
Leo bila ya shaka tutaanza kujua ilikuwaje Taifa lenye viongozi wenye akili timamu na watu wasomi liliweza kuingia mkataba wa Richmond katika mazingira ya ajabu kama yale. Taarifa ambazo zimefika kuanzia jioni ya jana ni kuwa hatimaye ripoti hiyo ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wabunge na watanzania wengine itasambazwa kwa Wabunge wote.
Baadaye jioni wabunge wa CCM watakutana na kukaa pamoja kuchukua msimamo wa pamoja. Hadi hivi sasa dalili zinaonesha kuwa kuna uwezekano wa angalau waziri mmoja kujiuzulu kabla ya mjadala huu kuanza. Kama hili litafanyika litakumbushia kujiuzulu kwa Waziri wa Viwanda Idi Simba na Waziri Ngasongwa kufuatia kashfa ya Kodi za Sukari miaka kadhaa iliyopita.
Jina ambalo linatajwa na baadhi ya wachunguzi wa mambo ni la Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Dr. Ibrahim Msabaha ambaye wakati mkataba huu unaingiwa alikuwa ndiye Waziri wa Nishati na Madini. Wakati huo huo utaona kuwa Waziri wa sasa wa Wizara hiyo naye anachunguzwa kuhusu mkataba wa Buzwagi na inawezekana na yeye akaamua kuachia ngazi.
Hata hivyo kuna uwezekano mwingine kuwa hakuna Waziri atakayejiuzulu zaidi ya kupigiwa kelele na wabunge wengine na watajitetea kuwa walifanya yote kwa "nia nzuri" na hasa wakati huu ambapo tunasubiri ujio wa Rais Bush Tanzania, sidhani kama Rais Kikwete atataka kugubikwa na suala la mabadiliko ya mawaziri au hata waziri mkuu. Ila hilo la angalau waziri mmoja kujiuzulu linawezekana zaidi.
Vyovyote itakavyokuwa kama nilivyosema mwishoni mwa mwaka jana ni lazima tujifunze kuzungumza na kukamilisha mambo ili tuendelee na mambo mengine. Suala la Richmond lisingestahili kuchukua muda huu wote kama lingeshughulikiwa mapema. Hivyo ni matumaini yangu kuwa baada ya yote yanayopaswa kufanyika tutalimaliza suala la Richmond kwa hatua kuchukuliwa na makosa kusahihishwa na tuangalie mambo mengine.
Unaweza kusikiliza matangazo yangu ya leo kwenye
Title: KLH News Episode: Mchawi wa Richmond kufunuliwa leo?
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2008-02-05T21_55_51-08_00
Enjoy!
mambo ya wajanja wa H-Taun hayo
ReplyDeleteInabidi watu waelewe kuwa huwezi kufanya dili na watu wa houston. Wahuni wengi sana hapa (Houston). Wengi wao wanarudishwa nyumbani au wanakimbia au wanaozea lupango. Sasa jamani mtu hata awekichaa angeweza kujua kuwa hii kampuni ni wasanii tu
ReplyDeleteIsambazwe basi hiyo ripoti kwenye internet wadanganyika tulioibiwa kodi zetu tujue.
ReplyDeleteRICHMOND PRINTING,
ReplyDeleteMamaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!,
Isije ikawa ni kampuni ya Kuchapisha magazeti ikajidai inajua mambo ya umeme??
hapo hata sijaelewa
Hii blog safi sana sana. Hatuondoki humu bwana uchuzi
ReplyDeleteSerikali inabidi ichukuwe sheria ambayo wananchi wataridhika, kwa kufumbia macho suala hili kunafanya raia kuwa na chiki na viongozi . Kama nchi jirani ya Kenya walifichaficha sana mambo yanawaudhi raia wao sasa mwenge umewaka pale kuuzima kimbembe!
ReplyDeleteMaana yangu ni viongozi wetu rudisheni imani kwa wananchi,wabongo wakipagawa itakuwa sooo!
sisi tunaokaa marekani tunajua kabisa houston Tx ni ya mazabe kila kitu ni utapeli mpaka watanzania wanakaa uko utapeli kila kona tuko nao very careful hata wakikupa deal inabidi ulichunguze kwanza saa at least wangetuuliza sisi kuhusu houston TX before hawajasaini hizo paperz na Richmond...ukute hiyo Richmond walioleta uko ni mazabe tu ni kampuni ya wabeba box wala sio nishati..anyway its a pay back time..lazima wajiuzulu next time the we learn thru the hard way...
ReplyDeleteUkicheki archives za Blogu ya Michuzi, utakuta wadau waliwaumbua kampuni ya Richmond zamani! Mpaka walitoa na listi ya jinsi kampuni invyodhulumu nchi. Tena hiyo ni kabla dili na Richmond haijakamilika. Hii skandali ni aibu kwa nchi yetu bora tunaona hatua zinachukuliwa sana.
ReplyDelete