Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hii kali..lakini mbona hii issue ni simple sana kuisolve..hao wenye biashara wachagua watu waliosomea biashara wawaendeshee biashara zao kama CEO's wao wabaki serikalini wapokee dividends end of the year from they companies.Huku wazungu wanafanya hilo all the time. Tatizo bongo njaa..mtu kabla ya ubunge hana kitu kapata uwaziri kafungua kampuni ambayo anasimamia day to day activities pia kampuni hiyo hiyo inasurvive kwa tenda za serikali..yani inakuwa ngumu ku separate the two...kikwete aaache kulopoka its not as clear cut..hao wakitoka serikalini na biashara zao zinakufa...maoni tuu
ReplyDeletedu kabakia sheni pekee,hata kipanya naye kaanza! haya yetu siye macho
ReplyDeletedu kipaji unacho,hapo naona aliyebaki darasani ni Shein tuu,huyu Shein ninavyomjua hata biashara ya ice cream hajawahi kufanya.Hawa ndio viongozi!!!
ReplyDeleteHuyu mzee Shein in mwadilifu sana kiasi kwamba hafai kufanya kazi katika nyakati hizi ambapo wezi ni wengi serikalini. Juzi juzi nimefanya naye ziara mkoani Kilimanjaro na nikagundua kweli Dr Shein ni mtakatifu wa Mungu. Ratiba yake ya kazi ilikuwa inaanza saa 2 asubuhi na kumalizika saa nne usiku. Hongera mzee lakini serikali kama ya sasa siyo ya kiwango chako. Utawasaidia vipi sijui ili wawe kama wewe na mwenzako JK ambaye naye mali hajaziweka mbele saaaana.
ReplyDeleteHapo JK anasema yaani hadi baba yetu makambaa..naye anapiga ze bizinesi...aaa aaaaaaaa
ReplyDeleteSwala la kukataza watu kujihusisha na biashara katika karne hii haliko "realistic".Hata hao walioweka ma CEO wengine bado wanajihusisha na biashara.Bado sijaelewa JK anataka kuzuia viongozi kufanya biashara kwa muundo gani,ila ukisoma ilani ya uchaguzi aliyoinadi kwenye uchaguzi mkuu hii ni kinyume na ilani ambayo inawahimiza viongozi kuwa mfano katika ujasiliamali.na sijajua kwa nini amelenga wabunge na mawaziri peke yao.kwa nini ameacha makatibu wa wizara na wakurugenzi mbalimbali.Cha msingi ni kuhakikisha uadilifu wa viongozi,what they do in their free time should not matter.kwa hiyo cha kufanya ni kupalilia tabia ya uadilifu kwa sababu kiongozi asiye muadilifu hata ukimkataza kufanya biashara bado ataliletea hasara taifa na kiongozi muadilifu hata akiwa na biashara hawezi kudhurumu umma.Sera ya rais mkapa ya uwazi ingeweza kutumika hapa,tenda zote ziwekwe hadharani na aliyeshinda tenda ielezwe vigezo vilivyomshindisha,watanzania wote wanaosomeshwa na serikali nje na ndani ya nchi ijulikane wazi vigezo vilivyotumiwa kuwapa nafasi hizo.Ukienda wizara ya sayansi utakuta faili la wanafunzi wanaosomeshwa Marekani lakini hata siku moja hakuna tangazo la scholarship za kusoma marekani,kwa nini?hii sio kwa sababu viongozi wanafanya biashara bali ni kwa sababu hakuna uwazi katika utendaji wa serikali,siri ni nyingi mno.mpaka mikataba ya madini nayo ni nyaraka za siri...Haifai.Kikwete fikiria tena mpango wako wa kukataza viongozi kufanya biashara ili usisababishe "mutation" ya uovu utakaokuwa mkali zaidi.Je unajua kuwa hata kilimo cha umwagiliaji ni biashara?kuna biashara nyingine kutokana na magnotude yake huwezi kugharimia CEO mwingine but yourself,that does not make a person a bad leader in free market economy and democracy...zemarcopolo
ReplyDeleteJAmini JK hamumjui???? Hii yote geresha hakuna lolote alikuwa nafurahisha kadamnasi. Ni kitu ambacho hakitekelezeki hata kwa kufikirika tu. Ulaya yapo makampuni Tz hayo yanayoitwa makampuni hayana sifa za kuw akampuni bali kijibiashara ch amtu na familia yake. Kama wammeshindwa kusimamia sheria ya kutangaza mali hii itakuwa danganya toto wala haitekelezeki. Anatafuta mbinu ya kuwaongezea mishahara, marupurupu na maposho hao mawaziri na wabunge kw akisingizio kuwa wamezuia kujiongezea kipato zaid. Vinginevyo kwani huwa wabunge wanakazi gani kama si vikao vya kuchuma na kugawa pipi majimboni ili wachaguliwe tena. Hawa wansiasa hakuna wanachokifanya cha maana hadi biashara iwakwaze kama si kutumia uongozi kuanzisha na kuendesha biashara.
ReplyDeleteAhhh hata wazo lenyewe si muafaka. Wote wafanye biashara na mitaji wapewe kwani hawa wankopesheka ili baade waache kutegemea mishahara na rushwa kuendeshea maisha yao. Naamini mawaziri na wabnge wangekuwa na miradi kama Mengi hata UFISADI ungepungua kwani ungeathiri miradi yao. Mfano wnagehakikisha Tanesco inafanya kazi vyema ili kupata Umeme na sio kupandisha tu bili wakati wao wanalipiwa hizo bili na serikali na ndo maana hawaoni uchungu.
Wote wawe na miradi kuanzia JK hadi mtendaji wa kijiji ili kujikwamua na umaskini kwa kuzalisha na si kutegemea sadaka za lazima wanazotoza wananchi (kodi) kujiendeshea maisha yao na family zao. Kila kiongozi ajiulize amezalisha nini.
Nchi inajengwa kwa kuzalisha na si kwa kakaa na kupiga poroja za siasa na kukusanya posho. Hivi kila waziri angekuwa na likiwanda tungekuwa tuaexport kiasi gani? watumie bongo zao kuwa wajasiriamali na si kubuni naman ya kupata hela zaidi wa kuuza na kukodisah nchi. Hao wanayokodisha kwa wakenya na kwa akina mbeki wangejikodishia wenyewe hata kodi ingeongezeka kwani payto lingebaki TZ.
Viongozi wafanye bishsara lakinikwa njia halali. Wakopeshwe kwani wanakopesheaka vinginevyo huu mduara wa umaskini utaendelea kwani kidg kinachozalishwa na walalahoi na akina mengi ndicho kinachoibiwa hivyo kamwe nchi haiendelei. Mkizalisha sana wao wanajiongezea mishahara sana. waambieni nao wazalishe ili waone uchungu si hiyo miposho na missada ya kodi inawapa kibiri cha kufikiri wanaweza kuendelea kuishi kwa kutegemea jasho la wengine.
Ambaye hazalishi na anapokea mshara unaotokana na mkulima kule kamachumu anayeshindwa hata kupeleka mtoto shule hana jina jingine zaidi ya kuwa ni KUPE MNYONYAJI:
KAZI NI KUZALISHA SI KUPIGA SIASA WAKATI MAISHA YAKO YANAENDESHWA NA MLALAHOI ASIYEJUI KESHO ATAKULA NINI . HIVI HAWAGOPI DHAMBI? MBONA TUNAWAONA NYMBA ZA INBADA WAKITOA MASADAKA NA MICHANGO KUMBE HELA SI ZAO vile tu wamejipatia uwezo wa kujichukulia kwa kisingizio cha jina MISHAHARA NA POSHO.
WAZALISHE WOTE NA TUJUE BIASHARA ZAO TUJUE WAMEACHA KUTUNYONYA.
Yeye JK kutaka kupiga marufuku wanasiasa kuwa na biashara je lile shamba lake la mananasi ataikabizi kwa wananchi. Hawezi kusema kuwa hayo mananasi yote ni matumizi ya familia yake. Kama sikosei tender zote za mahoteli na export anazishikilia yeye. Hivyo ni gumzo tu hakuna lolote litakalotendeka.
ReplyDeleteWaende wote tutachagua wapya, lazima mchele upepetwe kutoa pumba. Kwani Tanzania nzima hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza ni wao tu miaka nenda miaka rudi? Katika watu million 34 watu sijui 50 ndio watutie joto?
ReplyDeleteTena wala hata wasisubiri huo muswada upitishwe na Bunge, waondoke na mapema maana walikuwa wakijali maslahi yao na biashara zao. Ngoja tuisikie hiyo sheria huko Bungeni itakavyojadiliwa, ntamsikiliza Mbunge wangu kwa hamu kama atasema kitu, akipinga tu namrekodi na kumsubiri wakati wa kampeni za uchaguzi.
Tatizo kubwa wanalokabili wa-Tanzania ni ukosefu wa akili.Wa-Tanzania wanachuma matunda ya upumbavu wao wenyewe.
ReplyDeleteMy logic is simple, u cannot have an an incompetent elected President without stupid voters.
The President is acknowledging a problem but his proposed solution is tantamount with treating a malaria patient with viagra!!!
The real problem is not when politicians also do business, the problem occurs when they use their political position to unfairly solicit business and to lobby for their interests in Parliament ahead of national interests. Sasa kwani ukiwa na wafanyabiashara matajiri amabao sio wanasiasa unadhani watashindwa kuwarubuni viongozi wa Serikali katika kuleta ufisadi. Kwani Jeetu patel amd Sailesh Vithlani ni wanasiasa?
Solution ya kuzuia wafanyabishara kuhujumu taifa kiuchumi kwa kutumia nadafi zao za siasa ni kuwa na rule of law, transparent governance and a system of checks and balances.
Leo hii tunaambiwa kampuni ya TICTS ya akina Karamagi ime-renew mkataba na Serikali kwa miaka 25, the whole proposal submission process and bidding process is fucked up, uwanja wa ushindani kuhakikisha Serikali awards contracts to contractors with best proposals hakuna, watu wanageiana kinyemela mikataba minono na kutupa sis vi tenda mshenzi vya suppy sijui kalamu na vichongeo.
Leo hii tenda zinatolewa lakini hakuna sheria ya Open Records inayompa Raia haki ya kujua ni kampuni gani zili bid, vigezo vilikuwa ni vipi,kila kampuni imepata pointi ngapi kwa kila kigezo na hadi kufikia mshindi, watu wachache wanakula mamilioni ya dola ya wa-Tanzania na nyinyi munakubali, sasa mimi niwasaidie vipi kama hamna uchungu na nchi yenu?!!