kama si ule usemi wa mgeni njoo mwenyeji apone, basi ujio wa joji kichaka hapa bongo unaweza kuuita bahati ya mtende. kwa nini? yaani ghafla tu kila barabara kumesimikwa mistimu mipya na taa za barabarani kuwashwa. na huu ni mmoja waomilango ya sea view. sijui akiondoka itaendela kuwepo ama vipi..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ni culture yetu hatujipendi...

    tunatakiwa tujipende kwanza ndio tutaweza kupenda jirani vizuri....

    Nakumbuka nikiwa mdogo home tulikua tunatumia sahani tu za kawaida lakini kabati limejaa masahani mazuri mazuri tuu lakini hamna kugusa ni vya wageni wakija....wageni wenyewe wa heshima mara moja kwa mwaka...why.....???

    Naona culture yetu ndio inatufanya tusijipende...na hii nchi inaongonzwa na wananchi wenye the same culture kwa hiyo mlooongo utaendelea hivyo hiyo..taa zingetakiwa ziwe kila siku kwa usalama wetu sio kumwonyesha mgeni tunacho that is it crap...kama huna mwache aje akuone uanvyoishi sio kujititipua halafu kesho akiondoka basi tena....

    ReplyDelete
  2. Michu kwa kweli na wewe sasa umezidi, manake huu ni umbea wako ili tu hao unaowaita wadau wako waweze kusuuza vinywa vyao kukumbushia akili zao kuwa wanafahamu kiswahili, Hizi nguzo zinasimikwa kwa kampeni iliyoanza hata kabla ya ufahamu wa ujio wa huyo umsemae...Kuna kampuni moja ya mmbongo ilianza kwa kuwasha Dom, na Dar kuna baadhi ya mitaa inawaka siku nyiiiiingi, sijui wewe hutembelei au ni nanihii zako tu..... Mwanza nao wako mbioni..NA KAMA KAWAIDA YAKO BANIA NA HII USIIPELEKE HEWANI

    ReplyDelete
  3. HUYO MGENI ALISHAOMBWA PESA KWA UWEKAJI TAA MIAKA MINGI NA ALIAMBIWA ZIMESHAWEKWA NA PICHA ALIPELEKEWA PAMOJA NA DATA SASA AMESEMA ANAKUJA KUANGALIA JINSI ZILIVYOTUMIKA KAMA SAHIHI AONGEZE NYINGINE, HIVYO HIZI NI ZILE ZA CHAPCHAP AKIONDOKA NAZO ZITAONDOKA ALKINI TUTAAMBIWA ZIMECHUKULIWA NA VYUMA CHAKAVU. DAR ES SALAAM BONGOOoooooo

    ReplyDelete
  4. ALA, KUMBE TUNAWEZA!!!!

    ReplyDelete
  5. MICHUZI, WEWE UKO INFORMED BWANA, NA WEWE UNAKUWA KAMA WAOSHA VINYWA? HII NI PROJECT YA MUDA MREFU SANA YA KAMPUNI NGULI YA MATANGAZO YA A1 OUTDOOR. A1 OUTDOOR WANAWEKA TAA HIZI KUANZIA INFRASTRUCTURE MPAKA KULIPIA UMEME THEN WAO WATATAFUTA WATEJA NA KUWEKA MATANGAZO YAO, WANAWEKA MIJI SALAMA KWA KUWASHA TAA ZA BARABARANI AMBAZO MAMLAKA HUSIKA ZIMESHINDWA, WANARUDISHA KWA WANANCHI KIDOGO NA OF COURSE KUPATA MRADI WAO, IT IS A VERY EXPENSIVE PROJECT, UKITAKA KUJUA HAIHUSIANI NA JOJI KICHAKA, ANGALIA DODOMA, ROSE GARGEN ROAD, TOURE DRIVE, NA MITAA MINGINE ITAKAYOKUWA INAKUJA, TAA ZATAWAKA WADAU!!!

    ReplyDelete
  6. Ha ha haaaa... Umeniacha hoi Bw.Michuzi yaani hizo ni taa au ni nguzo??? Ha ha haaa

    ReplyDelete
  7. This abuse of common sense beggars belief really,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...