DEGE LILILOKUJA KUBEBA MAHUJAJI JANA USIKU BADO HALIJAONDOKA INAGWA LIMESHAPIGWA STATI MUDA MFUPI ULIOPITA NA MAHUJAJI WAKO UWANJANI WAKISUBIRI SAFARI. MADEGE MENGINE MAWILI YANATEGEMEWA KUTUA DAR KUOKOA JAHAZI KABLA YA MSTARI MFU WA USIKU WA MANANE LEO
HABARI ZINADATISHA KWAMBA SERIKALI INAFANYA KILA LIWEZEKANALO KUHAKIKISHA MAHUJAJI WANAHUDHURIA HIJJA MWAKA HUU, IKIWA NI PAMOJA NA KUTUMIA JUHUDI ZA KIDIPLOMASIA KATIKA KUHAKIKISHA MASUALA YA KIUFUNDI NA PROTOKALI YANAWEKWA SAWA.
UCHUNGUZI WA GLOBU HII UMEBAININISHA KWAMBA PAMOJA NA 'SLOT' AMA NAFASI YA KUTUA HUKO SAUDIA KUWA MOJA YA VIKWAZO, PIA INASEMEKANA KUNA SHERIA MPYA ZA ANGA HUKO SAUDIA AMBAZO HAZIRUHUSU KILA NDEGE KWENDA KUTUA KULE BILA KUVETIWA NA WENYEWE....HII BILA SHAKA NI KUJIHAMI NA UGAIDI.
TUTAENDELEA KUPASHANA. SUBIRA YAVUTA KHERI...


Jamani huko Bongo mbona mnatuchanganya,na hii nini?
ReplyDelete2007-12-12 09:24:47
Na Eshy Mushi
Safari ya Mahujaji yaiva
Hatimaye, kundi la kwanza la Mahujaji zaidi ya 1,000 waliokuwa wamekwama kwa siku nane kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, jana lilifanikiwa kuondoka kwenda kuhiji Mecca, Saudi Arabia.?????????????????
Hiyo ndege inaweza kuwa mbovu ndiyo maana wameiacha iwe imepigwa start ikiwaka muda wote.Vinginevyo wakiizima tu inaweza isiwake tena ikabakia museum Airport.
ReplyDeleteLakini nionavyo mimi ni bora izimikie airport,ikizimikia angani sijui wakishuka abiria watafanyaje kuisukuma huko hewani hadi iwake .
Wakivaa yale makoti ya kuelea angani pengine wanaweza isukuma kama imezimika hadi ikawaka angani bila wao kudhurika na wakaiwahi kuidandia ikishawaka huko hewani.
michuzi, sasa tuambie:-
ReplyDelete1. nani amewajibishwa na kwa kiwango gani.
2. maandamano ni lini ili hata 'kafiri' mie nikahudhurie.
3. ikishindikana maandamano, ponda atuambiwe mgawo wake ngapi.
Ndugu zangu waislamu, poleni! Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma anaona nia za ndugu zetu walio katika kusubiri safari ya kwenda Mecca kuhiji. Lolote lile litakalotokea, tumwachie Allah! Hii ni mitihani tu katika kuitafuta pepo: O'C -Sinza
ReplyDeleteDini Saudia ilikuwa zamani sio sasa watu wanafuata mji mtakatifu ulioko huko, na umaskini nao mbaya, nchi yetu isingekuwa maskini haya yote yasingewakuta hao Mahujaji, na hata huko Saudia unafikiri kwa mfano ingekuwa ndiyo Wamarekani wako stranded kwa muda wote huo ungesikia cha slot au nini?
ReplyDeleteMie ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awatue kwa hili, wakijaaliwa kwenda Hijja sawa wasipojaaliwa basi maana Mwenyezi Mungu ameona nia zao za kutaka kufanya ibada, na inasemwa ukinuia kutenda jambo jema basi Mwenyezi Mungu atakulipa kwa yale uliyonuia. Lakini hiyo stress waliyonayo hata sipati kuifikiria kwa siku zote hizi walizokuwa wakisubiri. Na kama wakifanikiwa kwenda kuhiji basi kwa taabu zote walizopata (kama maswahaba walivyotaabika enzi hizo) Mwenyezi Mungu atawalipia.
Ninawaomba wawe na moyo wa subra kwani kila kitu ni majaaliwa ikishindakana mwaka huu basi kwa watakaokuwa hai mwakani Mwenyezi Mungu atawajaalia kwenda huko kuhiji. Waislamu tunaamini katika kudra, na kila jambo lina sababu yake, sababu ya jambo hili kuwa hivi itajulikana tu, kama ni bahati mbaya, uzembe wa makusudi au makusudi mazima ya kukomoana. Yote tumwachie Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi, maana anajua yaliyo dhahiri na sirini.