rais wa shirikisho la soka nchini (tff) na mchezaji wa zamani wa taifa staaz na pan african leodegar chilla tenga leo anajitosa kugombea kiti cha urais cha shirikisho la soka kwa nchi za afrika mashariki na kati katika uchaguzi mkuu unaofanyika leo hoteli ya peacok millenium towers kijitonyama, dar. wapinzania wake ni kamal shadadd wa sudan na ashebia giorgis toka ethiopia. uchaguzi huo unafanyika kabla michuano ya 34 ya ubingwa wa soka katika nchi za afrika mashariki na kati yanayoanza kesho hapa dar na arusha hadi december 22. wadu na tumuombee tenga ashinde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Huyo M-Ethiopia mshamba anamwomba Tenga ajiondoe hata kabla ya uchaguzi,demokrasia ya aina gani hiyo.Tenga asiposhinda basi kuna mbinu atakua amechukua hela akaamua kulala mbele na atatutambua.

    ReplyDelete
  2. Tenga ni kichwa anaweza mambo, apewe hiyo nafasi nyeti nina uhakika anauweza kuleta mabadiliko makubwa katika medani hii ya soka EA. Heshima imerudi soka la bongo alhamdulillah uzalendo umeanza kurudi, sio enzi zile za akina Ndolanga na mwenzake Masanja wanagawa posho za wachezaji wanaoenda kwenye mechi ya kimataifa nyuma ya basi!! kama hawana ofisi, kudadadeki, Isipokuwa nae aangalie ndani ya tff yake kuna kundi la wanyama wanaomzunguka na wanaonekana wana uchu wa fisi. Epuka vikashfa vya kichwara kama vile uuzaji wa tkt feki n.k. Kwa ujumla wake mie namkubali, hebu mpeni hilo pande!

    ReplyDelete
  3. Khaa!
    Mbona ka Msomali!?!
    Mweeh!

    ReplyDelete
  4. Mzee tenga, mafaniko tumeyaona kwenye soka l;a bongo.... Tunakutakia mafanikio kwenye kinyang'anyiro cha leo na ujue kwamba tayari hao majamaaa washakugopa ndio maana muEthiopia alikuwa anakupigia ndogondogo ujitoe, mwambie akalaghe baho....
    All the best.

    Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake!!!

    ReplyDelete
  5. Watu wengine bwana na comment za kitoto.Ei kama msomali.Umekosa cha kusema just keep your mouth shut.Sio lazima ucomment kila kitu.

    ReplyDelete
  6. huyu jamaa anaonekana ni kichwa! kama mdau alivyosema hapo hapo juu Tenga fanya kazi kama ilivyoonyesha unaweza kufanya kazi, na fisi wengi wapo hapo .wasio na akili wasipewe nafasi tena kama kule wale wa jangwani na msimbazi ndio sumu ya mpira wa tanzania kabisaaaaaaaaaaaaaa!! yaani wananikera hayo wajinga wanao jiita makomandoo!!.Tenga kila la heri katika majukumu yako mapya,ongeza bidii na sio ukubwa badilisha mpira wa africa mashariki kwa mujibu wa majukumu yako, tumia nafasi hio kujifunza kwa wanamashariki wengine na unoneshe TFF. akaksante.

    ReplyDelete
  7. Tafadhali naomba muandishi wa habari hapo juu arekebishe kidogo CV ja Bw. Leodgar Tenga. Bw. Tenga alikuwa mchezaji wa timu ya taifa na Yanga vilevile, sio Panya. Yanga Kandambili sio Panya, mpo hapo wazee. Ingawa tuko Ulaya miaka mingi lakini kumbukumbu bado zipo.

    ReplyDelete
  8. Watu wengine bwana.Tenga aliichezea Pan African na ni timu yake ya mwisho kuichezea kabla hajastaafu soka.Michuzi hakukosea timu yake ya mwisho ni Pan upende usipende.

    ReplyDelete
  9. watu wengine hawajui mpira wa bongo huyu jamaa tenga alikuwa mchezaji wa shoka taifa stars,yanga halafu pan africa enzi hizo mabo yalikuwa moto moto, watu walimwachia nchi nyerere.

    ReplyDelete
  10. 10:57 watu wote bongo sio lazima wawe wabantu kama wewe, kwa taarifa yako kuna wambulu,wamang'ati,wasandawe,hadzapi,warangi,wamasai. wote hawa ni watanzania walikuwa bongo kabla ya wangoni kuja bongo. unatakiwa utembee nchini uone makabila mbali-mbali, acha kumsikiliza mtikila na ujinga wake, hatufanani lakini tunapendana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...