Nimepata nafasi ya kuzungumza na Dr. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza Mkataba wa Richmond. Dr. Mwakyembe ametoa tisho la wazi na dhahiri kwa wale wote ambao ni watumishi wa serikali na walienda mbele ya kamati hiyo na kusema vitu vya uongo kuwa "jambo hili si la mzaha" na ya kuwa kamati yake "itawapa fundisho ambalo haliwezi kusahulika". Yafuatayo ni mahojiano yangu na Dr. Mwakyembe dakika chache zilizopita.

Title: KLH News Episode: Walioongopea Kamati: "Tutawapa fundisho la kukumbukwa" - Mwakyembe

Enjoy!
Mwanakijiji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kama kweli atafanya hivvyo itakuwa historia kubwa ya kizazi .matatizo mengi ya viongozi wa kiafrika huwa wanasahau kuwa ukinya sehemu unayolala .saa ya kulala ikifika linakuwa tatizo lako pia si ile harufu wanapata watu wengine.hapo ndiyo kazi inaanza kuwa gumu

    ReplyDelete
  2. We really need the output. Jamani kwa kweli mamilioni yanazidi kuteketea nasikia sasa tume imejimuvuzisha US kwa uchunguzi zaidi, na yule Hosea wa Takukuru taarifa aliyotoa kwamba Richmond ni 'clean deal' aliitoa wapi? AIBU kabisa kwa taasisi kubwa kama ile kutoa taarifa feki zakukaanga. Watu wamekuwa wakilalama toka mwanzo lakini wakubwa wakanyamaza kimya kama hakuna tatizo. Ah! kwa kweli we are finished. Mwakyembe tunataka mje na taarifa zakueleweka sawa kabisa na gharama ambazo mnaingia kwa kutumia fedha hizi hizi za walala hoi na hatua zichuliwe vinginevyo kwa kweli kabisa kabisa kabisa wananchi tutazidi kupoteza imani kwa serikali yetu. Kwani tunasikia mashahidi/mashuhuda hivi sasa wanafundishwa nini cha kusema na end result wanatofautiana wenyewe kwa wenyewe. Isiishie kwenye mafaili kama ripoti za tume za akina Warioba na mambo yao ya rushwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...