ama kweli mgeni njoo, mwenyeji aupune; tumeambiwa leo tuwe smati na ikiwezekana tupige suti. hii imekaaje wadau, maana nimewaendea na fulanazzz yetu wamenitoa mkuku...
halafu leo mji kiiimyaaaaa. wengi wanarudi makwao mapema maana barabara kibao zinafungwa mchana huu. soma zaidi hapa www.dailynews-tsn.com ama www.habarileo.co.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Michu! kwanini hujapiga ile kaunda suti yako uliyovaa siku ya kuapishwa kwa JK? ingekuwa mwake mkubwa, lkn kama inakubana siyo issue hata ivyo umetoka chichaaaa

    ReplyDelete
  2. Kweli tabia ya kukaa na ma model ni mbaya haya ona michuzi kaanza kushika kiuona ! haya taratibu uko bomba kaka

    ReplyDelete
  3. kweli africa malimbukeni nyie mkienda nchini kwao wanawanyima uhuru wenu na kuwa fungia wananchi ndani sasa kwanini mwaharibie watu weekend yao kwa kuwafungia makwao kwasababau ya bwana KICHAKA anakuja.mara ngapi KIKWETE anapita hapa England mimi niko london siwahi kusikia yuko zaidi ya viombo vya habari Tanzania kujifagia Rais yuko nje ya nchi kwa ziara maalum.hapa hata kwenye local news paper sijasikia kitu kama hicho ukoloni ukikuingia inakuwa tabu sana.Juzi kunampuuzi hapa kazini eti ananiuzi mama yako anakuja ulaya unazani atarudi AFRICA eti atafurahia sana nakupata cultural shock.nikamwambia for your information anaijua dunia kuliko hata wewe.

    ReplyDelete
  4. suti imetulia hiyo michuzi ,haya tunasubiria habari za mgeni wetu ,

    ReplyDelete
  5. Mheshimiwa Rais Kikwete,Shikamoo.Chonde chonde baba kwa unyenuekevu tunakuomba siku ya jumatatu ui declare iwe public holiday maana kwa kweli siku hiyo it is useless kujaribu kwenda kazini kutokana na wingi wa bara bara zitakazofungwa kulingana na taarifa ya Tibaigana.Hata Dubai wakati wa ujio wa Mzee Bush serikali ilitangaza public holiday ili kupunguza msongamano.

    ReplyDelete
  6. Ahhhh!! 'Smart Casual' hiyo mkulu,ila kitambulisho unacho kaka??hawachelewi kukutimua hata wewe Mcheza Kwenu!!

    ReplyDelete
  7. Kwani suti huna bro? Hebu kabadirishe haraka!

    ReplyDelete
  8. Miswaki mmepiga lakini? Barabara mmefagia lakini?
    Yaleyale ya ujio wa Clinton!!!

    ReplyDelete
  9. Bro tunasubiri sana news toka huko!! kuhusu ujio wa huyu Mshkaji, Leo sitoki hapa! Nakusikilizia tu!

    ReplyDelete
  10. Hapo umetoka mwake, usiende vaa suti, utapata ugumu wa kupiga posture/pause sahihi ya kupata picha nzuri. Halafu ume match hiyo CAmera yako, shati na viatu? Kapige kazi Michu uje utupe yaliyojiri katika ujio huu. All the BEST. MKWELI

    ReplyDelete
  11. Sasa Michu ndugu yangu..kuambiwa muwe smart ndio hivo?
    Yani hapo umeona umemalizaaa??Ndio umevunja ya mwisho wa sanduku ama?
    Acha masihara wewe..watakutimia na mtumba wako huo halafu wadau tukose wa kutupasha habari za jikoni.
    Nenda kabadilishe haraka uwahi kufanya coverage acha utani na kazi,hizo ulizovaa sio nguo ni mararuo.
    Usimaindi ni ushauri tu,wadau msinimeze

    ReplyDelete
  12. Imetulia kiasi lakini si kwa sababu ya mzee kichaka tu,Smartness ni wakati wote hasa maeneo ya kazi.Kifulana bro kimetulia hasa wakati wa investigative habari kama vile za rich,hepa,twin na singo minarazi.
    Tupo tyuned wadauzi kuona yanayojiri huku jijini bongoland

    ReplyDelete
  13. Naungana na mdau hapo juu.Mimi ninaandika nikiwa Kigali Rwanda,unajua Bush akitoka Tanzania anakuja Rwanda.Ila kuanzia jana waamerica wameshaanza kujaa uwanja wa ndege,ukionekana umevaa kanda mbili maeneo ya uwanja wa ndege polisi inakuchukua mpaka siku Bush akiondoka...sasa kweli hiyo ina maana gani.Nawashaangaa viongozi wa Africa kila siki Gadaffi akileta hoja ya Africa kuwa Moja hakuna anayekubaliana nae sababu ya uchoyo wa madaraka,mnadhani Africa ikiwa moja tutazidi kunyanyaswa hivi.najua hata Rais kagame akienda America kuna kipindi anatoka hajaonana na Bush au watu kukamatwa au Kugunga barabara kama sisi tunavyofanya.Kweli ukoloni haujaisha.

    ReplyDelete
  14. hapo kaka Michu umetoka mchicha ile kishenzi.Utafikiri unaenda ukweni.

    ReplyDelete
  15. wallahi umependeza,sio kujitia kwenye suti zao,tuonyeshe utamaduni wetu.sasa tunasubiri picha za kichaka.

    ReplyDelete
  16. kaunda ya nguvu,imetulia kulko suti za kina Lowassa

    ReplyDelete
  17. Michuzi hao ndugu zako wanaandamana leo lakini wiki ijayo wengine wataonekana ubalozi wa marekani wakiomba visa, sasa nashindwa kuelewa wanaandamana nini?

    ReplyDelete
  18. secret service watawakaguwa hadi nguo za ndani kuangalia kama hamna mabomu,wewe subiri muone.Wale jamaa wanawahi miezi kama miwili kabla ya ziara ya Rais wa marekani.Kama hamjavaa VIP mpya mnarudishwa home na wale mnaovaa nguo za ndani za mitumba,vitenge ama zenye mikwiji bora msiende watawaumbuwa mbele ya umati.

    ReplyDelete
  19. Wapendwa, hata Jakaya angeenda na mabilioni ya kujenga barabara za Washington Wazungu wangemlamba Miguuu..
    Tuache majungu, fanyeni kazi uchumi ukue ndio muwe na kibuli..

    Babat

    ReplyDelete
  20. Hii picha inanipa hofu, michuzi ulikuwa unguja(zenji) muda si mrefu uliopita.wasiwasi wangu isijekuwa wazee wa baraza walikulipia kila kitu na haya mambo ya kujishika kiuno yakawa ndiyo matokeo yake.Maana zenji na mombasa ndiyo mambo yao.UKiingia kichwa kichwa watu wanagharamia kila kitu,malazi,makulaji nk.

    ReplyDelete
  21. Michuzi anza kwenda mazoezini, kitambi utakuwa kama trafiki au mameja jenerali wetu !! tehe tehe tee !!! yule trafiki mayebo bado yupo?

    ReplyDelete
  22. Mbigiri, acha matusi kwenye hii blog. kama huna la kuchangia kalale.

    ReplyDelete
  23. kikwete akienda marakani waandishi wa habari wanavaa jeans na kijamba koti,nyie mnaambiwa mvae suti!!WHY?WHY KUWA SMART...mbona bush mtu wa kawaida tuu..mdau norway

    ReplyDelete
  24. Aisee mbona hii suti yako inafanana na sare ya Bitebo salon,ama baada ya zali la kukosa ile suti Bitebo amekufadhili ha ha ha haa

    ReplyDelete
  25. Jamani Kikwete akija Marekani anakuja kuomba misaada.Bush akienda Tanzania anakuja kugawa pesa.Sasa hatuoni hizi tofauti????

    Wazungu husema money talks.Tuwabane mafisaidi kina Lowassa,Rostam wazrudishe pesa.Then Kikwete aje Marekani kutoa misaada.Na huku barabara watafunga,suti watavaa.

    Mnaonaje??Umaskini mbaya sana.

    ReplyDelete
  26. Kweli kaka Michuzi leo umetoka mwake kama vile sio wewe haya kaka all the best huko vumbini au matopeni baada ya mvua kunyesha kwa siku kadhaa,mpelekeni na kule kijichi ambapo hakuna daraja ili aone mkoje kaka bongo tambarare. Mwosha vibibi......

    ReplyDelete
  27. Kwa nyie mnaokandia hiyo safari ya bUsh bongo, Mimi nina methali tatu tu za lugha yetu ya kiswahili nataka niwakumbushe "Mtumikie Kafiri, upate mtaji wako" , "Baniani mbaya kiatu chake dawa" na "Mwenye pesa sio mwenzako" ingawa hii ya mwisho kwa kweli sikumbuki kam mwalimu wangu wa kiswahili alinifundisha ama nimetunga. La msing ni kwamba watanzania tusijifanye Masikini jeuri wakati dhiki tunayo na ya kujitakia , Hawa watu kama kina Bush and Co. wasingetunyanyasa kama tusingemaliza uchumi wa mnchi kwa kuleana na kuwaachia watu kama kina LOwasa wakala nchi kiasi kwamba wakayuacha hoi. Maana yule bwana huko umasaini nasikia na idadi yake ya ngombe anaweza kulisha nchi nzima kwa siku tatu, wamasai wote wanachunga ngombe za Lowassa, haya mambo hayako Marekani na nchi zilizoendele, Viongozi ni waadilifu na wako very accountable, juzi juzi kuna jamaa Uingereza ilibidi aachie ngazi kwa kisa kuna mtu kwenye kampeni yake alipokea pesa tena ndogo tuu kam zawadi kwa njia ziizotakiwa na kuitumbukiza kwenye kampeni. Mpaka WATANZANIA tutakapoacha kunyanyasana wenyewe kwa wenyewe na kuacha hulka ya kuwa Mwizi ndio anapewa heshima kubwa katika jamii kuliko mtu anaetafuta haki yake, KINA BUSH WA Ulimwengu huu ni wengi na watatutawala MILELE. !! Kaka Michuzi mie sikujua kama na wewe ni mtu wa kumaindisha kivazi!! Ungeenda kwa huyo designer bora wa Bongo bwana Hassanali akakutengeneza sawasawa !! but not bad at all u tried !!

    ReplyDelete
  28. YAP HAPO MR MICHUZI NAKUPATIA B+. U LOOK CASUL

    ReplyDelete
  29. We michuzi, lile shati liko wapi bwana wewe!! Mgeni kaingia unatakiwa uwe umewekelea like shati lako bwana we!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...