mandhari ya dar inabadilika siku hadi siku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. tanueni jiji hilo sio kila kitu mnarundika sehemu moja.

    ReplyDelete
  2. Yakhe ni kweli kabisa, lakini yote hii inaonesha jinsi architectures wa Bongo walivyo na akili finyu na upanuzi wa jiji. Panueni huo mji na mshughulikie hizo barabara zenu.

    ReplyDelete
  3. hii ni view ya Dar sasa...dayuum?? Pia ile calendar yetu vipi Kaka Michu....ya Dar kumbuka ulituahidi.

    ReplyDelete
  4. Vilevile viongozi haswa ambao mnatembea nchi za nje na kujionea maendeleo ya wenzenu, hamuoni haya hata mmeshindwa kuomba misaada kwa hao mnao watembelea ili warekebishe hiyo hali ya ukosefu wa maji na upungufu wa umeme!!!
    badala ya kujidai eti mnatangaza utalii na mali asili ya TZ??? Watu woote ulimwenguni wanayo hiyo habari tangia enzi za Nyerere na nyie tafuteni miswada mipya kama vile inavyostahili uongozi mpya na mambo mapya.

    ReplyDelete
  5. jengeni na mikoani sio dar tu

    ReplyDelete
  6. mji unajitahidi lakini na usafi wa mazingira kama barabara kubwa na safi,mapipa ya taka,bustani za maua na vivuli na miti ni muhimu sana naomba wafanye kampeni mji uwe wa kijani...bila kusahau vyoo safi
    wenu mbeba box.

    ReplyDelete
  7. Yes, inabadilika kila siku kwa gharama ambazo zinastahili kutumika kujenga hayo majengo mwezini, sio katika sayari ya dunia (kichekoooo). Kiini macho tu hiki bro Michu

    ReplyDelete
  8. Mabadiliko at what cost?

    ReplyDelete
  9. Nyie wala vumbi, gharama ya pesa mlioitumia kujenga hayo majengo mawili yenye vioo vya buluu, mngewapa wachina ama wakorea wakajengee majengo kwao, mngeshangaa kwani wao wangejenga magorofa 20 yenye miundo mbinu bora zaidi yenu wala vumbi.. (ma-free ways, parking structures, modern equipment etc). Poleni sana. Hiki si kitu cha kujivunia hata kidogo. Ni kitu cha kujisikitikia

    ReplyDelete
  10. Nimechoka sasa, kha! kila mtundiko....wabeba boksi...wala vumbi, Michuzi naona sasa hii globu yako inatengeneza matabaka

    ReplyDelete
  11. hivi nyie kina anonymous... asili yenu wapi?? kama ni Tanzania mbona pole!!! comments mnazotoa utadhani nyie ni wa huko ughaibuni wakati mmetoka hapahapa bongo!! hivi kweli ukanyonya titi la mama mchafu unaweza baadae ukaja kuyatapika uliyonyonya baada ya kukua na kujua usafi ni nini au utampiga sopu sopu huyo mamako aliyekuwa mchafu?? kuweni wastaarabu kidogo na muappreciate kile kidogo nchi yenu imeweza kufanikiwa kukipata.... angalau rudini mlete huo ustaarabu wenu mlioupata huko mje mplan miji na kuweka resources ziendeleze kwenu.... wahenga walisema nguo ya kuazima haistiri maungo!!iko siku mtarudi..sijui mtashukia wapi??!!

    ReplyDelete
  12. Ndugu zangu waTanzania mlio Tanzania wala msibabaishwe na hawa wanaojiita wabeba box na madharau yao utafikiri hawakutoka huko. Ukifika huku ndio utajua ninamaanisha nini. Yaani huku maisha yao ni ya ajabu sana. Wao huku ni watu wa daraja lachini kabisa. Tunadharauliwa na kila mtu. Kazi tunazozifanya ndio kama mnavyojua tena aibu tupu. Tunashindwa kurudi nyumbani kwasababu hakuna kitu cha maana tulichokifanya huko nyumbani tunabaki kukashifu tulikotoka. WaTanzania wa UK kwa kweli tunatia aibu sana, ushitikiano hakuna kutwa tunashindana tu kwa mambo ya kijinga.

    ReplyDelete
  13. Na weye unayesema kwamba wajenge na mikoani kwani dar es salaam si mkoa au umejisahau ukafikiri dar ni nchi? Embu rekebisha kauli yako. Jiji lenyewe hili matatizo tupu si bora kuhamia huko unakoita mikoani?

    ReplyDelete
  14. Na weye unayesema kwamba wajenge na mikoani kwani dar es salaam si mkoa au umejisahau ukafikiri dar ni nchi? Embu rekebisha kauli yako. Jiji lenyewe hili matatizo tupu si bora kuhamia huko unakoita mikoani?

    ReplyDelete
  15. Mimi ni mufwatiliaji muzuri wa blog hii, na kama sikosei tulianza kuliona neno "wabeba boxi" siku nyingi sana kabla ya kuja liona neno "wala vumbi". Hivyo, ndugu yangu "tizedi" wa december 14 saa 11.07 am nafikiri umepata picha nzuri ya historia ya mwelekeo huu.

    ReplyDelete
  16. nashukuru kuona kuwa kuna watz walioko huko majuu nao wameona ujinga wa wenzao wanaojifanya wameloea kwenye nchi za wenyewe! Kinachosikitisha zaidi ni kuwa ukichunguza sana utaona hao wanaojitia kuponda kwao ni wale wenye matatizo mengi toka wametoka huku bongo na badala ya kukaza buti wajinasue na umaskini na ujinga wao "uliotukuka" wameona wakawe wadowezi na walowezi nchi za watu... wanafikiri wanaturingishia eti wako ulaya kama vile sie hatujafika huko!! kwa taarifa yao wengine tumezunguka dunia nzima na tumeona home is still the best maana huku home kama ni kazi nzuri za heshima tunazo.. kama ni luxury na comforts in life tunazo.. na tunaheshimika maana michango yetu kwa nchi, jamii na familia zetu inaonekana wazi...... in short utu wetu uko pale pale na hakuna anayetunyanyapaa!! Ndugu yangu anony wa 14 dec,07 11:12 pm.. umenikuna sana maana umedokeza kuhusu hao wenzetu waliokosa mwelekeo.... infact im about to start a " re-entry programme"kuwasaidia hao walowezi warudi home tuwasaidie wapate kianzio na namna ya kujifitisha tena in their society!they are a lost sheep!!! Ni kama the prodigal son aliyekimbia kwa babake kwenye neema na kwenda kuwa mtumwa huku akila makombo yanayotupiwa mifugo ya tajiri yake!!

    ReplyDelete
  17. Mtazamo wangu ni huu: Ni kweli kwamba Jiji limebadilika, majengo mapya yameongezeka! Ni kweli kwamba hayo 'majengo pacha' yamejengwa kwa fedha za walipa kodi nyiiiingiii heri fedha zingepelekwa kujenga zahanati na kununua dawa kukoa maisha ya akinamama na watoto. Ni kweli tunahitaji kupanua jiji kusogeza huduma za jamii kwenye vitongoji si wote tuje Kariakoo na Posta. Baadhi ya Benki zimeanza kufanya hivyo bado Wizara zetu na ofisi nyingine za Serikali. Barabara zetu jamani bado ni kitendawili! Ali Hassan Mwinyi wameanza kumega vipande lakini mmh mashaka! Na nyie mlioko huko nje mlete fedha za kigeni kuchangia maendeleo ya kwenu sio mnakaa huko na kuchonga tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...