baada ya kuidigest hoja ya rais Kikwete juu ya kuzuia wabunge na mawaziri kujihusisha na biashara hili ndio tamko langu... Samahani kwa mchanganyiko wa lugha.
Swala la kukataza watu kujihusisha na biashara katika karne hii haliko "realistic". Hata hao walioajiri ma-CEO kwenye makampuni yao bado wanajihusisha na biashara.
Bado JK hajaweka bayana anataka kuzuia viongozi kufanya biashara kwa muundo gani,ila ukisoma ilani ya uchaguzi aliyoinadi kwenye uchaguzi mkuu hii ni kinyume na ilani ambayo inawahimiza viongozi kuwa mfano katika ujasiliamali.
Na hakuweka bayana kwa nini amelenga wabunge na mawaziri peke yao.Kwa nini ameacha makatibu wa wizara na wakurugenzi mbalimbali.Cha msingi ni kuhakikisha uadilifu wa viongozi,what they do in their free time should not matter.
Kwa hiyo cha kufanya ni kupalilia tabia ya uadilifu kwa sababu kiongozi asiye muadilifu hata ukimkataza kufanya biashara bado ataliletea hasara taifa na kiongozi muadilifu hata akiwa na biashara hawezi kudhurumu umma.
Sera ya rais Mkapa ya uwazi ingeweza kutumika hapa,tenda zote ziwekwe hadharani na aliyeshinda tenda ielezwe vigezo vilivyomshindisha,watanzania wote wanaosomeshwa na serikali nje na ndani ya nchi ijulikane wazi vigezo vilivyotumiwa kuwapa nafasi hizo.
Ukienda wizara ya sayansi utakuta faili la wanafunzi wanaosomeshwa Marekani lakini hata siku moja hakuna tangazo la scholarship za kusoma marekani,kwa nini? hii sio kwa sababu viongozi wanafanya biashara bali ni kwa sababu hakuna uwazi katika utendaji wa serikali,siri ni nyingi mno.mpaka mikataba ya madini nayo ni nyaraka za siri...Haifai.
Kikwete fikiria tena mpango wako wa kukataza viongozi kufanya biashara ili usisababishe "mutation" ya uovu utakaokuwa mkali zaidi.
Je unajua kuwa hata kilimo cha umwagiliaji ni biashara? kuna biashara nyingine kutokana na magnitude yake huwezi kugharimia CEO mwingine but yourself. That does not make a person a bad leader in free market economy and democracy.
Naomba kuwakilisha hoja.
Mdau ZP
Hiyo sheria ya conflict of interest iko mahala kwingi tu na siyo kwetu peke yake. Haiwezekani wewe uwe waziri halafu ufanye biashara ambayo inaleta mgongano katika kazi yako. Watu wanalalamika kuhusu Waziri ambaye alikuwa mfanyabiashara na akawa wizara ya madini na akafanya biashara/kwa kununua hisa katika mradi wa kuzalisha umeme na sasa wana mkataba wa kuizuia tanesco umeme. Je ni nani ambaye angeweza kumkatalia waziri huyo kusaini huo mkataba wakati tanesco iko chini ya wizara ya madini na nishati? Halikadhalika kwenya sekta ya mafuta na madini na sekta nyinginezo, je ukiwa unafanya biashara utaweka maslahi ya nchi mbele au utaweka maslahi yako binafsi kulinda biashara zako? Haiwezakani kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja hakuna suala la uwazi wala nini hoja ni ubinadamu hata ingekuwa wewe ungeangalia maslahi yako na familia yako ni nature ya wanyama wote walivyo ila binadamu wamezidi.
ReplyDeleteKama mnataka hao wabunge na mawaziri wafanye biashara, nisisikie mtu anamuita mtu mwingine fisadi kwa sababu itakuwa ni uonevu. Umefika wakati sasa tuwe wazi na wakweli ukiamua kuwa Kiongozi wa ngazi za juu basi uwe Kiongozi na iwe marufuku mtu kufanya biashara akiwa Ikulu au akiwa Waziri Mkuu au waziri yoyote yule. Kama mtu anataka kuwa mjasiriamali na aende akawe mjasiriamali ajenge nchi kwa njia hiyo. Hii nayo itaweka limit ya vipindi vya ubunge na uwaziri na si lazima uwe mbunge miaka 20 au uwaziri kila awamu ya rais. Ukiona umekuwa waziri vipindi viwili mfululuzo na unataka kufanya biashara achia ngazi wapishe wengine wafanye kazi.
Nakubaliana kabisa na Mheshimiwa rais na anony wa 4.23.00 pm EAT, lazima viongozi wachangue moja, vinginevyo tuwaruhusu hata majaji wawe na makampuni ya uwakili na maofisa wa polisi wawe na makampuni ya ulinzi hapo nadhani kila mwananchi ataelewa kuwa ni lazima uchague jambo moja. Tusipowaruhusu hawa na tukaruhusu mawaziri na wabunge kufanya biashara tutakuwa tunawaonea. Kama unataka biashara unaweza kuwa mbunge kwa term moja au mbili halafu uingie ktk biashara. Hili jambo liko wazo na viongozi wanalielewa vizuri ila kwa kuwa hawajali maslahi ya nchi wamelifumbia macho!!!
ReplyDeleteJe wachangiaji mliotangulia mnajaribu kusema kuwa wafanyakazi wote wa serikali wahusishwe katika mswada huu? Swala la conflict of interest si lazima liwahusu wafanyabiashara tu, naomba muitafute na kuiangalia filamu inayoitwa Sicko ili kupata mtazamo mpana juu ya hili.Jaji unaweza kumkataza kufungua kampuni ya uwakili, lakini kwa nini umkataze kufungua duka la biskuti? Naomba kupinga hoja ya aliyesema kuwa swala la kutojali maslahi ya taifa ni swala la kibinadamu, hapana hapana na hapana. Hilo ni swala la watu wabinafsi wasio wazalendo.
ReplyDeleteTanzania ni nchi ya kidemokrasia ambayo maamuuzi kwa kawaida huwa hayafanywi na mtu mmoja. Kama kuna kiongozi anayeweza kuwezesha biashara yake kunufaika kwa dhuruma basi ijulikane kuwa kiongozi huyo amefanikiwa kuwa-lobby viongozi wengine wanaoshiriki katika kufanya maamuzi. Somo hapa ni kwamba lobbying ni kitu anachoweza kufanya mtu yeyote hata kama sio kiongozi. Rais kikwete anapaswa kuja na utatuzi utakaozuia lobbying in general not only by gov. officials. Na kuwakataza viongozi kufanya biashara sio utatuzi, utatuzi ni kuweka checks and controls ili kuhakikisha kuwa viongozi hawa mis use madaraka yao. Je Kikwete atawakataza viongozi kuwa na ndugu kwa sababu watawapendelea ndugu zao? au atawakataza kuwa na marafiki kwa kuogopa "conflict of interest"? Kiasi cha wawekezaji Tanzania ni kidogo, na kukataza kundi kubwa la watanzania kuwekeza ni kukumbatia umasikini na kufungua mianya kwa uchumi wa Tanzania kuendeshwa na wawekezaji toka nje.
ReplyDeleteMara nyingi nimethibitisha usemi kwamba tanzania ina wasomi wengi sana lakin hawajaelimika!!! kuna kusoma na kuelimika, kuelimika ni pale tu msomi anapoweza kutafsiri elimu yake kwa vitendo huku akizingatia uhalisi wa mazingira yake kujiletea maendeleo!
ReplyDeleteNchi yetu ni tajiri lakin watu wake ni maskini!sio tu tunahitaji watu hodari na wabunifu ktk kujiletea maendeleo hususan viongozi, lkn zaidi sana mazingira bora kabisa yatakayotuwezesha kuendelea.
utawala, bunge na mahakama kila moja ina kazi na majukumu yake ktk uongozi wa nchi, kwa historia na mazingira ya nchi hii, hatuwezi kuendelea kama tutakuwa na wafanyabiashara wanaoongozwa kwa motive ya kupata faida lkn hao hao ni wabunge wanaotunga sheria zinazoratibu biashara zao, au watawala wanaosimamia kanuni na taratibu hata za biashara zao, au majaji wanaosimamia haki hata pale biashara zao zinapokuwa dhalimu!!! kwa hali namna hii usitarajie watu wa nchi hii kuendelea.Ndio maana mwl. nyerere alikuja na wazo la miiko ya uongozi ambayo ilizingatia sana hali yetu kama watanzania!!!!
Ni vzr kuchagua tu,biashara au utumishi wa umma!! kimoja kati ya hivi, si rahisi kufanya vyote na bado ukawa mwema na mwadilifu, ni rahisi sana kuishia kuwa dhalimu na fisadi!!kwa njia moja au nyingine au moja kwa moja!!
Kwa hali ya nchi yetu ilivyo,tukubaliane kutenganisha vitu hivi viwili tofauti, biashara na utumishi wa umma.rais kikwete yuko sawa, hata kama ilani ya chama chake inasema viongozi wawe wajasiriamali, kwani ni mangapi yameandikwa kwenye ilan lkn hayatekelezwi vilivyo!!ilan si msahafu!! siyo something final!!
Watanzania tuamke tupiganie kuwa na maadili yetu kwa mustakabali wetu, kipindi cha majaribio kilikwishapita siku nyingi!! tusifanye majaribio tene, tujifunze kuwa makini, tuthamin taifa letu na kizazi chetu leo,kesho hata karne ijayo!!!
Naungana na ninyi wenzangu mliotangulia kutoa mawazo yenu .Tatizo la watanzania tulio wengi ni wanafiki,maamuzi haya aliyoyatoa Raisi wa nchi si mageni duniani labda hapa kwetu Tanzania hatukuwa na utamaduni huo ,.na ndio maana viongozi waliotangulia walifanya biashara nyingi sana wakiwa madarakani hata ikulu,sisi wananchi tumekuwa tukilalamika chinichini na kilio chetu sasa kimesikika cha ajabu tunaanza kumuona aliyetoa amri hiyo hafai anaonea wananchi,biashara ya mazao huwezi kufananisha na biashara ya umeme au madini hivi mtu kama Rostam Azizi anayemiliki makampuni ya madini,magari na mitambo mikubwa huko ktk machimbo mbalimbali ukimpa wizara hiyo ya madini au hata kwa wadhifa wa ubunge wake alionao ni tenda gani atakosa kutokana nacheo chake? Kwa kweli zipo biashara za kuhujumu taifa na zipo biashara za kulijenga taifa kwangu mimi mkulima sina wasiwasi nae na alichokisema Raisi ni kwamba namnukuu viongozi wasijishughulishe na biashara zao wakati wapo madarakani badala yake wanaweza kuwa asign wengine kufanya kazi hizo bila wao kukingia kifua kwa kutumia nyadhifa zao,mfano tenda ziwe wazi na anyefanya tenda asiwe yeye kama ilivyo sasa.nia si kumfanya kiongozi huyo labda kuwa masikini atokapo ktk madaraka anachotaka yeye kiongozi anapotoka madarakani basi awe na shughuli ya kufanya na siyo kutumia muda wa kazi kufanya shughuli za kibiashara binafsi.Kwangu mimi hii ni sawa kabisa kwani viongozi wetu wa sasa waliowengi hawafanyi kazi za nchi kama walivyotueleza ktk kutaka kura wengi hufanya shughuli zao na kuwakoshesha haki zao wananchi wanapotaka kusaidiwa matatizo yao.Hivi mtu kama Karamagi atafanya kazi za serikali saa ngapina huko bandarini kunamngoja?bado hajatosheka ,muhimu kiongozi anapokuwa madarakani kwanza awe ametosheka ndio agombee na hili ndilo tatizo tulilonalo ktk nchi za kiafrika,hivi leo uumpe nchi MREMA na alivyochoka vile iatakuwaje?naona biashara ndio zitakuwa nje nje.Mimi nasema ni vyema wanwnchi tungemuunga mkono Raisi wetu kwa ushujaa anaouonyesha kweli ameamua kutusaidia wanyonge na sisi tupate vijitenda wapo watakao pinga lakini ndio hao hao mafisadi ,jambo jingine naomba mungu wote watakaobainika kutuletea maisha magumu wakamatwe na watiwe ndani na kufilisiwa naomba kuwakilisha.
ReplyDeleteWote hapa nadhani tuna nia njema na taifa letu. Lakini kifupi ni kwamba katika nchi maskini kama ya kwetu ambapo sheria zinawabana wanyonge tuu naamini kabisa viongozi wetu lazima wawe mfano. Ni ukweli usiopingika viongozi wa juu wanapata tenda na hizi biashara kwa kutumia majina yao na wala si kwa sababu ya uadilifu au ujasiliamali wao.
ReplyDeleteIweje mtu anakuwa kapuku miaka yote na anapoteuliwa kuwa waziri anakuwa na majumba, makampuni, hisa, among many others? kwa kipato kipi? tunahitaji sheria makini kusudi ikifika siku ya siku tuweze kuwaweka kwenye mstari hwa wenzetu. Maana naamini TZ inapoelekea inakuwa na watu wanaoona mbali. Kwani haya ya Mkapa, Lowassa, Sumaye, Yona tumeyajuaje? Let us have the rules and we shall play by them when these folks leave the offices. Kifupi uongo na uzandiki utapungua kwa hawa jamaa.
Kifupi, ni vyema tuweke sheria yaa kuwabana hawa watu maana ukitumia common sense tuu, huwezi kufanikiwa maana tuna mifano mingi ambapo sheria imapply selectively kwa wanyonge na kuwaacha viongozi akina Dito wakipeta.
So I fully support this law and should be applicable to all higher governement officers. hata kama wakitumia majina ya watoto wao na wake zao..Iam sure at the end of the day we SHALL KNOW!
By the way kuwa tajiri siyo kosa wala dhambi, dhambi ni kuwa na utajiri kwa kuwadhulumu maskini! Ambao ndo asilimia 80% ya watanzania. Kwa hiyo watu lazima tuwe makini, hatupingi utajiri wa watu hapa, work hard like any other citizen, pay due taxes and no body will bother you. But hii ya Mkapa na wenzake kutumia ofisi zao. Its highly unfair and should be condemned by any Tanzanian mwenye uchu na nchi yake.
anon 5;46:00 pm eat hapa si swala la biashara kichaa kinachozungumzwa hapa ni biashara kubwa mfanowaziri wa viwanda na biashara kuwa na kiwanda chake au viwanda vyake inakuja kesi ya mgomo kiwandani wafanyakazi wanadai nyongeza ya mishahara na wewe unahitaji kuonana na waziri huyo kwa maswala ya kitaifa kwa hali ilivyojitokeza kwa akili yako atashuhulika na jambo gani? atakushuhulikia wewe au atashuhulikia shuhuli yake?ili kiwanda chake kisisimame? sidhani kama utamuona hata uso wake haraka sana sekretari ataambiwa mwambie nina kikao kifupi ndio maana halisi ya CONFLICT OF INTEREST ndugu yangu usifananishe issue hii na biashara ya kiduka cha biskuti ni tofauti kabisa huo si mfano hai,unapinga na na mtoa hoja ya kwamba swala la kutojali maslhi ya taifa nilakibinadamu ukasema ni la kibinafsi ,kumbuka mbinafsi ni huyo huyo binadamu na si mwingine,naomba uelewe ya kwamba kama binadamu lazima tuwe na tofauti kubwa tu,tpo tunaoonatamko hili ni zuri na wapo wanaoona halifai sasa hao ndio wabinafsi ,kwa sababu wafanyayo haya si wengi ni wachache kwa maana ya viongozi na familia zao na waliopo karibu nao,ipo mifano hai wakati wa Mkapa wapo waliofanya biashara za mafuta kwa kupitia jina lake na hata siku moja hakuna aliyewanyima vibali vya kuingiza mafuta nchini na ukiwaangalia ni ndugu au jamaa wa karibu na mambo mengine mengi tu, tumeonewa kiasi cha kutosha na sasa ndio umefikia kikomo wanaanza kuhaha viongozi na mafisadi
ReplyDeleteMh mambo ya bongo wakati mwingine ni magumu kuyaelewa. mmesahau kuwa bongo mfanyakazi wa serikali akitoka nje ya mkoa ni lazima aombe ruhusa kwa kuajiri wake, hata kama ni weekend na anauhakika wa kuwa kazina bila ya kuchelewa!!!
ReplyDeletebiashara ya wabunge ni vihiace, nyumba za kupanga na uchuuzi mwingine mdogomdogo na sioni sababu ya kuukataza bila kuongeza kipato cha wabunge ili waweze kuikabili hali halisi ya extended families.
Hakika hadithi hizi za siasa hulandana hebu soma nukuu hii…… (kolazarzar@yahoo.com)
ReplyDeletePerestroika Defined (1987)
Perestroika means overcoming the stagnation process, breaking down the braking mechanism, creating a dependable and effective mechanism for acceleration of social and economic progress and giving it greater dynamism.
Perestroika means mass initiative. It is the conference of development of democracy, socialist self-government, encouragement of initiative and creative endeavor, improved water and disciplined, more glasnost, criticism and self-criticism in all spheres of our society. It is utmost respect for the individual and consideration for personal dignity.
Perestroika is the all-round intensification of the Soviet economy, the revival and development of the principles of democratic centralism in running the national economy, the universal introduction of economic methods, the renunciation of management by injunction and by administrative methods, and the overall encouragement of innovation and socialist enterprise.
Perestroika means a resolute shift to scientific methods, an ability to provide a solid scientific basis for every new initiative. It means the combination of the achievements of the scientific and technological revolution with a planned economy
Perestroika means priority development of the social sphere aimed at ever better satisfaction of the Soviet people's requirements for good living and working conditions, for good rest and recreation, education and health care. It means unceasing concern for cultural and spiritual wealth, for the culture of every individual and society as a whole.
Perestroika means the elimination from society of the distortions of socialist ethics, the consistent implementation of the principles of social justice. It means the unity of words and deeds, rights and duties. It is the elevation of honest, highly-qualified labor, the overcoming of leveling tendencies in pay and consumerism. . . .
I stress once again: perestroika is not some kind of illumination or revelation. To restructure our life means to understand the objective necessity for renovation and acceleration. And that necessity emerged in the heart of our society. The essence of perestroika lies in the fact that it unites socialism with democracy and revives the Leninist concept of socialist construction both in theory and in practice. Such is the essence of perestroika, which accounts for its genuine revolutionary spirit and it's all-embracing scope.
The goal is worth the effort. And we are sure that are effort will be a worthy contribution to humanity's social progress.
[Source: Mikhail Gorbachev, Perestroika (New York: Harper Collins, 1987), quoted in Mark Kishlansky, ed., Sources of the West: Readings in Western Civilization, 4th ed., vol. 2 (New York: Longman, 2001), p. 322.]
Huyo Kikwete ameongea pumba tu kama kawaida. Hakuna sehemu ya katiba ambayo inamkataza kiongozi kufanya biashara. Suala ni mgongano wa kimaslahi. Kama anaweza akahakikisha uwazi na ukweli na utawala wa sheria katika serikali yake, haya yote ya mgongano wa kimaslahi yanaweza kuwa kupungua kwa asilimia kubwa sana.
ReplyDeleteTatizo ni rais mwenyewe kukaa anatoatoa hotuba. Wakati wa uongozi wa kutoa hotuba umeisha muheshimiwa Kikwete. Chapa kazi na watu waone matunda ya kazi zako, siyo ukae unaongea ongea tu. Debe tupu haliachi kupiga kelele mkuu.
Kwa mtizamo wangu naona tunajichanganya tena hii inaweza kuharibu kila kitu, haya mambo maadili yote yalikuwepo zamani ila tuliyabadilisha kwa ufisadi wetu Azimio la Arusha lilikuwapo na likasaidia sana kupunguza ufisadi sasa watu wanaojua wakabadilisha sasa mnashangaa nini ?
ReplyDeleteMuchuzi kama utakumbuka zamani kulikuwa na ile tume ya Mzee wetu Sulein Kitundu hivi alikufa nayo ile tume? Tume ya maaidili ya viongozi.
Kwa sasa hivi ningemshauri JK ni bora kutumia Chinese style ukiharibu tunakuchenchia kinomanoma
kuna viongozi wengi sana wameamriwa kulipa mshahara back
sasa mtu kama yule wa PCB alikuwa pale kwa miaka 20 na hajakamata mtu si bora aturudishie mshahara wetu
Dawa ni kuondoa ushkaji na upambe nchi itakwenda
Mleta hoja ana hoja ya msingi.
ReplyDeleteMambo haya yalikuwepo wakati wa lile azimiola Arusha lililozimwa na azimio ibuka la Zanzibar.
Binafsi nakumbuka baba akiwa mwanasiasa alikuwa anawapa watu ruksa ya kukaa bure nyumbani kwetu maana alifuata sana lile tamko na andiko madhubuti kwamba kiongozi wa siasa asiwe na hisa katika kampuni wala asiwe na nyumba ya kupangisha n.k.
Sasa leo hayo yamefutwa na tunajua kuna viongozi kibao tena wa ngazi za juu wana hisa nyingi katika CRDB na kwingineko na sera ya CCM ni watu kuwa Wajasiriamali bila kuwaondoa viongozi.
Nadhani hili suala haliwezi kutamkwa kiurahisi rahisi hivi na rais bila kuwa na backing yake ya kisheria na kisera.
Na si rahisi mtu kukurupuka tu na kusema kuwa hapo kuna mgongano wa kimasilahi kama ilivyo kwa majaji kuanzisha biashara za uwakili, sasa mbona walimu kibao wanafundisha privately kupitia kiitwacho 'tuisheni' nakadhalika, mbona madaktari kibao wana maduka ya dawa na zahanati zao na hospitali huku wameajiliwa serikalini. Mbona... Mbona...Mbona....!
Orodha ni ndefu hivyo ni kweli kabla rais hajatamka suala hili alipaswa yeye na wizara husika ya maadili wakae chini walitazame suala hili kwa undani na kwa upya na kupendekeza sera na baadaye kuunda mswada wa sheria UKIELEZA WAZIWAZI NANI WANAOHUSIKA NA PIA UDIFAINI WAZIWAZI NI SHUGHULI GANI HIZO AMBAZO HAWATAKIWI KUHUSIKA NAZO NaA SABABU ZINAZOUZIKA NKWA UMMA ZITOLEWE.
Ukitamka tu kijumla jumla Biashara na Wanansiasa, haya ni maneno mapana sana, hivyo sheria itoe ufafanuzi unaopaswa ili kuondoa utata.
Maana hata CCM yenyewe ina vitega uchumi na wanafanya biashara je viongozi wake wawajibishwe kwa kuwa siasa na biashara avikai chungu kimoja?
Nakubalia na raisi 100% labda uchague moja...kuongoza au kuwa mfanya biashara...wabunge wengi tu wa vijijin lakini anuani zao ni za DAR....wengi wanaishi dar lakini wanawakilisha vijijini...eti ni wabunge
ReplyDeletenchi zilizoendelea zinaweza kuwa na kiongozi na pia mfanya biashara kwa vile wao kila kitu kina recordiwa na ukizidi kuwa mfanya biashara watu hawakupi kura....hapa kwetu wabunge wanazidi kutajirika kupitia jina au uongoze....
Ni kweli ukitaka kuw ambunge then be so otherwise waachie wengine wataongoza...
Naomba kuwakilisha....
watu wote mliochangia mada hii hajui kuchambua mambo na mnasoma haraka haraka na kuruka mistari,hamsomi "fine print" bila shaka wengi wenu mtakuwa mmekumbwa na mortgage meltdown tayari.
ReplyDeleteMtoa mada amesema , sawa sheria inaweza kupitishwa, lakini utawabana vipi viongozi hawa kutowapa marafiki, wajomba na shangazi biashara hizi? baora sasa hivi inajulikana wazi biashara ya nani, na tutawabana vipi. lakini " MUTATION" ikitokea [ mfumo mwingine kabisa ] ambapo biashara itakuwa kwa mjomba, hapo tutalia na kusaga meno, kwa sababu legally bishara haipo kwa kiongozi, iko kwa mjomba, kiongozi hatuna means za kumbana,atasema kampuni siyo yangu, at the same time anaipa kampuni tenda za mabilioni. FIKIRI.
Hii inanikumbusha kwenye kitabu cha Murder in the name of God
ReplyDeletewatu wanaiba kwa kutumia jina la Nyerere wanafanya mambo kujinufaisha wenyewe wanajidai wanaendeleza nchi sijui nchi gani au mifuko yao
Ukiangalia kwenye miiko ya azimio la arush kila kitu kipo pale sasa kubadilisha kwao huku ili kujinufaisha
Je ni kwanini tumkataze Zitto kabwe kufanya biashara ya mitumba, au Mungai kulima chai, au Msabaha kuwa na kihiace au Mama Anna Makinda kufungua shule?
ReplyDeleteWell, huyo anayesema kiongozi anaweza kumpa rafiki yake biashara ni kwa vile TZ hatujui kucontol hela zinavyoingia na kutok.
ReplyDeleteUSA ukipewa hela kuna Tax gift, sasa kama mtu anampa ndugu yake na jina linabadilika kwenye biashara basi tax gift ilipwe. Na kama mbunge huyo au kiongozi wangekua wanaonyesha mapato yao kwa mwaka hata kama ni penny interest kwa mwaka lazima ilipiwe tax...
Wakiweza kufanya hivyo kila kitu kitakua shwari lakini bila kucontorl mapato ya wananchi kakuna ujanja hapa
Cha muhimu ni kuwa na TAX income au idara muhimu ya kujua mapato ya watu nchini....
Ila kabla mtu hajaanza uongozi mimi kweli ningeona waonyeshe hela zao sote na kila mwaka wawe wanakua audited
hapo i dont think mr president is doing justice to the cabinet members or MP, as far as tanzanian politics are being a mister doesnt guarentee you an employement its not long term employment so i dont think people should throw their investiments for tempolarly bases, what we need is nothing less than transparency, all tender should be decided according to the business law,
ReplyDeletegod bless tanzania n no where else