIVES-wasiotaka mabadiliko ya kuendana na wakati.Mfano huyo jamaa anayesema "hasara".Huyu jamaa bado yupo miaka ya gizani ya wasichana kuonekana kuwa ni mitaji.
    LIBERALS-wanaotaka mabadiliko kulingana na wakati.
    Bwana majita umenukuu kwenye kipengere #1 kuwa mtu mzima ni yule mwenye miaka 13 na hawezi kuruhusiwa kuanza shule darasa 1,kama nilivyokuelewa ni juu ya kuanza shule si kuolewa.
    Kwa wale mnaoisapoti hii sheria sidhani kama mtaruhusu vibinti vyenu(kwa wale mliokuwa nao) waolewe wangali wachanga namna hiyo.Kwa kweli hii sheria imeshapitwa na wakati,haina nafasi katika jamii hii ya sasa.Kumbukeni kuna sheria pia inayopinga mtu kutembea na mtoto wa shule,sasa mtoto wa miaka 14 kwa miaka hii bado yupo shuleni kama si darasa la saba(wale waliochelewa) basi ndo atakuwa kaanza form 1.Mnaosapoti hii sheria hampo kwenye karne hii bado mnaishi miaka ya 1970 kwenda nyuma

    ReplyDelete
  15. We annon Dec 5 :3:37 PM EAT unaonekana wewe ndo bwege kabisa na hata hujui unachosema. Nadhani pia shule yako ya hovyo na kwa hakika hukustahili kusema lolote hapa kweye hii mada. Sheria ya kupiga kura na sheria ya kuolewa haziko sawa hata siku moja. Hakuna sheria ambayo huwa iko sawa na nyingine. Maana kungekuwa hkuna maana ya kuitunga kama inaingiliana na nyingine.

    Kwa kawaida, mtu kuwa tayai kuolewa siyo kwamba ndo yuko tyari kupiga kura. Mpiga kura ni mtu tofauti kabisa kabisa na anayeolewa na uwezo wao wa kufikiria pia ni tofauti.

    Kwa hiyo usije ukadhania kuwa mtu anayeoa au kuolewa ndo anaweza pia kupiga kura. Siyo lazima! Kule ulaya ukimakamatwa na binti wa chini ya miaka 17 umekwisha habari yako. Lakini akiwa na 17 na kuendelea hakuna neno. Ni mtu mzima. Lakini hakuna nchi inayoruhusu mtu wa miaka 17 apige kura.

    MADA KAMA HIZI UKIONA HUNA POINTS USICHANGIE. HII SIO KAMA MADA YA KUTAFUTA KAZI ULAYA. NI MADA INAYOTAKA UFAHAMU WA HALI YA JUU. Kama huwezi sema points kaaa kimya angalia wengine wanasema nini.

    Acha wehu

    ReplyDelete
  16. Mahakama ya KADHI bado hali ni kama hivi. Je ikija tutaenea kweli humu bongo...............

    Mahujaji wadai kichwa cha mtu

    na Mobini Sarya


    SAKATA la mahujaji zaidi ya 1,500 waliokwama kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya hijja, lilichukua sura mpya jana baada ya mahujaji hao kuonyesha hasira na kusema aliyesababisha kushindikana kwa safari hiyo hadi jana, alistahili kuchukuliwa hatua kali.

    Wakizungumza kwa jazba jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, walisema kuwa kosa lililofanywa na kuwasababishia wao kushindwa kutimiza moja ya nguzo tano muhimu za Uislamu ni kubwa mno.

    Mahujaji hao, akiwemo baba mkwe wa Rais Jakaya Kikwete, waliokuwa wasafirishwe na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATC) kwenda Mecca, Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya hijja, wamekwama kwa siku kadhaa Dar es Salaam, baada ya ATC kukosa ndege ya kuwasafirisha.

    Huku siku za kuswali Imrah zikiwa zimekwisha, mahujaji hao waliamsha hasira na chuki jana wakisema kuwa watu waliowakwamisha wametenda kosa kubwa kuliko hata kuua na wanapaswa kukatwa vichwa kwa mujibu wa maandiko ya dini yao.

    "Tumenyimwa haki yetu ya kwenda hijja, watu waliotukwamisha kwenda huko huku tukiwa tumekamilisha taratibu zote, wametenda kosa baya kuliko kuua na wanapaswa kukatwa vichwa, hata kuwakata vichwa tunaona ni adhabu ndogo kwa sababu kwa mujibu wa maagizo ya Mwenyezi Mungu, kumzuia mtu kufanya ibada ni mbaya kuliko kuua.

    "Tutajadili hukumu yake baada ya safari hii kushindikana kabisa, kwani adhabu ya kuua tu haitoshi kwa sababu wamewazuia watu wasiende kufanya ibada yao," alisema mmoja wa mahujaji ambao safari yao iliandaliwa na Taasisi ya Muslim Hajj Trust wakiongozwa na Juma Nchiha.

    Hata hivyo, mahujaji hao wameitupia lawama serikali kwa kushindwa kutoa ndege ya dharura kwani ATC ni shirika lake na mwenyekiti wake, Mustapha Nyang'anyi aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

    Naye baba mkwe wa Kikwete ambaye ni baba wa Mama Salma Kikwete, mzee Rashid Yusuph Mkwachu, aliyekuwa ameongozana na watu wanne wa familia yake, alisema kuwa kwa wiki nzima amekuwa akiaga Ikulu kwamba anasafiri, lakini safari hiyo inashindikana kila mara jambo ambalo si tu limemchosha, bali pia limemkera.

    Akiongea huku akiwa anatembeatembea kama sehemu ya mazoezi baada ya kukaa kwa muda mrefu, mzee Mkwachu aliwataja watu anaoongozana nao kuwa ni mama yake mdogo Salma, Jamilah Omari, shemeji yake, ambaye ni mjomba wake na Salma, Hassan Mohamed Kinyozi na dada wa Salma, Mwanakombo Bakari.

    Alipouulizwa ni kiasi gani cha gharama amelipa kwa ajili ya safari nzima, alisema kuwa hajui kwani yeye aliambiwa tu ajiandae kwa safari hiyo ya hijja. Hata hivyo, mawakala wa kuwasafirisha walisema kuwa kila mtu alipaswa kulipa dola za Marekani 2,400 ambazo zinajumuisha gharama za malazi na chakula.

    Mzee huyo ambaye anasafirishwa na tasisi ya Muslim Hajj Trust, alisema kuwa kilichowakwamisha hapo, anafikiri ni kuhujumiana kwa mashirika ya ndege, ndiyo maada wameshindwa kuondoka na kubainisha kuwa ingawa hii ni mara yake ya kwanza kwenda hijja, lakini hajapata kusikia watu wakikwama kwa kiasi kama hiki.

    Katibu wa Taasisi ya Alh-Bir, Abdallah Harith Mohamed, alisema kuwa waliingia mkataba na ATC kuwasafirisha kwa safari hiyo ya hijja baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya ATC, Nyang'anyi, ambaye ni Muislamu na mtu aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Saudia Arabia, kuwaomba Waislamu kusafiri na kampuni yake baada ya kuwa ameteuliwa na rais kuiongoza.

    "Sisi tulikuwa tumeachana na shirika hili, hata Taasisi ya Jambo Travel wao kwa miaka 10 walikuwa wakisafiri kwenye shirika la Emirates, ni mwaka huu tu… Mustapha Nyang'anyi alikuja kutuomba tukaona ni Muislamu mwenzetu kumbe ni matatizo matupu," alisema Mohamed.

    Alieleza kuwa wakati taasisi zote zinaingia mkataba na ATC, walielezwa kwamba wana ndege ya kukodi aina ya Boeing 747-100 yenye uwezo wa kubeba abiria 480.

    Hata hivyo, alisema ilipofika Novemba 30, ATC wakawaambia ndege hiyo imeharibika, lakini hadi sasa hawajaletewa ndege nyingine licha ya kuwekeana mkataba.

    Aidha, alisema kuwa kampuni hiyo imewatia hasara kubwa kwani kila mtu anayesafiri kwenda huko, kabla hajagongewa visa, lazima awe amelipa gharama zote kati ya dola za Marekani 2,400 na 3,200 za malazi chakula na usafiri wa ndani.

    "Lazima ATC watalipa hizi gharama zote na fidia ya usumbufu kwa mahujaji… ngoja tukae wote tutajadili hili jambo," alisema Abdallah.

    Wakizungumzia maandamano yao waliyofanya Jumamosi ili kushinikiza wasafirishwe walisema kuwa baada ya kufika Ofisi za kampuni hiyo na kukutana na Balozi Nyang'anyi, akawahakikishia kuwa tayari wamekwishakodi ndege kutoka Saudia kutoka kwa kampuni ya mtu binafsi na itawasili Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana.

    Lakini pamoja na taasisi hizo kufanya bidii ya kuwapeleka mahujaji zaidi ya mia tano uwanjani hapo, hakuna ndege iliyofika zaidi ya kuambulia kulala hapo.

    Alisema baadhi ya mahujaji waliopandwa na hasira walitaka kuingia kwenye njia ya kurukia ndege ili kuzuia ndege zisiruke kama shinikizo la kutaka kupewa ndege itakayowapeleka Mecca.

    Mahujaji hao walisema kuwa kwa mujibu wa taratibu za hijja inabidi kila anayekwenda huko akae angalau siku nane za mwanzo kwa ajili ya kuswali swala 40, lakini kwa uzembe wa ATC, zimesalia siku mbili kati ya 10 na mbaya zaidi ikifikia Desemba 11 hawajafika huko, hawataweza kwenda kwani viwanja vyote vitakuwa vimefungwa.

    Alipotafutwa na waandishi wa habari, Balozi Nyang'anyi alisema yeye si msemaji wa ATC. Alipokumbushwa kuwa Jumamosi aliongea na waandishi, alisema kuwa alikuwa anatuliza mzuka na kuokoa jahazi lililokuwa linazama.

    Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Milton Mahanga, aliyefika uwanjani hapo, alisema kuwa alikuwa hajui lolote kuhusu ATC ambayo ipo chini ya wizara yake, kushindwa kuwasafirisha mahujaji.

    Hata pale Dk. Mahanga alipotakiwa na waandishi aseme lolote kuhusu kukwama kwa mahujaji hao, alisema kuwa kwa kuwa alikuwa hajui na amefika hapo kwa shughuli binafsi anayepaswa kulisemea hilo ni Waziri Andrew Chenge.

    ReplyDelete
  17. `Mahakama ya KADHI bado hali ni kama hivi. Je ikija tutaenea kweli humu bongo...............'

    Hii hoja ni ya kishabiki na haina mantiki, aliyeandika anatakiwa aende shule.Sio kila kinachotamkwa na Muislamu ni sheria, na sheria za dini si sawa na sheria za kibinadamu, kwani aleyezitunga anajua zaidi ya wewe unavyofikiria.

    Tunaomba mnapotoa hoja za kidini mfikirie na mtumie hekima na sio kuropoka tu.

    Maneno ya hawo mahujaji na mahakam ya kadhi yanaingilianaje? Msiogope kuitwa wezi kama nyie sio wezi. Na pilipili msioila inawawashia nini? Naona kila kitakachoongewa na waislamu sasa hivi kinalinganishwa na mahakama ya kadhi, kwani kama walivyosema, `ukitaka kumuua mbwa kwanza umuite majina mabaya....' Hiyo ndio ajenda ya siri.

    ReplyDelete
  18. `Mahakama ya KADHI bado hali ni kama hivi. Je ikija tutaenea kweli humu bongo...............'
    Ni kweli nakubaliana na anos wa hapo juu..aloposti mada hii yeye mwenyewe ana jazba za kidini. Pengine hajui umuhimu wa waislamu kutoa pesa chungu nzima ili kwenda Hajj na hilo halihusiani na mahakama ya kadhi. Kisheria wanastahiki wakereke na kuhodhi suala hilo, na kero walizopewa kwani kwa sasa wenzao washafika Saudia na wameanza ibado huku wao bado wako Bongo. Nahisi alotuma mada hii katikati ya mada ingine hana dira, mdini na ni kundi moja na mchungaji mtikila mropokaji...nawaomba radhi wanablog kwa mimi pia kumjibu hapa..imenibidi!
    lakini nikirudi kwenye mada asili, suala la kuolewa mtu miaka 14 inategemea na msichana mwenyewe. Ndio maana kama umesoma vizuri sheria hiyo inasema...msichana anaweza kuolewa kunzia miaka 14 iwapo mzazi wake ataridhia. Inamaanisha kwamba wazazi wenyewe watakaposhauriana na kwa kuzingatia mwenendo na maisha ya muolewaji na anayeona...suala hilo halina tatizo lolote. kwa upande wangu naona ni sawa katika baadhi ya sehemu. Kwa mfano mtoto kamaliza la 7 na hakufanikiwa kuendelea na elimu kutokana na sababu zozote zile tofauti tofauti. Kama katokea mchumba ambaye wazazi wake wamechunguza na kuona kuwa atamfaa binti yao na pale binti pia anaporidhia, basi hakuna tatizo lolote. Badala ya kuacha mtoto huyo akazurura zurura ovyo na pengine kujizalia mitoto ambayo baba zao hawajulikani katika umri mdogo ni bora akaolewa. Tanzania kwa hivi sasa tunakabiliwa na matatizo muhimu katika jamii yetu kama kupata mimba katika umri mdogo( hata chini ya miaka 14, watoto wa kike kupata mimba mashuleni kuania shule za msingi, utoaji mimba, vijana wadogo kupata magonjwa sugu ukiwemo ukimwi(I mean here STD), biashara ya ngono kwa wasichana wadogo na mengineyo ambayo haipaswi jamii kuyafungia macho na ni dhihirisho dhahiri kwamba watoto wadogo wanshiriki ngono katika umri mdogo. Kwa hivyo tusikurupuke na kupinga kitu kishabiki bila kufikiria kwa undani, pengine sheria hiyo ikibaki hivyo hivyo itasaidia wale wanotaka kutekeleza suala hilo kwa kujali masuala mbalimbali. Bali tu kusiwepo kulazimishana. Lakini iwapo kina sisi tunataka kuolewa tukiwa na miaka 35 baada ya kutembea na mamia ya wanaume na hata kukaa nao kinyumba kutokana pia na sababu zetu mbalimbali..ruksa! uwanja uko wazi. lakini kwa wanoiona ngono kuwa ni kinyume na maadili yao na ni dhambi basi pengine sheria hiyo inaweza kuwafaa!

    ReplyDelete
  19. We anon wa Dec 10 2:20 pm nyie ndio wale wa Islamophobia! Nenda kasome kwenye wikipedia ujue islamophobia ni nini? Hivi mtu kucheleweshwa kusafiri wiki nzima kunzia tarehe 3 Dec mpaka leo tarehe 10 Dec unataka wanyamaze kwa kuwa wakisema watu watawaona vibaya? Hivi ingelikuwa wewe umetoka huko Iringa, Kigoma na hata Bukoba huna ndugu Dar unasubiri kusafiri tangu hiyo tarehe kumi ungenyamaza kimya?

    Watu wanamess up kwenye kazi zao, watu wamelipa nauli wasafiri hawajasafiri wewe unaleta masuala ya islamophobia? Tatizo hapo ni ATC kutowajibika wangewasafirisha hata kwa majahazi yenye tanga wangekuwa wameshafika huko waendako tangu hiyo tarehe. Kwa kuwa ni waislamu basi wanyamaze, je hiyo ATC inaweza kuwalipa fidia wasipoweza kwenda kufanya ibada yao? Kumbuka kuna madhara ya kisaikolojia pia pale mtu anapokuwa anasubiri jambo bila kuambiwa mustakabali wake utakuwaje, je ATC inaweza kuwalipa fidia kwa hilo? Kama walijua hawana ndege kwanini wasikatae kuchukua pesa za watu? Wengine wamelipiwa nauli na ndugu na jamaa zao, wamejiandaa kwa safari ambayo hutokea mara moja kwa mwaka, na mwakani anaweza asiweze kwenda huko alikopanga kwenda sasa.

    Hivi ni lini mashirika yetu yatafanya kazi kwa ufanisi bila kutegemea wageni hii ni aibu kubwa kwa ATC na viongozi wake. Wewe unaeleta porojo za magazeti hapa hebu jiweke kwenye nafasi yao na nani ana uhakika na hicho kilichoandikwa kama pengine ni njia ya kuuza gazeti mie huwa simezi kila nikisomacho kwenye gazeti na luninga bila kutafakari kwa nini huyu mtu ameandika hivi ndio faida ya kwenda shule!!

    ReplyDelete
  20. Nafikiri hii sheria inafaa kama huyo mtoto hayuko shule na yu tayari kuolewa, siku hizi watoto wa kike wanaanza kubalehe wakiwa na umri wa kuanzia miaka 10 na kuendelea, miaka 12 mpaka 13 ameshamaliza darasa la saba.

    Halafu pia iko sheria nyingine inayowalinda watoto wanasoma shule ambayo hata kama ana zaidi ya miaka 14 mtoto huyu mwanafunzi haruhusiwi kuolewa.

    Vile vile watoto wanaanza ngono mapema, sio Tanzania tu ni sehemu nyingi hata huko Uk kuna watoto 16 yrs wanazaa. Utakuta mtoto wa miaka 14 keshaanza ngono na si mtoto tena, manake ameshakuwa mwanamke, hapo ndipo kuna utata unakuja hii sheria ibaki ili nikikufuma unajivinjari na binti yangu nikuoze kwa idhini yangu au iondolewe ili watoto/wanawake wadogo wasiolewe kwa umri mdogo.

    Lakini pia kuna suala la kuangalia afya ya mzazi mtoto wamiaka 14 uzazi wake unakuwa wa tabu kwa sababu via vyake vya uzazi bado ni vichanga. Lakini nikirudi kule kule kwenye mmomonyoko wa maadili hao hao ambao tunataka walindwe na mabadiliko ya sheria hii wanabeba mimba wakiwa katika huo umri mdogo wa miaka 14.

    ReplyDelete
  21. Tembea ujionee usiropokwe na maneno, kama wewe si mwisilamu mahakama ya kadhi inakuhusu nini? Mbona Kenya iko mahakama ya kadhi sijasikia wakenya wakiilalamikia?

    Watu wanachodai hapo muhusika ajiuzulu kama hujaelewa hawezi kuwaacha watu Solemba mpaka leo hakieleweki eti waogope kusema kisa watu watahusisha na mahakama ya kadhi!! Eboo

    Halafu usituvurugie mada watu wanaongelea mambo ya maana yanaohusu mustakabali wa watoto wao. Tuambie kuhusu hii sheria ya ndoa inayoruhusu watoto kuolewa wakiwa na umri mdogo.

    ReplyDelete
  22. Nyie ma-annon mnaochangia mada ya mahakama ya kadhi naona nanyi hamna points. Mimi nimeweka ile habari ili uweze soma na kuilewa. Siyo kutoa comments tu kichwa kichwa. Ukisoma habari kwa makini, utaona issue kama kukata kichwa, au kukaa kwenye njia ya kurukia ndege. Yote sababu ni kukosa ndege ya kwenda Madina.

    Haiingii akilini mtu yoyote mwenye akili timamu, bila kujali dini, kwamba kwa kuwa wewe umelipia safari na unatoka Kigoma, basi unaweza kumvuruga mtu yoyote hata asiye husika kwa namna yoyote unayotaka wewe. Sidhani kama ni kweli kitu kama hicho kipo na kama kipo kuna tatizo kubwa sana. Hapa nadhani ni suala la ufahamu.

    Kwa mantiki hiyo hiyo, ndio maana tuahoji, je iwapo hali ni hivi hatuna mahakama ya KADHI, je ikiwapo tutaenea hapa bongo????!!!! Tuwe objective bila kujali dini wala nini. Ni issue iliyo wazi kabisa kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...