WADAU KUNRADHI KWA HABARI YA AWALI. KUMEKUWA NA MABADILIKO KIDOGO. JK ATATANGAZA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI SAA TISA ALASIRI KATIKA UKUMBI WA TAMISEMI, DODOMA, NA SIO SAA NNE HII AMA IKULU NDOGO YA CHAMWINO.
HABARI ZINASEMA HIVI SASA JK ANASHAURIANA KWANZA NA ALIOWATEUA KATIKA BARAZA HILO KABALA HAJAWATANGAZA. HADI SASA MAJINA YA NANI ATACHUKUA WIZARA IPI HAIJAJULIKANA.
TUFANYE SUBIRA, LEO HILI ZEGE HALILALI...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Michu, its almost 1 am, hata hakulaliki....ok, tunakusikiliza, ila sijaelewa, ina maana hii bulogi ina mahali pa kusikiliza sauti nk wakati tunaendelea na kusubiri ama?

    ReplyDelete
  2. MICHUZI MBONA TUMEAMBIWA SAA TISA WEWE CHANZO CHAKO NINI

    ReplyDelete
  3. we michuzi ni muongo sana unajifanya uko karibu sana na taarifa kumbe uzushi tu,mpaka utonywe na mtu ndo unajua,ukawadanganye wa ughaibuni sio sisi,kwa taarifa yako mawaziri wanatangazwa saa tisa

    ReplyDelete
  4. nashauri arudie utaratibu wa nyerere katika kupangua na kutangaza wajumbe wa baraza la mawaziri. ghafla mungu ibariki inapigwa rtd; watu mnakimbilia redioni na ghafla waziri mkuu mpya anatajwa pamoja na baraza la mawaziri kupanguliwa na kupangwa upya. huu uzungu wa press release, mheshimiwa umekushinda. nakata tamaa kuhusu mambo mengine.

    ReplyDelete
  5. mheshimiwa rais kikwete, tumia mfumo wa babu nyerere ambapo ghafla rtd inapiga wimbo wa taifa; watu wanajongea redio kusikiliza kulikoni na kutangaziwa kwamba, waziri mkuu kawekwa mpya na wajumbe wa baraza la mawaziri wamepanguliwa; haya mambo ya kisasa ya press release na kuwaweka wapigakura roho juu, hayafai yanakupunguzia maksi.

    ReplyDelete
  6. ukimwi utuweke roho juu; tanesco c/o mafisadi watuweke roho juu basi mpaka na rais wetu kututangazia baraza la mawaziri mpaka roho zitutoke?

    ReplyDelete
  7. Ubabaishaji bwana wa nyumbani! Hebu ona, hata time ya kutaja hao wababaishaji inababaishwa!

    Until when our leaders will start to tell us a truth and only truth!...Inamaana Mh.Rais hakujua kwamba anahitaji time ya kuzungumza na hao jamaa before mpaka atoe muda wa utata wa saa 4 asubuhi?

    Zengwe linaanza kwa Mh. hawa wachaguliwa wanamalizia tuu.

    Ubabaishaji mtupu!...na mineno kibao ya kutisha waandishi! Mara mkishelewa hakuna kuingia etc.

    Nina wasiwasi na watu wa mipango wa Mh.

    NB: Michuzi acha kuitenga hii msg. Itoe hapa ktk blog yako!

    ReplyDelete
  8. Acha kuwarusha roho watu Michuzi ngoma bado mbichi hadi saa tisa au kumi. Sasa hivi JK yupo na wale aliowateua kuwahoji mmoja mmoja kama wana biashara na mali then anawatoa na kuweka mwingine kwa hiyo bado tusubiri mie nipo Chamwino hapa

    ReplyDelete
  9. MIchuzi unatuzengua,huna lolote kama alivyokuponda Anonymous said unajifanya kuzinyaka habari za CCM lakini kumbe kuna mtu anakutumia sms,ndo unakurupuka.Acha miyeyusho yako tumekuchoka.

    ReplyDelete
  10. Huu ni ubabaishaji, yale yale....!

    ReplyDelete
  11. NAKUBALIANA NA WADAU WENGI MLIOCHANGIA HAPO JUU, KUHUSU KUWAWEKA WANANCHI ROHO JUU KUFIKIRIA UTEUZI KWA KUBADILISHA MUDA HADI MARA 2. HIVI NI DHARURA ZIPI ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUAHIRISHA HIVO? WATU HATUJALI MUDA, BADO TUNA MATATIZO KWA HILO. NO HURRY IN AFRICA, Oh, MY GHOSH - HADI LINI?

    ReplyDelete
  12. Something I hate about you Michuzi is that 'you are much know' while you know nothing!

    You embrace 'big guys' for your own personal gain!....One of the most hypocrite I have ever seen!

    ...and something that sums up about you is a 'bookless egoistic individual'

    You will never win in your battle because you are selfish!

    ReplyDelete
  13. Hivi we Anonymouse 9:58 una akili nzuri kweli?michuzi kasema saa tisa we unasema muongo alafu hapo hapo unasema watatangaza saa tisa huo ni uchizi , hujui kusoma nini ?
    alafu mnamtukana michuzi bure wakati yeye ndio anayetup update chap chap saa zingi hata kuliko watu walioko bongo hawana habari ambazo michuzi kazirusha usiku !haya ni maoni tu

    ReplyDelete
  14. michu wakati mwingine kuwa mwellewa na ujue tuliopo huku ni watu wazima, hivyo unavyosema visivyo tokea utajuta.

    ReplyDelete
  15. vasco da gama kaua bendi kweli leo!
    inawezekana nae anataka kujilowassa nini?

    ReplyDelete
  16. Nafikir kuna watu wengine mnashindwa ku reason hapa, mnamlaumu michuzi hasa kwa kosa gani, kulikuwa na press release kutoka state house baraza ni saa nne leo, michuzi akatuhabarisha, then kukawa na second press release kuwa baraza ni saa 9, Michu katuhabarisha, sasa hapo amekosea nini!! au ndugu zenu wamewadanganya kuwa wamo barazani so mnataka confirmation!!!

    ReplyDelete
  17. Wewe anonymous wa 11:02:00 unamponda Michuzi kweli unachefua watu humu. If you hate Michuzi dont visit this blog, simple!

    Sio unakuja hapa kuanza allegations against mtu ambaye in my eyes ni pioneer and trendsetter. Haya si maneno ya kujikomba but ni pure fact. Ukisema leo upange list ya 100 influential Tanzanians jina la Michuzi liko ndani. Hapa hatuongelei influence za kifisadi, bali jinsi blog hii inaweza kuhabarisha na kushape thinking ya wabongo toka Japan, to Kigoma mpaka Brazil. Ebu angalia hits tuu anazopata on this site. Im sure I speak for many nikisema kuwa this blog is ndio stop ya kwanza kila ukiwasha kompyuta.

    Na kwa watoto waliomfahamu michuzi juzi inabidi muelewe kwamba huyu photojournalist ameanza kuwika tangia enzi za picha za black n white kwenye Daily News. If pictures say a thousand words, this dude and his camera knows how to make a picture talk. Hizo ni enzi za cencorship ambapo magazeti yote ya serikali na huwezi kucriticize the muajiri wako. Michuzi alikuwa na uwezo wa ku provide critical commentary in just one photo!

    Yeye si mtoto wa fisadi aliepewa channel rahisi za kwenda kusomea photography ughaibuni na kukabidhiwa kazi baada ya kugraduate. No, ni mvuja jasho who has worked his way up against all odds. He is a humble guy and human, humu amefanya makosa saa nyingine na kuweka picha zisizostahili, akishauriwa anaziondoa na anaendelea kujifunza kwani anajua katika fani yake he is both an expert and a student of his captive audience.

    Its time wabongo tujifunze kujenga na kuenzi vipaji vya raia wetu. Kipaji na charisma ya huyu bwana ntavisifu always.

    ReplyDelete
  18. Endelea na kazi yako Michuzi, achana na wehu hao, ni wajomba zake na Lowasa mwizi. Angalieni sana nyie ndugu zake tutamchoma moto Lowasa kama tunavyowachoma wezi wengine.

    ReplyDelete
  19. kweli wadau wana kimuhemuhe.. Michuzi hatangazi baraza la mawaziri. msimlaumu yeye kuhairisha. It is Vasco Da Gama and his clonies.
    Serenity and vigilant is important.

    ReplyDelete
  20. kweli wadau wana kimuhemuhe.. Michuzi hatangazi baraza la mawaziri. msimlaumu yeye kuhairisha. It is Vasco Da Gama and his clonies.
    Serenity and vigilant is important.

    ReplyDelete
  21. Hilo suala la kwamba Mh. JK yupo na wateule akiwahoji limetokea wapi? Maana ni rahisi kuhoji kwamba je hiyo siyo kazi ya CID? Kutafuta undani wa wabunge (na nchi kwa ujumla)?

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  22. Jamani tupuzeni jazba "TARISHI HAUWAWI"...ndugu yetu anasaidia sana kutupasha yanajiri nyumbani,vingine wa kulaumiwa ni spika aliyeanza kupotosha habri za kutangaza baraza;hata ikulu wanashangaaa nani alisema juma3.
    Nina uhakika kuna watu watabisha hata hapo Michuzi atakapotoa list ya baraza jipya....haahaaa!
    Kikubwa inaonyesha kuna watu wameshapata nani yupo na nani kaachwa;JK kasitukiakaamua aanze kazi upya.
    Tulizeni mori!Naomba niwaache na kibao cha enzi zile kwa vijana wa zamani"mambo badoX2;mabo bado magoma moto moto ya..............

    ReplyDelete
  23. Hivi jamani tumeingiliwa na kichaa humu ndani saa 10:51, ndugu yake mapisto nini?,unampenda ,humpendi michuzi ni wetu tu, kama wivu kajinyonge...naona umepotea njia...

    Achana nao kaka yetu , kazi yako safi sana. Mlitaka michuzi atudanganye ndio mfurahi, mjumbe hauwawi, najuwa tuna moto wa kutaka kujuwa, tulizeni mpira kwanza. wenzangu na mie mmeenda sokoni au ndio mmeshinda kwenye blog?, ndio maana muda hauendi...!!!

    mdau uk

    ReplyDelete
  24. Sasa mnamlaumu Michuzi wa watu kakosa nini? Michuzi hawana wema hawa viumbe wazito wana ugonjwa wa Sononi nilikwambia siku nyingi, cha msingi wasamehe. Mbona blogu ni nyingi waende wakasubirie huko kwenye blogu nyingine sio kutoa maneno ya kashfa humu ndani. My friend you have thick skin otherwise hawa wagonjwa wasononi usingewaweza.

    Wengine wanafikiri watatangazwa wao au wajomba zao ndio maana viroho viko juu. Sasa kama huhusiki kinachokufanya usiende kufanya shughuli zako utakaporudi ndio uingie kuona kilichojiri ni kitu gani eeh! Kwanza hamumlipi kaka wa watu senti tano na si lazima yeye atuletee hizi habari ni hiari yake akiamua hata sasa hivi kusema jamani namwaga manyanga hii blogu basi imenishinda sidhani kama kuna mtu anaweza kumlazimisha.

    Tutofautishe kati ya kujitolea na huduma uliyonunua na tusiwe wepesi wa kuhamishia sononi zetu kwa mtu asiyehusika.

    Hilo baraza halinifanyi nikaacha shughuli zangu, nikashindwa kunywa maji au kushinda kwenye computer I have bills to pay na hakuna atakayekuja nilipia kati ya hao mawaziri. Kwa unayemlaumu Michuzi 'Get a life looser!'

    ReplyDelete
  25. breaking news...........Zakia Meghji nje

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...