hata hivyo mdau peter anaishauri serikali kuitupia jicho sekta ya usafi kwani kwa waendesshaji binafsi ni mzigo mzito ukizingatia watu hawana utamaduni wa kulipia huduma kama vile maji na umeme na takataka ndio kabisa, hivyo wanabaki kulemewa na gharama za uendeshaji.
peter anapendekeza kwamba serikali itenge bajeti kwa sekta ya usafi na kutoa malipo kwa waendeshaji binafsi kwa niaba ya wananchi kwani kama inavyofanya kwa makandarasi wa ujenzi wa barabara na shughuli zingine kwani ansema watu hawalipii huduma hiyo na kila siku gharama zinapanda. pia ametoa rai kwamba wanaoagiza magari na vifaa vya takataka toka nje wasamehewe kodi kama wanavyosamehewa wawekezaji wengine.
kampuni ya mdau peter iliyo kwenye jengo la iliyokuwa national steel company ana magari 12 kwa ajili ya taka ngumu na za majimaji (liquid and solid waste) ambayo endapo hali itaendelea kuwa hivi kwa watu kutolipia huduma hiyo na serikali kukauka, kuna hatari akafa kifo cha mende


Hayo ndiyo mambo sasa sio wale jamaa wanatembeza magari mabovu na machafu eti wanakusanya uchafu wakati magari na watendaji wake nu uchofu tosha.... Michuzi, asante sana kaka haya ndio mambo tunatakiwa tuyafanye na kijana Peter afunge buti na kupiga mzigo... Sasa Mwekezaji swali langu ni kwamba kazi anayoifanya Peter ni nzuri katika kutunza mazingira, "Alipewa msamaha wa kodi???" au kwa vile ni mzawa, teh teh teh
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania na Watu wake...
Hapo anatwanga maji kwenye kinu tu.
ReplyDeletemagari 12 kwa jiji la Daresalamu!
Ataanzia wapi aishie wapi? Atazoa wapi aache wapi?
Anyway. All the best!
siungi mkono tabia za watu wanaomua kuwekeza halafu wanataka kusamehewa kodi na huduma zao zilipiwe na serikali.Bw Peter hongera kazi unayoifanya ni nzuri sana,lakini ni vyema ukabuni mbinu mbalimbali za kuendeleza kuwekeza bila kutegemea serikali.swala la kuwa wananchi hawako tayari kulipia hii huuma ilibidi ulifanyie utafiti kabla hujaanza biashara na swala la kodi pia ulibidi uliweke kwenye bajeti zako za awali.yule bw mwenye hospitali ya moyo naye alikuwa ana madai kama yako,sasa tujiulize ni wapi tunaelekea iwapo kila mtu anayetaka kuwekeza anataka huduma yake ilipiwe na serikali na asamehewe kodi.usivunjike moyo na changamoto unayoipata,kazi buti na endelea na kazi nzuri uliyoianzisha,swala la serikali litakubadilisha mwelekeo na unaweza kuishia njia ya panda.ni bora kuanza kupalilia tabia kwa wananchi kujilipia huduma hii kuliko kukata tamaa na kuiomba serikali kufidia malipo hayo.kila la heri...zemarcopolo.
ReplyDeletenilipo itupia jicho picha hizo nilidhani ni kwa mama eliza, duh kumbe hata bongo mambo haya yapo hii imekaaa vizuri wadau kuliko yale matreka yanayoharibika kila siku barabarani na kusababisha foleni za magari, binafsi nimeipenda hii ilibidi watu kama hawa wapewe support ya nguvu na sirikali badala kodi atakazo tozwa yeye mwenyewe atakoma, na pia sie wabongo tubadilike tujifunze kulipia huduma jamani.
ReplyDeleteKazi nzuri Peter Hongera sana!
ReplyDeletemwanangu Peter au tall tunavyokuita kwenye kijiwe cha supu leaders nakuaminia.we kaza buti,wanaosema oh unafanya biashara ya kunyonya ninihiii achana nao,huo ndo ujasiriamali na one day yes utamzidi bill gates mshiko!!!!!!!!!
ReplyDelete