Licha ya kuahidiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la ndege la Tanzania Balozi Mustafa Nyang'anyi kuwa ndege ya kukodi kutoka Medina ingewasili saa moja jioni hiyo,ndege hiyo haikuwasili na ndipo Mama Salma Kikwete aliamua kuwasabahi mahujaji hao uwanjani hapo.
Mama Kikwete aliwaomba mahujaji hao wavute subira wakati suluhisho la tatizo hilo linatafutiwa ufumbuzi.
Aliwaletea Salamu za Rais Jakaya Kikwete na kuwaambia kuwa Rais anawapa pole na analifuatilia jambo hilo kwa karibu ili kuona mamlaka husika inatatua tatizo hilo.
Baadaye Mama Salma alikutana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo David Mataka na Balozi Nyangányi uwanjani hapo.


Ahsante Michuzi kwa kutupa habari hii, sie wengine tuko mbali tuna ndugu na jamaa wako stranded hapo wiki nzima ATC haiwaelezi kinachoendelea zaidi ya watu kuingia na kutoka kama kwenye hive.
ReplyDeleteTatizo ATC haina ndege halafu imechukua karibu mahujaji 1000 itawasafirishaje? Watu wana wiki sasa wanasubiri kusafiri wengine wametokea mikoani.
ATC inabidi iache mtindo wake wa kufanya kazi kizamani kama inataka kurudi kwenye biashara, kila siku tunalilia kuendesha mashirika yetu wenyewe lakini sijui kwa nini hatuna ufanisi.
Tunashukuru kwa habari za kukwama mahujaji.Hii kwakweli inaonyesha ni jinsi gani uwajibikaji bado unavyoleta matatizo katika nchi yetu. Tatizo kama hili la kukwama mahujaji ni tatizo ambalo lingemhusisha mojakwa moja waziri wa mawasiliano kuona ni jinsi gani suala zima la kusafiri linatiliwa kipaumbele. lakini inasikitisha kuona Rais anamtuma Mke wake kuongelea suala hilo na kuwakilisha mawazo ya Mumewe kuwa huko Ikulu yuko "busy" anashughulikia suala hilo. Hivi jamani hili suala ni la Rais? Kama Rais wetu ataanza hata kuwa "Ocupied" na Shughuri za mahujaji na dhani hakuna atakacho fanikiwa kufanya, kwani mambo ya kufanya yatakuwa mengi mno! Rais aache mabo ya mahujaji kwa waandamizi wake!
ReplyDeleteRais!! kuna mambo mengi sana ambayo unapaswa kuyapa kipa-umbele zaidi ya mahujaji!
watu weusi tuna shida sana yaani ni utapeli mtupu,halafu unasema bongo tambarare,wacha niwahi kujibebea box mie kwenye nchi ambazo ziko organize katika kila sekta nyie endeleeni kula vumbi na matapeliwenu hao.
ReplyDeleteSafari za mahujaji has always been na utata to some extent.
ReplyDeleteBack in 1999 in Zanzibar mahujaji walisubiri ndege SIKU TATU, ya nne ndege ikawa itue Zanzibar saa kumi na mbili asubuhi...ikatua saa mbili usiku!...ndege imetua inanuka haja kubwa na ndogo ya mbuzi! (i am serious, i was there)...walisafiri baada ya ndege kufagiliwafagiliwa...
Hili la ndege ATC, ATC hakuna ndege yenye ubavu huo. Wakategemea kukodi, the deal went SOUR AT THE BEST POSSIBLE TIME.
Anonymous said...
"watu weusi tuna shida sana yaani ni utapeli mtupu,halafu unasema bongo tambarare,wacha niwahi kujibebea box mie kwenye nchi ambazo ziko organize katika kila sekta nyie endeleeni kula vumbi na matapeliwenu hao."
- WEWE BEBA MABOXI TU HUKO, YOU ARE NAIVE
Hapana si kweli kwamba Rais alimtuma Mama wa kwanza kwenda kuongela suala la wasafiri na kuwaelezea kwamba rais ana shughulikia usafiri wao.Ila katika hao walio kuwa wanasafiri alikuwemo Baba Mzazi wa Mama wa Kwanza na kaka yake na wadogo zake.Na Mama wa kwanza alikwenda kama mtu tu ambaye ana ndugu zake wanasafiri na wako katika wakati mgumu.Mtu yoyote anaweza akafanya hivyo.
ReplyDeleteAsante
Mwakipesile
Mwakipesile uliyosema yana ukweli kuwa baba mzazi wa salma na familia yake walikuwepo. Ila Raisi pia ameingilia kutokana na baba mkwe wake kugandishwa, hapo ndio utachoka na bongo. Ticket ununue ndege haipo..kwanini umeuza tiketi?? si wangeachia mashirka mingine kama South Africa Airlways hivi??
ReplyDeleteJambo lolote la kheri linamitihani yake ndugu zangu,hizo zote ni kheri, haraka haina baraka huenda mwenyezi mungu anaepusha jambo hapa, tuwe na subira wataenda tu ikiwa mungu mwenyewe kapenda kwa sasa bado hajaamua kama mtalazimisha nyie wanadamu kama kawaida yenu haitafanikiwa safari tumuombe mungu zaidi tuondoe jazba na mipango ilikuwa mizuri tu ila bahati mbaya hakuna swala la uzembe nchi yetu haina ndege ila rais ana ndege
ReplyDeleteNyongo lazma ichemke hapo bro. kisha jazba ipande hapohapo, maana $2,400/- si ndogo kuikusanya mlavumbi ni tabu kidogo kisha kuitumia vilevile hapo imekua tabu pia. ikiwa kwenda kumuabudu Mungu wake mtu inakua ghasia na najis zipo benet mwanawane harufu kwa kwendta mpele mwanawane wakati unatohara mh!
ReplyDeleteila watanzania tuko wajamaa tunaweza tukaruhusiwa watatu wanne tupande hiyohiyo ya rais mpaka mahujaji wote waishe.Afadhali kuwa na chakula kidogo tukagawana kidogokidogo kuliko chakula kingi tukaanza kugombea> watanzania tuwe na tabia njema unaweza na timiza wajibu wako
Wewe muhd hapo juu, yaani siku Mungu akikushika utajiju, yaani uzembe wa binadamu wewe unamu-accuse Mungu? Yaani wazembe pale ATC hawafanyi kazi zao halafu wewe unataka kumsingizia Mungu? eti hajapenda, jamani tumuogope muumba wetu jamani.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu katika imani yangu ya kiislam ametutaka tuwe na subira kwa maana yeye ndiyo mpangaji wa yote hii ardhi na mbingu pamoja na viumbe vyote ardhini na majini ni vyake hivyo anajua udhaifu wetu kikamilifu kama ni uzembe au si uzembe yeye ndiye ajuaye ya kwamba kiumbe wake kadanganya au kasema kweli na si mimi na wewe naomba umwamini allah karim kwamba anatujua vizuri sisi kuliko sisi tunavyojuana.Mimi naamini ya kwamba Mungu sasa ametaka na wameanza kuondoka kundi moja na mengine yatafuata,wanadamu ni watu dhaifu hukimbilia mambo kulaumu bila kufikiri mara mbili hija si kitu cha kuparamia je wale wote kweli wapo safiii.
ReplyDeletembona hapo wanaume wameingia na ni sehemu ya wanawake tu jamani
ReplyDelete