mwanamuziki aliyewahi kupigia twanga pepeta deo mwanambilimbi (kati juu, na kulia chini)mmoja wa wasanii wenye mafanikio makubwa baada ya kuamua kuanzisha bendi zao wenyewe. yeye anatamba na kikosi chake cha kalunde band na alikuwako kutumbuiza usiku wa juzi wakati wa hafla ya kuzawadia wanamichezo bora nchini iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa michezo - taswa - kwenye hoteli ya landmark, ubungo, dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. duhh wadada kama wapo texas hivi hawa akina kalunde kwao itobora (jina naona linafanana na huko) hawana vitu vya kikwao wakakoleza mpaka waonekane kama wapo texas?

    ReplyDelete
  2. Michuzi, enzi zile wamarekani walivyotoa ule wimbo wao maarufu wa msaada wa janga la njaa Ethiopia "We are the world", watanzania pia walitoa wimbo wao (kwa bahati mbaya nimeusahau jina) Mmoja wa wale waTanzania was a Mwanambilimbi kama sikosei alikuwa anapiga kinanda. Ndio huyu?

    Halafu kuna mwenye ule wimbo wa watanzania tuwasiliane manake nautafuta sana.

    ReplyDelete
  3. hao wanahitaji msaada wa uvaaji hilo joto na boots na kudansi vipi jamani/

    ReplyDelete
  4. jamani anon feb 24 11:47 ndio hivyo na cc tunataka tuwe ktk fashion,huku hizo boots tunaziita travota huko mwaziitaje?then tell us wata so in up there besides legings na respect me ya missy eliot.
    i like her brand mpk kishanshuda wa beckham kavaa na umbo lake lile we acha tu

    ReplyDelete
  5. Hivi Mzee Michu unafahamu kwamba kitu pekee kinachozorotesha maisha ya wabongo ni SERIKALI KUWEKA MBELE POLITICS.Ukiangalia kwa undani zaidi part iliyopata maendeleo zaidi ndani ya bongo ni SIASA.mara Mtanzania huyu ni mwenyekiti wa something Africa,mara huyu ni spika wa bunge la africa.Politicswise we r very good,kitu kibaya zaidi ni kwamba watu wachache sana wananufaika na hii siasa.Mambo mengine kama Michezo na music ambayo watu wengi wangenufaika kama ingetiliwa umuhimu tupo vry shallow,Serikali imetumbulia macho siasa(nazungumzia toka enzi za mzee Nyerere)watu weusi wengi duniani wanafanikiwa kwa kupitia michezo na music.
    KILICHONIUMA ZAIDI NI KWAMBA WEWE UMEZUNGUMZIA HABARI ZA HAFLA ZA KUZAWADIWA WANAMICHEZO BORA NA HUJAELEZA CHOCHOTE KUHUSU HIYO HAFLA,NANI KASHINDA NINI?...ETC
    PLEASE MICHUZI WRITE LESS ABOUT POLITICS AND MORE ABOUT MUSIC AND SPORTS FOR THE SAKE OF NEW GENERATION.Its me AB

    ReplyDelete
  6. Anonymous hapo juu sunday feb 24 9.55
    TUNAJUA UKO TEXAS HUNA HAJA YA KUSEMA TEXAS;TEXAS HUNA HATA JEMA LA KUONA NI KUPONDA TU KILA KITU NDIO MNAISHIA KUPEBA VIZEEE TU HUKO NA SHULE MMEZIKIMBIA FAMILIA ZENU HUKU ZINAJUA NNASOMA KUMBE NI KWENYE HOMES TU ZA WATOTO TAAHIRA

    ReplyDelete
  7. MZEE DEO MWANAMBILIMBI SIKU NYINGI SAAAANAAA MZEEE ENZI ZA BANGWE KIGOMA HALAFU BULUBA SHY NAKUKUMBUKA SANA VIPI FRANK YUPO WAPI SIKU HIZI? MPE HI PAMOJA NA WENGINE BROTHER NA SISTER WAKO NIMEWASAHAU MAJINA....!

    ReplyDelete
  8. deo looh miaka mingi, hongera sana kwa mafanikio yako -Debby TAZAMA Oyster-bay.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...