basi la upendo toka dar kwenda mbeya lilipata ajali jana mchana sehemu za mafinga, iringa, baada ya kulivaa roli la tela lilokuwa limeegeshwa pembeni. watu kadhaa walijeruhiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Poleni sana. Wala vumbi mwapenda kulinganisha bongo na majuu. Ajali kama hiyo inaletwa na umasikini wetu. Zingejengwa barabara zenye at least 'lanes' nne hakuna kupishana uso kwa uso. Inatia uchungu

    ReplyDelete
  2. inaelajali haina kinga lkn kwanini kwa wenzetu kama uingereza sio sana kutokea maajali kama bongo? bongo ajali ni kawaida na watu 20 au 30 wanapoteza maisha katika ajali 1 tu je kukitokea ajali 5 kwa wiki unafikiria watu watakuwa ni wangapi jamani........polisi wa usalama wawe waangalifu na madereva.... au hao matajiri wenye magari wasiajiri watu ovyo ovyo bila hivyo itakua kama vita vile kwa watu wanavyokufa kw ajili ya ajali.

    ReplyDelete
  3. Jamani hizi ajali zitaisha lini????????? Ndugu zetu wanakufa kila siku. Tatizo ni nini???????????? Mungu tusaidie.

    ReplyDelete
  4. Nyinyi madereva wa bongo utafikiri mnamapepo kila siku mnasikia ajali zinatokea kila sasa na zinasitisha maisha lakini bado tu mnaendesha magari utafikiri punguani jitahidini kuwa waangalifu acheni uzembe mwingine unazuilika

    ReplyDelete
  5. watanzania tusidanganyane ajali zinaepukika.nafananisha na hapa uk magari mengi sana ila ajali ni negligible.driving licence unasomea kama unataka cheti cha diploma.dar licence ni katika sekunde unapata.pesa yako tu.iam serious men!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. watazamaji wote sasa...wanangoja kuwaibia majeruhi na maiti...

    ReplyDelete
  7. Inasemekana watu wawili wamefariki hapo - dereva wa Upendo Coach na abiria mmoja mfanyakazi wa hopitali ya rufaa Mbeya.

    Rest in Peace.

    ReplyDelete
  8. mh jamani ajali hizi naona mara zote ni kusababishwa na mwendo mkali wa madereva, hii si y kupinga, ndugu wa ulaya (uk) si lazima kuwa na lane kumi na tano kumi na tano ndo ajali zisitokee, ishu ni uangalifu tu barabarani na si kingine, utaovertake vipi katika kona, wakati unapanda mlima, huu si uzembe? gari watu 70 we wabeba watu 100 unategemea nini hasa?, mwendo ni 80km/hr we uanenda 150km/hr na roho za watu, pia kingine madereva huwa wanakunywa pombe na kuvuta bangi, wengine hawalali vya kutosha akifika mjini analamba dumbwizi lakeeee (bia) mpaka asubuhi anaenda kuanza safari huku dumbwizi lake bado lipo kichwani weka gambe toa gambe weee, hii ni sababu tosha ya ajali. madereva kuweni makini jamani na vyombo hivi vya usafiri mana mwapoteza maisha ya watu buree, sina mengi

    ReplyDelete
  9. mtoa ushauri wa kwanza hapo juu, acha dharau zako za kijinga. wewe kuwa nje ya TZ ndio kunakupa kiburi cha kusema watu wa nyumbani wala mavumbi? Labda familia yako wewe. Kwanza hata huko uliko tukiangalia kazi unayoifanya labda ni ya ovyo kabisa. Mimi nina uhakika Michuzi ungetafiti kazi wazifanyazo walioko nje, ungewaonea huruma. Pia ungetamani hata kuwaajiri. Wengi sometimes mnatumia lugha ya dharau wakati kule nyumbani mmetoka kwenye dhiki sana. Nasema hivi nikiwa nje, na wala sioni kama ni swala la kudiriki niseme mtu wa TZ anakula mavumbi. Wewe mjinga kweli! Nchi gani haina wala mavumbi? Dhiki zipo kote duniani. Huo ni ulimbukeni. Watu kama yie hata ukiagalia utakuta ulienda nje sababu ya hela ya babako aliyotuibia serikalini kwa cheo chake. Ndugu zetu wamekuwa maskini sababu yenu. Tuheshimiane tu, dharau mwiko. Utakosa baraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...