mwalimu wakiwa na makamu wa kwanza wa rai mh. aboud jumbe, waziri wa mambo ya nje dk. salim ahmed salim, mama maria na mama graca simbine, na samora machel ikulu na msaidizi wa mwalimu mzee butiku enzi hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kuuliza si ujinga,hizi picha za zamani black and white mnazitunza vipi nakumbuka kipindi kile digital camera na computer vilikuwa hamna.Kuna gazeti moja la kiingereza la kila siku Tanzania huwa wanazo nyingi(wanaziandika 'From our files').Cku hizi wamekuwa wakali hawataki hata uzitoe copy!!Kama umezidokoa huko muhidin shauri yako

    ReplyDelete
  2. Nadhani huu ni mwaka 1975 mara baada ya uhuru wa Msumbiji (Mozambique) kutoka kwa wareno.Baada ya kumtembelea Mwalimu huko ikulu,Samora Machel pia alipitia Mbeya kuwashukuru wananchi katika jitihada zao za kuisaidia Frelimo katika harakati za uhuru!ALUTA CONTINUA!!!

    ReplyDelete
  3. Braza Michu umeiona hiyo pozi ya mzee Aboud Jumbe?. Nimeipenda sana.

    ReplyDelete
  4. Wakati inachukuliwa picha Hiyo Mzee Aboud Jumbe Alikuwa proper President of ZANZIBAR ISLAND na ulimwengu ulitambuwa hivyo kwa hiyo ibakishwe Hiyo historia kama ilivyokuwa kwa faida ya vizazi vijavyo na sio vyenginevyo Kumradhini na Asanteni

    ReplyDelete
  5. Miaka ya 70 Salim Ahmed Salim alikuwa yupo UN , alirudi na kuwa Waziri wa Ulinzi kabla ya kukaa uwaziri Mkuu katika miaka miwili ya mwisho kabla ya Mwinyi kuwa rais, yaanai mwaka 1985. Kwa hivyo hii picha ni ya miaka ya mwanzono mwa 80 huko, ni juzi tu !!

    Baada ya hapo Jume alivuliwa madaraka na Salim akawa naibu Waziri Mkuu wa na waziri wa Ulinzi chini ya Mwinyi , upoooo?

    ReplyDelete
  6. by MBUMUNDU



    Jamani wadau nitashukuru sana endapo mtanipa majibu sawia ya haya maswali yangu yafuatayo;

    1.Kwanini Nyerere alimpenda na kumwamini sana Dr.Salim hata kufikia kumpandisha vyeo vikubwavikubwa haraka haraka,kufanya juu chini(japo alishindwa)ili Salim awe Katibu mkuu UNO,Kumbembeleza awe rais wa Tanzania mara kwa mara etc etc.What is the secret behind?Ni uadilifu na uchapakazi au kuna kingine zaidi??

    2.Kwanini wana CCM na hata wasio CCM,Wapenzi wa Rais Kikwete na hata wasio wapenzi wake,wafuatiliaji wa karibu wa siasa za Tanzania,huwa once wanapoanza kuujadili mchakato wa kumpata mgombea wa Urais wa CCM mwaka 1995,huwa wanasema Nyerere alifanya zengwe ili Mkapa ashinde,ilhali kura zilipigwa kihalali na kuhesabiwa kihalali na mshindi(Mkapa)kupatikana kihalali katika ile raundi ya pili.Jee CCM ilikuwa na plurality system hata kusema Kikwete alipopata kura nyingi katika raundi ya kwanza japo hakufikisha zaidi ya 50% ya kura zote basi ndiye angekuwa mshindi na uchaguzi usirudiwe?Na jee kama CCM walikuwa na clear majority system na Mkapa ndiye akashinda,sasa zengwe liko wapi hapa?

    ReplyDelete
  7. Mnakumbuka ule wimbo - MWALIMU NYERERE JUU! ABUDU JUMBE JUU!

    ReplyDelete
  8. Kumbe Aboud Jumbe naye alikuwa mtu wa mabobish!!

    Nimeipenda pozi yake, inasema 'japo niko tartiiibu lakini niko maniki na sina wasiwasi'.

    Itabidi nami nijidai na hilo pozi on nitakapopiga my next snap!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2008

    aboud jumbe alikuwa kibaraka wa nyerere, alichaguliwa na nyerere baada ya karume kuuwawa, hakuna mtu amevuruga uhuru wa visiwani kaka huyu jumbe, it was easy for nyerere kuanzisha ccm i.e. tanu plus asp, kama karume angekuwa hai ccm isingekuwepo visiwani, karume na ujambazi wake wote alikuwa anajali watu wake wa visiwani,pia kitu muhimu alikuwa sio kibaraka wa mtu ye yote, karume was his own man, and in short period accomplished a lot for the islanders. unaona jumbe amekaa mikogo, mifuko yake ilijaa pesa za karafuu walizodhulumiwa ndugu zetu wa pemba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...