Michuzi na Chemi wajameni!
Naomba mnisaidie kuwapa taarifa waTz wenzetu kuwa mshindi mwenza wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu ametoka Tanzania na anaitwa Prof. Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dre es Salaam.
Hii nondo ni kubwa ila imepita kimya kimya sana jamani.
Huko US Al Gore amekaribishwa ikulu kwa Bush, tunakumbuka mapokezi wa Prof. Wangare Mathaai Kenya. Tanzania tunawaza nini jamani? Huyu rais wetu vipi uwiii, na huyu waziri Prof.Msolla wala sijamsikia, nimesikitika sana.
Huyu si Bongo Celebrity pia?
Ni wazo tu Kwa kiinglish Nobel Peace Prize is a prestigious award and this year Prof Yanda was a joint recipient of this world's top prize with Al-Gore for co-authoring the Inter-Government Panel for Climate Change report. vicensia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Ni jambo kubwa na la kujivunia watanzania.Lakini sisi kama kawaida yetu ni mara chache sana tuna support vitu kama hivi sisi mara nyingi ni ujinga na vitu visivyo na maana.Huyu bwana kashinda prize kubwa kama hiyo yenye heshima kubwa duniani who wants to know!? sisi tuambie richard kashinda big brother kwa kumfinger mtu aaah safi kabisa tutampongeza na mpaka ccm itakuwepo uwanjani kumpokea so sad.
    Hongera mzee,ndo maana watu hawataki hata kurudi bongo mambo yenyewe ndio kama hivi.

    ReplyDelete
  2. Huyu Mtanzania hakushinda pamoja na Gore ila Gore ameshinda pamoja na chombo kiitwacho Inter-governemental Panel for Climate Change, labda mtu wetu naye alikuwemo humo, lakini siyo jina lake yeye binafsi. Nampongeza hata hivyo na tunapaswa kujivunia lakini tukumbuke pia wajumbe wengine kwenye hiyo Panel hawakutajwa-tajwa kwa hiyo kama yeye hakujitangaza tusilaumu mtu. Siku zote Watanzania wakichaguliwa kwenye vyombo vya kimataifa inatangazwa na wote tunafurahia, sidhani kwamba huyu ameonewa. Mimi niliwahi kushibdwa tuzo ya kimataifa mara mbili na zote hakuna aliyetangaza, mara ya kwanza nilikuwa bwana mdogo enzi za ukiritimba na mara ya pili sikutaka mwenyewe lakini wenzangu nchi zingine walitangazwa kwao. Inabidi mtu mwenyewe uwafahamishe watu iwapo jumuiya ya kimataifa haikukutangaza.

    ReplyDelete
  3. ''...mshindi mwenza wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu ametoka Tanzania na anaitwa Prof. Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dre es Salaam...'' Uwongo huu umeutunga mwenyewe?!! Kama hujui IPCC ni chombo sio mtu! Chombo hicho kina watu wengi sana na shughuli nyingi za kimataifa zinazohusiana na Climate change!

    ReplyDelete
  4. IS it possible,huyu mbongo, ashinde tuzo kama hili, na sisi wabeba mabox,ambao tuna PC mpaka vyooni,tusijue.MICHUZI hebu tueleze vizuri

    ReplyDelete
  5. kwanini hadi ajitangaze ndo tumsupport!!! kwani ilikuwa siri alipokabidhiwa hiyo nobel prize!! ni kitu kikubwa, na kama hatukujua basi inamaana tu wazembe hata wa kusoma news, na kufuatilia mambo ya dunia!! angekuwa amepata mijihela kwenye hiyo nobel, tungemtambua haraka sana, ni aibu kwetu. ni kitu cha kujivunia nchi nzima, ameweka jina la nchi yetu juu, amelitangaza haswa, kwamba kunawatu wakipewa opportunity, they can make miracles!! bravo for him.

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na anon 8 nov 7.46: Watu inabidi wajitangaze wenyewee. Sidhani kama ni kazi ya nchi kuchunguza nini kinaendelea katika kila nchi na kujua watz wanashiriki ktk nini. Manake mara nyingi unakuta mtu kaandika paper kuingia kwenye vitu kama hivyo sasa nchi kama nchi itajuaje.. mimi anko wangu alishiriki kwenye noble prize huko UK akashika nafasi ya pili or so... lakini haikutangazwa, however university aliyokuwa it was such a BIG DEAL. Lakini yeye alijuwa kama anataka ijulikane TZ ni lazima awafahamishe nini alifanya na kufika hapo. So people you should stop blaming the country for every little thing.

    ReplyDelete
  7. Hii si ndo habari yenyewe Michu au?

    UDSM don becomes a joint recipient of Nobel Peace Prize

    from ippmedia.com

    2007-12-01

    The University of Dar es Salaam has announced that one of its dons, Prof Pius Yanda, was among co-authors who on October 12 this year jointly received the prestigious Nobel Peace Prize. In a statement released in Dar es Salaam on Thursday, the university's public relations office said Yanda was a joint recipient of the world`s top prize with former US vice-president Al Gore for co-authoring the Inter-Government Panel for Climate Change (IPCC) report.

    Yanda, according to the statement, is a professor of Physical Geography specialising in natural resources management and environment and is currently engaged in a research project that provides high resolution information on predicted future climate change and associated impact on natural and social systems in various parts of Tanzania.

    The project is conducted in collaboration with Michigan State University of the US and the Livestock Research Institute of Nairobi. However, in the IPCC report, the statement said, Prof Yanda participated in the project, entitled `Climate Change Impacts, Adaptation and Vulnerability,` with specific focus on Africa.

    Findings presented in the report include that of vulnerability of Africa to climate change and climate variability, a situation aggravated by the interaction of multiple stresses occurring at various levels and law adaptive capacity, noted the statement.

    Another finding states that climate change could result in low-lying lands being inundated, with resultant impacts on coastal settlements. The report also notes that human health, already compromised by a range of factors, could further be impacted by climate change and climate vulnerability.

    ReplyDelete
  8. Michuzi mi nawaomba watanzania waende kwenye link ya www.ipcc.ch hapo ndipo wasome kama kweli huyo Prof wao anastahili hizo sifa kwani kama mimi binafsi sioni chochote cha kupigia kelele. Nashanga sijui naye huyo Prof anashindwa kusema ukweli

    ReplyDelete
  9. Tafsiri sahihi ni kuwa Prof Yanda alikuwa mmojawapo wa wajumbe wa Intergovermental Panel on climate change. Na zawadi ya Nobel Prize kuhusu 'climate change' ilipewa kwa pamoja kwa Intergovernmental Panel on Climate Change na makamu wa rais mstaafu wa USA Al Gore.
    Kutokana na Prof. Yanda kuwa mmojawapo wa 'mjumbe wa wajumbe' wa Intergovernmental Panel ndio maana hakuna sababu ya kubai kuwa kapata hiyo nishani ya Nobel Prize 2007.
    Mbeba-Box-Mkuu
    Detroit
    USA.

    ReplyDelete
  10. Mimi naomba nimjibu Mpenda Nchi hapo juu ili kuanzia leo aelimike kwamba ni wajibu wa nchi kutafuta habari zote zinazohusu nchi hiyo ili kuweza kuwa na datasource iliyo credible(samahani kwa kutumia maneno-zungu).Ndiyo maana hata takwimu kama za pato la taifa watu hawana uhakika nazo!Kwa mfano unaposikia kwamba uchumi wa Tanzania hupo mikononi mwa wafanyabiashara wasiozidi 30 unafikiri nini miongoni mwa waTz milioni 40!takwimu hizi inabidi nchi ifanyekazi ya ziada ikiwa ni pamoja na kupata taarifa kama ya mtanzania huyu.Senyandumi

    ReplyDelete
  11. 1:58 naona huelewi haya mambo ya nobel price....na sister aliyeleta hii habari pia naona hakuelewa pia...

    Nobel price award inakuja na dola $150,000 price. Sasa kama uko mwenyewe kwenye hiyo category unakusanya yote ndio maana mama wa kenya alifaidika...kama ni group sometimes inakwenda kwenye group kuendeleza research au mkigawana kama mko 100 au 1000 basi ni hela ndogo sana....

    Professor mmoja alishawahi kunifundisha kitambo mwaka huu ameshinda kwenye mambo ya uchumi. yeye wako watatu kwa hiyo hela yake ni nyingi hapo...

    Sio kuwa Tanzania hatuthamini ushindi huu lakini zipo award nyingi sana hasa kwenye UN na wanapokea wabongo kila siku za chini chini ...kama mtu unataka publicity basi una ita vyombo vya habari unawaambia..

    Kuna habari nyingine zinajiuza zingine ni wewe mwenyewe uziuze. Ndio maana huku hata shule ndogo tu zina public relationship dept. Hii ni kwa vyuo vya nyumbani public relationship yao kama ipo basi ingepeleka haya mambo kwenye habari kama mhusika hakutaka kufanya hivyo....

    ReplyDelete
  12. I am sorry nilikua naamaanisha 1.5 million sio laki moja na nusu kama nilivyosema hapo juu

    ReplyDelete
  13. We unayesema mna pc mpaka chooni huna habari, huo muda wahabari utaupata wapi? wakati kutwa kubeba box. HONGERA PROF NYANDA.

    ReplyDelete
  14. Labda ni kutokuelewa... lakini nimepitia hii link ya IPCC nikakutana na "the IPCC Synthesis Report Core Writing Team members" nimekuta majina kibao lakini sikuliona jina la huyu Profesa wetu. Vicensia unaweza kutuhabarisha zaidi undani wa habari hii? Usikute yeye hakuwemo KIIVYO ndio maana alikaa kimya??

    ReplyDelete
  15. ni kweli huyu prof jina lake ni mmojawapo wa wajumbe wa IPCC (working group I). Nafikiri kama wadau wengine walivyosema hapo juu-ni kuwa ingekuwa sahihi kusema kuwa "Prof mmojawapo ni mjumbe wa kamati ya IPCC, ambayo imeshinda hiyo tuzo" si sahihi kusema kuwa huyo prof amegawana na Gore!!

    ReplyDelete
  16. Kwa wote waliojadili habari hii na wana blog hii na nyinginezo zote. Ni vizuri na ni haki na wajibu wetu kutoa habari kama hizi kwa uhuru. Lakini ninachoomba wanablog tuwe makini hasa pale unapo point finger kwamba fulani hajatimiza wajibu wake, then unakuja gundua kwamba ulicho mlaumia si sahihi..inakuwa si vyema. Tuchunguze kidogo na hasa kwenye habari ambazo ni very official. Kwa mfano cha kwanza was to go online and google IPCC then ingia kwenye web site yao,http://www.ipcc.ch/index.htm kisha, tutumie habari, tuisome.Ukiangalia website hiyo, utakuta kuna mtanzania zaidi ya mmoja katika shughuli au work groups mbalimbali, so who is who? na nchi nyingi tu zinawakilishwa ndani ya IPCC, including Kenya. TUDUMISHE UPATIKANAJI WA HABARI SAHIHI KWA NJIA YA BLOGS.Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...