kuna wadau wametaka kuona crib yangu. basi ni hiyo ya pili kushoto inayoangalia gaden. ukitaka kuja panda daladala la ukonga. omba msaada kwenye tuta karibu na kwa mpemba sokoni ukonga magereza, ukishuka ingia shoto kijia cha vumbi halafu nenda weeeeee mbele utakuta transfoma ya tanesko, kata kulia ongoza na njia hiyo hiyo, mbele utaona shule ya msingi, geuke kulia utakuta genge, ukivuka genge mbele utaona mtaro wa maji (sasa umekauka) vuka na ukishafika kwenye kontena la kijani utakuta jamaa wanacheza puli. ulizia utaoneshwa mara moja. karibuni kwetu wadau...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. DUUH HAYO MABATI YANATISHA AMANI INABIDI WAKAZI WOTE WAPO WACHOMWE SINDANO ZA KINGA YA TETENASI.

    ReplyDelete
  2. wale mliotaka mpewe ambulance za uhakika niambieni hapa ambulance zitakuwa na kazi gani?Pia mliokuwa mnataka kampuni ya posta iachane na old fashion ya kutowa huduma oneni haya.
    Na hizi kampuni za kuzima moto,ambulance(paramedic) sijui kama zinahijika bongo.90%+ ya wakazi wa dar wanaishi sehemu kama hizi.Hata sehemu zile zenye majina makubwa mikocheni,mbezi nk kuna barabara ama niseme vichochoro havipitiki vizuri sababu barabara ambazo ni two ways si exactly two ways bali kichochoro ambacho inabidi gari moja lipite wakati lingine linasubiri.Kazi ipo kwetu

    ReplyDelete
  3. Ukitaka mtu anayeishi maeneo kama haya akupe direction ya kwenda kwake utachoka.

    ReplyDelete
  4. ahhahahahahahhaha! kaka Michuzi kumbe na wewe hujatuliaa eheeee?! ahahahhahaahha,

    ReplyDelete
  5. Michuzi unasema utakuta watu wanacheza "puli"??? au ulimaanisha puulu? mi navyojua puli halichezwi hadharani

    ReplyDelete
  6. Michuzi nae miyeyu sometime.Hilo garden liko wapi?Maelezo yalivyo marefu sidhani kama yanaendana hiyo picha/ramani.

    ReplyDelete
  7. Nikiwa natua bongo kama niko na wazungu kwenye ndege wakiangalia hiyo mipango miji huwa najisikia aibu sana, nikilinganisha na kwao !!!

    ReplyDelete
  8. Hapo hakuna tofauti na maisha ya wanyama !!!

    ReplyDelete
  9. Dah kumbe tuko jirani..Asante nimepata kwa kuomba chumvi, msisahau hii jadi jamani.

    mdau-canada

    ReplyDelete
  10. kwa hiyo kama jamaa hawachezi puli siku hiyo kwa michuzi hufiki!! Umenikumbusha mambo ya Bombii nyumbii, mam an'osh'vyomb', utakut kuna jogo ana wik, hap hap ndipo nyumban kwetu

    ReplyDelete
  11. Wadau mimi ijumaa niko off. Naprint instructions nachukua camera yangu naenda kumtembelea Brother michu. Sasa je brother michu utakubali ku publish picha ya eneo lako na vituo ulivyoelezea au nyumba uliyoelekeza hapo juu au nisisumbuke?

    ReplyDelete
  12. Michuzi nihesabuni kwenye chakula cha jioni leo mie nipo hapo kwani mie ni jirani yako!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  13. Nani Anabisha Bongo New York???Kudadadeki

    ReplyDelete
  14. WEWE ANON 3 KUMBE UWAJUI WABONGO KWA KUBADILISHA MAJINA PULI ANALOKUELEZA MICHU NI MCHEZO WA BAO.

    ReplyDelete
  15. Duhh!! hapo kazi ipo Michuzi unasema "Geuka kulia utakuta genge" Sasa je ukikuta Kandoro ameshalibomoa na askari wake wa jiji si ndio mdau ameshapotea tena! Maana moja ya vielelezo vya ramani kutakuwa hakuna tena!! MUNGU IBARIKI TANZANIA, ISHALLAH TUTAFIKA TU!!
    KIDUME, USA

    ReplyDelete
  16. Waafrika bwana! Hamkosi kubwabwaja? Mlitaka kujua kwa Brow Michu huyo kawapatia ramani, Sasa mambo ya kuulizana mabati yatakuwa na tetanasi or Ramani ya nyumba or limepanda limeshuka, Nini ? Wengi wenu mnaomwaga tetere hapo kwenu hakuna bati bado ni nyasi tu zingeonekana Juu.

    Au mnataka kusema mnatoka Kilimanjaro nyie? Teh teh the eeeeeeeee. Mtajiju, Brow Michu asante kwa Maelekezo siku tukizuka hapo Bongo tutamiti tu.

    ReplyDelete
  17. Michu, Huko kwako siwezi kufika hiyo inayosema Transfoma ya Tanesco kwani nyingine ni transfoma za nani? na hao wanaocheza pull wanafanya hivyo masaa 24 na kama siku hiyo puu ni bovu huko kwako hakufikiki?

    ReplyDelete
  18. Hao waliokandya sijui tetenus, sijui nini wote wanatoka Tandale kwa Mtogole au Uwanja wa Fisi au Manzese kwa mfuga mbwa! Ndio wako kwenye denial. Sasa hiyo tetenus huko kwenye bati unaenda kutafuta nini? Nyumba nyingi za Dar mabati yanashika kutu kwa ajili ya chumvi ya baharini.

    Huyo anayeona aibu eti akiwa kwenye ndege juu naye pia ni wa ajabu. Unaona aibu ya nini? Kwani hapo hawaishi watu? Mbona huko Ulaya na Amerika kuna watu homeless wanaishi barabarani! Tena wengine wanaishi kwenye trailers na watoto miaka nenda maka rudi.

    Mlitaka akupeni ramani ya nyumbani kwake au picha ya nyumbani kwake muanze kumnyanyambua? Angalau yeye ana kwake anapaita kwake, wengi wetu hapa ni kupanga, kuishi kwa mjomba O'bay baada ya kubebwa kutoka bush, na kuishi nyumba za serikali au mashirika, siku wenye nyumba zao wakitutimua itakuwa kazi kweli kweli!

    Haya na wewe Michuzi hiyo garden mbona siioni. Au hutaki wageni kwako maana hayo maelekezo ni ya kufukuza wageni kabisa.

    ReplyDelete
  19. mjomba michu kumbe kwako kuzuri hivyo maana kumekaa kama london vile kuna mchezo mmoja kwenye chanal ya londo ya bbc one kinakua kila monday to friday jioni kinaitwa eastender kikianza kinaanza kuonesha ramani kama hiyo kumbe kweli bongo ni uhaibuni siku hizi

    ReplyDelete
  20. Ha ha ha ha, Michuzi wewe mwisho!

    ReplyDelete
  21. Anon wa Monday, February 25, 2008 1:29:00 AM EAT Hujatulia kabisaaaa...! Kamchezo ndio kako nini ..? ila madokta wanawaambia hakana madhara so keep it up. LOL...

    ReplyDelete
  22. michu Hauja tuambia huko ni zone ngapi?nahiyo ndinga inayo fika huko ni aina gani?

    ReplyDelete
  23. Oops! Ramani.... Kun'radhi michuzi. Nyumba yako haina namba? I'ld luv to pay my visit, na nitakuja na kamera tayari kuwapa wadau uhondo. Tafadhali nipe namba ya nyumba, incase "wacheza puli" kama hawatakuwepo (hasa kama ni day-time) tusipotee. Lol! Michu weeee. Kama kiwanja chako hakina hati na namba, wewe ni fisadi.

    ReplyDelete
  24. Wadau, mpango wa miji sio lazima uzingatie 'mistari minyofu, au miduara, au 3Ds' bali mafisadi wanaruhusiwa na kuruhusu kujenga ovyo ovyo ilimradi ikawa-usiku-ikawa-asubuhi.

    Hainiingia akilini kuwa mtu asiye fisadi (kwa tafsiri ya kileo) anaweza kuruhusu au kuruhusiwa kujenga namna hiyo! Michuzi, bangaluu lako ni namba ngapi? Hapa jamani sio kwamba tunakandia, bali tuchukue somo, kuwa hata mtu akibeba boksi akapata chake, basi ni vema azingatie KESHO.

    Kilichonifurahisha ni kuwa japo kwa akina kaka misupu kumekaa shaghala baghala watu (pengine vijana) wanapiga puli. Mchezo huu hauchezwi hadharani, ni kweli. Mnaotaka kwenda jitahidini mida ya saa moja-mbili na kuendelea mtawakuta 'wachezaji.' Jamani, puli madhara yake sio makubwa ukilinanisha na ngwengwe!

    Hivi wadau, kuna haja ya kuvaa soksi ukiwa unacheza puli? Huko kwa akina misupu ni kwa timu, yaani, mnashirikishana mawazo, pengine. Tehe!

    ReplyDelete
  25. Du michuzi hii kali,kwa haya maelekezo hata nani hafiki ila BONGO KUZURI BWANA NANI ANASEMA BATI ZIMEOTA KUTU!!! HIVYO NI VIGAE HA HA HA HA HAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  26. Nawe michuzi usituzingue bwana unadhani watu hatuna kumbukumbu,hii picha uliiweka tarehe 17 dec mwaka jana kuhusu mipango miji leo kumekuwa kwako au unatusanifu sie tunaeishi huku? never mind nyumbani ni nyumbani tu.ukikatiza mitaa hii siku za week end utazimia mwenyewe kulivo live,mdundiko,mnanda,sangula. Kalaga baho

    ReplyDelete
  27. ASante Michuzi kwa kuleta hapa jamvini tatizo la kutowekwa majina ya mitaa au vichochoro kwenye makazi yetu. Au ule mpango wa kutoa majina wa akina Dito ulikuwani wa Uhindini tu?? Madiwani na mipango miji kazi kwenu. Rugby management style hiyo.

    ReplyDelete
  28. duh unatisha braza Michu kumbe maskani una garden,ila unakaa mbali to Uk hadi town mornie najua si mchezo kwa sisi watu wa daladala,au una motokaa mwezetu?
    Lakini poa nyumbani ni nyumbani,mcheza kwao hutuzwa! au vipi?

    ReplyDelete
  29. kwa nini watu wakikomenti hapa mbaka wajionyeshe kama wapo nje ya nchi?????????????????????????????

    ReplyDelete
  30. NDIO WAKO NJE YA NCHI KWANI HUJUI KUWA MTANDAO NI NJE YA NCHI UKIINGIA KWENYE INTERNET CAFE UKAFUNGUA MTANDAO BASI UNAKUWA UKO KWENYE GLOBAL WORLD HAUKO TZ TENA! AU HATA UKIFUNGUA MTANDAO OFISINI KWAKO MUDA WA KAZI, AKILI YAKO YOTE INAKUWA HAIPO HAPO INAINGIA KWENYE MTANDAO NA KUTOKA NJE YA NCHI!!!!!!

    ReplyDelete
  31. Kaka Michu, nimefuata direction zako kuja kwako sasa nime-losti, sasa pale kwenye transfoma la tanesko mimi sijaona njia hapo kuna kauchocholo hivi ndio hako au vipi maana hakuna njia kulia hapo???? Wewewwweee kaka kwa ma fixi- maana hautaki tufike kwako sio unamwogopa mama mwenye nyumba nini ndio umeamua kutupitisha hii ruti yako ndefu hivi? Nipe shoti kati basi..kesho nitafika hapo tupige stori kidogo!

    ReplyDelete
  32. Hongera sana ndugu yangu kwani una kwako. Kama unavyojua tena ukiwa na nyumba Dar basi wewe umeula.

    ReplyDelete
  33. Wadau hakuna aibu this is home, be proud, leteni chemsha bongo tuendeleze mazingira yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...