Mzee wa kazi, Issa:

Hongera kwa kazi yako pevu na ya uwazi. Mimi ni mgeni kabisa katika blog hii lakini nimeipenda sana na nitategemea nitakuwa mdau mzuri popote nitakapokuwa dunia hii.

Nimekerwa na suala hili la wadau kuchangia mada halafu hawataki wajulikane. Ninawaomba watanzania tuwejuwe hizi ni zama za uwazi na ukweli, sayansi na teknolojia. Mimi nafikiri watu wakiandika majina yao, hata kama siyo halisi, itakuwa rahisi kubadilishana mawazo.
Wakati mwingine mtu atataka kuongezea hoja ya mdau. Sasa unapokuta aliyandika ni 'anonymous' inakuwa vigumu maana utakuta ukurasa mzima umejaa ma'anonymous'. Mimi nafikiri wadau wakiandika majina ukifanya vizuri utasifiwa, ukichemsha utakosolewa. Na kukosolewa ndiyo njia ya kujifunza! Mimi naamini tunaishi ili kila mtu awe faida kwa mwingine. Hapa ni elimu mtindo mmoja!

Pia wadau wajiamini kwamba wanachosema ni genuine, kutokutaka kujulikana ni kwamba hujiaamini. Mnaona Dk. Mwakyembe na kamati yote walivyojiamini?

Kazi kwenu wadau!
John Paul

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. John Paul, sasa wewe ndugu yangu una hamu ya kutukanwa au nini? nakuonea huruma sana, sababu umeamua kulitoa jina lako humu ndani utatukanwa hadi ndugu zako wakuonee huruma, ila sababu hizi ni zama za "freedom of speach", usi-mind sana.

    ReplyDelete
  2. Mdau John, uliyoyaandika ni kweli tupu! Hiyo kitu tanfanya kule Jambo Forum!

    I liked mostly your last paragraph. Good observation.

    Masanja

    ReplyDelete
  3. Bro. Michu. Mi naomba muniwekee picha ya Shule Kongwe kuliko zote nchini Tanga School.(Tanga Tech.)Inasemekana shule hii ilitimiza miaka 100 mwaka 1996. Yani kwa maana hiyo inamiaka zaidi ya 110. Pia ndio shule waliyosoma viongozi wengi akiwemo Jakaya Kikwete na hata myule Bro. Dito. Haya lete raha!!

    ReplyDelete
  4. Mi nahisi hili jina john paul ni feki. Na kama sio basi mbona hakuweka jina lake la ukoo? Kaweka lake na la baba yake. Embu acha kutupa hadithi za kutokuwa annonymous sisi.

    ReplyDelete
  5. Huyu Bwana John Paul,Nadhani anafikiria watanzania Bado wajinga,wapumbavu,Huyu Jamaa ni Ktk kikosi cha Polisi cha Jk,Wanajaribu kupeluzi Majina ya wachangiaji wastory zitakazo wahusu,Kwanza yeye ametumia Jina lake Feki Africa hatuna majina ya kizungu sie.Kama ni john Basi second name ni mwizi.Hii ni dunia ya uwazi lakini siyo kwa africa,africa ni Bado sana,kuna ubabe,unyanyasaji,ufisadi etc

    ReplyDelete
  6. Michu, mi naona kwenye comment kungekua na namba ingesaidia vizuri. Ila kuweka jina nalo mhu! labda la uongo sawa

    ReplyDelete
  7. Ni kweli - jina lake feki. Kama siyo feki basi aweke na picha yake kama Chibiriti na wengineo ili tumwone!

    ReplyDelete
  8. Huyu Jamaa yeye mwenyewe hajatumia Majina yake ya kweli,Twende hivi bilakujulikana,Kwani comments hazielewiki bwana John Paul Feki? Wabongo Wajanja Sasa sio wale wazamani,Hamna wakumpeleleza hapa kama mlivyowafanyia JambaoForums,Tanzania uhuru wa wavyombo vya habari bado sana,Mnataka watanzania waendelee kukubali tu uozo mnaofanya mkichota Pesa za walalahoi

    ReplyDelete
  9. Bwana John umenichekesha hadi mbavu zinauma, we unanikumbusha ile hadithi ya mbweha aliyetamani kipande cha mkate alichokibana mdomoni kunguru, akaanza kumsifu kunguru kuwa sauti yake ni nzuri angependa kuisikia saa ile, ili akianza kuimba kikidondoka na kuondoka nacho, na alifanikiwa,
    Ndugu humu tunapunguza machungu ya kero zetu na madhila hivyo uhuru wa mtu uheshimiwe mradi havunji sheria.

    ReplyDelete
  10. wenye majina wanatukanwa hadi matusi ya nguoni;mfano-ukitoa picha au maelezo kutaka kujua kitu fulani. nani atakaeandika jina mtu na akili zake atukabnwe na kudhalilishwa na wasio enda shule!

    ReplyDelete
  11. Huyu bwana mshamba nini?Ulietoa comments 7.59pm Feb 26 umenimaliza mbavu.Sikulala kwa kichomi baada ya kucheka mpaka watu wakahisi nimeheuka!Ndugu yangu John Paul Baba Mtakatifu wa Jina ukitaka watu watie majina yao na ya wake zao ANZISHA BLOG YAKO BABA!Simple,muulize Michuzi,akikubania muulize Mjengwa,akikubania waulize Yahoo!Ebo,unataka majina yetu ukayafanyie biashara gani,hebu ishia!Huja anza kutoa hoja unataka majina ya watu,ukija anza kutoa hoja utataka majina ya wake za watu.Kuwa mstaarabu ndugu yangu,Mjini hawaingii namna hiyo.We Kada nini?Hakuna aliyezuiwa kutumbukiza jina lake,au namba yake ya simu,hata mtaa na namba ya nyumba anayoishi kama anataka wageni.Shida iko wapi?

    ReplyDelete
  12. huyo mwehu chaneni naye ukiandika jina uspoandika wewe unachotaka jina ama kuona wamechangia nini juu ya mada,alaaaaaah

    ReplyDelete
  13. Wewe bwana "JOHN PAUL" ...una matitaizo kidogo naona. haya, huo ugeni wako ndio unatuletea ushamba wako humu kwenye blog...AU Umetumwa wewe? Sasa mtanzania mwenzetu hilo jina la "John Paul" ni lako kweli wewe? Usitudanganye wewe Kibaraka wa Mafisadi mkubwa wewe. Ondoa upuuzi wako humu! Anza! Kila mtu ana uhuru wa kuandika na kuongea kwa uhuru, unadhani tuko Uchina hapa? Ebo?

    Haya basi, si unataka jua jina langu, mie naitwa Edward Lowassa...Ha ha ha!

    ReplyDelete
  14. Sikiliza wewe fala,

    majina ya unayatakia nini,

    Kwan hata nikikupa jina langu talifanyaje>??

    Tunaweza tukaweka majina na yakawa feki vilevile kwa ulivyofanya.

    Cha msingi kama serikali mbovu ni mbovu tu, hata mkifanyaje, tutasema tu.

    Kwanza nakushangaa sana, yaani unaona itakua rahiiiiiiiiisi sana eeee??

    kwa taarifa yako kamwambie aliekutuma kua jamaa wameshtuka, JARIBU MBINU INGINE,

    mZXY**KKA&&NCJ WE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...